MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, jana aliwasili Tarime na kulakiwa na mamia ya mashabiki, wanachama na wananchi wa wilaya hiyo.
Kuwasili kwa Mbowe wilayani hapa akija kuwaongezea nguvu wagombea wa ubunge na udiwani wa chama hicho, kulibadili kabisa mwenendo wa mambo katika maeneo mbalimbali aliyopita akiwa ndani ya gari na hata alipolazimishwa na wafuasi wake kuteremka chini na kutembea nao kwa miguu huku akisimama katika eneo moja baada ya jingine kuwasalimia wapiga kura wa jimbo hilo.
Msafara wa kumlaki Mbowe aliyewasili majira ya saa 8:00 mchana, ulioongozwa na wapanda pikipiki wanaokadiriwa kufikia 200, ulianzia katika Kijiji cha Komaswa, kilichopo umbali wa kilomita zipatazo 23 kutoka Tarime mjini.
Mara baada ya kupokewa katika kijiji hicho, Mbowe aliyekuwa amevalia kombati alilazimika kusimama katika Kijiji cha kwanza cha Mika kilichopo wilayani Rorya baada ya kuombwa afanye hivyo na wafuasi wake kwa dakika zisizozidi tano.
Akizungumza katika salamu zake hizo za kwanza kabisa, Mbowe alisema amekwenda Tarime kwa nia moja ya kusambaratisha kile alichokiita mtandao wa ufisadi ambao umekuwa ukilitafuna taifa kwa kipindi kirefu hata kuwanyima haki wananchi wenye kipato cha chini.
Katika hali isiyotarajiwa, polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kuufuatilia msafara huo wa Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA uliokuwa ukivuta makumi ya watu kila ulipokuwa ukipita wakitumia magari yaliyokuwa na namba za usajili za nchi jirani ya Kenya.
Kwa mara ya kwanza gari lililokuwa na polisi liliwasili katika eneo la Mika alipokuwa akihutubia mwanasiasa huyo likiwa na namba mbili tofauti; KAD 493 E na 493 KAU E.
Mshindo wa ukubwa wa msafara uliofika kumpokea Mbowe ulizidi kuwa mkubwa baada ya kuwasilia katika eneo la Buhemba ambako kina mama walionekana wakiacha shughuli zao na kujumuika na wana-CHADEMA kumlaki kiongozi wao mkuu huku wakionyesha alama ya vidole ya V, inayotumiwa na chama hicho kuonyesha ushindi.
Hali hiyo ya watu wengi kutaka kumlaki, ilisababisha alazimike kusimama katika eneo hilo na kuwahutubia wananchi waliokuwa na hamu ya kumsikiliza huku wakipunga bendera za chama hicho na matawi ya miti.
Akihutubia hapo, alianza kwa kusema, CCM na Jeshi la Polisi wanapaswa kutambua kuwa, matumizi ya nguvu za kupita kiasi, risasi na mabomu ya machozi haviwezi kufua dafu mbele ya nguvu ya umma.
Kamanda wenu nimekuja kukiambia Chama Cha Mapinduzi na Jeshi la Polisi kwamba, mabomu, risasi na nguvu zao wanazotumia mbele ya umma wa wananchi wa Tarime haziwezi kusaidia kwa vile nguvu zao haziwezi kupingana na nguvu ya umma, alisema Mbowe na kupokewa na mshindo wa makofi na vigelegele.
Alisema pamoja na kwamba, polisi wamekuwa wakiwapiga kama mbinu ya kuwatisha, CCM haiwezi kamwe kushinda ubunge wa Tarime katika uchaguzi ulio huru na wa haki.
Akizungumza kwa sauti ya juu, Mbowe alisema ni jambo la kusikitisha kwamba, tangu kampeni zilipozinduliwa Septemba 14 mwaka huu, Jeshi la Polisi limekuwa sehemu muhimu ya kampeni za CCM.
Nawaambia ndugu zangu haki ya mwana-Tarime kamwe haiwezi kupotea, namwambia Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) na mgombea wake, haki ya wananchi wa Tarime wenye mapenzi mema na CHADEMA hawatakubali kuona ikipotea, alisema Mbowe.
Baada ya kumalizia kuhutubia eneo hilo, msafara wake ulianza kuelekea katikati ya mji wa Tarime kupitia barabara za Nyerere na Nyamwaga hadi kwenye viwanja vya Mennonite, ambako pia kulikuwa na mamia ya wananchi, tofauti kabisa na ilivyokuwa ikifikiriwa awali.
Hali ilizidi kubadilika baada ya kukamata barabara ya Nyamwaga, ambako watu walioona msafara huo, waliacha kazi walizokuwa wanafanya na kufuatilia.
Kitendo hicho kilisababisha biashara zilizokuwa kandokando ya barabara hiyo kufungwa kwa muda kutokana na utitiri wa watu waliofurika kuelekea kwenye viwanja vya Mennonite.
Mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo, Mbowe aliwaomba wananchi wote kukaa kimya kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Chacha Wangwe, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari katika eneo la Pandambili nje kidogo ya mji wa Dodoma, Julai 29, mwaka huu.Alisema lengo lake kubwa la kufika mjini hapa ni kuendeleza mapambano ya kuhakikisha kwamba jiimbo hilo linabaki mikononi mwa CHADEMA kama njia pekee ya kumuenzi marehemu Wangwe.
Napenda kuwaambia kwamba leo (jana) nimekuja hapa kwa kazi moja tu ndugu zangu... nayo ni kuendeleza mapambano ya kuhakikisha kwamba tunakomboa jimbo letu na kuendelea kuitawala Halmashauri ya Wilaya ya Tarime. Kufanya hivi ndiyo njia pekee ya kumuenzi marehemu Wangwe, alisema Mbowe.
Mbali ya hilo, Mbowe alieleza kusikitishwa na kukerwa na tuhuma zinazoelekezwa dhidi yake yeye na chama chake kwamba, alishiriki kusababisha kifo cha marehemu Wangwe.
Eti CCM wanasema mimi na chama chetu tumemuua marehemu Wangwe. Napenda kuwahakikishia kwamba hatukuhusika na suala hili na inawezekana kwamba hao wanaosema, ndio waliohusika, alisema Mbowe.
Alisema kutokana na chuki hizo za kupandikizwa, Tarime itaendelea kudumu na haki ya msingi itatolewa na Mungu kama kweli alihusika na kifo hicho, na kwamba huo ni mkakati wa vyombo vya dola kutaka kudhoofisha nguvu za chama chake pamoja na wabunge wake ambao wamekuwa mwiba mkali kwao.
Nawahakikishia kwamba mimi siogopi kitu chochote. Hawa hawawezi kunizuia jambo lolote lile, mimi nalindwa na Mungu na kama CCM hawalijui hili, naomba walitambue kuanzia sasa, alisema.
Alisema kwamba yuko tayari kufia Tarime ili kuona haki ya kila mtu inapatikana, kwani hii ndiyo kazi aliyofanya marehemu hadi wakati mauti yakimfika.
Mimi nasema jamani niko tayati kufia Tarime kwa ajili ya kuona haki za wananchi wote wa hapa zinapatikana baada ya mateso makubwa mliyoyapata kutoka CCM kwa miaka yote iliyopita... nawauliza mko tayari kurudia makosa? alihoji Mbowe.
Mbali ya hilo, Mbowe alitumia fursa hiyo kutangaza kwamba, kuanzia kesho anakusudia kuanza kufanya kampeni katika jimbo hilo akimnadi mgombea wake wa ubunge, Charles Mwera na yule wa udiwani, John Suguta, akitumia helikopta kama ilivyo kawaida yake.
Mytake:
Neno eti lina maana gani?pesa ya Helikopta ni nani analipa??Lafu sula la kutumia sympathy ili watu wamhurumie nadhani ni kukosa mwelekeo ,matumizi ya neno ndugu inaonesha jinsia anvyopunguza gap la ukabila ambalo limetawala watu wake wa karibu.Unaweza kuta helikopta ni mtaji wa Mbowe na anatumia Ruzuku ya chama kujiingizia kioato..Kama chama kinauzika Helikopta ya nini?walitumia helikopta kiteto na wakashindwa..
lets wait and see
Duuuu???? kaaazi kweli kweli,
Mkuu Gembe kama hiyo ndiyo your take kutoka katika habari hiyo kweli naamini bado tuna safari ndefu sana kujikwamua!
Anyway, Kudos Chadema na hongera Mbowe kwa ushujaa ulio uonyesha kukanyaga Tarime na kukatilia mbali tantaralila zote kwamba huwezi kanayaga tarime, mara ukifika utapigwa, mbona kinyume chake umepokelewa kama shujaa?? Mungu awatie shime wote wapambanaji! inshalah tutashinda.