Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Kweli Tanzania tuna wanasiasa. Mimi namwamini Dr. Slaa lakini kwenye hili inatakiwa afuate ushauri ambao wengine tulisema mapema. Waacheni hawa wafiwa waomboleze kifo cha bwana wao.

Unajua kuingiza siasa kwenye kila kitu itatuletea balaa. Hakuna haja ya kuingiza siasa hata kwenye misiba. Wakifanya hivyo watu wa mitaani sawa nitaamini, lakini wanapofanya wasomi na viongozi wa umma inakuwa balaa kabisa.

Wanasiasa wa vyama vyote waacheni hao mama waomboleze kifo cha bwana yao.

Tunaweza kuiandama familia kama huyo aliyekufa alikuwa ni fisadi, au katuibia vilivyo vyetu, lakini kwa hii ya Wangwe, mungu amechukua, wacha tuwaachie ndugu na familia.
 
Teh teh teh,mkuu unachekesha kweli yaani.Katika pitapita yako yoote umeenda kuibua gazeti la mafisadi na kulileta hapa.Mkuu acha hizo bwana kumbe uko biased sana? Ngoja na mimi niweke kitu hapa chini maanake ni jino kwa jino au kichwa kwa ulimi,muulize mtikila.
 
Date::9/29/2008
Mke mwingine wa Wangwe aibuka kumpinga mke-mwenza mdogo

Mke wa kati wa Marehemu Chacha Wangwe, Dotto Mohamed, ambaye anapinga maelezo ya mke mdogo Mariam Wangwe kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimetelekeza familia hiyo baada ya kifo cha baba watoto wao.
Na Kizitto Noya

KIFO cha Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe kinazidi kuibua mengi baada ya mke wake wa kati Dotto Mohamed kukana maelezo ya mke mdogo Mariam Wangwe kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitelekeza familia.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dotto alisema kauli ya Mariam ni nzito mno kuitoa sasa kwani anaamini matukio yanayoendelea baada ya kutokea msiba huo, ndiyo yanayoweka pazia la mawasiliano kati ya Chadema na familia ya Marehemu.

"Sijaisoma taarifa yote ila mtoto wangu ameniletea gazeti ambalo bado ninalo. Mimi ninashindwa kufikiria wala kuwaza kuanza kukilaumu Chama kwamba kimetutelekeza kwani ni mapema mno kufanya hivyo na wote bado tuko kwenye majonzi," alisema Dotto na kuongeza:

Nasema nashindwa kukilaumu chama kwa sababu tangu kutokea kwa msiba huo hakuna aliyetulia, familia bado ina majonzi, chama chenyewe bado kinalia na hata jamii inaendelea kumlilia Wangwe nasema familia yangu bado ina imani na chama na hatuwezi kukilaumu sasa," alisema.

Dotto alisema anaamini Chadema inaongozwa na watu wenye busara hivyo hawezi kuinenea mabaya kabla ya kuridhika kwamba viongozi hao wameanza kupingana na busara hiyo.
"Ninihitaji muda kupima hekima ya chama kabla sijakihukumu kwani kinyume chake nitakuwa sijakitendei haki," alisema.

Alisema mpaka sasa bado anaamini kuwa Chadema iko sambamba na familia ya marehemu Wangwe kwani hata kwenye arobaini iliyofanyika kijijini Komakorere chama hicho kilituma wawakilishi.
Mke huyu wa pili wa Chacha Wangwe anaishi jijini Mwanza na jana alikuja jijini Dar es Salaam kuwachukua watoto wake wawili waliokuwa wakiishi na Mariam, mke mdogo wa Wangwe.

Jana Dotto aliiambia Mwananchi kuwa katika safari yake hiyo pia amepanga kukutana na Mariam na kuzungumza naye ili ajue kiini cha shutuma zake kwa Chadema.

"Kuja kwangu Dar es Salaam ni pamoja na kuwachukua wanangu wawili ambao wamekuwa wakiishi na Mariam; katika ujio huo tutakaa tuzungumze anieleze kwa nini ameamua kuzungumza maneno hayo sasa,".

Alisema hata kama Mariam atafanikiwa kumshawishi aamini maneno yake, bado atahitaji muda kukubaliana naye kwani anaamni kuwa bado ni mapema mno kutoa shutuma hizo.

"Sisi bado tuna imani na Chama na hatuwezi kujua chama kinatuwazia nini hivyo narudia: ni mapema mno kutoa shutuma hizo kwani wote bado tuko kwenye majonzi," alisisitiza.Akizungumzia kauli ya Dotto, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema ndiyo aliyotarajia kusikia kutoka kwa familia ya marehemu Wangwe.

"Nafikiri kauli hiyo ndiyo niliyotarajia kutoka kwa familia ya Wangwe ninayemfahamu kwa sababu kama utakumbuka tangu mwanzo wa msiba, sisi (CHADEMA) tulikuwa tukisakamwa sana lakini tulikaa kimya kwa busara ili tusimkamate mchawi asiyetuhusu," alisema.

Dk Slaa ambaye alisisitiza kwamba hamfahamu Mariam kama mke wa marehemu Wangwe, alisema anasikitishwa na kauli yake ambayo anaamini kuwa imelenga kukichafua chama.

Hiki anacholalamikia kwamba Chadema hawakuhudhiria arobaini ya mume wake, nashindwa kuelewa. Kumbuka mimi nina miaka 60 na tangu nianze kufahamu arobaini, najua zinafanyika mahala alikozikwa marehemu.

Wangwe alizikwa Komakerere na arobaini yake ilifanyika huko na Chadema tulituma mwakilishi. Hii arobaini aliyoifanya Mariam na Profesa Wangwe Dar es Salaam hatukuijua wala wao hawakutaka Chadema iijue," alisema.
Akifafanua alisema ingawa Mariam alitoa taarifa ya arobaini aliyoifanya Dar es Salaam, waalikwa katika taarifa hiyo ni wabunge kwa majina yao na sio Chadema kama taasisi.

Alisema pamoja na kasoro hiyo wabunge wa Chadema Suzan Lyimo na Grace Kihwelu walihudhuria kwa kofia zao lakini waliwakilisha chama kwa salamu ambazo zilisomwa na Lyimo katika hafla hiyo.

"Mimi Dk Slaa nilialikwa kwa ubunge wangu na sio ukatibu mkuu wa Chadema na Mbowe alialikwa kwa jina lake na sio uenyekiti wa Chadema vivyo hivyo wabunge wengine. Sasa Chadema inapolaumiwa tunashindwa kuelewa," alisema na kuendelea

"Mimi namshauri Mariam akutane na wazee wamshauri kwanza badala ya kukurupuka na kutoa maneno ya kukipaka matope chama. Yeye anataka athaminiwe, atathaminiwaje kama yeye Mariam hataki kukithamini chama," alihoji

Kauli ya Dotto na Dk Slaa imekuja siku tatu baada ya mke wa tatu wa Marehemu Wangwe kuzungumzia utata wa kifo cha mumewe na kukitupia lawama Chadema kwamba kimeitelekeza familia baada ya kifo hicho.

Mariam alienda mbali zaidi na kumtaka spika wa Bunge Samwel Sitta kuchunguza kifo hicho akidai kuwa haridhiki na uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi.

Wangwe, mwanasiasa machachari aliyepata umaarufu kwa kuibua hoja tata bungeni, alifariki dunia katika ajali ya gari wakati akisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kuhudhuria mazishi ya mfanyabiashara na mbunge wa kwanza wa jimbo la Tarime Bhoke Munamka.

Lakini mazingira ya kifo chake yalizua utata mwingi baada ya kuchukuliwa kama agenda ya uchaguzi mdogo katika kampeni zinazoendelea sasa jimboni humo kumpata mrithi wa kiti chake.

Tayari Jeshi la Polisi limemfungulia mashtaka Deus Mallya aliyekuwa akisafari na marehemu kwa tuhuma za kusababisha mauaji hayo.

Lakini mke huyo mdogo wa Wangwe anaona juhudi hizo za polisi ni ndogo na hivyo, serikali na Spika Sitta hawana budi kuongeza uzito wao.

"Sipendi mambo haya yaishe hivi hivi," alisema mama huyo. "Familia ya Wangwe haijaridhishwa na namna polisi wanavyofuatilia kifo cha Wangwe."

"Wasiwasi wangu ni uchunguzi unaofanywa na polisi kwani hawajawahi hata kufika kuniuliza kuhusu kifo cha Wangwe nikiwa kama mke wake."Labda maelezo yangu yangewasaidia kwa kiasi fulani.

Akizungumzia hali ilivyokuwa katika kipindi cha kuelekea kifo cha mumewe, Mariam alisema mambo yalikuwa magumu sana nyumbani, hasa baada ya Wangwe kusimamishwa nafasi yake ya makamu mwenyekiti wa Chadema.

Pia Mke wa pili wa marehemu Chacha wangwe,Doto amesema

cha msingi ni viongozi kusaidi kulea watoto tisa aliowaacha marehemu ambao ni Zakayo na Rhobi (18) ambao ni mapacha, Bob (17), Pendo (16), Beatrice, (15) na Wangwe mwenye miaka 14 ambao ni watoto wa mke mkubwa nayeitwa Ghati.

Kwa yeye Doto ana watoto wawili, Mwajuma (11) na Ghati (6) wakati Mariam ana mtoto mmoja anaitwa King (1).
 
Teh teh teh,mkuu unachekesha kweli yaani.Katika pitapita yako yoote umeenda kuibua gazeti la mafisadi na kulileta hapa.Mkuu acha hizo bwana kumbe uko biased sana? Ngoja na mimi niweke kitu hapa chini maanake ni jino kwa jino au kichwa kwa ulimi,muulize mtikila.

Ben,

Majira ni gazeti la mafisadi? Mimi sijui hata nani anamiliki, labda tuambie mwenzetu mmiliki wa hilo gazeti ni nani?

Mimi ni msomaji mzuri wa gazeti la majira na mwananchi maana naona muda mwingi wanaandika habari za maana. Ndio maana mara nyingi na forward habari toka Majira na Mwananchi. Hii ya kwamba ni gazeti la kifisadi ndio unaniambia wewe.

Kwahiyo hata hao viongozi wa CHADEMA Kinondoni ni mafisadi?

Aidha hujakatazwa kuleta hapa habari yoyote ambayo unaona inafaa. Binafsi nitaichambua hiyo habari na wala sio messenger.
 
Marehemu alikuwa mzuri katika exploration ya wake...naona wako wa kutosha kabisa.
Sasa katuachia wapinganaji wao kwa wao....
 
Kweli Tanzania tuna wanasiasa. Mimi namwamini Dr. Slaa lakini kwenye hili inatakiwa afuate ushauri ambao wengine tulisema mapema. Waacheni hawa wafiwa waomboleze kifo cha bwana wao.

Unajua kuingiza siasa kwenye kila kitu itatuletea balaa. Hakuna haja ya kuingiza siasa hata kwenye misiba. Wakifanya hivyo watu wa mitaani sawa nitaamini, lakini wanapofanya wasomi na viongozi wa umma inakuwa balaa kabisa.

Wanasiasa wa vyama vyote waacheni hao mama waomboleze kifo cha bwana yao.

Tunaweza kuiandama familia kama huyo aliyekufa alikuwa ni fisadi, au katuibia vilivyo vyetu, lakini kwa hii ya Wangwe, mungu amechukua, wacha tuwaachie ndugu na familia.

Mkuu hata wewe unajua nilikua nikiheshimu sana mchango wako lakini nimekuta wewe ndio walewale unaetaka kuuchafua upinzani.Leo hii unapokaa nyuma ya kompyuta yako na ku-type bila kujua hadi Dr.Slaa anatamka aliyotamka yalianzia wapi? Hivi si huyo mjane unayedai aachwe aomboleze msiba wa bwana wake ndiye amekua akishirikiana na akina Rostam na Makamba kukichafua chama? wewe uko very biased sikufichi,na mkuu unapokua biased namna hiyo kunadumaza hata akili ya kukufanya upambanue mambo ya muhimu.

Leo hii unaweza kushuhudia watu wakikurupuka na kumlaumu Dr.Slaa bila kujua kauli za huyo mwanamke zinachochewa na wabaya wa CHADEMA,ndiyo mana sikushangaa mambo uliyochangia hapo juu mkuu wangu maanke wewe ni moja wapo wa watu wanaojidai independent kumbe uko tayari kuona upinzani ukichafuliwa na unaushabikia na kuanza kumrushi Dr Slaa shutuma nzito bila subira.

Kwanza huyo mwanamke anawadhalisha wanawake wote hapo bongo anapotumia neno kama 'mambo ya kike'.Huyo nadhani anahitaji ushauri kabla ya kupayuka kwenye media
 
Ben,

Majira ni gazeti la mafisadi? Mimi sijui hata nani anamiliki, labda tuambie mwenzetu mmiliki wa hilo gazeti ni nani?

Mimi ni msomaji mzuri wa gazeti la majira na mwananchi maana naona muda mwingi wanaandika habari za maana. Ndio maana mara nyingi na forward habari toka Majira na Mwananchi. Hii ya kwamba ni gazeti la kifisadi ndio unaniambia wewe.

Kwahiyo hata hao viongozi wa CHADEMA Kinondoni ni mafisadi?Aidha hujakatazwa kuleta hapa habari yoyote ambayo unaona inafaa. Binafsi nitaichambua hiyo habari na wala sio messenger.

Hapooo hapo sasa! ( Msondo Ngoma )
 
Mkuu hata wewe unajua nilikua nikiheshimu sana mchango wako lakini nimekuta wewe ndio walewale unaetaka kuuchafua upinzani.Leo hii unapokaa nyuma ya kompyuta yako na ku-type bila kujua hadi Dr.Slaa anatamka aliyotamka yalianzia wapi? Hivi si huyo mjane unayedai aachwe aomboleze msiba wa bwana wake ndiye amekua akishirikiana na akina Rostam na Makamba kukichafua chama? wewe uko very biased sikufichi,na mkuu unapokua biased namna hiyo kunadumaza hata akili ya kukufanya upambanue mambo ya muhimu.

Leo hii unaweza kushuhudia watu wakikurupuka na kumlaumu Dr.Slaa bila kujua kauli za huyo mwanamke zinachochewa na wabaya wa CHADEMA,ndiyo mana sikushangaa mambo uliyochangia hapo juu mkuu wangu maanke wewe ni moja wapo wa watu wanaojidai independent kumbe uko tayari kuona upinzani ukichafuliwa na unaushabikia na kuanza kumrushi Dr Slaa shutuma nzito bila subira.

Kwanza huyo mwanamke anawadhalisha wanawake wote hapo bongo anapotumia neno kama 'mambo ya kike'.Huyo nadhani anahitaji ushauri kabla ya kupayuka kwenye media

Ben,

It doesn't matter aliyoyatamka yameanzia wapi, huwezi kusema humtambui mke wa mtu, unaweza usimtambue mkeo lakini kuingilia familia ya mtu mwingine sio siasa. Hata uchukie vipi bado hiyo sio siasa.

Pili mimi sijali kabisa kama huheshimu mchango wangu. Siko hapa kufurahisha mtu au kutaka kuheshimiwa na mtu. Sio mtu wa misifa na hutanikuta nikiabudu misifa. Kama huheshimu michango yangu ndio vizuri, utanifanya nifikiri zaidi. I am here for a challenge na sio kuabudiwa full stop!

Nitaandika kile ninachokiamini na kukitetea hata kama natapingwa na kila mtu. Sifuati upepo nafuata ninachokiamini. Na kwenye hili naamini ni makosa kuwaingiza wajane kwenye mambo ya kisiasa bila kujali ni chama gani. Hata kama watasema ambayo mtu huyapendi, kuna njia zingine za kuongea nao. Mtu mwenye majonzi sio rahisi sana akawa makini kwenye anachosema na nwanasiasa yeyote inatakiwa alijue hilo.
 
Ben,

Majira ni gazeti la mafisadi? Mimi sijui hata nani anamiliki, labda tuambie mwenzetu mmiliki wa hilo gazeti ni nani?

Mimi ni msomaji mzuri wa gazeti la majira na mwananchi maana naona muda mwingi wanaandika habari za maana. Ndio maana mara nyingi na forward habari toka Majira na Mwananchi. Hii ya kwamba ni gazeti la kifisadi ndio unaniambia wewe.

Kwahiyo hata hao viongozi wa CHADEMA Kinondoni ni mafisadi?

Aidha hujakatazwa kuleta hapa habari yoyote ambayo unaona inafaa. Binafsi nitaichambua hiyo habari na wala sio messenger.

Ni kweli kabisa na nashukuru kulitambua hilo maanake hakuna wa kuweza kunikataza kuweka habari yoyote.Hata wewe Hautakatazwa kamwe,ila acha kuwa biased maanake wewe ni muumini mzuri katika kupinga double standard and i thought you dont support it,but what's happening now? Pia wewe si ni mtu ambaye ni independent?

Je,kama wewe ni msomaji mzuri wa hayo magazeti ,hukuona umuhimu wa kupost pia habari ya gazeti la mwananchi.Niliposema uko biased nimekosea? wala usipoteze muda hapa kujitetea let us move on!
 
Kweli Tanzania tuna wanasiasa. Mimi namwamini Dr. Slaa lakini kwenye hili inatakiwa afuate ushauri ambao wengine tulisema mapema. Waacheni hawa wafiwa waomboleze kifo cha bwana wao.

Unajua kuingiza siasa kwenye kila kitu itatuletea balaa. Hakuna haja ya kuingiza siasa hata kwenye misiba. Wakifanya hivyo watu wa mitaani sawa nitaamini, lakini wanapofanya wasomi na viongozi wa umma inakuwa balaa kabisa.

Wanasiasa wa vyama vyote waacheni hao mama waomboleze kifo cha bwana yao.

Tunaweza kuiandama familia kama huyo aliyekufa alikuwa ni fisadi, au katuibia vilivyo vyetu, lakini kwa hii ya Wangwe, mungu amechukua, wacha tuwaachie ndugu na familia.

You maybe right but you're missing a point at the last paragraph; kwa nini uwandame memba wa familia ya fisadi? Makubwa haya!
 
Ben,

It doesn't matter aliyoyatamka yameanzia wapi, huwezi kusema humtambui mke wa mtu, unaweza usimtambue mkeo lakini kuingilia familia ya mtu mwingine sio siasa. Hata uchukie vipi bado hiyo sio siasa.

Pili mimi sijali kabisa kama huheshimu mchango wangu. Siko hapa kufurahisha mtu au kutaka kuheshimiwa na mtu. Sio mtu wa misifa na hutanikuta nikiabudu misifa. Kama huheshimu michango yangu ndio vizuri, utanifanya nifikiri zaidi. I am here for a challenge na sio kuabudiwa full stop!

Nitaandika kile ninachokiamini na kukitetea hata kama natapingwa na kila mtu. Sifuati upepo nafuata ninachokiamini. Na kwenye hili naamini ni makosa kuwaingiza wajane kwenye mambo ya kisiasa bila kujali ni chama gani. Hata kama watasema ambayo mtu huyapendi, kuna njia zingine za kuongea nao. Mtu mwenye majonzi sio rahisi sana akawa makini kwenye anachosema na nwanasiasa yeyote inatakiwa alijue hilo.

Kwanza kanusha kauli yako ya kuabudiwa,ukiangalia hapa JF katika members wote,who is weak enough to worship you? who? Hapana mkuu haya ni matusi,eti kunaweza kuwa na members wa kukuabudu?

Unasema kuingiza siasa katika ndoa za watu au wake za watu,je wakikubali kutumiwa kisiasa wanategemea nini? Si wamejiingiza wenyewe?

Ungekua unaitakia CHADEMA mema ningeweza kukuelewa,lakini wewe ni muumini mkubwa wa double standards.
 
Lugha ya kikurya inapotumika kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Tarime ni sawa? Je suala la wengine kutofahamu lugha ya Kiswahili kwa ufasaha ndio iwe kigezo,tunaienzi kweli lugha yetu Kiswahili?
 
Ni kweli kabisa na nashukuru kulitambua hilo maanake hakuna wa kuweza kunikataza kuweka habari yoyote.Hata wewe Hautakatazwa kamwe,ila acha kuwa biased maanake wewe ni muumini mzuri katika kupinga double standard and i thought you dont support it,but what's happening now? Pia wewe si ni mtu ambaye ni independent?

Je,kama wewe ni msomaji mzuri wa hayo magazeti ,hukuona umuhimu wa kupost pia habari ya gazeti la mwananchi.Niliposema uko biased nimekosea? wala usipoteze muda hapa kujitetea let us move on!

Mimi nimeanza kusoma gazeti la majira na nika post hiyo habari? Sasa ulitaka mpaka misome magazeti yote ndio niamue cha kupost? hata ningeamua hivyo bado ningeanza ku post habari moja na kisha nyingine.

Lakini pia mtu ana post kitu ambacho kinaendana na hoja husika. Toka jana mimi naandika kuhusu kuwaacha hao wajane wa marehemu, kutokuwaingiza kwenye mambo ya siasa. Nilipoona hii habari nikaona inaendana na kile ambacho nimekuwa nikiandika toka jana na ndio maana nikaipost.

Kama hukubaliani na kilichoandikwa, basi jadili na sio kuanza kusema kwamba ulikuwa unaheshimu michango yangu. Kama ulikuwa unaheshimu pia unahaki sawa ya kutoiheshimu na hutasikia hata siku moja mimi nikikushambulia wewe binafsi.

Niko kwenye hii mijadala miaka mingi sana ninajiamini na ninachoandika na niko tayari kupingana na mtu yeyote hata wale ambao ni mrafiki. Kama hulipendi hilo sawa, mimi sitakunyonga wala kukushambulia wewe, nitaendelea kujadili hoja zako.
 
Wacha waenzi lugha yao....muraah uhohiree....amanang'ahana ghasarikile na lisisiem muraaaaaaa
 
Kwanza kanusha kauli yako ya kuabudiwa,ukiangalia hapa JF katika members wote,who is weak enough to worship you? who? Hapana mkuu haya ni matusi,eti kunaweza kuwa na members wa kukuabudu?

Unasema kuingiza siasa katika ndoa za watu au wake za watu,je wakikubali kutumiwa kisiasa wanategemea nini? Si wamejiingiza wenyewe?

Ungekua unaitakia CHADEMA mema ningeweza kukuelewa,lakini wewe ni muumini mkubwa wa double standards.

Ben,

Wewe ndiye uliyeanza kwa kuandika ulikuwa unaheshimu michango yangu. Hiyo ni weakness kubwa sana, inatumiwa na watu wanaotaka kuonewa huruma.

Wengine tunapojadili hoja we don't carer mwandishi aliandika nini jana. Unaweza kutumia maandishi ya nyuma kama tu kuna contradictions lakini sio kwa kusema eti ulikuwa unaheshimu mawazo yangu, who cares?

Andika hoja zako na songa mbele, unaheshimu mawazo ya mtu au hauheshimu hilo ni chaguo lako.

Double standards? sawa, zionyeshe hizo double standards ziko wapi na hilo ndilo la kujadili.
 
Huu ni utetezi wenye kupoteza muda tu,you are so biased!

Halafu unakua mtu usiyeelewa,nani kawaingiza hao wanawake kwenye siasa? si wao wenyewe? au hapa nako unataka kusema ni kwa sababu tangia jana ulikua ukiliongelea hilo suala ndiyo maana hutaki kubadili mawazo?

Kuwa na msimamo hakumaanishi uendelee kushikilia lile baya la kuupotosha umma,kufikia hapo nadhani basi maana halisi ya Msimamo inasumbbua watu wengi sana.

Ila tafadhali naomba uaache kufikiria kwamba inawezekana kuna watu wanakuabudu humu ndani,please and please.Ondoa hayo mawazo.

Pia kuwa kwako katika forums muda murefu hajalishi sana bwana,mbona kingunge amekua kwenye siasa enzi na enzi lakini ameendelea kuwa kichefu chefu kwa wananchi na aibu kwa kizazi hiki?
 
Lugha ya kikurya inapotumika kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Tarime ni sawa? Je suala la wengine kutofahamu lugha ya Kiswahili kwa ufasaha ndio iwe kigezo,tunaienzi kweli lugha yetu Kiswahili?
Kuna wachagga kiasi hapo, wewe chana kichagga tu nao watakupa kura! Kama ulikuwa hujawahi kwenda kampeni za mikoani hukujua hilo, kampeni ni kwa vilugha tuu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom