I mean ya jukwaa la Wahariri kuhusu yaliyojiri Tarime...
Twaisubilia kwa hamu, ila wasi wasi huenda wakaiminya mpaka hapo uchaguzi upite!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I mean ya jukwaa la Wahariri kuhusu yaliyojiri Tarime...
CCM wazidi kuparurana uchaguzi jimboni Tarime
Na George Ramadhan, PST, Nansio
Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wamekuwa wakitoa kauli za kukosoana kuhusu mwenendo wa kampeni katika Jimbo la Tarime wameongezeka baada Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza, Clement Mabina kudai kuwa upinzani wa siasa uliopo jimboni huko umesababishwa na Jumuiya za chama hicho kutotimiza wajibu wake kikamilifu.
Tofauti na aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho mkoa wa Tanga, Mwita Waitara ambaye alidai kuwa kampeni za chama hicho zimepoteza mwelekeo kwa kuwa zinawatumia watu wa makao makuu kufanya kampeni na kuwaacha wale wanaojua siasa za jimbo hilo, Mabina yeye alieleza chanzo cha CCM kupata upinzani mkubwa.
Mabina alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Mwanza kilichofanyika mjini Nansio wilayani Ukerewe.
Alisema kimsingi CCM hakikuwa na upinzani wilayani Tarime, lakini hali hiyo ambayo imejionyesha katika chaguzi mbalimbali jimboni humo imesababishwa na wana CCM wenyewe hususan Jumuiya za chama hicho ikiwemo UVCCM.
Alifafanua kwamba upinzani uliopo Tarime dhidi ya CCM, ulitokana na Jumuiya za chama hicho kusahau matatizo yaliyokuwa yanakabili vijana wa wilaya hiyo.
``Upinzani uliopo Tarime tumeuweka sisi wenyewe kwa kusahau matatizo ya vijana ambao tulikuwa tunawatazama tu wakikaa vijiweni bila kazi hatimaye waliamua kufuata njia yao wenyewe,`` alisema.
Mabina aliongeza kwamba hali hiyo inapaswa kuwa fundisho kwa Jumuiya ya Vijana wa CCM kutimiza wajibu kikamilifu kwa kushughulikia matatizo ya vijana kila yanapojitokeza.
SOURCE: Nipashe
Siasa za CCM zahitaji uvumilivu kwa hakika.
Tulifikiri huu ni wakati wa viongozi wa CCM kuwaambia wana Tarime watawafanyia a nini tofauti na wakati wa marehemu Chacha,badala yake wanatumia fitina na majungu kutaka kupata ushindi usio stahili.
Hatua ya viongozi wa CCM kuanza kugeukana ni ishara kuwa mbio za sakafuni zinafika ukingoni.Nasikitika sana kwa kuwa makamba na msekwa wamejibebesha gunia la misumari na sasa linawachoma.
Bado tutajionea mengi zaidi ya kutia aibu

FFU wanaweza kukabiliana na raia wenye hasira na mishale endapo hawatatumia njia za kidiplomasia!
Mwana JF mwenzetu JJ Mnyika yuko mikononi mwa polisi pamoja na mgombea ubunge jimbo la Tarime kwa Tiketi ya CHADEMA, mgombea udiwani (nadhani wa Buhemba) pamoja na Dr. Kapwani. Mpaka sasa wameshikiliwa na polisi huko Bomani - Buhemba. Ni wakati wakitokea mkutano wa hadhara.
Hii ni taarifa ya awali, zaidi tutafahamishana
Habari ya kusikitisha,kulikuwa na Taarifa kuwa Vigogo wa CCM kwa kupitia Mwenyekiti wametoa kibali cha kukamatwa kwa Viongozi wa Chadema kwa madai ya kuchochea fujo.....lakini ukweli wa mambo ni kwamba fujo za Tarime zinafanywa zaidi na wafuasi wa CCM na sio vyama vya Upinzani....hilo limethibitishwa pia na Mkuu wa Polisi wa Tarime Constantine Massawe,ambaye nae nafikiri atahamishwa huko kwani kuna Taarifa Wakuu wa Nchi wanasema haeleweki....na inawezekana ana ushabiki wa Chadema...CCM wana wakati mgumu Tarime,sasa wameamua kutumia Polisi kuwatisha wapiga kura...siku hizi za mwisho kabla ya kupiga kura.....Ndg Mnyika atakuja hapa kutupa ukweli wa mambo,kwa sababu watakuwa nje baada ya muda mfupi!!!