Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
KATIKA hali isiyotarajiwa, wapiga kura katika uchaguzi wa marudio kata ya Sukuma, wilayani Magu, leo wamekuta

karatasi za uchaguzi wa kata zilizopo jimbo la Tarime.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Wilfred Lwakatare, karatasi hizo ziko katikati ya vitabu vya kura za

wagombea wa udiwani wa kata zilizoko MAgu.

Anasema kati ya karatasi 50 utakuta kuna karatasi kati ya tano na kumi zenye picha na majina ya wagombea wa

Tarime.

Kura hizo walikuwa wakiwapa wapiga kura wazee na sasa wasimamizi wa uchaguzi katika vituo wamegombezwa na

wasimamizi wa uchaguzi.

Lakini kwa mujibu wa viongozi wa Chadema taarifa kama hizo zimekuwa nyingi mno kiasi cha kuwa sasa wamekuwa

makini hawataki kujichanganya na kuacha kupambana kulinda kura zao. Wamesema kwanza kutoka Magu hadi Tarime ni

umbali mrefu ambao hawawezi kusafirisha kura hadi Tarime.

Chadema wanasema hilo linawezekana ni kosa la uchapaji, japo watafanyia kazi kila taarifa baada ya uchaguzi na

msisitizo kwao ni kulinda kura zinazopigwa na kulinda pia kuingia kwa mtu au kura zozote kutoka nje ya vituo au

nje ya Tarime.

HABARI NDIO HIYO:
 
Mkuu kithuku,

Sasa imagine public figure kama huyo anaongea huu upuuzi.Wanatarime pambaneni na huyu mtu awatake radhi.Hili ni zaidi ya tusi.Sasa ina maana watu ni duni namna hii? kumbe viongozi wa CCM ndivyo wanavyotuona sisi wananchi? Yes,nimetumia CCM kwa sababu huyo ni katibu mwenezi wa hicho chama.
 
Kikao cha CCM kimemalizika jana saa tano usiku katika hoteli ya CMG. Kimeamua mambo mazito matatu yafuatayo:

1) Vituo vya sirari, tarime mjini, nyamongo, nyamwaga, bumera, trm sec na vituo vya itiryo ambako chadema wana nguvu mawakala wa ccm wamepewa laki tatu ya kuwapa mawakala wa chadema na wasimamizi wa vituo wanapewa laki tano.

2) Polisi wameambiwa kuhoji barua za mawakala wa chadema na hivyo kuwazuia kuingia kwenye kituo kwa muda wakati zoezi la kupiga kura likiwa linaendelea. Ingawa sio jukumu la polisi kufanya hivyo lakini mkakati ni kwamba wakati polisi wanawazuia mawakala nje ya kituo huko ndani msimamizi anapata muda wa kuweka mambo sawa.

3) wasimamizi kutohoji picha za wapiga kura na wanatakiwa wafuate majina ya wapiga kura yaliyobandikwa nje ya kituo ambako vijana wengi majina yao hayapo. pia kuwazuia mawakala wa chadema kutumia daftari la kudumu lenye picha ya kila mgombea waliopewa na chama chao.


Wadau milioko Tarime je hayo hapo juu yametendeka? Na je wapiga kura wamejitokeza kwa kiwango kipi? na je mazingira ya usalama yapo vipi? na je kura wanaanza kuhesabu saa ngapi? tunaomba updates
 
Na huko Tarime, wanaambiwa karatasi za kujumlisha hazijafika, kuna taarifa kwamba zimebadilishwa. Vijana wengi wamezuiwa kupiga kura.

Kila la kheir
 
Nadhani hii iunganishwe kule katika hoja ya uchaguzi wa Tarime
 
MAkamanda msiwe na hofu CCM tunawapiga kwa mbali sanatu zaidi hata ya mwaka 2005, tutawapa fundisho zuri sana tu.
 
According to my realible source in tarime,chadema is leading so far though the gap is so narrow.
Any change might happen but there'll be no landslide win for sure and CCM are so determined to winning at any cost!
 
According to my realible source in tarime,chadema is leading so far though the gap is so narrow.
Any change might happen but there'll be no landslide win for sure and CCM are so determined to winning at any cost!

Wataona cha mtema kuni!
 
Wakti tukisubiri matokeo naotoa changamoto kwenu wana JF kwa utabiri wangu wa hali itakayofuata baada ya ya matokeo..

USHINDI kwa CCM utazua balaa...kutakuwepo na hali mbaya sana Tarime kiusalama, na yawezekana CCM wakapoteza imani zaidi toka kwa wanachi..

USHINDI wa Chadema, utakuwa ushindi kwa CCM...chama tawala kitaweza kuonyesha dunia kwamba wao wanafuata demokrasia ya kweli pamoja na kwamba wamekwisha fanya mengi machafu.

Tatizo kubwa ni viongozi wa chama tawala ambao hawatapenda kupoteza kabisa jimbo hilo kutokana na rasilimali za jimbo hilo ambazo tayari serikali imekwisha ingia mikataba ya shirika la kigeni...
Kulingana na akili ya Wadanganyika, ambapo viongozi ni reflection yetu sisi basi Ushindi wa CCM ktk jimbo hili ni LAZIMA!..hivyo uchaguzi huu ni mwanzo tu wa mambo mengi yanayofuata...

Leo hii sii wananchi wa Tarime wanaopanda mbegu zao, isipokuwa chama tawala
(serikali) ndio Kinapanda.
 
uchaguzi wa tarime ni mtihani kwa amani na utulivu wetu......ni vema serikali ikajitahidi kadiri iwezavyo ili haki itendeke na ionekane imetendeka .....ili mapigano wasitokee yakatutia dowa...
 
uchaguzi wa tarime ni mtihani kwa amani na utulivu wetu......ni vema serikali ikajitahidi kadiri iwezavyo ili haki itendeke na ionekane imetendeka .....ili mapigano wasitokee yakatutia dowa...

PM.. mbona that is too late; .. sasa hivi ni kuangalia ni kwa kiasi gani tu hali haiwi mbaya zaidi ya ilivyo. Doa la Tarime halijaanza kwenye uchaguzi huu, wamekuwa wakinyanyaswa, kupigwa, kuuawa n.k bila nchi yetu kushtuka. Na hata Wangwe alipoamua kulishtua Bunge akaambiwe afute kauli yake!
 
MAkamanda msiwe na hofu CCM tunawapiga kwa mbali sanatu zaidi hata ya mwaka 2005, tutawapa fundisho zuri sana tu.

Mkuu,

Please ukipata updates utupatie tafadhali. Ila wasijaribu kutumia nguvu kulazimisha ushindi.Maanke CCM na ZANU-PF lao moja.
 
Update 1:

Kata ya Nyarukoba, kituo cha Genkuru:

Kituo A:
CCM - 42
CHADEMA - 78

Kituo B:

CCM - 22
CHADEMA - 70
 
Vituo vilivyopatikana kwa haraka ni hivyo, maeneo mengi ndio wamemaliza kupiga kura na zinaendelea kuhesabiwa. Matokeo yanaweza kupatikana kwa wingi saa 3 zijazo
 
Mkuu Invisible,

Heshima mbele mkuu.tunashukuru sana kwa updates bro.

Yaani hawa jamaa wameanza kupigwa za uso mcana mchana? Ole wao wabake demokrasia
 
Asante sana usieonekana!ila mbona vyama vingine sijaona?NCCR na DP
 
Asante sana usieonekana!ila mbona vyama vingine sijaona?NCCR na DP
Ukiona hivyo, elewa vyama hivyo vina kura kidogo sana, niliviweka kando, niliweka top two. Well, vituo vingine nitakupeni hata vyama vingine.

Ahsante FL kwa kunikumbusha hili
 
Hapo nadhani Makamba anatamani ingeongezwa siku moja ya kupiga kampeni tena.It's too late.

Wakishaona hivyo wataanza kupanga mkakati wa kuiba kura,na wataiba kwa kupaniki hadi washtukiwe.Wanatarime lindeni haki yenu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom