Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mkuu usinivunje mbavu, Sasa sijui hata kuandaa ajenda za vikao na mabalozi au wafadhili wa sera za chama chake anaaandaa vipi.Ndiyo maana Tanzania inaburuzwa na nchi kama Kenya na Rwanda kwa sababu ya kuongozwa na Makamba Types
 
hawana njia ila ni serikali ya mseto tu ndio njia pekee ya kutokea, kwa sababu wazungu wameshamuonya muungwana kuwa this time hawataruhusu watu wa ccm ku-cross kutoka bara na kwenda kupiga kura huko kama zamani.

tayari watu wako huko mkuu! Ila tatizo this time ni ugumu wa maisha kule zenj, jamaa wameunganishwa ktk matatizo hivyo kura zitakuwa za uzanzibar zaidi kuliko cuf na ccm, ni uwanja mpya kwa wanasiasa wa zanzibar, wanalazimika kuhubiri u zanzibar wao na hatima ya wananchi wao, atakyecheza vizuri karata hiyo ataingia ikulu hata kama ni kwa mseto.

Nakubaliana kuwa muungwana ana kazi pevu zanzibar kuliko hata aliyokumbana nayo mkapa au hata ile aliyoiacha mwinyi, mkuu mfuatilie vizuri shamhuna na sasa hata ile vita dhidi khatibu inaashiria sana jambo hili la 2010 kipaumbele ni zanzibar bila uoga wala nidhamu tukufu kwa muungano.

Niwakumbushe tu wana jf kuwa ally abeid karume alishabashiri hili wakati anatangaza rasmi kuwa 2010 yumo, sasa kama ni zanzibar au muungano hiyo itategemea siasa zetu kuelekea 2010.

Ni maoni yangu waungwana.
 
Unajua matumizi ya helikopta yanakuwa na ulazima kwa sababu ya ubovu wa miundombinu (hasa barabara). Sasa swali kuu la kuwauliza CCM ni 'walikuwa wapi kutengeneza barabara kwa miaka yapata 50!' Leo hii wanaanza kutumia helikopta! Hili swali haliwahusu Chadema.

Sina chama lakini nawachukia sana viongozi wa CCM kwa kutufanya watanzania wote mazezeta!
 
Kabisa mkuu,Hasa Taifa langu kuwa Maskini nitailaani kwa nguvu siku zote CCM.Leo hapa afrika Mashariki Tz ndiyo ingekua na uchumi mkubwa zaidi
 
Nadhani hapo unawasema CCM zaidi maanke CHADEMA hakuna wenye vitambi,wote ni makomandooo.Sema na akina kepteni komba huko CCM na tapiamlo Makamba
HE HE HE! DE KAPITENI HON. KOMBA (MP) mzee wa nambari wanii ehh! Baada ya kuminywa kuhusu kucharanga 30ml za TOT naona hata Tarime kasusa nini mbona vibweka vyake hatuvisikii?
Ila mkuu BEN unakosea cha KOMBA sio kitambi ni maumbile tu ya kijeshi,si unajua ni kapiteni bana! tehe tehe!
 
He he hee,na akian Jaka mwambi,Mwenyekiti Mstaafu Mkapa? Kaazi kweli kweli.

komba amesusa,safi sana. Je kitambi cha ncimbi,ni kwa kuwa yeye ni Deputy minister wa Jeshi ama? Duh,kaazi kweli kweli
 
Tarime sasa angani (Mwananchi)

*Aliyekataa kumpikia chai Nchimbi, atua Chadema

Na Waandishi Wetu, Tarime, Dar

NI TUKIO baada ya tukio katika kampeni za uchaguzi wa diwani na mbunge wilayani Tarime baada ya Chama Cha Mpinduzi (CCM) kuamua kujiimarisha kwa kuagiza helikopta mbili, siku moja baada ya Chadema kunogesha zaidi harakati zake kwa kuanza kampeni za angani.

Uamuzi huo wa CCM uliotangazwa jana, unafanya kampeni za vyama hivyo viwili vinavyopambana vikali jimboni Tarime kuwa "anga kwa anga".

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye katika kampeni za urais mwaka 2005 alizunguka sehemu kubwa ya nchi kwa kutumia helikopta ya kukodi, alitangaza juzi kuwa angeanza kutumia helikopta na baada ya vikwazo kadhaa vya kibali, alianza kutumia usafiri huo wa anga jana jioni.

Helikopta ya kukodi ya Chadema yenye namba Sy-Hsn ilitua mjini hapa jana saa 9:45 alasiri ikiwa na mkurugenzi wa sheria na katiba wa chama hicho, Tundu Lissu. Ilitua kwenye uwanja wa michezo Tarime.

Mara baada ya kutua uwanjani hapo Lissu alipokewa na umati wa wakazi wa Tarime, lakini chama hicho kikakataliwa kibali cha kufanya mkutano Sirani. Hadi jana jioni walikuwa wakihangaikia kibali.

Wakati Chadema wakijiweka sawa, CCM nao walitangaza kuanza kampeni za angani kama walivyofanya wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiteto, ambako vyama vyote viwili vilitumia helikopta.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere alisema jana kuwa maandalizi yote ya kukodiwa helikopta hizo mbili yamekamilika na wakati wowote zitatua mjini Tarime.

"Ni kweli tuna helikopta mbili zipo tayari... tunamsubiri Mbowe aanze kampeni za helikopta, nasi tutamfuata huko huko angani," alisema Nyerere na kusisitiza kuwa nia yao ni kudhihirisha kuwa CCM ndio chama tawala.

Kama CCM ikianza kutumia helikopta hizo leo, itakuwa ni mara ya pili kutumia baada ya kupambana na Chadema angani kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiteto, ambapo CCM ilishinda.

Huku mapambano ya angani yakitarajiwa kuanza leo, Chadema ililamba dume wakati katibu aliyetangaza kukataa kuhamishiwa ofisi za makao makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, kwenda "kumpikia chai (mwenyekiti wa umoja huo, Emmanuel) Nchimbi" kutangaza kujiunga na Chadema.

Mwita Mwikwabe Waitara, ambaye alikuwa katibu wa Jumuiya ya Vijana ya CCM mkoani Tanga, alikabidhi kadi yake ya CCM kwa viongozi wa Chadema jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Sirari.

"Nimeamua kujiunga na Chadema sababu ya sera zake ni nzuri na zinapingana na vitendo vyote vya uonevu na ufisadi," alisema Waitara, ambaye alidai kuwa kuondolewa kwake Tanga kulitokana na kusema bayana kuwa anaunga mkono kauli ya mgombea uenyekiti wa UV-CCM, Nape Nnauye na vita dhidi ya mafisadi.

"Waliniadhibu kwa kusema ukweli na kukabiliana na mafisadi, hivyo nina imani kuwa nikiwa Chadema, naweza kuwatetea wananchi vizuri kuliko CCM."

Katika kampeni zilizofanyika kwenye viwanja tofauti, kila chama kilikuwa na majigambo yake.

Kada wa CCM, Feruzi Banno alisema ushindi wa CCM hautegemei vijana wa mjini Tarime ambao alisema wengi hawajajiandikisha kupiga kura.

"Sisi tupo makini tunawajua wapiga kura na ndio tunawafuata kuwaomba kura katika vijiji vyote vya wilaya ya Tarime na ndio sababu tuna uhakika wa ushindi," alisema Bano, ambaye amewahi kuwa kiongozi katika jumuiya ya vijana makao makuu kabla ya kuwa katibu wa CCM katika wilaya mbalimbali

Naye katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alitarajia kuanza kampeni nzito za kata kwa kata katika Jimbo la Tarime.

"Maandalizi yote yapo tayari na hii ni hatua ya mwisho ya kuimaliza Chadema," alisema kada mmoja wa CCM ambaye yupo kwenye timu ya kampeni .

Katika hatua nyingine, wananchi wa Tarime, ambao wana vitambulisho vya kupiga kura lakini wana matatizo katika orodha ya wapiga kura, wameambiwa kuwa wanaweza kupata taarifa rasmi kuhusu mustakabali wao kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Trasiass Kagenzi alisema matatizo yote yamefanyiwa kazi na mkanganyiko uliotokana na orodha zilizobandikwa, hasa kwa watu waliofanyiwa marekebisho mwezi Agosti mwaka huu.

"Tumefanyia kazi tatizo hilo na sasa limekwisha kwa hiyo kila mtu aliye na kitambulisho cha kupiga kura, anaweza kutuma ujumbe kwenye namba 0753123179 ili kujua sehemu anayotakiwa kupigia kura," alisema Kagenzi.

Kagenzi alisema, ujumbe huo utakaokuwa wa bure kwa wapiga kura wote wanatakiwa kuandika namba tatu(3) mkato, namba ya kitambulisho cha kupigia kura na kutuma ujumbe kwenye namba hiyo.

Alisema hiyo ni mara ya kwanza kutumia utaratibu huo wa kisayansi ili kuwezesha watu wote kupata nafasi ya kupiga kura.

Alisema watu ambao hawakuandikishwa mwaka 2005 na waliofanyiwa marekebisho katika daftari hawataorodheshwa na hawatapiga kura.

Alisema hiyo ni kwa ajili ya kudhibiti wageni na watu ambao hawana sifa ya kupiga kura.

Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema orodha mpya imeshatolewa na kubandikwa katika vituo ikiwa na majina yote sahihi.

Kagenzi pia aliwataka wanasiasa wanaotangaza kuwa mgombea wao asipopita kutakuwa na umwagaji damu hawaitakii mema Tarime kwani wengi ni wageni na siyo wakazi wa jimbo hilo.

"Wengi wanaosema hayo ni watu waliokuja kushawishi watu mambo ya vita, lakini baada ya uchaguzi watapanda ndege na kuondoka na baadaye kutuacha Wana Tarime tukiwa na matatizo," alisema Kagenzi.

Aliwataka wananchi wengi kujitokeza ili kutumia haki yao ya kuchagua kiongozi wanayemtaka na ofisi yake iko wazi kwa mtu yeyote mwenye tatizo ili aweze kusaidiwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame alisema polisi walioko Tarime siyo wengi kama inavyoelezwa licha ya askari 450 kuwasili kwa ajili ya kusimamia vituo 406 wakati wa uchaguzi.

Makame, ambaye aliwasili tarime jana na kupokea taarifa ya msimamizi wa uchaguzi, alisema hakuna haja ya wananchi wa Tarime kuwa na hofu kwani polisi wako kwa ajili ya kuweka ulinzi na usalama.

"Kutakuwa na vituo 406 na polisi waliopo ni mmoja kila kituo na wengine watakuwa wakiangalia zoezi la usalama wakati wa uchaguzi," alisema Makame.

Alisema kutokana na uchaguzi wa Tarime kuwa na msisimuko na ushindani polisi wamejitahidi kuimarisha ulinzi ili kusitokee matatizo.

Makame alisema, mpaka sasa mambo yanakwenda sawa na atakutana na viongozi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.

Alisema mawakala wa vyama watakuwa katika kila kituo ili wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kufuata taratibbu za kukaa mita 200 toka kituo cha kupiga kura ili kuondoa malalamiko na vurugu.

Naye msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa alisema polisi hawana budi kujiimarisha ili kukabiliana na uwezekano wa kutokea kwa vurugu, huku akiwataka viongozi wa vyama kuacha kampeni za majungu na badala yake waheshimu kanuni na sheria za kampeni.

Alisema kiongozi aliyeshambuliwa alishindwa kufuata taratibu na kanuni za kampeni, na kuanza kutumia jukwaa vibaya kwa kusema mambo ambayo hayaendani na kampeni zao.

Alisema kushinda katika uchaguzi hakutokani na kurushiana majungu wala kutukanana bali kutumia jukwaa la siasa kwa kujinadi na kutoa sera ambazo zitawafanya wakubalike kwa wapiga kura wao.

Tendwa, pia alisema katika kampeni hizo, hakuna chama hata kimoja -kati ya CCM, NCCR-Mageuzi, Chadema na DP vilivyosimamisha wagombea- kinachofuata kanuni na sheria za uchaguzi za Tanzania, kitu ambacho alisema si sahihi.

Wakati huo huo, makada mbali mbali wa CCM wametoweka katika kampeni za ubunge na diwani mjini hapa akiwepo makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa ambaye amerejea jijini Dar es Salaam kimya kimya.

Wengine ambao walikuwa kwenye kampeni na kuondoka ni pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Stevin Wassira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo na Chakula, Gaudensia Kabaka Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mjumbe wa NEC Nimrod

Mkono.

Kiongozi mwingine wa CCM ambaye ametoweka, ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, James Wanyacha lakini hata hivyo wakati viongozi hao wakiondoka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana, Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ambaye amekuwa akitoa mchango mkubwa kwenye kampeni za CCM wamebaki.

Uchaguzi mdogo Jimbo la Tarime unatarajiwa kufanyika Jumapili Oktoba 12 mwaka huu ambapo mchuano mkali ni kati ya CCM na Chadema katika nafasi zote za ubunge na

udiwani wa Kata ya Tarime mjini.

Imeandaliwa na Mussa Juma, Fita Lutonja na Mpoki Bukuku
 
Nakumbuka wakati CHADEMA wanakubaliana kutumia helikopta, CCM na wawaona karibu wengine walibeza. Kinachonishangaza sasa ni kitendo cha ccm kutumia eti helokopta mbili hapa tarime! inashangaza sana na kuleta maswali mengi kuhusu hii timu ya kampeni inayoongozwa na mawaziri wa serikali waliokimbia ofisi zao kuja kufanya mambo ya chama kama kweli wapo makini ama ni ulimbukeni.

Kwangu mimi kuiga si kubaya hasa kama unachokiiga kina nia ya kurahisisha kazi na majukumu yako ama ya umma lakini kikubwa toa credit basi kwa uliyemuiga.

Marekani wanatumia mabasi kwa sababu barabara zao hata kama ni mbovu lakini si kulinganisha na 'njia' zetu tunazoziita barabara.

ACKNOWLEDGING some1 DOES NOT MEAN YOU ARE A FOOL
 
tayari watu wako huko mkuu! Ila tatizo this time ni ugumu wa maisha kule zenj, jamaa wameunganishwa ktk matatizo hivyo kura zitakuwa za uzanzibar zaidi kuliko cuf na ccm, ni uwanja mpya kwa wanasiasa wa zanzibar, wanalazimika kuhubiri u zanzibar wao na hatima ya wananchi wao, atakyecheza vizuri karata hiyo ataingia ikulu hata kama ni kwa mseto.

Nakubaliana kuwa muungwana ana kazi pevu zanzibar kuliko hata aliyokumbana nayo mkapa au hata ile aliyoiacha mwinyi, mkuu mfuatilie vizuri shamhuna na sasa hata ile vita dhidi khatibu inaashiria sana jambo hili la 2010 kipaumbele ni zanzibar bila uoga wala nidhamu tukufu kwa muungano.

Niwakumbushe tu wana jf kuwa ally abeid karume alishabashiri hili wakati anatangaza rasmi kuwa 2010 yumo, sasa kama ni zanzibar au muungano hiyo itategemea siasa zetu kuelekea 2010.

Ni maoni yangu waungwana.
A delicious "food for thought!!!"
 
Nakumbuka wakati CHADEMA wanakubaliana kutumia helikopta, CCM na wawaona karibu wengine walibeza. Kinachonishangaza sasa ni kitendo cha ccm kutumia eti helokopta mbili hapa tarime! inashangaza sana na kuleta maswali mengi kuhusu hii timu ya kampeni inayoongozwa na mawaziri wa serikali waliokimbia ofisi zao kuja kufanya mambo ya chama kama kweli wapo makini ama ni ulimbukeni.

Kwangu mimi kuiga si kubaya hasa kama unachokiiga kina nia ya kurahisisha kazi na majukumu yako ama ya umma lakini kikubwa toa credit basi kwa uliyemuiga.

Marekani wanatumia mabasi kwa sababu barabara zao hata kama ni mbovu lakini si kulinganisha na 'njia' zetu tunazoziita barabara.

ACKNOWLEDGING some1 DOES NOT MEAN YOU ARE A FOOL

Mabasi yanatumika lakini vile vile wanatumia ndege kwa safari ndefu.....Lakini issue hapa ni kuwa Tanzania hatukutakiwa kuwa maskini kwa rasilimali tulinazo mpaka sasa watu wanashinda kutembea na gari ndani ya kajimbo kadogo kama Tarime mpaka watumie helikopta.

Kwa CCM ila sidhani kuwa wanashindwa kuwafikia wananchi kwa sababu wana magari, pesa na kila kiongozi wa serikali anawatetemekea, ila kwa wao ni showoff kwa wananchi kuwa nao wanaweza hata kukodi helikopta.
 
Marekani wanatumia mabasi kwa sababu barabara zao hata kama ni mbovu lakini si kulinganisha na 'njia' zetu tunazoziita barabara.

Lakini si ndiyo hizo ambazo hao wanaogombea kuwawakilisha wanazitumia kila siku? Watawakilisha vipi kama wanakwepa kuziona adha zao za kila siku? Si watakupeleka ukawatetee ili barabara zao zitengenezwe? Utafanyaje hivyo kama hiyo inabaki kuwa ni nadharia tu?

Kwa mfano, utawawakilishaje watu wa kigamboni huku unakwepa kutumia kivuko wanachotumia kila siku?
 
sasa hii JF,inaelekea wapi? sasa we have sunk so low that sasa tunajadili choppers,i wonder what visitors to this forum think of us
 
Ni sahihi muda wa kampeni ndo umekwisha hivi.
Sasa unashangaa hao wana helikopta moja na hao mafisadi wanao leta helikopta 2 je utasemaje hapo?

Wote wanatakiwa watupatie gharama walizotumia kwenye huu uchaguzi na wapi walipata hizo pesa. I wish our foreign donors come forth and twist their hands to demand the breakdown of their shameless spendings. How come that our major parties spend lavishly in a minor election with no regard to the stinking poverty our people are facing?
 
Watu wa Tarime wamezoea kuchinjana na wala siyo sababu ya kuchonganishwa na wana siasa mimi nafikiri mpaka wetu ulitakiwa uwe mto Mara huko Tarime wana tabia ya Kenya ambako wamezoea kuchinjana

Ndugu Mtanzania, acha Ukabila. Waombee ili waache shari.
 
sasa hii JF,inaelekea wapi? sasa we have sunk so low that sasa tunajadili choppers,i wonder what visitors to this forum think of us

Si chopa as chopa mkuu. Suala la chopa lina uhusiano na masuala mengine kama ambavyo baadhi ya michango inavyoonyesha. Inaelezwa kuwa chopa inarahisisha mawasiliano, ni kweli. Lakini katika eneo dogo la wilaya kuna umuhimu wa kurahisisha mawasiliano kiasi hicho? Kama umuhimu huo upo, basi kuna kasoro kubwa katika miundombinu, ambayo inachelewesha mawasiliano.
Kama hilo ndilo, nadhani mjadala unapanuka zaidi na kuanza kuangalia hali ya miundombinu badala ya chopa kama chopa katika kampeni. Hili ni moja tu, ukiamua kunyambulisha unapata mambo mengine mengi sana kwa mfano, unahitaji fedha kukodi chopa, wanapazipata wapi hawa wanaozikodi na kuzitumia kwenye kampeni?
Kila mara tumesikia vyama vikilalamikia kuwa havina fedha, lakini wakatiw a kampeni ghafla wanapata fedha za kuweza kukodi chopa, zinatoka wapi?
Haya ni machache tu kati ya mengi yanayoweza kuibuliwa kutoka kwenye mjadala huu mkuu.
Niaonavyo
 
Wote wapuuzi. Yaani kweli Tarime wanahitaji helikopta? Wenzao wanatamba kwa kutumia mabasi kufanyia kampeni wakati sisi tunatambiana kwa helikopta! Mawazo yale yale ya wingi wa mashabiki ndio wingi wa kura. Mimi ningewasifu kama wote wangetumia baiskeli kuonyesha wanaelewa hali duni ya wananchi wao, kupunguza madhara ya mazingira na kuonyesha umuhimu wa mazoezi maana baada ya kampeni vitambi vyote vitakuwa history! Huku ni kutia chumvi kwenye kidonda na kuwadharau hao wapiga kura.

Ndugu yangu usiturudishe kwenye teknolojia ya kizamani,lazima ulimwengu wa sasa hivi unatakiwa upeleke mambo kwa kasi.Fikra hizo za kwako ndio zinazo umiza migongo wakulima wetu kwa kutumia jembe la mkono kwa tija ndogo.Mimi nimependekeza kule kyela wafanyabiashara wajiunge pamoja kuanzisha makampuni ya usafiri ya kwenda vijijini.Hiyo hatua itapunguza mda wa wananchi kutembea kwa miguu na kupoteza mda wa uzalishaji mashambani. Chukulia usafiri wa anga kuwa sio starehe ni kitu cha kuokoa mda,ili mwili uwe na nguvu ya kufanya kazi zingine.
 
TARIME: Helikopta ya CCM fedha za ufisadi, ya Chadema fedha ya halali

Field Marshall, Mwanakijiji, Bubu Ataka kusema na wengineo hivi eti mna habari kuwa kama serikali ilivyoishiwa ndivyo vivyo hivyo Chama tawala kilivyo taabani kifedha.

Je, hela za kukodisha helikopta au ni ya serikali? Na kama sio wamezipata wapi?

Habari tulizonazo ni kwamba wale wenye uchungu na kula nchi bila kusumbuliwa na ambao bado wanatamani kwa udi na uvumba kuwa rais na waziri mkuu 2015 kama sio 2010 wameamua kukuwadia CCM na kukusanya nusu ya fedha toka kwa mafisadi kwa mafisadi kwa ahadi kuwa CCM itafanya juu chini wasichukliwe hatua zozote za kisheria.

Ndio maana ya kichwa cha habari: TARIME: Helikopta ya CCM fedha za ufisadi, ya Chadema fedha ya halali !

Juu ya hayo kuna kiasi kidogo toka mkataba wa IPTL, mkataba wa Richmond na kampuni zake dada na usisahau ule mkataba wa rada mbovu toka Uingereza ama vile hakuna nchi nyingine tena duniani inatengeneza rada!

akili,
tanga
 
Ndugu yangu usiturudishe kwenye teknolojia ya kizamani,lazima ulimwengu wa sasa hivi unatakiwa upeleke mambo kwa kasi.Fikra hizo za kwako ndio zinazo umiza migongo wakulima wetu kwa kutumia jembe la mkono kwa tija ndogo.Mimi nimependekeza kule kyela wafanyabiashara wajiunge pamoja kuanzisha makampuni ya usafiri ya kwenda vijijini.Hiyo hatua itapunguza mda wa wananchi kutembea kwa miguu na kupoteza mda wa uzalishaji mashambani. Chukulia usafiri wa anga kuwa sio starehe ni kitu cha kuokoa mda,ili mwili uwe na nguvu ya kufanya kazi zingine.

lakini Mkuu, unaonaje kama utaratibu wa kuboresha usafiri wa anga lingekuwa jambo la kudumu badala ya kufanya wakati wa kampeni tu? Nina imani kuwa baada ya kampeni, tarime hawataona helikopta tena kwa ajili ya usafiri wao
 
Si chopa as chopa mkuu. Suala la chopa lina uhusiano na masuala mengine kama ambavyo baadhi ya michango inavyoonyesha. Inaelezwa kuwa chopa inarahisisha mawasiliano, ni kweli. Lakini katika eneo dogo la wilaya kuna umuhimu wa kurahisisha mawasiliano kiasi hicho? Kama umuhimu huo upo, basi kuna kasoro kubwa katika miundombinu, ambayo inachelewesha mawasiliano.
Kama hilo ndilo, nadhani mjadala unapanuka zaidi na kuanza kuangalia hali ya miundombinu badala ya chopa kama chopa katika kampeni. Hili ni moja tu, ukiamua kunyambulisha unapata mambo mengine mengi sana kwa mfano, unahitaji fedha kukodi chopa, wanapazipata wapi hawa wanaozikodi na kuzitumia kwenye kampeni?
Kila mara tumesikia vyama vikilalamikia kuwa havina fedha, lakini wakatiw a kampeni ghafla wanapata fedha za kuweza kukodi chopa, zinatoka wapi?
Haya ni machache tu kati ya mengi yanayoweza kuibuliwa kutoka kwenye mjadala huu mkuu.
Niaonavyo

Hapa lazima tuseme ukweli unapoamua kuingia kwenye chama hivi vingine lazima ujitolee kwa asilimia kubwa. Kwa uelewa wangu Chadema inaongozwa na watu makini hivyo sidhani kama mpango wa helikopter ni wa Mh. Mbowe mwenyewe ni wa chama na ni ubunifu wa kupewa sifa. Hivyo ndugu yangu pale kuna kujitolea kwa hali na mali si kama hao mafisadi wanachota BOT na kwingine ili wafanye kampeni. Cheki marekani jinsi uchaguzi unavyoendeshwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom