Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Upinzani unanishangaza maanake wanatakiwa kujifunza kutokana na historia.Leo hii hainiingii akilini kuona watu Kama CUF,CHADEMA wanaungana na Mamluki Paul Kyara.

Huyo jamaa ni kikwazo kikubwa cha mageuzi nchini
 
Siasa za kigoma nitofauti na mara,

Siasa za kigoma zinamilikiwa na msikiti wa legezamwendo na msikiti wa wagoma(ujiji), hawa niwapinzani wa jadi. mgombea akitoka msikiti huu basi msikiti mwingine hawakubaliani nae.

Ukiondoa wanasiasa matajiri kama nashon bidyanguze waliosalia huangukia kwenye huu mtego, bahati mbaya zitto haeleweki anaswali msikiti gani?
 
Kaka wa Chacha Wangwe aihama CCM
Makubo Haruni, Tarime
Daily News; Tuesday,August 12, 2008 @00:02

Anajiandaa kuwania ubunge kupitia NCCR-Mageuzi

KAKA wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, Peter Wangwe, amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na anajiandaa kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi ili kugombea ubunge katika jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na ndugu yake kwa takribani miaka miwili.

NCCR- Mageuzi mkoani Mara ilitangaza kumpata mgombea wake huyo, Peter mwenye umri wa miaka 55, ambaye kwa miaka 11 alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime. Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Mara, Steven Sebeki alisema jana kuwa chama hicho kitamsimamisha Peter kuwania ubunge baada ya kukubali kung'oka kutoka katika chama tawala, CCM.

Sebeki alisema licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kumnyemelea Peter aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa miaka 11 kabla ya kustaafu udiwani mwaka 2005, amekubali kujiunga na NCCR- Mageuzi na juhudi zinafanywa za kuanza kumnadi muda wa kampeni utakapowadia.

Peter maarufu kwa jina la Keba, alikiri kusaka nafasi hiyo kupitia upinzani, ingawa alisema hajachukua kadi ya chama chochote kati ya CUF na NCCR-Mageuzi, kwa maelezo kuwa bado yuko katika mazungumzo ya kifamilia kumtafuta atakayetunza familia ya marehemu Chacha.

Peter, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema ameamua kuondoka CCM ambako alikuwa Meneja Kampeni kwa miaka 20, kwa madai ya kufungwa mdomo na mwanachama wa chama hicho anaposema ukweli kuhusu masuala mbalimbali ya serikali, kuliko ilivyo kwa upinzani ambako kama alivyokuwa mdogowe, alisema wazi bila kukoromewa na ye yote kuhusu hujuma na ufisadi akitetea wapigakura wake.

''Ni kweli viongozi wa vyama hivyo wamenifuata na kunitaka kugombea kwa tiketi ya vyama vyao, lakini NCCR- Mageuzi kilinitaka zaidi,” alisema Peter na kuongeza: “Mimi kwa sasa sina hata raha na wala sijisikii kuwa ndani ya CCM, walionifanyia hila wakati wa kura za maoni mwaka 2005, nilipogombea ubunge na kunifanya nishike nafasi ya nne, na kutokana na kurudisha jina ambalo lilikuwa halikubaliki, upinzani uliibuka mshindi kwa kura nyingi,” alidai mwanasiasa huyo.

Alipoulizwa kuhusu taratibu za vyama vya upinzani kuungana na kumpata mgombea mmoja kushindana na CCM, Kamishna Sebeki alisema kila chama kipo katika mbio za kushika dola, hivyo kwa kipindi cha uchaguzi mdogo, itakuwa ni zamu ya NCCR-Mageuzi kusimamisha mgombea na kuungwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), CUF na Tanzania Labour (TLP), vyenye ushirikiano.

Wakati NCCR-Mageuzi ikiwa na uhakika wa kupata mgombea, vyama vingine havijatoa tamko licha ya wananchi nao kutoa maoni mbalimbali kuhusu watu wanaofaa kushika mikoba ya Chacha aliyekufa kwa ajali ya gari katika eneo la Pandambili Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Julai 28, mwaka huu, akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Tayari wapo wanaotajwa kupewa nafasi ya kuwania kiti hicho, wakiwamo mwanasiasa wa siku nyingi, Enock Haruni (Macho), mtunzi wa vitabu vya kujifunzia katika masomo ya sekondari, Nyambari Nyang'wine, Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ryoba Kangoye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Charles Mwera na John Heche. Kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, uchaguzi mdogo utafanyika siku 90 tangu kifo cha mbunge, hivyo kwa utaratibu huo, nafasi ya Wangwe itajazwa mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.
 
.....kahama CCM for the reason eti kafungwa mdomo? i think theres degree of dishonesty hapo...hopefully wapinzani wataweka mtu makini ili washinde waendeleze kazi ya mpiganaji Chacha Wangwe.
 
NCCR wako hoi yoyote mwenye dalili za kushinda jimbo hilo wao watamkubali kwa mikono yote..!!

Ila sijui huyu kwenye familia yuko kaibu kiasi gani sababu iwapo atasimamishwa na NCCR na ataungwa mkono na Chadema, TLP na CUF basi sioni dalili za Prof Samwel Wangwe kugombea kwa tiketi ya CCM.
 
NCCR wako hoi yoyote mwenye dalili za kushinda jimbo hilo wao watamkubali kwa mikono yote..!!

Ila sijui huyu kwenye familia yuko kaibu kiasi gani sababu iwapo atasimamishwa na NCCR na ataungwa mkono na Chadema, TLP na CUF basi sioni dalili za Prof Samwel Wangwe kugombea kwa tiketi ya CCM.

Kumuenzi mdogo wake, at least for now, si vizuri kwa Prof Wangwe kugombea kurithi kiti cha ubunge wa Tarime kilichoachwa na mdogo wake huku akutumia tiketi ya chama kilichokuwa kinapingana na chama kilichokuwa kikiwakilishwa mdogo wake hata kama inajulikana kua mdogo wake alikuwa na mitafaruku huko kwenye chama chake. Prof angefanya hivyo tu iwapo mdogo wake angekuwa ametangaza kuhama upinzani muda mfupi kabla ya kupoteza uhai wake. Vingenvyo inabidi Prof asubiri hadi kipindi cha mdogo wake kiishe mwaka 2010 ndipo agombee kama mgombea fresh, siyop kama mgombea anayetaka kundeleza mapambano yaliyoachwa na mdogo wake.
 
Indume
Naona umenisoma, hakika CCM haina chake hapa nyumbani na si vinginevyo,
Nyumbani wapi sasa Mkuu?? TANZANIA au Tarime??
**Ni-kama unasema kuwa ni MWIKO kwa Mtanzania asiye Mkurya kugombea Ubunge na kuziba pengo la marehemu Wangwe.Remember:Tanzania First,then Tarime-that should be the mentality.
 
Nyumbani wapi sasa Mkuu?? TANZANIA au Tarime??
**Ni-kama unasema kuwa ni MWIKO kwa Mtanzania asiye Mkurya kugombea Ubunge na kuziba pengo la marehemu Wangwe.Remember:Tanzania First,then Tarime-that should be the mentality.

Ukiacha majimbo ya Dar es Salaam, huko kungine ni UKABILA mtindo mmoja.
 
Tunapenda madaraka kwa kiwango gani? Huyu anaamini katika itikadi gani? Alikuwa mtendaji akitekeleza sera za CCM, kumbe moyo wake haukuwa huko kabisa (kama angekuwa huko asingekuja na hii hadithi ya kuhama hivi sasa).
Anahama kwa sababu anazibwa mdomo au njaa ya madaraka? Kama ni kuzibwa mdomo ndio amegundua sasa baada ya bafasi ya ubunge kwua wazi? Mbona hakulijua hilo tangu awali na kuondoka? Huyu ni opportunist tu
 
Je Singida mkuu? Morogoro je? Sasa kama watu kutoka sehemu nyingine hawakujitokeza ulitaka wananchi waache kupiga kura?
 
Kama kuna yeyote, iwe chama au mtu, anayetaka kushinda tarime, basi aandae rushwa ya kuwazidi wengine
 
Kama kuna yeyote, iwe chama au mtu, anayetaka kushinda tarime, basi aandae rushwa ya kuwazidi wengine



Mkuu,Takrima si imepigwa marufuku? Hivi mbona hili taifa letu tunafanyiana mizaha kila kukicha? Kwa mtindo huu chaguzi za kidemokrasia hazina maana.ni bora ambae anatumia nguvu kutwaa madaraka na kuaachana na huu upuuzi ambao ni wastage of time and resouces and the worst of all Division among the members of society.Nadhani bado dhana ya Demokrasia hapa Tanzania tumeidandia tu na itatuumiza sana
 
Je Singida mkuu? Morogoro je? Sasa kama watu kutoka sehemu nyingine hawakujitokeza ulitaka wananchi waache kupiga kura?

Hauwezi kujitokeza kusiko KWENU, kwenye KABILA yako. Labda uwe na fedha nyingi kama akina Dewji, RA, yule wa Gairo,...Kwa sababu ya UFUKARA uliokithiri wa watu wetu; Pesa peke yake ndio inaweza kuupiku ukabila.
 
Kama kuna yeyote, iwe chama au mtu, anayetaka kushinda tarime, basi aandae rushwa ya kuwazidi wengine

Jimbo la Tarime kama yalivyo majimbo ya PEMBA, pesa haijakuhakikishia USHINDI. Chacha Wangwe hakuwa na pesa wakati anashinda UBUNGE kule.
 
Kwa hiyo, Peter Wangwe (NCCR- MAGEUZI) na Prof. Samwel Wangwe (CCM) ndo watagombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Tarime ili kuchukua nafasi ya Chacha Wangwe (RIP). oh, kumbe ni akina Wangwe....
 
safi sana kwa wanatarime huko ndiko Demokrasia inatakiwa ianzwe kwanza
 
Mods hebu baada ya muda tuunganishe hii thread na ile ingine ya wagombea na uchaguzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom