Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Ngoja na sisi familia ya KOLIMBA tujikusanye na twende kwenye vyombo vya habari kudai TUME HURU ya kuchunguza utata wa kifo cha baba yetu dhidi ya wauwaji CCM
 
Pia sitaki watu waheshimu mawazo yangu maana hiyo ni weakness kubwa mno kuheshimu mawazo ya mtu. Hakuna mtu mwenye yeyote hapa duaniani ambaye mawazo yake yote ni sahihi

Hapa umevunja kimya changu kwa kuonyesha ni kiasi gani wewe ni dhaifu, mbishi asiye na uelekeo na mtu asiye na upeo.
Kama utaki watu waheshimu mawazo yako unafanya nini mbele ya sceen yako? Ondoka nenda ukalale. Usipotezee muda walewanaotaka kuchangia mawazo ya kuheshimika. Wacha wao waendelee. g9t nenda kalale.
 
Hapa umevunja kimya changu kwa kuonyesha ni kiasi gani wewe ni dhaifu, mbishi asiye na uelekeo na mtu asiye na upeo.
Kama utaki watu waheshimu mawazo yako unafanya nini mbele ya sceen yako? Ondoka nenda ukalale. Usipotezee muda walewanaotaka kuchangia mawazo ya kuheshimika. Wacha wao waendelee. g9t nenda kalale.

Wasomi wa JF bwana, yaani kwa andiko moja unaweza kujua mtu hana upeo? Kwi kwi kwi!!

Inatakiwa uitwe profesa wa JF! Ndio maana maana nchi ina maprofesa wengi kupiga ramli kuliko wa kujua na kufundisho mambo.

Wengine tunakubaliana/kupingana na mchango wa mtu kwenye hoja husika. Mambo ya kuheshimu mawazo ya mtu ndio yalizaa zidumu fikra za mwenyekiti, ziwe mbaya au nzuri.
 
kwa hiyo Tyson ana wake watano na watoto 39 na Wangwe alikuwa nao watatu na watoto 9? teh teh teh teh na hawa ndio viongozi wanaotuingiza karne ya 21,nafikiri kuna haja ya kujadili hili swala maana lina impact kubwa sana kwenye jamii!
 
Hivi watu kama hawa, wamefikaje hata kushika madaraka makubwa ya nchi? Haitendei haki kabisa familia ya Wangwe. Inaelekea utu haupo kabisa sasa kwa wanasiasa.

Mtamzania,
Unakumbuka yale mapendekezo yako baada ya Mtikila kusema uongo na kupigwa mawe? Uli-question kwa nini wale wasikilizaji hawakwenda mahakamani? Now I think you understand; there are no ethics in this country; we told you from the top man to the man in the street, we lack common sense; the rule of law! Did you think an "so called elder" will give such vapour? This contry's ethical standard is rotten to an extend that is unimaginable!
 
CCM: Ruksa kutumia kifo cha Wangwe kisiasa

2008-09-30 11:36:47
Na Simon Mhina


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni `ruksa` ndugu wa Marehemu Chacha Wangwe kutumia jukwaa la kampeni za Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Tarime kuzungumzia hisia zao juu ya mazingira ya kifo cha ndugu yao.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Pius Msekwa alisema ndugu hao wana haki kuzungumzia kifo hicho kwenye jukwaa la CCM kwani hizo ndizo haki za binadamu.

Akifafanua, mwanasiasa huyo alisema ndugu hao ukiwaondolea jukwaa la siasa, hawana sehemu nyingine ya kusema, kutoa dukuduku zao na kuonyesha hisia zao.

Msekwa ametoa kauli hiyo akijibu malalamiko ya viongozi wa Chadema kwamba baadhi ya vyama vimekigeuza kifo cha Wangwe kuwa mtaji wa kisiasa katika uchaguzi huo.

``Jamani nyie hamfahamu haki za binadamu, wale wana madukuduku yao, lakini wamekosa mahali pa kusemea, wanapopanda kwenye majukwaa yetu wanaona hiyo ni sehemu muafaka, ruksa hatuwezi kuwazuia,`` alisema.

Hata hivyo, Msekwa alisema wanaolalamikia kifo cha Wangwe sio CCM, bali ndugu zake.

Alisisitiza kwamba nchi yetu imetoa uhuru wa kujieleza kwa kila mwananchi, ili mradi asivunje sheria, hivyo wanachokifanya ndugu wa Wangwe ni sahihi.

``Kwa mfano juzi nimesikia mjane wa marehemu yeye akitumia jukwaa la vyombo vya habari kutoa hisia zake mbona hakunyimwa? Kwa hiyo na sisi hatuwezi kuwanyima fursa hiyo kama wanataka,``alisema.

Alipoulizwa kama haoni suala hilo ni sawa na uchochezi, Msekwa alisema mtu kudai kwamba haelewi mazingira ya kifo cha marehemu wake kilivyotokea sio uchochezi.

``Tutaendelea kuwakaribisha ndugu wa Wangwe kwenye mikutano yetu na hatuwezi kuwapangia cha kuzungumza,``alisema.

Alisema wameamua kufanya hivyo, kwa vile ndugu wa marehemu wamejirizisha kwamba kifo hicho kilijaa utata.

Pia alisema malalamiko kama hayo hayakuanzia kwenye jukwaa la CCM, bali kwa kaka wa Marehemu huyo Profesa Wangwe.

Kuhusu mwenendo wa kampeni, Msekwa alisema hakuna vitisho vyovyote vinavyotolewa na Polisi na hao wanaodai kuna askari `wamemwagwa` hawaelewi mambo.

Alisema vikosi vya askari vilivyomwagwa ni kwa ajili ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuwa amini dhidi ya wezi wa ng`ombe.

``Unajua huku kuna wezi wa Ng`ombe na mapigano ya koo, hivyo lazima polisi wawe wengi,``alisema.

Alipoulizwa kama Polisi wamemtuma atoe msimamo huo, Msekwa alisema tataribu za Polisi ziko wazi, hawawezi kuletwa sehemu kwa nia ya kuvuruga, bali kulinda amani.
Alisema raia wema hawana sababu yoyote ya kuogopa Polisi.

SOURCE: Nipashe

Wameishiwa hoja? Nahisi wanaelekea kuzama.......Prove me wrong
 
Zito sasa hatarini!!!!!

2008-09-30 23:04:57
Na Mashaka Mgeta, Tarime


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe anachunguzwa kwa tuhuma za kuongoza zoezi la kuchoma moto T-shirt za Chama cha Mapinduzi (CCM) na ikibainika ni kweli, yuko hatarini kuburuzwa kortini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tarime asubuhi leo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Stanley Kolimba amesema tukio hilo linaweza kuharibu utulivu na amani katika kampeni za uchaguzi zinazoendelea.

Akasema baada ya uchunguzi kukamilika, Mhe. Zitto na wanachama wengine wa chama hicho wanadaiwa kuchoma T-shirt hizo, watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Fulana hizo zinazodaiwa kurejeshwa na wana-CCM, zilichomwa katika mkutano wa hadhara wa Chadema wilayani Tarime.

Mkutano huo ulikuwa ukihutubiwa na Mhe. Kabwe ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, na ulifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Nyamisangura wilayani humo.

Aidha, katika mkutano huo, Bw. Kolimba amedai kuwa kuna chama kimoja cha siasa kimeleta vijana kutoka kijiji kilichoko mpakani cha Kurya nchini Kenya, na wilaya nyingine nchini kwa lengo la kufanya vurugu katika uchaguzi huo.

Hata hivyo, hakukitaja chama hicho cha siasa lakini hivi karibuni kulikuwa na madai kutoka chama cha Chadema kuwa CCM wameingiza vijana wilayani Tarime.

Pia amedai kuwa wanawake wamekuwa wakifanyiwa vitisho ili wasihudhurie katika mikutano ya vyama vya siasa, jambo ambalo linawanyima fursa ya kushiriki katika uchaguzi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tarime ambaye ni msimamizi wa uchaguzi, Bw. Trasias Kagenzi ametunishiana misuli na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. Ryoba Kangoba.

Hatua ya kutunishiana misuli ilifuatia mgombea huyo kuwasili katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi, akitoa madai ya kuwepo kwa zoezi la uandikishaji wa shahada za wapiga kura.

Hata hivyo, wakati akimtambulisha kwa waaandishi wa habari, Bw. Kagenzi alisema Bw. Kagomba amekuja pale kama mgombea na si mwenyekiti wa Halmashauri.

Hali hiyo ilimfanya Bw. Kangoba kujibu mapigo kuwa asingeweza kumfuata ofisini kwake kama angekuwa anatumia kofia yake ya Uenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya na badala yake angemuita ofisini kwake (Kangoba).

Uchaguzi huo unaofanyika, Oktoba 12 mwaka huu, unafuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, marehemu Chacha Wangwe ambaye alifariki katika ajali ya gari.

SOURCE: Alasiri
 
mshenziii mkubwa hii ndio anaona ukvunjwaji wa amani

pumbafuuuuuuuuuuuu mkubwa we dc na CCM YAKO!!!WALE FFU WALIOKUTWA WANANUNUA KADI ZA CCM WALIKUWA WANAIMARISHA UPENDO????????
DEM U
 
Habari imekaa kisarakasi. Ryoba ni mgombea wa CCM na hajawahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri. TV zimeonyesha mkutano uliohutubiwa na Zitto, wakati fulana zinachomwa Zitto alikuwa juu ya jukwaa ambalo ni gari aina ya FUSO lililovunjwa vioo na wahuni waliotumwa na tajiri anayegombea udiwani. Hivi hao polisi waliomwagwa huko si ndio wenye jukumu la kuhakikisha hakuna vitendo vyovyote vya kuvunja amani? Walishindwaje kuzuia hizo fulana zisichomwe? Wakukamatwa hapo ni Tossi ili wananchi wajue uhalali wa fedha yao inayolipwa kwa Tossi na genge lake kama posho.
 
Serikali ya Kenya yaombwa kudhibiti vijana kuingia Tarime
Frederick Katulanda,Tarime

MKUU wa wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba amemtaka mkuu wa wilaya ya Kurya Magharibi nchini Kenya kuchunguza na kuzuia kundi la vijana ambao wanadaiwa kuingia kinyemela Tarime na kufanya vurugu katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa mbunge na diwani.


Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, mkuu huyo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, pia alivionya vyama vyote vya siasa kuepuka vitendo vya vurugu ambavyo vimekuwa vikitawala kwenye kampeni hizo na kuhatarisha usalama.


Alisema tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi, mambo mengi yamejitokeza, akiyataja kuwa ni kupigwa mawe jukwaani kwa kiongozi wa chama cha DP, Mch. Christopher Mtikila, kushambuliwa kwa mawe kwa gari la Chadema, uchomaji wa hadharani wa fulana za CCM ikiwa ni pamoja na kuzuia vyama vingine kufanya kampeni na vitisho dhidi ya wanawake.


"Pia kuna madai kuwa lipo kundi la vijana ambao wamekua wakitoka nchini Kenya katika wilaya ya Kurya Magharibi na kuja kufanya vurugu katika uchaguzi wetu," alisema.


"Tayari nimeshawasiliana na mkuu mwenzangu wa wilaya ya Kurya Magharibi ili kuona kama kweli kuna kundi la vijana waliokuja. Ikiwa itabainika hivyo, msako mkali utafanywa kuwakamata wahusika.


"Haya yote nataka kueleza kuwa tunayashughulikia na nachukua nafasi hii kuwakumbusha viongozi wote wa vyama kuzuia wafuasi wao kufanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuwafikishia maazimio ya kikao cha juzi cha tathimini ya maendeleo ya uchaguzi."


Alisema kuwa serikali imeshaanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwakamata watu wote wanaotuhumiwa kuhusika katika vurugu ambao alisema mapaka sasa idadi yao imefikia 10.


"Katika kukabiliana na uvurugaji wa mikutano ya kampeni, tumeliagiza Jeshi la Polisi kuimarisha na kuongeza ulinzi katika mikutano mbalimbali ya kampeni na pia kuhakikisha watu wote waliokamatwa katika vurugu wanafikishwa mahakamani," alieleza.
 
Huyu mkuu wa wilaya pamoja na polisi tayari wana powers za kupambana na wafanya vurugu. Inabidi wazitumie kwa nguvu zote ili kuzuia watu kuumizwa au mali za watu kuharibiwa.

Wala hana sababu hata ya kuiomba Kenya, ina maana mipaka yetu inaingiwa na wageni bila walinzi wa nchi kujua? Kama mkuu wa wilaya ina maana kashindwa kazi.

Tume ya uchaguzi na msajili wa vyama inabidi walivalie njuga hili suala la vurugu, vinginevyo huko tunakoenda kutakuwa kubaya zaidi.

Hata ufisadi ulianza hivi hivi, kidogo kidogo mpaka sasa ni donda ndugu. Mheshimiwa Masha, timiza wajibu wako kwa kuhakikisha vyama vinaendesha kampeni na kufanya uchaguzi katika mazingira ya amani. Demokrasia na fujo wapi na wapi?
 
Wakati sisi tuna anagalia mwenendo wa Kampeni basi Kolimba amekuwa katika plan B ya kuhakikisha kwamba CCM inashinda .Yeye na Afisa tawala wa Wilaya ya Tarime , OCD na Tossi wako katika plan B wakati sisi tuna angalia kwenye jukaa ambao hoja hutolewa .Kolimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime ni kuharibu kabisa maisha ya wana Tarime .Kolimba anahusika hata kuwasaidia wauaji kuachiwa kwa jina la wana CCM.Ushahidi ninao .
 
Huyu mheshimiwa ana nafasi nzuri sana ya siasa za Kitanzania...

ushauri wangu... atumie kichwa/akili zaidi kuliko kutumia moyo unasema nini?

I'm out
 
Huyu mheshimiwa ana nafasi nzuri sana ya siasa za Kitanzania...

ushauri wangu... atumie kichwa/akili zaidi kuliko kutumia moyo unasema nini?

I'm out

Kwa mara ya kwanza Kasheshe anaelekea kuelewa na kujua kwamba Zitto can make it .

Hivi mimi nikinunua shati langu ama ukanipa shati likawa langu then nikaona umenipa na sijakupenda ama nimekuchukia then why I cannot sell it ama tupa ama choma ? Je nikichukua uamuzi wowote kati ya huo hapo juu ni kosa kisheria ? Maana naona fulani watu wamepewa kule CCM lakini wameamua kuzichoma moto kuna kosa lipi kama wamegundua mafulana hayo ni sanda zao ?
 
The beginning of the end for Zitto Kabwe... very sad indeed...
 
Na bado. ZIlizochomwa sio Tshirts za ccm, ila ni za wananchi wa Tarime walizohongwa na ccm. Chochote unachompa mtu kwa ridhaa yako, kina kuwa sio mali yako tena, na mmiliki ana uhuru wa kukitumia atakavyo. Hata kama wangetumia kuchambia ni juu yao.

Lakini kubwa hapa kwa wananchi wa Tarime ambapo mie nawaunga Mkono na kuona kuwa picha nzuri kwa umma wa watanzania ambao wamekuwa wakiibiwa na mafisadi kwao kuambulia tshirts, kofia na kanga! sasa wameng'amua na kuwaonyesha kuwa hivyo havina nguvu tena. Wanahitaji sera na umakini wa mgombea kujua kuwa atasimamia nini katika kuwaondolea umaskini.

Hakuna kulala hadi kieleweke. Teketezeni takrima zote za namna hii. Ilimradi wanatarime hawalazimishwi kuzitoa! piga kibiriti!

Kama hizo tshirts wanazipenda wao kina msekwa na kina makamba wakazivae wao na watoto wao. Mbona wao hawazivai?
 
The beginning of the end for Zitto Kabwe... very sad indeed...

Masatu, suprisingly you are easily twisted with this- likely-to-be a cooked story and all the time try to be analytical when people reacts to CCM in this same manner!!!!!!!!!!!

Is this statement into your wish list??????? haha ha haaha haha!!!!!!!!!!!!!1
 
mshenziii mkubwa hii ndio anaona ukvunjwaji wa amani

pumbafuuuuuuuuuuuu mkubwa we dc na CCM YAKO!!!WALE FFU WALIOKUTWA WANANUNUA KADI ZA CCM WALIKUWA WANAIMARISHA UPENDO????????
DEM U
Tuliza munkari bibie
 
Wana-JF,

Where is the crime in burning T-Shirts?

Hii ishu inanikumbusha kule kwa watani wa jadi wakati wa Kenyatta na KANU yake. Wanasiasa kama Martin Shikuku na Jim Seroney walikua hawataki kua ndani ya chama cha KANU because it simply didn't reflect the wishes of the majority but an oligarchy of some sorts.To express their disgust nadhani walimchinja jogoo during a political rally to symbolise the fact that KANU was dead and didn't represent the people.What happened next was the arbitrary arrest of those leaders Kenyatta felt were being too progressive for his comfort.

So is the burning of these T-shirts a reflection of disgust by the people towards sisi-yemu?...and if so where is the crime?...Najua watasema 'incitement'...but we know this is so lame.

Change is an idea that cant be stopped...especially when its time has come.

Baaden.
 
Hapa umevunja kimya changu kwa kuonyesha ni kiasi gani wewe ni dhaifu, mbishi asiye na uelekeo na mtu asiye na upeo.
Kama utaki watu waheshimu mawazo yako unafanya nini mbele ya sceen yako? Ondoka nenda ukalale. Usipotezee muda walewanaotaka kuchangia mawazo ya kuheshimika. Wacha wao waendelee. g9t nenda kalale.

Mkuu,

Kula zako tano.Haa! hata mie nilishangaa sana.heshima mbele mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom