Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
CCM walidhani vitisho vya Polisi na kauli za kejeli za Msekwa na Makamba zitawapa ushindi. Wanatarime hongereni, ni ukombozi dhidi ya makucha ya kifisadi ya CCM. Tukipata wilaya hata 30 kati ya 120 na ushee Tanzania, kama Tarime,tutakuwa tumepiga hatua kubwa.
 
Huyo FairPlayer asiwababaishe wakuu, aibu tu imemkumba na anaumwa sana kutokana na huu ushindi.Muhurumieni tu!
 
kama ni kweli mungu ibariki tanzania


Mie bado siamini. Pamoja na nguvu yote ya fedha, magogo/vigogo, double helicopter, na fabrications kuhusu kifo cha Wangwe?


Mkubwa,
Mgombea wa UDP amepata kura mia tatu na ushee, NCCR kura mia tisa na ushee, CCM kura 28 elfu na CHADEMA 34,800..

Kwa matokeo hayo kura nyingi inaelezwa zimeharibika.

Tunasubiri tupewe figures kamili.



Kubwagwa kwa kishindo ndiyo ilikuwa hofu kubwa kwa CCM.





.
 
Taarifa imetolewa rasmi na msimamizi wa uchaguzi, nadhani details zitapatikana muda si mrefu bila shaka baada ya mabomu kutulia,maana kuna kelele za darfur darfur darfu!!!! hongera chadema kulinda viti vyenu!

Kama kawa ebwana hiyo imek fresh kabisa
watanzania wote tungekuwa kama wananchi wa Tarime ingekuwa mwake kinoma
hongera
 
CCM walidhani vitisho vya Polisi na kauli za kejeli za Msekwa na Makamba zitawapa ushindi. Wanatarime hongereni, ni ukombozi dhidi ya makucha ya kifisadi ya CCM. Tukipata wilaya hata 30 kati ya 120 na ushee Tanzania, kama Tarime,tutakuwa tumepiga hatua kubwa.


Natamani mkumsikia makamba atakavyowajibu waandishi wa habari hovyo.Chiligati bado anaogopa kujitokeza hadharani maanke juzi tu vijana wa Tarime walimtoa mkuku
 
Tazama ilivyo vyema na kupendeza, wananchi wapige kura kwa haki na matokeo yatoke kwa haki.

sina hakika sana kama natakiwa kufurahia dhidi ya ushindi huu maana still hili lilikuwa jimbo la chadema. vyama vya upinzani vijitahidi kujithibitisha uwezo wao kwa wananchi kwa vitendo ili 2010 waweze kuyachukua majimbo mengi zaidi ya ccm na sio kuendekeza porojo kama Chama Cha Mafisadi (CCM) kilivyofanya ktk uwepo wao wote.

Hongera chadema, nguvu mliyoianzisha iendelee ili 2010 mgawane majimbo 50/50
 
mkubwa,matokeo rasmi haya hapa.

Vituo 406
idadi 146919
waliopiga kura 67,733
kura halali 64,765
haribika 2,938
udp 305
nccr 949
ccm 28,696 42.6%
chadema 34,545 51%

aliekuwa mgombea wa sisiemuu kangoye aaliche;ewa kufika wakati matokeo yanatangazwa.alipofika amedai kuwa hayatambui matokeo ya uchaguzi huo.chakushangaza alishasaini karatasi za matokeo lakini anang'ang'ania majumuisho kwa upya.

I think he has gone mad

ninatanguliza shukrani kwako, mungu akubariki kwa taarifa inayojibu hoja zote.

Sisi kama wana ccm tunayakubali matokeo haya ingawaje si kwa urahisi hususani kwa mgombea wetu kangoye na wenzetu wa tarime.

Tusonge mbele na tuijenge nchi yetu kwa amani.
 
Naona mkuu umenuna.

Yaani lundo loote la ma-zecomedy mlilipeleka huko halafy wanatarime na CHADEMA wakawa-prove wrong?

Na bado mna kazi,halafu kasome kwenye gazeti la Nipashe huko Mbeya wamachinga wamewapa kichapo mgambo kwa kuwafukuza maeneo yao ya biashara ili mkwere apite.

Haya ndiyo mapambano yanaanza,sijui una lakusema? Naona angalao wewe unajitahidi kujitokeza hapa leo,hongera ila pole sana mkuu.Nakuombea majeraha ya moyo yapone

hiyo ndio demokrasia ,ukishindwa unakubali matokeo na sio kulalamika hata kampeni haijaanza.

Mimi nakubali % kadhaa kuwa ccm visiwani huwa wanaiba kura lakini huku bara ni mapepe tu ya wapinzani.

Hongera kwa ushindi .
 
Tena wawe makini sana maanake upinzani hata ukifikisha 40% ya wabunge 2010.Basi 2015 CCM watakua kuzimu na akina KANU,UNIP etc
 
Phil,

Tumesimama wima. Tumekubali kushindwa. Ndo demokrasia.

Hongereni Chadema. Matokeo sasa ni rasmi.

Kidumu chama cha mapinduzi
 
Mkamap na FairPlayer,

Nashukuru kwa kuonyesha uungwana.Wanasiasa wetu waige sasa mfano wenu wakukubali matokeo wanaposhindwa.Nguvu ya umma haishindwi hata siku moja kuleta mabadiliko
 
What does the Tarime results mean? Hivi ni kweli wenzetu wa mikoani eg Tarime, Karatu etc ni more informed and competent citizens kuliko sisi tunajiona tupo mijini mfano sisi wa Dar es Salaam na miji mingine mikubwa? Come on shame upon us!!!!
 
Ohhh,
NINA RAHA SANA HATA NIKICHINJWA LEO, SICHINJIKI.

HONGERA MBOWE, SLAA, ZITO, KANGOYE NA TIMU NZIMA YA CHADEMA. ZAIDI SANA HONGERENI WANATARIME KWA KUTUFANIKISHIA HILI. HONGERENI SANA JF KWA MAWASILIANO, TARATIIIBU TUNAANZA KULIUMBA TAIFA.
 
KJ
Matumizi ya helikopta kwa CHADEMA ni halali hawana ten cell system kama ya CCM.Kutokana na hali hiyo mawasiliano yao ni lazima ukutane na wapiga kura wengi kwa kadiri inavyowezekana.Hiyo inarahisisha usafiri na kunadi sera kwa watu wengi inavyowezekana.
Ukumbuke vilevile CHADEMA ilizushiwa tuhuma nzito sana,ni bahati nzuri wapiga kura wa Tarime wanajua kupembua mchele na pumba.Mtu anayestahili kuulizwa ni Makamba, kwa nini atumie helikopta wakati chama chao kimetawala kwa miaka zaidi ya 45?Kwa nini miundombinu ya barabara haijatengemaa na anawaelezeje wapiga kura wa Tarime kuhusu hali hiyo.Mimi kwa maoni yangu CHADEMA unawahukumu bure wakati hawajapewa ridhaa ya kuongoza nchi.
 
Tunawashukuru ndugu zetu wa tarime kwa kuonyesha ukomavu wa siasa. Watanzania the rest inabidi tujifunze kutoka Tarime. Mura muda wa kufurahia kapelo na T shirt za kijani umepitwa ni kudumisha ufisadi. Watanzania hatujachoka kiasi cha kuhitaji kuvishwa sare na wana CCM. Just imagine fedha zote zinazotumika kutengenezea hizo sare wanatoa wapi?? CCM wakae chonyo sasa tupo kwenye zama za tofauti tunahitaji utekelezaji tu mbwembwe kwaya na ngonjera tushachoka navyo.

Tarime Oyeeee Chadema Oyeeeee.

kwa wenzangu na mie wasioelewa somo mpaka kwa vitendo sasa nadhani washaelewa.
bilashaka 2010 tutaingia Dar na kujichukulia vilivyo vyetu.
 
Nyie mlioko huko Tarime,baada ya shamrashamra zote kwisha basi pitieni pale hospitali/dispensary tukawajulie hali wahanga wa uchaguzi. Kuna vijana wa chadema walipigwa mapanga. Mkiwapitia kuwaona mtawatia nguvu zaidi.
 
Tunawashukuru ndugu zetu wa tarime kwa kuonyesha ukomavu wa siasa. Watanzania the rest inabidi tujifunze kutoka Tarime. Mura muda wa kufurahia kapelo na T shirt za kijani umepitwa ni kudumisha ufisadi. Watanzania hatujachoka kiasi cha kuhitaji kuvishwa sare na wana CCM. Just imagine fedha zote zinazotumika kutengenezea hizo sare wanatoa wapi?? CCM wakae chonyo sasa tupo kwenye zama za tofauti tunahitaji utekelezaji tu mbwembwe kwaya na ngonjera tushachoka navyo.

Tarime Oyeeee Chadema Oyeeeee.

kwa wenzangu na mie wasioelewa somo mpaka kwa vitendo sasa nadhani washaelewa.
bilashaka 2010 tutaingia Dar na kujichukulia vilivyo vyetu.
 
Yaani hata kura zilizoharibika ni Zaidi ya mara 9.6 ya kura za mgombea wa Mtikila?

Na ni zaidi ya mara tatu ya mgombea wa NCCR?

Na ni zaidi ya mara 2.3 ya kura za DP na NCCR?

Mbona mtikila atakua kituko? Kwa hiyo ukiangalia wale mamluki wameumia zaidi wakidhani watagawa kura za CHADEMA.Wamepata Fresh!
 
Hongera sana mbunge mteule Mhe.Charles Mwera, natumaini utakumbuka kulipa fadhila kwa wapiga kura wako na wananchi wa tarime kwa ujumla kwa kuwapa utumishi bora.

Hongereni sana wananchi wa Tarime kwa kupata Mbunge aliye chaguo lenu, wekeni sasa tofauti chini mpeni support anayoihitaji, kwa pamoja endelezeni ujenzi wa Tarime.

Hongereni sana, tena sana Uongozi na wanachama wote wa CHADEMA, uwezo wenu mliouthibitisha kupitia uchaguzi huu mdogo unastahili kutambuliwa na kuheshimiwa haswa!
Shime kaza kamba, 2009 na 2010 ziko mlangoni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom