Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Haya yanayotokea Tarime hayana tofauti hata kidogo na yale yalitokea wakati wa uchguzi wa Zimbabwe ambpo mgombea wa Urais wa MDC Tsavangarai na wafuasi wake walipigwa na polisi na wafuasi wa Mugabe. Viongozi wa CCM wanaliona hili lakini kutikana na ufisadi na ubinafsi wao wamenyamaza kimya. CCM ni aibu tupu kwa Watanzania na huu uchaguzi kamwe CHADEMA haiwezi kushinda na wala hauko huru.
 
Taarifa zilizothibitika kutoka Tarime zinaeleza kuwa wananchi wanne wa Tarime wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA wamejeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga na watu wawili kwa sababu zinazoweza kuwa za kisiasa.

Taarifa zinaeleza kuwa watu hao wanne walikuwa eneo amabapo helkopta inayotumiwa na CHADEMA katika kampeni za ubunge na udiwani ilikuwa inasubiria kutua.Wakati wananchi na wafuasi wa CHADEMA wakiwa wanasubiri kuwasili kwa viongozi wa chama chao,ilitokea gari ambapo walishuka watu wawili wakiwa na mapanga na ghafla wakawavamia watu hao kwa kuwakatakata kwa mapanga.

Akithibitisha kuwahudumia watu hao hospitalini, daktari (jina ninalo) amethibitisha na kueleza kuwa mmoja wa majeruhi ameshonwa nyuzi kumi na tisa (19) kwa nje.Hakutaja idadi ya nyuzi alizoshonwa kwa ndani.

Hali hii inajitokeza zikiwa zimebaki siku tatu tu wanatarime watumie haki yao kikatiba kumchagua mwakilishi wao.

hii habari pia imebandikwa na halisi (one of the respected member hapa JF) kule kwenye thread ya ubunge wa Tarime na namna ambavyo polisi wamefika eneo la tukio lakini wakagoma kuwafuatilia wahusika.

Hii sasa inatisha, nilijua kuwa mamia ya polisi walioletwa Tarime "kuzuia vurugu" walikuwa na lao jambo na sasa yanazidi kuonekana:

1. mara polisi wanakamatwa wakinunua kadi za kupigia kura
2. polisi wanaonekana na jezi ambazo hazina namba zao
3. polisi wanawapiga wanachadema wanaotoka mkutanoni bila sababu yoyote
4. polisi wanahusishwa na matukio ya uvunjaji amani Tarime
5. Na hii ya leo ya polisi kukataa kufuatilia wahusika wa vurugu Tarime.

Haya yote yataendelea hadi lini? Mheshimiwa Kikwete, unaruhusu Tarime igeuzwe kuwa Pemba ndogo?
 
Nimeipata post ya Halisi na ninaiweka hapa kusisitiza point yangu hapo juu, Asante mzee wa gumzo kwa kuanzisha hii thread hapa maana sasa naona "zile fujo" ambazo polisi walikuja kuzizuia Tarime sasa "zinatokea". Natumaini Mods wataiacha hii thread ijitegemee hapa kwa updates zote zinazoendelea kuingia.

halisi said:
HATARI:

KUna taarifa za watu watatu kukatwa na mapanga mbele ya polisi Tarime na watuhumiwa kutoroshwa na gari la kiraia linalojulikana. Polisi badala ya kushughulikia watuhumiwa, wakakimbia na gari lao.

Saa moja baadaye uongozi wa polisi unafika eneo la tukio na wakati wanaendelea kukagua, gari lililowatorosha watuhumiwa linafika, na wananchi wanapiga kelele kusema hilo! Hilo!, linageuza na kukimbia, mkuu wa polisi anaamuri gari la polisi liwafukuze, dereva wa polisi anacheka na kukaidi amri ya bosi wake. GAri linatokomea na polisi wanaendelea kubaki walipo.

MAONI:
-Hii ni hatari na matokeo yake huenda kukazuka mauaji ya kutisha.
-Jimbo moja lisiwe mwanzo wa maafa kwa Watanzania
-JK lazima atoe tamko la kukemea na kuwaambia watu wake waache UJINGA

Nakubaliana nawe Halisi, JK atoe tamko kama anaruhusu haya yatokee. Yaani ubunge tu una thamani ya maisha ya watu wangapi?
 
Ubishi unaoendelea hivi sasa juhusu chopa umenikumbusha mbali sana kwenye miaka ya sabini kabla ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC. ( EAC iliendeshwa kwa michango ya nchi zetu tatu pamoja na wafadhili kama benki ya dunia, shirika la fedha n.k.)

EAC ilitaka kuwajengea wafanyakazi wake nyumba za kuishi. Michoro ilitengenezwa na kuwasilishwa kwa serikali zote tatu - Kenya, Uganda na Tanzania. Wakati hiyo michoro ilikubalika Uganda na Kenya, hapa Tanzania ilikataliwa - sababu hizo nyumba zingezidi nyumba za serikali kwa uzuri na kwa nchi masikini kama Tanzania zilikuwa ni anasa !!!. Hivyo wafanyakazi wa EAC Tanzania walijengewa nyumba za kiwango cha chini kuliko wa nchi hizo mbili k.m. zile za Chang'ombe.

Nakumbuka pia TV ilivyopigwa marufuku kuwa ni anasa ili Watanzania tusiweze kuangalia maendeleo ya wenzetu duniani lakini watawala walikuwa nazo. Ilifikia hatua ya kuona vitu kama magari, mafriji n.k kama anasa wakati watawala wakitembelea magari yenye vyoyozi. Hayo ni ya zamani tuyaache lakini mtu anayethubutu sasa hivi kutaka wanaTarime wasione helikopta eti ni anasa ana tofauti gani na huyo aliyewanyima wananchi TV kwenye karne ya ishirini ?.

Sasa hivi pamoja na umasikini wetu wa kujitakia, Tanzania iko kwenye chati za juu kwa magari ya anasa, simu za bei mbaya, tafrija za mamilioni n.k. halafu anatokea mtu anambeza Mbowe kwa kujaribu kutafuta njia ya haraka ya kuwafikia wananchi na kuwafungua macho dhidi ya dhuluma wanazofanyiwa. Hata MAFISADI wenyewe wamefunguka macho na kuiga lakini JF kuna watu wanamtupia vijembe !!!

Hivi huyu mtoto anayezaliwa leo na asiwe na habari kuwa chopa ni nini - huku ni kumdumaza kifikra na kiubunifu - atawezaje kuwa na dream ya kuimiliki vitu kama hivyo siku moja ?. Matatizo ya miundo mbinu si kwa Tarime peke yake bali kwa nchi nzima na si lazima wakati wa kampeni eti ndiyo mtu aonje ladha yake ama kwa kutembea au kuendesha baiskeli. Haya ni mawazo mufilisi na naomba Mola atuepushe kuongozwa na watu kama hao. Tunahitaji wanaoona mbali na hapa nawapa Chadema pongezi. Fikra potofu lazima zipigwe vita kwa sababu hii ni karne ya ishirini na moja.
 
yaani nimepitia kamusi zote zinazopatikana kwenye mtandao na sikupata hili neno sasa ikabidi tu niulize jamii inisaidie.

Ku Enzi na hedhi ni tofauti Enzi ni tofauti neno enzi kama kweli ni kweli na hedhi ni ile tu ya kuzuga zuga na mtimanyogo fulani maana unalazimika kusema hivyo BILA kusema hivyo inamaana hutopata unachokitafuta.

ILI ni weke bayana CHADEMA wana mhedhi CHACHA ama wanamuenzi.?Maana nimeona Mbowe akitumia neno hilo sana ktk kampeni zake.
 
yaani nimepitia kamusi zote zinazopatikana kwenye mtandao na sikupata hili neno sasa ikabidi tu niulize jamii inisaidie.

Angalieni matumizi ya Lugha waungwana...Alidhamiria kusema "kumuenzi" maana neno "Hedhi" lina maana tofauti,na hapo mahali si pake
 
Ku Enzi na hedhi ni tofauti Enzi ni tofauti neno enzi kama kweli ni kweli na hedhi ni ile tu ya kuzuga zuga na mtimanyogo fulani maana unalazimika kusema hivyo BILA kusema hivyo inamaana hutopata unachokitafuta.

ILI ni weke bayana CHADEMA wana mhedhi CHACHA ama wanamuenzi.?Maana nimeona Mbowe akitumia neno hilo sana ktk kampeni zake.

nimezidi kuchanganyikiwa kabisa hapa. ndugu yangu unahitaji breki kidogo maana huko unakoelekea kunatisha. Sasa hedhi, enzi na mbowe vinahusiana nini hapa?
 
Kwa wale wanaotetea matumizi ya helikopta kwa sababu barabara ni mbovu.

Mbona tunawalaumu waheshimiwa wabunge na mabosi serikalini wanapokazania kuwa ni lazima wanunuliwe mishangingi kwa sababu hiyo hiyo, yaani barabara hazipitiki? Hivi toka tuanze kuwanunulia hiyo migari, hizo fedha zingewekezwa kwenye hizo barabara si angalau leo wengi wao wangekosa kisingizio. Sisi ni watu wa bling. Na helikopta kama yalivyo hayo mashangingi ni bling pia. Na wote tunajijua tunavyopenda cheini zetu za dhahabu, hata kama bado tunakaa katika chumba cha kupanga!

Mpaka leo sijasikia jambo la maana linalozungumziwa kuhusu mwananchi wa Tarime kutoka pande zote zinazogombania uchaguzi huu. Wamebaki kutambiana na kuonyeshana ubabe. Sera ni kama za Sarah Palin, ku-appeal to the lcd wakati matatizo ya mwananchi yanafagiliwa chini ya jamvi. Lakini hamna cha kushangaza kwa sababu fundamentally wote ni wale wale. Wakiingia hao wengine nao wataendeleza libeneke kama kazi!
 
Matumizi ya Helikopta ktk kampeni za chama hayawezi kuwa na sifa nzuri ya aina yoyote ile zaidi ya ku prove kuwa ndivyo tulivyo.. Kwanza ni aibu kubwa kwa kiongozi kusema barabara mbovu wakati wananchi wako unaotafutra kura zao, barabara hizo ndio maisha yao ya kila siku..Ulichotakiwa wewe kama kiongozi kupelekwa muswada bungeni ioli kwanza upate kuwaambia wananchi jinsi ulivyotetea ujenzi wa barabara hizo..Pia zingatieni kwamba tatizo la viongozi kushindwa kufika sehemu hizo ni moja ya sababu kubwa ambayo inaweza kupitisha miswada kama hiyo maanake ndio kula yenu. Kwa mtazamo wowote ule wewe ni mshindi kwa wananchi wako. Focus ya kampeni siku zote huwa ni wananchi sio swala la kufikiria viongozi.

Leo hii ya kuwafuata wananchi na helikopta utadhani unawapelekea misaada ya chakula na dawa kumbe ni kampeni za chama...Nooo guys mnaharibu nyotre Chadema na CCM..
Wakuu wangu Chadema kusema kweli haya ni makosa niliyasema ktk uchaguzi uliopita na nitaendelea kupinga matumizi ya Helikopta kwani viongozi mashujaa wote toka kina Washington hadi Castro waliepuka sana kuonyesha tofauti zaoi na wananchi wa sehemu hizo. Kama kulikuwa na Umuhimun wa kutumia helikopta basi mgeenda hadi Musoma kisha mkachukua mabus ama magari madogo, pikipiki na kadhalika mkipitia vijijini ambapo wananchi wangeweza kuwaona mkipita na bendera zenu zikipepea kuelekea Tarime...
Na maandalizi ya msafara yangetakiwa kufanywa mapema kiasi kwamba wananchi wa vijiji vyote vinavyounganisha Musoma na Tarime wangekuwa na taarifa ya msafara huo..Trust me, hii ndio njia nzuri ya kujitangaza...
Hamuwezi kuamini lakini nakumbuka vizuri sana wakati mwalimu Nyerere alipotembelea Kibara, wilaya ya Mwibara kati ya mwaka 1966 au 67, hiyo kumbukumbu nimeibeba hadi leo hii..Nakumbuka vizuri tukiwa peku peku tukifukuzia magari ya serikali kwa miguu hadi makao makuu ya chama. Sura za wananchi na mpasuko wa roho bado nauona kama vile ilikuwa jana tu..Na sababu kubwa niliyokuja gundua ni kwamba ilikuwa mara yangu ya kwanza na pengine the only chance ya kumuona kiongozi wangu (Nyerere)..
Pamoja na yote haya najua kama hata sisi raia ndivyo tulivyo kwani kuiona Helikopta ni bora na maajabu zaidi kwetu kuliko kumwona kiongozi mwenyewe!..Ni ushindi wa mazingaombwe!
 
Mkandara,

Yaani Tanzania yetu ina mambo ya ajabu kweli kweli. Watu wanatumia ujinga na umaskini wa raia kufanya mambo ya ajabu ajabu.

Priorities zetu ziko mrama kweli kweli. Hata CCM wako madarakani zaidi ya miaka 40, barabara hazipitiki, wanapeleka helikopta, ndio yale yale ya shule mbovu, peleka mtoto nje, au hospitali mbovu, peleka wagonjwa India.
 
Kwa wale wanaotetea matumizi ya helikopta kwa sababu barabara ni mbovu.

Mbona tunawalaumu waheshimiwa wabunge na mabosi serikalini wanapokazania kuwa ni lazima wanunuliwe mishangingi kwa sababu hiyo hiyo, yaani barabara hazipitiki? Hivi toka tuanze kuwanunulia hiyo migari, hizo fedha zingewekezwa kwenye hizo barabara si angalau leo wengi wao wangekosa kisingizio. Sisi ni watu wa bling. Na helikopta kama yalivyo hayo mashangingi ni bling pia. Na wote tunajijua tunavyopenda cheini zetu za dhahabu, hata kama bado tunakaa katika chumba cha kupanga!

Mpaka leo sijasikia jambo la maana linalozungumziwa kuhusu mwananchi wa Tarime kutoka pande zote zinazogombania uchaguzi huu. Wamebaki kutambiana na kuonyeshana ubabe. Sera ni kama za Sarah Palin, ku-appeal to the lcd wakati matatizo ya mwananchi yanafagiliwa chini ya jamvi. Lakini hamna cha kushangaza kwa sababu fundamentally wote ni wale wale. Wakiingia hao wengine nao wataendeleza libeneke kama kazi!

Ndugu yangu,

Fuatilia kwa makini utagundua kuwa kuna chama kinatoa sera zake Tarime na kina historia ya kutetea maslahi ya Tarime na kuna vingine ambavyo vinaleta chuki na ugomvi kwa wakazi wa Tarime.
 
Huu utafiti umefanywa na Thomas Ngawaiya

Na Godfrey Lutego

Uchaguzi mdogo wa mbunge na Diwani wa jimbo la Tarime mkoani Mara unafanyika kesho huku ushindani mkubwa ukiwa kati ya mgombea wa chama tawala, CCM, Bw. Christopher Kangoye nawa chama cha upinzani, CHADEMA, Bw. Charles Mwera.

Vyama vingine vinavyoshiriki katika uchaguzi huo unaofanyika kujaza nafasi ya aliyekuwa mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe aliyefariki kwa ajali ya gari ni NCCR Mageuzi na DP cha Mchungaji Christohper Mtikila. TLP wanawaunga mkono NCCR Mageuzi huku CUF wakikaririwa kutokuwa na upande wowote katika uchaguzi huo.

Wagombea hao wa ubunge na udiwani na viongozi wakuu wa vyama vyao, wapambe wao na wanachama na wafuasi wa vyama vyao kwa zaidi ya wiki mbili wamekuwa katika kampeni za kunadi sera zao ili kuomba kura wachaguliwe kuwakilisha wananchi wao katika kipindi kilichobaki kufikia mwaka 2010 uchaguzi mkuu utakapofanyika.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na Taasisi ya Utawala bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA), CCM ina nafasi kubwa ya kutwaa jimbo hilo kwa ushindi wa asilimia 65 ikifuatiwa na CHADEMA iliyokuwa inalishikilia inayopewa nafasi ya kupata asilimia 35 na vyama vinavyobaki vinatarajiwa kupata asilimia 5.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa CEGODETA, Bw. thomas Ngawaiya anasema tathmini iliyofanywa na taasisi yake inaonesha CCM watalipoka jimbo hilo kwa CHADEMA.

Hata hivyo, tathmini hiyo inatofautiana kidogo na tathmini iliyotolewa na gazeti moja likikariri wanaodaiwa kuwa wananchi wa Tarime kuwa CHADEMA itaendelea kutetea jimbo hilo kwa ushindi wa asilimia 50 huku CCM ikipata asilimia 45 na vyama vingine vilivyobaki asilimia 5.

Kwa kurejea tathmini hiyo, kinachojitokeza hapa ni kuwa, zote mbili zinakubaliana na ukweli kuwa, vyama vilivyobaki, NCCR Mageuzi na DP havina nguvu na vinasindikiza tu wenzao katika uchaguzi huo ndio maana vina nafasi ya kupata asilimia tano kwa tathmini zote.

Lakini kwa kurejea malumbano ya kisiasa yanayoendelea katika uchaguzi huo kuhusu DP na NCCR Mageuzi na viongozi wake kutuhumiwa kuipinga CHADEMA na kuisaidia CCM ishinde, CCM ndiyo inapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda kwa faida ya utengano wa wapinzani. Waswahili husema, vita ya panzi furaha ya kunguru.

Ni wazi basi kuwa kuvunjika kwa umoja wa vyama vya upinzani vya CHADEMA, NCCR Mageuzi, TLP na CUF na kitendo cha TLP kutomuunga mkono mgombea wa CHADEMA ingawa pia haisemi inamuunga mkono nani wakati CUF pia ikisema haiungi mkono mtu yeyote kunaipa CCM ahueni ya kukataliwa na wapiga kura Tarime.

CCM inapata ahueni hiyo kwa sababu tayari wapinzani wamegeukana na hivyo kufanya wanachama wa vyama vya upinzani ambavyo vina nguvu huko Tarime, NCCR Mageuzi ambacho kinatamba kuwa na wanachama kwenye vitongoji vingi na vijiji vingi kuliko CHADEMA na TLP na CUF wasimpigie kura mgombea wa CHADEMA, Mwera.

Hatua ya Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia na Katibu Mkuu wake, Dkt. Sengondo Mvungi ya kuipinga CHADEMA hadharani na kuikana kutokana na kampeni zake za kibabe na vurugu ilikuwa ni hitimisho na ushahidi tosha wa jinsi gani CHADEMA na mgombea wao hawana lao tena kwa wanachama wa NCCR Mageuzi.

Mbaya zaidi ni hatua ya Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Bw. Tundu Lissu kuthibitisha kuwa ndoa ya vyama vya upinzani vya TLP, CHADEMA, NCCR Mageuzi na CUF haipo tena kwa sababu ya matamshi na vitendo vya viongozi na wanachama wa vyama hivyo akirejea waliyosema Tarime kwenye kampeni na pia kabla ya kampeni wakiihusisha CHADEMA na kifo cha Wangwe.

Bw. Lissu alikaririwa akisema kwa Wenyeviti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wa TLP, Bw. Agustine Mrema kudai CHADEMA ina mkono katika kifo cha Wangwe huku TLP ikidai Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alishangilia kifo hicho alipokuwa Afrika Kusini kulitosha kuonesha kuwa wao si wamoja tena, ndoa yao imekufa na ilimalizwa kwa Bw. Mbatia kuituhumu kwa rafu Tarime kiasi cha kutaka chama hicho kifutwe.

Ni wazi basi CHADEMA inapambana kubakiza jimbo hilo mikononi mwake ikiwa chama mkiwa, kisiye na msaidizi, mtetezi wala jirani wa kugombolezea hali inayofanya kiwe na wakati mgumu zaidi licha ya kuongeza nguvu za Bw. Mbowe kuungana na timu yake kampeni huku akitumia helikopta kumnadi mgombea wake na pia kujiunga kwa aliyekuwa Katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga, Bw. Mwita Waitara.

Kimahesabu ya yamkini, kama vyama vyenye asilimia tano vitaisaidia CCM kwa sababu wapinzani wamefarakana, basi katika tathmini ya kwanza, CCM itajipatia kura asilimia 70 na hata ya pili asilimia 55 na hivyo ina maana itaishinda CHADEMA ambayo itaendelea kubaki na 50
ya awalina 45 ya pili hasa ukizingatia kuwa, mwaka 2005 ilipata kura za huruma za wana CCM waliosalitiana na pia uchaguzi ulikuwa nchi nzima wakati sasa ni jimbo moja hivyo CCM imejipanga kwa nguvu zote kulitwaa jimbo hilo.

CHADEMA kupewa asilimia 50 na wananchi wenyewe wakati ndio kilikuwa chama tawala katika jimbo hilo ni ushahidi tosha kuwa, haikubaliki tena kwani baada ya kiliyofanya kwa miaka miwili, ilitarajiwa iwe imeongezeka umaarufu na kujijengea uhalali zaidi wa kuchaguliwa pale.

CHADEMA ina hali ngumu zaidi kwa sababu hata Polisi ambao ndio walipaswa kuwa watetezi wao wakuu, kimbilio lao wamekerwa na ubabe na vurugu zao walizowafanyia Polisi waliokuwa wakiwalinda kwenye mikutano yao ikiwa ni pamoja na kuwatukana kuwa wametumwa na CCM na kuwaponda mawe, kukaidi amri zao kiasi cha kuwafanya wasambaratishe maandamano yao yasiyo halali waliyofanya wakidai wanawasindikiza wagombea baada ya kampeni.

Ni wazi uhusiano wao na Polisi si mzuri, umekuwa wa paka na panya ndio maana ilifikia wanachama na wafuasi wa CHADEMA kumkamata mtu waliyedai ni Polisi akinunua kadi za CHADEMA kwenye ofisi za chama hicho jambo ambalo Kamishna wa Polisi anayesimamia Operesheni maalum, Bw. Vicent Tossi kukanusha hakuwa Polisi wao.

Vitendo vyao vya vurugu vikiwemo vya wanachama na wafuasi wake kudaiwa kumpiga Mchungaji Mtikila mawe kwenye mkutano wake wa kampeni kwa madai kuwa katumwa na CCM, hatua ya Naibu katibu Mkuu, Bw. Zitto Kabwe kuwaongoza wafuasi na wanachama wao kuchoma moto bendera ya CCM na wanachama na wafuasi wengine kumvisha mbwa, t-shirt yenye picha ya mgombea wa CCM ni ushahidi tosha wa madai ya Polisi dhidi ya CHADEMA kuwa chenye vurugu lakini hodari wa kulalamika kuonewa.

Ni jukumu la wananchi wa Tarime kuchagua kusuka au kunyoa kwani kama ni sera wamezisikia na kwa muda huu wanajua nani mwenye sera za amani na maendeleo ambayo imekuwa sera kuu ya CCM na hivyo watakuwa na nafasi ya kuchagua kati ya pumba za wanaoeneza chuki, uhasama, vurugu na fitina, kukatana mapanga au CCM ambayo imejikita kutumikia wananchi ili hatimaye waneemeke.

Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bw. Pius Msekwa ambao wamekuwa Tarime kwa muda mrefu wakiongoza timu ya kampeni ya CCM wameinadi vyema CCM kama chama makini, chenye mwelekeo, kilicho na dola, chenye mgombea safi, msomi na aliye tayari kuendelea kuwatumikia wananchi wa Tarime kwani tayari alishawanunulia vitanda vya sh. milioni 600 katika hospitali yao na hivyo ni jukumu la wananchi wa Tarime kuonesha kwa vitendo kuwa waliwaelewa vyema viongozi hao kwa kuichagua CCM na wagombea wake wapate maisha bora.

Wananchi wa Tarime wanapaswa kupima maisha bora yaliyotokana na zaidi ya sh. bilioni 10 ambazo Halmashauri ya wilaya ya Tarime imekuwa ikipata kutokana na ruzuku ya Serikali Kuu na pia makusanyo ya Halmashauri ambayo ilikuwa inaundwa na CHADEMA ambayo wameyaona kwa miaka hii miwili na nusu kama yanalingana na fedha hizo.

Madai ya marehemu Wangwe kuhusu ufisadi wa fedha ndani ya CHADEMA yanapaswa kuwa taa ya kuwamulikia waone ukweli wa ahadi za CHADEMA kwa watu wake hasa wa eneo kama Tarime lenye makusanyo makubwa ya mapato kutokana na biashara kutokana na kuwa eneo la mpakani na Kenya kama yanalingana na walichofanyiwa.

Walichofanya CHADEMA kulipia ada wanafunzi ndicho CCM imekuwa ikifanya na inaendelea kufanya kwa kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure au kwa kuchangia kidogo kupitia mikopo kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu na hivyo hakuna jipya bali utekelezaji wa sera makini za CCM hivyo ni vyema wakapewa wenye nazo wazitekeleze badala ya kuwaachia wanaojaribu kuziiga.

Kuhusu madai makuu ya wana Tarime yanayofanya wawe mbogo kuwa ni maskini wakati wanazungukwa na madini, tayari Serikali kupitia Tume ya Jaji Mark Bomani ambayo Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Kabwe alikuwa Mjumbe wake imerejea sheria za madini kwa lengo la kunufaisha wazawa hivyo hawana haja ya kuendelea kuifanya kama ajenda ya kuinyima kura CCM kuiiadhibu.

Mbali ya sheria kupitiwa upya, tayari wenye migodi Tarime kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali wameonesha nia ya kutatua matatizo ya maeneo ya migodi Tarime wakianza na kuanzisha mahusiano mazuri na wakazi wa huko hivyo hilo halipaswi kuwa ajenda ya kuinyima kura CCM kwani ndiyo yenye Serikali inayosimamia sheria wanazozililia.

Ukiacha hoja hiyo, CCM huenda ikanufaika pia na umoja uliojionyesha katika uchaguzi huu wa makundi ambayo awali yalikuwa yanapingana ya Bw. Chambiri na wenzake kwa hatimaye kupata mgombea aliyekuwa anakubalika na wengi tangu mwaka 2005 na hivyo kufanya kura za CCM zisigawanyike kama ilivyotokea uchaguzi wa 2005 ambapo waasi walimpigia Wangwe kuwakomoa waliompitisha Chambiri. Kwa wana CCM wenye mawazo ya uasi bado, huu ni muda wa kutafakari faida ya walichofanya 2005.

Kimsingi hakuna faida bali hasara ambayo imefanya sasa CCM itumie nguvu ya ziada kiasi cha Bw. Makamba na timu yake kubwa kwenda huko wakitumia helikopta mbili kulikomboa jimbo ambalo awali lilikuwa lao wakasalitiana.
Kwao usaliti unapaswa kuwa fundisho kuwa uhalifu haulipi.

Je, Waitara ataisaidia CHADEMA? Jibu ni hapana. Pamoja na kujitoa kwa mbwembwe za kukataa kuwa mpika chai wa Mwenyekiti wa UVCCM, Bw. Nchimbi, bado Waitara hakuwa tishio katika UVCCM na CCM yenyewe ndio maana akaishia kushika nafasi ya tatu katika kuwania ubunge wa Tarime kwa tiketi ya CCM.

Kimsingi wana Tarime wamempa jibu ambalo hata UVCCM walimpa kwa kumrejesha makao makuu kuwa Karani wakimaanisha kuwa, alikuwa hajaiva kiuongozi. Hatua ya wana CCM Tarime kumpa nafasi ya tatu ilikuwa ni sawa na kumwambia pia hajaiva, ajaribu tena bahati.

Lakini pengine Waitara amejipambanua tu ni kiongozi wa aina gani. Ni mwenye kupenda madaraka ndio maana alisema hawezi kuwa karani wakati elimu yake ni ya Chuo Kikuu na anawazidi makatibu wengine wa UVCCM. Viongozi kama hawa ni hatari, hawaifai UVCCM wala CCM. Pengine wanafaa CHADEMA ndio maana ameenda huko na kukaribishwa kwa mbwembwe zote kama shujaa.

Na kama hivyo ndivyo, ni hatari kuchagua chama cha watu wanaopenda madaraka na wako tayari kumwaga damu kwani Waitara amekaririwa akisema, watalinda kura hata kwa kumwaga damu ili mradi tu lazima washinde. Huyo ndiye aliyekuwa kiongozi wa CCM kimakosa kwani kuna madai awali akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kabwe, walijiunga na CHADEMA alipoona hakupata kitu, akarudi CCM na sasa karejea kulikomfaa tangu awali.

Ni vipi basi wananchi wa Tarime wamsikilize mtu asiye na msimamo, mwenye kutangatanga na mkabila kwani katika malalamiko yake, alilalamikia CCM kukumbatia wageni wa Dar es Salaam kunadi mgombea wa CCM Tarime na kuacha wazawa wa huko bila kujali kuwa, kama suala ni hilo, hata watu wa Tanga wangemlalamikia yeye kuwa Katibu wa UVCCM Tanga wakati ni mtu wa Tarime.

Wakati wanapochagua mbunge, wananchi wa Tarime ambao ni mchanganyiko wa makabila ambao bado wanauguza majeraha ya vita vya koo, Walenchoka na Wanyanchori na hivyo wanajua ubaya wake, wanapaswa kuachana na propaganda za kina Waitara wasijute baadaye.

Alipotangaza kutaka mafisadi washughulikiwe CCM huku viongozi wake wa juu, NEC na CC wakisema chama kama chama hakina mafisadi hadi itakapothibitishwa hivyo na mahakama, Waitara alikuwa anaonesha asivyo na maadili kwa wakubwa wake na wenye akili zao walijua ajenda yake ni umaarufu akidhani umaarufu binafsi unasaidia. Pengine kwa CHADEMA, kwa CCM maarufu ni chama, si mtu.

CCM inabaki kuwa chama chenye taratibu zake, chenye kuheshimu demokrasia ndio maana hata Serikali yake inaheshimu utawala wa sheria lakini kama familia, haikosi watoto watukutu watakaonyea kambi lakini kama mlezi, siku zote haitachoka kuwasamehe wanapokosea na kuwasaidia kuwaonyesha njia ili wajirudi na kutubu. Chama cha aina hiyo ndiyo cha kuchagua siyo vinavyomwaga damu.
 
Huu utafiti umefanywa na Thomas Ngawaiya

Na Godfrey Lutego

Uchaguzi mdogo wa mbunge na Diwani wa jimbo la Tarime mkoani Mara unafanyika kesho huku ushindani mkubwa ukiwa kati ya mgombea wa chama tawala, CCM, Bw. Christopher Kangoye nawa chama cha upinzani, CHADEMA, Bw. Charles Mwera.

......

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na Taasisi ya Utawala bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA), CCM ina nafasi kubwa ya kutwaa jimbo hilo kwa ushindi wa asilimia 65 ikifuatiwa na CHADEMA iliyokuwa inalishikilia inayopewa nafasi ya kupata asilimia 35 na vyama vinavyobaki vinatarajiwa kupata asilimia 5.

.....

Hata hivyo, tathmini hiyo inatofautiana kidogo na tathmini iliyotolewa na gazeti moja likikariri wanaodaiwa kuwa wananchi wa Tarime kuwa CHADEMA itaendelea kutetea jimbo hilo kwa ushindi wa asilimia 50 huku CCM ikipata asilimia 45 na vyama vingine vilivyobaki asilimia 5.

Mwalimu wangu wa hisabati shule ya msingi alinifundisha kuwa

65+35+5 = 105
50+45+5 = 100

Hesabu ya Thomas ni mbovu hapa na hii inaongea kwa nguvu sana kuhusu kila kitu alichoandika hapa. Tanzania hii.......MUNGU tusaidie
 
Mkuu Mugabe
Kumbuka Ngawaiya alikuwa zamani TLP akaasi na kurudi CCM kwa hiyo utafiti alio ufanya sijui yupo Tarime au kwa kuwauliza Makamba,Msekwa na Komba?
Amefanya utafiti akiwa na majibu tayari....
 
Mkuu Mugabe
Kumbuka Ngawaiya alikuwa zamani TLP akaasi na kurudi CCM kwa hiyo utafiti alio ufanya sijui yupo Tarime au kwa kuwauliza Makamba,Msekwa na Komba?
Amefanya utafiti akiwa na majibu tayari....

fidel,

mimi sina tatizo na chama au historia ya Ngawaiya. Mambo ya unazi wa vyama ndiyo yanaturudisha nyuma kila siku Tanzania na Afrika kwa ujumla hivyo sina tatizo na alikotoa majibu ya utafiti wake.

Tatizo liko kwenye math ya Ngawaiya - asilimia 65 kujumlisha asilimia 35 na kisha kujumlisha asilimia 5 - jibu lake linakuwa asilimia 105.

Sijui kuna uwezekano gani wa Tarime kuwa na asilimia 105 na wapiga kura.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom