Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Du hii sasa inaonekana itashinda kosovo hii!

Kuna haja ya kutumia risasi kweli? Kwa upande mwingine nafikiria polisi kwa upande mwingine wanachochea hizi ghasia na fujo.

Bila shaka sasa wananchi watafunguka macho na wataweza kung'amua hila na dhuluma ya watawala na kwa nini CCM pamoja na kupoteza mwelekeo bado inajivunia amani na utulivu. Wananchi walipoteza maisha Pemba na wengine kuikimbia nchi ya amani na kupokewa kama wakimbizi kwa majirani tuliowabatiza Manyang'au. Kiteto wananchi wamekung'utwa na kupewa ulemavu wa maisha na sasa mambo yamehamia Tarime - kisa ? Ushindi wa kishindo unatafutwa na manyang'au yaliyokaa kwa mtindo wa kula.

Ninachoshindwa kukielewa ni namna gani hata humu JF unapata watu wenye akili timamu? wanaotetea hii hali. Ni vigumu kuamini kuwa serikali inayoundwa na chama chenye wabunge zaidi ya asilimia 80, kinaweza kuhamisha jeshi lote la polisi kulinda wezi wa kura ili kurejesha jimbo moja la ubunge. Bila shaka jeshi pia liko tayari kama polisi watazidiwa na hii yote inatokea kwenye nchi ya amani na utulivu. Somethings are hard to believe.
 
Vilio, kwikwi Tarime

na Kulwa Karedia, Tarime

HALI ya hewa ya kisiasa katika Wilaya ya Tarime imechafuka na kama ilivyotabiriwa na gazeti hili juzi, kuna kila dalili kwamba mwenendo wa mambo umeanza kuchukua sura ya hatari.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa na ya kushangaza, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) jana jioni waliingilia kati mkusanyiko wa wanachama na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa ndani ya magari na wengine wakitembea barabarani wakirejea kutoka katika mikutano ya kampeni na kuanza kukabiliana nao kwa marungu na mabomu ya machozi.

Pengine kwa lengo la kuonyesha kwamba walikuwa wamejizatiti kukabiliana na rabsha zozote wakati huu wa kampeni, hatua hiyo ya FFU ilisababisha kuibuka kwa vurugu zilizofuatiwa na kukamatwa kwa viongozi kadhaa wa juu wa CHADEMA wakiwamo mgombea ubunge wao, Charles Mwera na yule wa udiwani, John Suguta.

Viongozi wengine wa juu wa CHADEMA waliokamatwa na polisi hao na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi, makao makuu ya wilaya ya jeshi hilo ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana ya chama hicho, John Mnyika.

Watu walioshuhudia tukio hilo, wakiwamo waandishi wa habari wanaeleza kwamba, lilitokea majira ya saa moja jioni wakati wana CHADEMA hao wakitokea kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea wao wa udiwani, uliofanyika katika Kijiji cha Buhemba.

Wafuasi hao wa CHADEMA, baadhi yao wakiwa ndani ya magari makubwa na madogo, huku wengine wakikimbia kwa miguu, walikutwa na zahama hiyo wakati wakiimba nyimbo za kuwasifu viongozi wao pamoja na wagombea.

Wakiwa njiani, ghafla polisi walisimamisha msafara wa magari hayo na kuwataka waliokuwa wakikimbia kandokando mwa barabara kutawanyika haraka, huku wakiwataka waliokuwa juu ya magari, kuteremka na kutawanyika.

Katika kutekeleza amri hiyo, polisi waliamua kutumia nguvu kwa kuwapiga virungu wananchi hao na hali hiyo ilipozidi, polisi waliamua kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kwa muda wa takriban nusu saa, polisi walitembeza mkong'oto huku wakifyatua mabomu ya machozi na risasi hewani hadi katikati ya mji wa Tarime na kuwafanya wananchi wengi kukimbia huku na kule kujinusuru.

Tukio hilo la kukamatwa kwa viongozi wa CHADEMA limetokea siku moja tu kabla ya kuwasili katika wilaya hiyo kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe leo.

Habari zilizozagaa wilayani hapa na zilizothibitishwa na Mbowe mwenyewe kwa simu zinaeleza kwamba, kiongozi huyo ameandaliwa mapokezi mazito wakati atakapowasili mjini hapa akitokea Mwanza.

"Ni kweli nimekamilisha mipango yote ya safari ya Tarime, nimejiandaa kikamilifu kuja kuwanadi wagombea wetu ambao naamini kwamba wanaweza kurudisha jimbo hilo ambalo tumekuwa tukilishikilia tangu mwaka 2005," alisema Mbowe kwa kujiamini alipozungumza na Tanzania Daima kwa simu.

Alisema kutokana na imani kubwa aliyonayo kwa wananchi wa Tarime, CHADEMA, inaweza kuibuka na ushindi kama mbinu chafu zinazotumiwa na vyama vingine hazitatumika katika uchaguzi huo ambao unaonekana kuwa na mvutano mkali kati ya vyama vya CCM na CHADEMA.

Katika hatua nyingine, Wilaya ya Tarime jana hiyo hiyo ilikumbwa na maafa baada ya watu watano kufariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyotokea katika Kijiji cha Nyasoro, Wilaya ya jirani ya Rorya, mkoani Mara.

Ajali hiyo ya pili kubwa kutokea katika kipindi kisichozidi wiki moja, ikihusisha lori la Benz lenye tela, lililogonga dalalada aina ya Toyota Hiace, ilisababisha kusitishwa kwa muda kwa shughuli za kampeni za ubunge na udiwani katika Jimbo la Tarime.

Miongoni mwa waliofariki dunia katika ajali hiyo ni mume na wake zake wawili, waliokuwa wakisafiri na daladala hiyo kutoka Tarime kwenda Musoma kwa shughuli za kifamilia.

Ajali hiyo ilitokea jana, saa 3:45 asubuhi, baada ya dereva aliyekuwa akiendesha lori hilo lenye namba za usajili KAZ 821Z, kutaka kulipita daladala lenye namba za usajili T 808 AHU, lililokuwa likiendeshwa na Mwijuma Amosi, akiwa kwenye mwendo kasi.

Lori hilo lilikuwa likitoka nchi jirani ya Kenya kwenda Musoma likiwa na shehena ya mafuta aina ya petroli yanayokadiriwa kufikia lita 12,000.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Lebaratus Barlow, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kwamba jeshi hilo linamsaka dereva wa lori hilo, raia wa Kenya.

"Baada ya kutokea ajali hiyo, dereva amekimbia na hatujui ameelekea wapi, lakini napenda kuwahakikishieni kwamba tunamsaka kwa udi na uvumbi kwa kusababisha vifo vya watu watano...naamini tukishirikiana na wananchi wa eneo hili, tunaweza kufanikiwa," alisema Barlow.

Kamanda huyo alisema miongoni mwa waliokufa katika ajali hiyo ni mume na wake zake wawili, lakini mke mmoja amenusurika katika ajali hiyo na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

Aliwataja waliokufa kuwa ni Msoboro Ghati (55), Ghati Manyinyi (40) Nyanoko Ghati (60) - wote wa familia moja - huku Werma Ghati akinusurika katika jali hiyo.

Daladala hiyo ilikuwa na abiria na 17 na kati ya hao 10 walinusurika kwa kupata majereha sehemu mbalimbali za mwili.

"Gari hili lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara ili kubeba abiria wengine, sasa yule dereva mwenye lori alijaribu kupita kwa kasi upande wa kulia na kujikuta akikutana na gari jingine ambalo kama angezidi kupita kwa mwendo kasi, basi wangegongana uso kwa uso, hivyo akaamua kurudi kushoto na kuizoa ile Hiace," alisema Kamanda Barlow.

Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kunasua miili ya marehemu watano waliokuwa wamekandamizwa chini ya magurudumu ya lori baada ya kuyapangua.

Licha ya kufanikiwa kuopoa miili hiyo, walipata wakati mgumu kutokana na kukosa vifaa vya kuopolea miili iliyokuwa imekandamizwa chini, jambo lililofanya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kuwalalamikia askari kwamba wanachelewesha kazi ya uokoaji.

Lakini kazi kubwa ya uokoaji iliyoongozwa na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha Operesheni Maalumu, Venance Tossi, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Issa Machibya, ilisaidia kuopolewa kwa miili hiyo baada ya kufanikiwa kufungua matairi ya kati, ambayo yalikuwa yamezibana.

Machibya alilazimika kuvaa glovu na kuanza kazi ya uokoaji huku akisisitiza kuwa hiyo ni moja ya ajali mbaya kutokea ndani ya siku tatu, baada ya Ijumaa iliyopita wanafunzi wawili kufariki dunia papo hapo baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupata ajali eneo la Msati, Tarime.

Wagombea wa vyama vyote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher Kangoye, na Charles Mwera wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walikutana ana kwa ana lakini walishiriki kazi ya uokoaji bila kujali itikadi zao.

Kwa upande wake, Mwera ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, aliwaambia waandishi wa habari kuwa amesikitishwa na tukio hilo, hivyo kuamua kusitisha kampeni kwa siku nzima ya jana.

"Hili ni tukio kubwa lililotupata wananchi wa Tarime kwa mara ya pili ndani ya siku tatu zilizopita...nimesikitishwa na hali hii, hivyo mimi na timu yangu ya kampeni tunaahirisha kampeni zetu hadi kesho (leo)," alisema Mwera.

Ijumaa iliyopita wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari ya Rebu walifariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Msati, wakati wakienda katika Kijiji cha Nyamongo kushiriki michezo huku wengine 64 wakijeruhiwa.

My Take: Kwa mtindo huu wanzilishi wa vurugu ni CCM na jeshi la polisi,hiki ni kielelezo cha dalili za kung'ang'ania madaraka kwa nguvu.Sasa kama Jimbo la Tarime tu,CCM wame-misuse dola namna hii,je kuachia ikulu itakuaje? Hapana ni bora tuanze kupambana nao kwa nguvu ili hata dola itambue kwamba si taasisi au jumuiya mojawapo ya CCM.Haya masuala ni kama ya Robert Mugabe na kibaki wa Kenya.Tanzania hatuko tayari kwa hili
 
Nimejaribu kumpigia john Mnyika lakini simu yake haipokelewi sasa sijui kama kuna mwenye taarifa kwamba waliachiwa ama vipi
 
UKISHAONA Chama cha kisiasa kinaingia kwenye shughuli za :

* Kuandaa vijana wasiosoma kuwa walinzi na wakaa vijiweni vya chama hicho,
* Kina wanachama na viongozi ambao hawakati au hawali tu asilimia 10 bali 90 ya malipo ya waendesha uchaguzi.
* Kinatumia kifo cha mtu kupata umaarufu au nafasi ya ushindi
* Kinawatumia waandishi wa habari, watu wenye akili zao, wengine mvi kichwani kusema uongo na kuandika wasicho na hakika nacho,
* Kinashirikiana na mafisadi kupata fedha za uendeshaji wake,
* Kinatumia redio na televisheni kuudanganya umma kwa mbwembwe za kujifanya BBC ya Afrika-kiatu changu- huku wakijua fika hawana lolote, kwani hawajapanda chochote wanapotaka kuvuna,
* Kinawatumia wanasiasa wenye njaa kali na wachovu kuchafua nafasi ya mwanahalisi wa Tarime kuwa na haki ya kushinda katika jimbo lake,
* Ukiona kina kasuku na kunguru badala ya viongozi

......basi jua moja tu. Chama hicho kimekwisha! Na wala upinzani Tanzania auhitaji ushauri wa Raila Odina bali njia ya kuwaumbua wale wapinzani wanaotumia na CCM kwa bei sawa na bure huku vitabu vikionesha wamelipwa mabilioni!

Unafiki kama huu wa wachungaji-wanasiasa hauhitaji kumuombea mtu akaadhirike akhera bali tunawaombea papa hapa duniani. Na muda sio mrefu watakaosoma Biblia sana, na watakaosoma Quran sana na watakaolilia mizimu yao kwa manafiki kama hawa majibu YATAONEKANA MCHANA KWEUPE!
 
kuwa chini ya serikali inayoongozwa na CCM haina maana ni tawi la CCM. Polisi siyo jumuiya ya Chama. Keshokutwa upinzani wakichukua madaraka, polisi wataendelea kuwepo na kufanya kazi zao kwa kuongozwa na sheria zao siyo itikadi au manifesto ya chama fulani.

Wabebeshe mzigo polisi wao wenyewe usiwasingizie CCM. Kama Polisi ni wabovu ni wabovu kutokana na upolisi wao; kama wako influenced na CCM tatizo siyo CCM bali Polisi.

Mkuu,

Hapa naomba kutofautiana na wewe kidogo.Uliyosema hapo juu ni sawa kwa kiasi fulani lakini unajua CCM yenyewe inaaminikwamba polisi ni jumuiya yao? isingkua hivyo,tusingeshuhudia hujuma zinazofanyika hadi polisi wanafanya kazi ya kununua shahada za CCM ambazo kimsingi kama ni kada wa CCM alifanya hivyo tungeelewa tofauti? But of all the people why police?

Katika Chaguzi nyingi zilizopita tumeshuhudia matumizi mabaya ya dola,na hata huu wa Tarime tunashuhudia police wakitumika,je police wanatumika na CCM kama taasisi gani haswa? Kimsingi ningewatambua kama police kama wangekua neutral.Kwa mantiki hii siwezi kuwatenganisha police na CCM jinsi lilivyo pia kwa TBC1 na CCM
 
Mkuu Huduma na Ben nawapa tano kwanza.Sasa in ishara ya wazi tatz wameanza kuamka hali ya Tarime inadhihirisha kuwa mlipakodi wa kitanzania akielimishwa haki zake za kiraia mapinduzi makubwa yanawezekana.Naomba Mwanakijiji,FMES,Kitila,Rev Kishoka na wengine wa mfano wenu fikra zenu zimeanza kupenya kwa kasi kwenye vichwa vya watz.
Naomba kwa kutumia ushawishi wenu wa hoja,muwashawishi Padre Baptiste Mapunda na Sheikh Gorogosi waanzishe a grand coaliation ya asasi za kiraia wakishirikisha wasomi na wafanyakazi na wanaharakati wengine kitu kinachoitwa Tanzania Electoral Support Network(TESN) kama ilivyokuwa Zimbabwe Archibishop Nkube alishawishi wanaharakati kuanzisha Zimbabwe Electoral Support Network(ZESN) baada ya kuzushiwa skendo na Dictator Mugabe na matokeo yake memeyashuhudia.
Kikianzishwa hicho chombo watz mlioko ughaibuni,mfanye lobbying uko ughaibuni kufinance advertisement kwenye vyombo vya habari kuhusu haki za kiraia za walipakodi wa Kitanzania.Elimu hiyo ya kiraia ikipatikana,itasaidia sana kuwaelemisha watz kupima hoja za wanasiasa kabla hawajafanya maamuzi.
Nina hofu kubwa kuwa Mafia don aitwaye Dawood Ibrahim wa dubai anainyemelea Tanzania kwa kupitia wafanya siasa na wafanyabiashara wa Kitanzania,naomba mungu atuepushe na balaa hilo.
 
polisi wanatekeleza amri ya Tambwe Hiza maana juzi alitangaza kuwa watakamatwa na wamekamatwa kweli!!!!
 
Polisi wawemakini sana,maana kama tarime hawaijui wasiende kichwakichwa hata sikumoja haijawi kutoke katika historia kuwa Mkurya akaogopa polis,
Watu wafikirie mara mbili kabla yakuwatibua Wakurya mziki wao huwa ni mkubwa kinoma hao polisi ni wachache mno.

Mkurya kichwani mwake kunakitu ambayo ikishtuliwa huwa anafanya kweli bila kuogopa wewe ninani.

Na wao sio wajinga Lazima serikari itambuwe kuwa hawa watu ni tofauti na wana siraha za jadi na niwapiganaji wazuri wa mikuki na mishare na pia wanajua kutengeneza mabomu ya petrol ala ala polisi msiwatibue hawa jamaa kwani kagera mnakumbuka hawa watu jinsi wasivyo waoga.

Polisi hawa watu msiwatibue watawamaliza,Nimesikia tu mziki uliotokea jana ni noma.

Mungu ibariki Tarime Mungu ibari Mara.
 
Mkuu Huduma na Ben nawapa tano kwanza.Sasa in ishara ya wazi tatz wameanza kuamka hali ya Tarime inadhihirisha kuwa mlipakodi wa kitanzania akielimishwa haki zake za kiraia mapinduzi makubwa yanawezekana.Naomba Mwanakijiji,FMES,Kitila,Rev Kishoka na wengine wa mfano wenu fikra zenu zimeanza kupenya kwa kasi kwenye vichwa vya watz.
Naomba kwa kutumia ushawishi wenu wa hoja,muwashawishi Padre Baptiste Mapunda na Sheikh Gorogosi waanzishe a grand coaliation ya asasi za kiraia wakishirikisha wasomi na wafanyakazi na wanaharakati wengine kitu kinachoitwa Tanzania Electoral Support Network(TESN) kama ilivyokuwa Zimbabwe Archibishop Nkube alishawishi wanaharakati kuanzisha Zimbabwe Electoral Support Network(ZESN) baada ya kuzushiwa skendo na Dictator Mugabe na matokeo yake memeyashuhudia.
Kikianzishwa hicho chombo watz mlioko ughaibuni,mfanye lobbying uko ughaibuni kufinance advertisement kwenye vyombo vya habari kuhusu haki za kiraia za walipakodi wa Kitanzania.Elimu hiyo ya kiraia ikipatikana,itasaidia sana kuwaelemisha watz kupima hoja za wanasiasa kabla hawajafanya maamuzi.
Nina hofu kubwa kuwa Mafia don aitwaye Dawood Ibrahim wa dubai anainyemelea Tanzania kwa kupitia wafanya siasa na wafanyabiashara wa Kitanzania,naomba mungu atuepushe na balaa hilo.

Mkuu Nsaji,

Heshima kwako zaidi mkuu,umenena maneno makuu sana.

Kwa kweli Mapinduzi makubwa yanahitajika Tanzania,hiyo elimu ya uraia nimelia nayo sana.CCM na serikali yake ni wazi kabisa hawataki kusikia kitu kama elimu ya Uraia.

Pia,suala la katiba mpya.Ni bora ikawa pia ajenda ya mwaka 2009 kwa vyama vyenye muungano katika kambi ya upinzani kushupalia suala lakatiba mpya na mabadiloko makubwa ya kutaka tum huru ya uchaguzi.Zilizopo zinatumika kama mojawapo ya raslimali za CCM kuendelea kuhodhi mamlaka.

Ni lazima Mtanzania akombolewe kutoka katika makucha ya mkoloni mweusi,sisi kumkataa mkoloni mweupe haikumaanisha kumkubali mkoloni mweusi.Now we want our country back.Revolution forever
 
Wandugu,
Kuna wakati huwa najaribu kutafakari haya yanayotokea huo Tarime kweli ni hizo siasa tu za kutaka kutwaa hilo jimbo au kuna jambo la ziada? Kwani kwa ufahamu wangu sijawahi kusikia jimbo lililojulikana katika harakati za uchaguzi baadae kutawaliwa na fujo, vurumai na visa kibao kama Tarime (ukiondoa zanzibar)...Sasa najiuliza ni huo ubunge tu huko Tarime au kuna kitu kingine kinachopelekea hizo vurugu hadi watu kuumizana na wengine kuwana na uhalibifu wa mali?
 
umesahau vioja vya ccm kule temeke? wakati mrema akigombea jimbo lile baada ya kihiyo kutimuliwa na mahakama, ccm ikongozwa na ditopile akina mkapa na vikaragosi wao wailifanya temeke isitawalike, laikni wakaangukia pua!
 
bongo kama kenya!

Bora hata Kenya walipo dhurumiwa walisimama kidete mpaka kikaeleweka, wasi wasi wangu ni kwamba wabongo tunatishika haraka na hii ndo siraha wameitumia hawa mafisadi myaka yote, hata kwa kuttishia mikanda ya vita vya Rwanda kwamba tukichagua wapinzani ndo tutakuwa hivo, Sema hapa naona wamepanda daraja sasa kuweka siraha za moto! richa ya vitisho vya maneno!

Mungu tu atunusuru mikononi mwa fisadi hawa wasio thamini utu wa watu zaidi ya madaraka! na hakika huu ni mfumo mpya wa ukoloni!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

POLISI WANATUMIA VITISHO, UKANDAMIZAJI KUISAIDIA CCM TARIME.
Dar es Salaam, Oktoba 7, 2008

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani vikali matukio ya hivi karibuni ya Jeshi la Polisi kutumia mabavu, vitisho na vitendo vya ukandamizaji ili kuwatisha wananchi wa Jimbo la Tarime kwa lengo la kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM) kushinda katika Uchaguzi Mdogo wa Mbunge wa Tarime na Diwani wa Kata ya Tarime Mjini. Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo wiki tatu zilizopita, mamia ya wananchi, hasa vijana, wa maeneo mbali mbali ya Jimbo la Tarime wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka mbali mbali ya kubambikiza. Licha ya kwamba sheria za nchi yetu zinaruhusu mahakama kutoa dhamana kwa wale wanaotuhumiwa kwa makosa hayo, karibu wnanachi wote waliokamatwa wakati huu wa kampeni za uchaguzi wamenyimwa dhamana kwa kisingizio kwamba wanahatarisha usalama wakati huu wa kampeni za uchaguzi mdogo.

Wakati wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakiwa wanakamatwa na kunyimwa haki yao ya kupata dhamana, wanachama wa CCM pamoja na makada wao wamekuwa hawachukuliwi hatua zozote za kisheria licha ya kufanya vitendo vya uvunjaji sheria wazi wazi. Kwa mfano, wagombea wa CCM pamoja na wagombea pandikizi wa CCM wa DP na NCCR-Mageuzi na/au wapambe wao wa karibu wametoa tuhuma za uongo na uzushi hadharani kwamba CHADEMA ndio inayohusika na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime Marehemu Chacha Zakayo Wangwe hakuna hata mmoja wao aliyekamatwa au hata kutakiwa kutoa maelezo polisi pamoja na kwamba tuhuma hizo za uzushi na uongo ni kosa la jinai chini ya sheria za nchi yetu.

Mfano wa pili unahusu tukio la kupigwa mawe kwa gari la CHADEMA aina ya FUSO likiwa limeegeshwa usiku na wanachama wa CCM. Wahalifu hao walipokamatwa na walinzi wa CHADEMA na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Wilaya waliachiliwa huru pamoja na kukiri kuwa walitumwa na kiongozi mmoja wa CCM kufanya uhalifu huo. Kiongozi wa CCM aliyetuhumiwa kuwatuma wahalifu hao naye hajakamatwa wala kuitwa kwa mahojiano na Jeshi la Polisi. Aidha wanachama wengine wawili wa CCM ambao walitajwa kuhusika na tukio hilo mpaka leo hawajakamatwa na kufikishwa Polisi huku Polisi wakisema kuwa wanawatafuta ilihali vijana hao wakionekana mitaani Tarime wakiendelea na kampeni za CCM.

Matumizi ya mabavu ya kipolisi kwa ajili ya kuibeba CCM hayajaishia hapo. Jana Jumatatu tarehe 6 Oktoba 2008 wagombea ubunge na udiwani wa CHADEMA Bw. Charles Mwera na John Heche Suguta, Mkurugenzi wa Vijana Makao Makuu John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Dk. Ben Kapwani pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA wilayani Tarime walikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kisingizio cha kufanya mkutano usiokuwa na kibali. Ikumbukwe kwamba Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 na Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge na wa Rais za mwaka 2005 hazizungumzii chochote juu ya vyama vya siasa kuomba vibali vya kufanya mikutano yao wakati wa kampeni za uchaguzi. Kifungu cha 51(5) cha Sheria ya Uchaguzi na kanuni ya 36(4) zinampa Msimamizi wa Uchaguzi jukumu la kuwapatia Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Polisi wa Wilaya nakala ya ratiba ya mikutano yote ya kampeni za uchaguzi. Sheria hizo zinasema wazi wazi kwamba nakala ya ratiba hiyo itahesabika kuwa ni taarifa ya mikutano ya hadhara ya kisiasa kwa madhumuni ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na Sheria ya Jeshi la Polisi Sura ya 322 ya Sheria za nchi yetu. Kwa maana hiyo, CHADEMA haikuwa na wajibu wowote kisheria wa kuomba kibali cha mkutano wake wa kampeni kwa Jeshi la Polisi! Hivyo, kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata wagombea na viongozi wa CHADEMA sio halali na kina tafisiri moja tu: kujaribu kuibeba CCM katika uchaguzi huo mdogo kwa kuwatisha wagombea, viongozi, wanachama na wapiga kura wanaoiunga mkono CHADEMA.

Inaelekea lengo la wazi la vitendo hivi ni kwanza kupunguza idadi ya wapiga kura ambao wanahisiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA na, pili, kuwatisha wananchi na wapiga kura wengine ili siku ya uchaguzi wasijitokeze kupiga kura kwa hofu ya kukamatwa na polisi na kufunguliwa kesi za uongo na za kubambikizwa. Walengwa wakubwa wa njama hizi sio wanachama na washabiki wa kawaida tu wa CHADEMA bali pia hata viongozi wao wa kuchaguliwa. Kwa mfano, hadi sasa hivi Diwani wa Kata ya Bumera (CHADEMA) na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mh. Tengera Marwa anashikiliwa na Polisi kwa kesi ya kubambikizwa ya mauaji. Aidha, CHADEMA ina taarifa za kikao cha ndani cha CCM ambacho kilihudhuriwa na Kamanda ya Kikosi Maalumu kilichopelekwa Tarime, Kamanda Tossi ambapo iliamuliwa kwamba madiwani na viongozi wa Wilaya wa CHADEMA ambao Kuwepo kwao katika kampeni za uchaguzi kunaiumiza CCM wakamatwe na kufunguliwa kesi za mauaji au kesi nyingine kubwa na zisizoruhusu dhamana kwa watuhumiwa. Katika kutekeleza mkakati huo tayari Diwani wa Kata ya Matongo (CHADEMA) Mh. Machage Machage, Mh. Tecla Johannes Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Nyandoto na mume wa Mh. Mary Nygabona wameshaamriwa wafike Kituo cha Polisi cha Tarime Mjini kwa ajili ya kuhojiwa.

CHADEMA inawakumbusha wananchi wa Tanzania kwamba vitendo vya kutumia mabavu, vitisho na ukandamizaji vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa niaba ya CCM sio jambo geni katika siasa za Tarime. Itakumbukwa kwamba kabla na wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, vitendo vya aina hii vilishamiri sana katika Jimbo hilo na kusababisha wananchi wengi kujeruhiwa na wengine kuuawa. Haya yote yalithibitishwa na Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama baada ya marehemu Chacha Zakayo Wangwe kuyasema bungeni na kuitwa mwongo na wabunge wa CCM na kulazimishwa na Spika wa Bunge Samwel Sitta kuthibitisha kauli yake au kuifuta. Kama inavyofahamika, marehemu Chacha Wangwe yeye mwenyewe aliandamwa sana na Jeshi la Polisi kwa kufunguliwa kesi nyingi za uzushi na za kubambikiza ili kuibeba CCM Tarime. Hata hivyo, itakumbukwa vile vile kwamba licha ya vitendo hivyo vya matumizi ya mabavu, mauaji, vitisho na ukandamizaji wakati wa Uchaguzi wa 2005, CHADEMA iliipa CCM kipigo kikali katika uchaguzi baada ya mgombea wake kumpita mgombea wa CCM kwa kura karibu elfu thelathini na CHADEMA kushinda udiwani katika Kata 12 kati ya ishirini za Halmashauri ya Wilaya ya Tarime! Vivyo hivyo katika uchaguzi huu mdogo wa Ubunge na udiwani, CHADEMA kinaamini kwamba kitapata ushindi mkubwa na kutetea kiti chake cha Ubunge wa Tarime na Udiwani wa Kata ya Tarime Mjini.

Mwisho CHADEMA inawaasa waandishi wa habari, wawakilishi wa mashirika na taasisi zisizokuwa za kiserikali, wawakilishi wa nchi na mashirika ya wafadhili kuibana Serikali ya CCM ikomeshe vitendo vya matumizi ya mabavu ya kijeshi, vitisho na ukandamizi wa wananchi wa Tarime na kuhakikisha uchaguzi huo mdogo unakuwa huru na wa haki. Aidha CHADEMA inalitaka Jeshi la Polisi liache mara moja vitendo vya matumizi ya mabavu ya kijeshi, vitisho na ukandamizaji dhidi ya viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA. Jeshi la Polisi linatakiwa kuheshimu sheria za Nchi ili na wajibu wao wa kuhakikisha uchaguzi mdogo wa Tarime unaendeshwa kwa amani na wananchi wa Tarime wanaachwa kuamua wenyewe ni nani wanamtaka kama kiongozi wao.

Tundu Lissu
KURUGENZI YA SHERIA, KATIBA NA HAKI ZA BINADAMU
CHADEMA MAKAO MAKUU
 
Mwanakijiji,

Ushakuwa Public Relation Officer wa Chadema?
 
CCM wanapenda rafu ata sijui why,cha msingi ni kuwanyima kura as wanapenda kuforce king.
Waacheni watu wa TARIME wamchague mtetezi wao kwa uhuru na amani eeeeeh.
Mungu twaomba uwaangazie watu wa TARIME wachagua mtu atakaewajari na kujari maslai ya nchi kwa ujumla.Amen
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom