KATIKA hali isiyotarajiwa, wapiga kura katika uchaguzi wa marudio kata ya Sukuma, wilayani Magu, leo wamekuta
karatasi za uchaguzi wa kata zilizopo jimbo la Tarime.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Wilfred Lwakatare, karatasi hizo ziko katikati ya vitabu vya kura za
wagombea wa udiwani wa kata zilizoko MAgu.
Anasema kati ya karatasi 50 utakuta kuna karatasi kati ya tano na kumi zenye picha na majina ya wagombea wa
Tarime.
Kura hizo walikuwa wakiwapa wapiga kura wazee na sasa wasimamizi wa uchaguzi katika vituo wamegombezwa na
wasimamizi wa uchaguzi.
Lakini kwa mujibu wa viongozi wa Chadema taarifa kama hizo zimekuwa nyingi mno kiasi cha kuwa sasa wamekuwa
makini hawataki kujichanganya na kuacha kupambana kulinda kura zao. Wamesema kwanza kutoka Magu hadi Tarime ni
umbali mrefu ambao hawawezi kusafirisha kura hadi Tarime.
Chadema wanasema hilo linawezekana ni kosa la uchapaji, japo watafanyia kazi kila taarifa baada ya uchaguzi na
msisitizo kwao ni kulinda kura zinazopigwa na kulinda pia kuingia kwa mtu au kura zozote kutoka nje ya vituo au
nje ya Tarime.
HABARI NDIO HIYO: