Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana aliwasili Tarime na kulakiwa na mamia ya mashabiki, wanachama na wananchi wa wilaya hiyo.
Kuwasili kwa Mbowe wilayani hapa akija kuwaongezea nguvu wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho, kulibadili kabisa mwenendo wa mambo katika maeneo mbalimbali aliyopita akiwa ndani ya gari na hata alipolazimishwa na wafuasi wake kuteremka chini na kutembea nao kwa miguu huku akisimama katika eneo moja baada ya jingine kuwasalimia wapiga kura wa jimbo hilo.
Msafara wa kumlaki Mbowe aliyewasili majira ya saa 8:00 mchana, ulioongozwa na wapanda pikipiki wanaokadiriwa kufikia 200, ulianzia katika Kijiji cha Komaswa, kilichopo umbali wa kilomita zipatazo 23 kutoka Tarime mjini.

Mara baada ya kupokewa katika kijiji hicho, Mbowe aliyekuwa amevalia kombati alilazimika kusimama katika Kijiji cha kwanza cha Mika kilichopo wilayani Rorya baada ya kuombwa afanye hivyo na wafuasi wake kwa dakika zisizozidi tano.

Akizungumza katika salamu zake hizo za kwanza kabisa, Mbowe alisema amekwenda Tarime kwa nia moja ya kusambaratisha kile alichokiita mtandao wa ufisadi ambao umekuwa ukilitafuna taifa kwa kipindi kirefu hata kuwanyima haki wananchi wenye kipato cha chini.

Katika hali isiyotarajiwa, polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kuufuatilia msafara huo wa Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA uliokuwa ukivuta makumi ya watu kila ulipokuwa ukipita wakitumia magari yaliyokuwa na namba za usajili za nchi jirani ya Kenya.

Kwa mara ya kwanza gari lililokuwa na polisi liliwasili katika eneo la Mika alipokuwa akihutubia mwanasiasa huyo likiwa na namba mbili tofauti; KAD 493 E na 493 KAU E.
Mshindo wa ukubwa wa msafara uliofika kumpokea Mbowe ulizidi kuwa mkubwa baada ya kuwasilia katika eneo la Buhemba ambako kina mama walionekana wakiacha shughuli zao na kujumuika na wana-CHADEMA kumlaki kiongozi wao mkuu huku wakionyesha alama ya vidole ya ‘V’, inayotumiwa na chama hicho kuonyesha ushindi.

Hali hiyo ya watu wengi kutaka kumlaki, ilisababisha alazimike kusimama katika eneo hilo na kuwahutubia wananchi waliokuwa na hamu ya kumsikiliza huku wakipunga bendera za chama hicho na matawi ya miti.

Akihutubia hapo, alianza kwa kusema, ‘‘CCM na Jeshi la Polisi wanapaswa kutambua kuwa, matumizi ya nguvu za kupita kiasi, risasi na mabomu ya machozi haviwezi kufua dafu mbele ya nguvu ya umma.

“Kamanda wenu nimekuja kukiambia Chama Cha Mapinduzi na Jeshi la Polisi kwamba, mabomu, risasi na nguvu zao wanazotumia mbele ya umma wa wananchi wa Tarime haziwezi kusaidia kwa vile nguvu zao haziwezi kupingana na nguvu ya umma,” alisema Mbowe na kupokewa na mshindo wa makofi na vigelegele.
Alisema pamoja na kwamba, polisi wamekuwa wakiwapiga kama mbinu ya kuwatisha, CCM haiwezi kamwe kushinda ubunge wa Tarime katika uchaguzi ulio huru na wa haki.
Akizungumza kwa sauti ya juu, Mbowe alisema ni jambo la kusikitisha kwamba, tangu kampeni zilipozinduliwa Septemba 14 mwaka huu, Jeshi la Polisi limekuwa sehemu muhimu ya kampeni za CCM.

“Nawaambia ndugu zangu haki ya mwana-Tarime kamwe haiwezi kupotea, namwambia Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) na mgombea wake, haki ya wananchi wa Tarime wenye mapenzi mema na CHADEMA hawatakubali kuona ikipotea,” alisema Mbowe.

Baada ya kumalizia kuhutubia eneo hilo, msafara wake ulianza kuelekea katikati ya mji wa Tarime kupitia barabara za Nyerere na Nyamwaga hadi kwenye viwanja vya Mennonite, ambako pia kulikuwa na mamia ya wananchi, tofauti kabisa na ilivyokuwa ikifikiriwa awali.
Hali ilizidi kubadilika baada ya kukamata barabara ya Nyamwaga, ambako watu walioona msafara huo, waliacha kazi walizokuwa wanafanya na kufuatilia.

Kitendo hicho kilisababisha biashara zilizokuwa kandokando ya barabara hiyo kufungwa kwa muda kutokana na utitiri wa watu waliofurika kuelekea kwenye viwanja vya Mennonite.
Mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo, Mbowe aliwaomba wananchi wote kukaa kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Chacha Wangwe, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari katika eneo la Pandambili nje kidogo ya mji wa Dodoma, Julai 29, mwaka huu.Alisema lengo lake kubwa la kufika mjini hapa ni kuendeleza mapambano ya kuhakikisha kwamba jiimbo hilo linabaki mikononi mwa CHADEMA kama njia pekee ya kumuenzi marehemu Wangwe.

“Napenda kuwaambia kwamba leo (jana) nimekuja hapa kwa kazi moja tu ndugu zangu... nayo ni kuendeleza mapambano ya kuhakikisha kwamba tunakomboa jimbo letu na kuendelea kuitawala Halmashauri ya Wilaya ya Tarime. Kufanya hivi ndiyo njia pekee ya kumuenzi marehemu Wangwe,” alisema Mbowe.
Mbali ya hilo, Mbowe alieleza kusikitishwa na kukerwa na tuhuma zinazoelekezwa dhidi yake yeye na chama chake kwamba, alishiriki kusababisha kifo cha marehemu Wangwe.
“Eti CCM wanasema mimi na chama chetu tumemuua marehemu Wangwe. Napenda kuwahakikishia kwamba hatukuhusika na suala hili na inawezekana kwamba hao wanaosema, ndio waliohusika,” alisema Mbowe.

Alisema kutokana na chuki hizo za kupandikizwa, Tarime itaendelea kudumu na haki ya msingi itatolewa na Mungu kama kweli alihusika na kifo hicho, na kwamba huo ni mkakati wa vyombo vya dola kutaka kudhoofisha nguvu za chama chake pamoja na wabunge wake ambao wamekuwa mwiba mkali kwao.

“Nawahakikishia kwamba mimi siogopi kitu chochote. Hawa hawawezi kunizuia jambo lolote lile, mimi nalindwa na Mungu na kama CCM hawalijui hili, naomba walitambue kuanzia sasa,” alisema.
Alisema kwamba yuko tayari kufia Tarime ili kuona haki ya kila mtu inapatikana, kwani hii ndiyo kazi aliyofanya marehemu hadi wakati mauti yakimfika.

“Mimi nasema jamani niko tayati kufia Tarime kwa ajili ya kuona haki za wananchi wote wa hapa zinapatikana baada ya mateso makubwa mliyoyapata kutoka CCM kwa miaka yote iliyopita... nawauliza mko tayari kurudia makosa?” alihoji Mbowe.

Mbali ya hilo, Mbowe alitumia fursa hiyo kutangaza kwamba, kuanzia kesho anakusudia kuanza kufanya kampeni katika jimbo hilo akimnadi mgombea wake wa ubunge, Charles Mwera na yule wa udiwani, John Suguta, akitumia helikopta kama ilivyo kawaida yake.

Mytake:
Neno eti lina maana gani?pesa ya Helikopta ni nani analipa??Lafu sula la kutumia sympathy ili watu wamhurumie nadhani ni kukosa mwelekeo ,matumizi ya neno ndugu inaonesha jinsia anvyopunguza gap la ukabila ambalo limetawala watu wake wa karibu.Unaweza kuta helikopta ni mtaji wa Mbowe na anatumia Ruzuku ya chama kujiingizia kioato..Kama chama kinauzika Helikopta ya nini?walitumia helikopta kiteto na wakashindwa..

lets wait and see

Duuuu???? kaaazi kweli kweli,
Mkuu Gembe kama hiyo ndiyo your take kutoka katika habari hiyo kweli naamini bado tuna safari ndefu sana kujikwamua!

Anyway, Kudos Chadema na hongera Mbowe kwa ushujaa ulio uonyesha kukanyaga Tarime na kukatilia mbali tantaralila zote kwamba huwezi kanayaga tarime, mara ukifika utapigwa, mbona kinyume chake umepokelewa kama shujaa?? Mungu awatie shime wote wapambanaji! inshalah tutashinda.
 
Sasa sijui watu kama akina Mtanzania waliotaka kupotosha tangu mwanzo sasa watasemaje?
 
katika hali ya kushangaza yusuf makamba aliingia mitini wakati mabalozi wanipotembelea Tarime kujionea kampeni za uchaguzi zinavyondeshwa...
swali: je tatizo ni lile lile la kutokujua kingereza au kulikuwa na nini mpaka awakimbie? nisaidieni...
 
Ochu,
Tatizo haliwezi kuwa kiingereza. Balozi alisema amelazimika kwenda Tarime baada ya kila siku kuwa anasoma habari zinazoonyesha kuwa mambo huko yanakwenda sivyo. Makamba ni mhusika mkuu wa hayo yanayotokea huko hivyo alichokimbia ni maswali ya balozi huyo. Usisahau, viongozi wetu ni waoga sana wanapokuwa na hawa wakuu toka nchi tunazoita wahisani.
 
Tatizo sio kiingereza, kwani mabalozi wengine suala la kiswahili kwao sio ishu. Makamba kuwakimbia jamaa hawa ni ile ya hali ya kuona niitawaeleza nini 'wafadhiri' hawa wanielewa hasa kwa kuwa hawa hawaitegemei Habari Leo kutoa habari. makamba na chama chake wamekuwa ndo watu muhimu sana katika kuleta fujo hapa tarime. Mbaya zaidi hata wasaidizi wakuu wa rais, mawaziri wamekuwa ni mashabiki na wacochezi wakubwa wa vurugu hizi.

UELEWA WA MTANZANIA HAUWEZI KUPIMWA KWA KUJUA LUGHA YA KIGENI
 
katika hali ya kushangaza yusuf makamba aliingia mitini wakati mabalozi wanipotembelea Tarime kujionea kampeni za uchaguzi zinavyondeshwa...
swali: je tatizo ni lile lile la kutokujua kingereza au kulikuwa na nini mpaka awakimbie? nisaidieni...

Wakati mwingine Polisi kumtambua mhalifu haisumbui, mhalifu akishamuona polisi naye akijui kishafanya matukio mengi ya uhalifu, mhalifu huyu akimuona polisi lazima akimbie. Hivyo usishangae alijihisi ni mhalifu mbele yao.
 
Tatizo sio kiingereza, kwani mabalozi wengine suala la kiswahili kwao sio ishu. Makamba kuwakimbia jamaa hawa ni ile ya hali ya kuona niitawaeleza nini 'wafadhiri' hawa wanielewa hasa kwa kuwa hawa hawaitegemei Habari Leo kutoa habari. makamba na chama chake wamekuwa ndo watu muhimu sana katika kuleta fujo hapa tarime. Mbaya zaidi hata wasaidizi wakuu wa rais, mawaziri wamekuwa ni mashabiki na wacochezi wakubwa wa vurugu hizi.

UELEWA WA MTANZANIA HAUWEZI KUPIMWA KWA KUJUA LUGHA YA KIGENI

Mkuu nadhani ni vyote, Kiingereza na kutojua atajibu nini.....viongozi wetu bwana! nakumbuka Dr Juma Ngasongwa kuna siku alikutana na mabalozi wa EU wakati yeye ni waziri wa biashara na viwanda, aliulizwa nini kifanyike kuongeza uzalishaji...alijibu nadhani tukipata vijenereta vitasidia sana kutatua shida ya umeme vijijini...I just turned the TV to channel 5 kuendelea na zecomedy enzi hizo. Makamba ni shida zaidi maana hana ufahamu na lugha ni tatizo, sasa angeongea nini jamani?

Ushi
 
katika hali ya kushangaza yusuf makamba aliingia mitini wakati mabalozi wanipotembelea Tarime kujionea kampeni za uchaguzi zinavyondeshwa...
swali: je tatizo ni lile lile la kutokujua kingereza au kulikuwa na nini mpaka awakimbie? nisaidieni...

Kwanini isiwe aliwakimbia kwasababu mabalozi hawajui Kiswahili? Hatua ya kwanza ya kujikomboa kikweli kweli ni kuanza kuthamini vilivyo vyako.
 
katika hali ya kushangaza yusuf makamba aliingia mitini wakati mabalozi wanipotembelea tarime kujionea kampeni za uchaguzi zinavyondeshwa...
Swali: Je tatizo ni lile lile la kutokujua kingereza au kulikuwa na nini mpaka awakimbie? Nisaidieni...

tatizo ni kwamba makamba kiingereza hakipandi ni lini umeshasikia anaongea na mgeni wa nje na lini amesafiri nje labda alipokuwa anaumwa, tofauti kabisa na mangula.
 
Kwanini isiwe aliwakimbia kwasababu mabalozi hawajui Kiswahili? Hatua ya kwanza ya kujikomboa kikweli kweli ni kuanza kuthamini vilivyo vyako.

tupewe sababu ya kukimbia basi ili tuache speculations...
 
Duh hii kali mimi naona cha kwanza Lugha cha pili ni yeye anahusika moja kwa moja na vulugu zile.
 
Kwanini isiwe aliwakimbia kwasababu mabalozi hawajui Kiswahili? Hatua ya kwanza ya kujikomboa kikweli kweli ni kuanza kuthamini vilivyo vyako.

Pamoja ya kwamba kiswahili ndiyo lugha yetu na inapasa tujivunie lakini kwa mtu ambaye anataka public office kujua lugha za kigeni siyo tu ni muhimu bali ni lazima walau kiingereza.
Hao mabalozi labda kwavile wako Tanzania muda mrefu kidogo wanaweza wakawa wanajuajua kiswahili.Wale ambao hawajamaliza hata mwezi?Lakini ndiyo tuseme Makamba hatoweza kusafiri kwenda nje ya nchi bila ya kuwa na mkalimani?Kuna vyama marafiki huwa wanaalikana,Makamba hawezi kwenda kuwapokea mpaka awe na Mkalimani?
Kisa najivunia kiswahili changu.Hayo mambo waachieni warusi na wachina,hayo ni mataifa makubwa ati lakini hivi vinchi vyetu ombaomba lazima tukazane kuzijua hizi lugha za mnaowaita wafadhili!
 
tatizo ni kwamba makamba kiingereza hakipandi ni lini umeshasikia anaongea na mgeni wa nje na lini amesafiri nje labda alipokuwa anaumwa, tofauti kabisa na mangula.

Kama kiongozi wa chama nadhani kujua kiingereza si ishu angeweza kuongea hata kupitia mkalimani.Na pia sitaki kuamini kuwa hajui kimombo ukizingatia umri alio nao na kama alipitia shule ze misheni kama anavyosema mwenyewe.
 
Hii kali kumbe umri ulikienda na kimombo kina panda? will try it with my grandpa!!
 
Pamoja ya kwamba kiswahili ndiyo lugha yetu na inapasa tujivunie lakini kwa mtu ambaye anataka public office kujua lugha za kigeni siyo tu ni muhimu bali ni lazima walau kiingereza.
Hao mabalozi labda kwavile wako Tanzania muda mrefu kidogo wanaweza wakawa wanajuajua kiswahili.Wale ambao hawajamaliza hata mwezi?Lakini ndiyo tuseme Makamba hatoweza kusafiri kwenda nje ya nchi bila ya kuwa na mkalimani?Kuna vyama marafiki huwa wanaalikana,Makamba hawezi kwenda kuwapokea mpaka awe na Mkalimani?
Kisa najivunia kiswahili changu.Hayo mambo waachieni warusi na wachina,hayo ni mataifa makubwa ati lakini hivi vinchi vyetu ombaomba lazima tukazane kuzijua hizi lugha za mnaowaita wafadhili!

Unajuaje hata hao mabalozi wote wanajua Kiingereza? Requirement mojawapo kwa nchi mbalimbali kwa mabalozi wanaokuja Tanzania ni pamoja na kujua Kiswahili ingawaje sio lazima sana.

Point hapo ilikuwa mna uhakika gani kwamba hao mabalozi hawajui Kiswahili? Pia kama
Makamba hajui Kiingereza angeweza kutumia mkalimani bila tatizo lolote.

Tatizo la TZ ni uwezo wa viongozi wetu kuongoza na wala sio tatizo la kushindwa kuongea Kiingereza.

Utajivunia Kiswahili wakati unakimbilia kiingereza kabla hata ya kujua huyo wa upande wa pili anajua kiswahili au la?

Ni muhimu sana kujua lugha lakini sio kwa maana mnayotaka kuionyesha kwenye mjadala huu.
 
Jamani, wakati Makamba anamjibu mgombea wa Chadema aliyetaka wafanye mdahalo kwa Kiingereza alisema yeye si maimuna? Sa mbona mnamzushia babu wa watu kuwa Kiingereza akipandi?
Mwenyewe alishasema kuwa asingeweza kukutna nao kwa sababu yuko busy na kampeni na ratiba yake haikuonyesha kuwa anakutana na mabalozi siku hiyo!!!!!
 
Yes, the problem is not English but is "what to explain to them once they will need him to comment how the campaign is going?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom