Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
---daaah, mimi na siasa kweli sawa na maji na paka....!! yaani kitu cha kwanza nilichoona kwenye thread hii ni hiyo avatar ya Mbogela! mnisamehe jamani..... 😉
 
Kura zimeanza kuhesabiwa na kwa taarifa za hivi punde ni kwamba Chadema inaongoza kata 4 kwa asilimia 80 zote za Tarime vijijini
 
Kura zimeanza kuhesabiwa na kwa taarifa za hivi punde ni kwamba Chadema inaongoza kata 4 kwa asilimia 80 zote za Tarime vijijini

duh! That's great.Thanks bro for imformation.
 
mimi nitashangaa kwa sababu sijui kama hila na akili zoote CCM walizotumia wakashindwa,na hata wakiiba halafu wakashinda bado nitawashangaa sana.

Yaani sarakasi zoote zile hadi mtikila kusema na mawe,unadhani ni hali ya kawaida katika siasa kweli? Hadi kumtumia Marehemu kwenye kampeni?

Mkuu ,Mkjj uliona wapi hilo?
 
mimi nitashangaa kwa sababu sijui kama hila na akili zoote CCM walizotumia wakashindwa,na hata wakiiba halafu wakashinda bado nitawashangaa sana.

Yaani sarakasi zoote zile hadi mtikila kusema na mawe,unadhani ni hali ya kawaida katika siasa kweli? Hadi kumtumia Marehemu kwenye kampeni?

Mkuu ,Mkjj uliona wapi hilo?

Asanteni sana wakulu kwa updates hizi, natumai kuna amani na usalama.
 
Hivi Chadema ikishinda kuna mtu atashangaa? it won't be me.

Mimi ni mmoja wa watakao shangaa, ebana CCM si mchezo aise wamecheza michezo yote ya kufuata sheria na rafu kwa sana. hapa watu wa Tarime wanaithibitishia Tanzania kwamba wana msimamo katika maamuzi yao.

Kwa upande mwingine itaonyesha wazi jinsi CCM wasivyoweza kusoma nyakati.
 
Jamani, CCM yote iko Tarime, wakishindwa uchaguzi huu ambao wamecommit resources zao zote including pesa, polisi, serikali ya mkoa, usalama wa taifa bah blah kwa kweli itakuwa pigo la mwaka.

Najaribu kujitahidi kuamini kwamba haki itatendeka, lakini knowing CCM tusubiri matokeo kamili kwa sababu kama tujuavyo trademark ya Nchi yetu ....... Only In Tanzania!!
 
Ccm inaweza kushinda manake baba yao nkapa yuko bagamoyo anapiga ramri toka asubihi mbaka saa hizi lazima washinde
 
tafadhali moderator, usi-move hii thread tuendelee nayo kuepuka kuchanganya mambo, unaweza kuiunganisha baadaye baada ya kutangazwa matokeo

tunaomba mliko tarime muhakikishe kuwa mnatupa kila linaloendelea, wenzenu tangu asubuhi tuko kwenye computer tunachungulia humu. mkitupa habari mapema tutaweza kutoka kidogo kwenye grcery
 
Wakuu Hamad Yusuf,Invisible na Halisi tunaomba kama mmepata updates mtupe wakuu
 
Mwanakijiji,

Kusema kweli mimi ni mmoja kati ya watu watakao shangaa kwa sababu najua wazi CCM wanafikiria nini... USHINDI kwa kila hali. Moelex23 kazungumza vitu vizito sana kiasi kwamba kuamini kwamba Chadema watatangazwa washindi inanipa taabu hata kama ushahidi wote unaonyesha Chadema ni washindi..Kushinda na kutangazwa mshindi ni vitu viwili tofauti mkuu.

Kama nilivyosema ikiwa CCM watakubali kushindwa mara hii tarime basi utakuwa ushindi mkubwa kwa CCM na tume ya uchaguzi kiasi kwamba madhambi yote ya nyuma yatawekwa kando na uchaguzi huu utatumika kama kigezo cha kuonyesha kukomaa kwa demokrasia nchini...
CCM watakuwa washindi wakubwa ktk mambo mengi yatakayofuata..jambo ambalo sii hulka ya Mdanganyika ku plan kitu kisha kusubiri mafao mbeleni..tunataka malipo ya uwekeshaji hapo kwa hapo!..iwe biashara, mapenzi, uchaguzi na kadhalika.. hakuna kitu long term plan kwa mswahili.
 
Huyo ndio msimamizi wa uchaguzi wa tarime mpaka aseme hivyo ? Jamani tusitake kupotosha watu kwa makusudi wewe zitto kwanza unatafutwa na polisi
 
Shalom toka Tarime

Matokeo ni hivi .

Nyamwaga Chadema wako juu na wamesha maliza kuhesabu
Nyanungu Chadema wako juu
Matongo Chadema wako juu

Sirari Chadema wanaongoza kwa kura zaidi ya 500
Bwirege Chadema wamesha ongoza kote
Nyamongo 1 wanaongoza
Nyamongo 2 matokeo bado

Tarime Mjini Chadema wamesha maliza kuongoza na Kiti cha udiwani kiko Chadema Zacharia Peter kaanguka .

Tunangoja majumuisho yote kabisa tuone lakini kwa uharaka hii ndiyo hali toka hapa hotelini kwangu .

Polisi wamesha anza vurugu zao .Maji yanamwagwa na watu wanarudi nyuma hatua moja na kuja mbele hatua 3.Hali ni tete watu zaidi ya 8 wakiwa na maguo ya CCM wamekamatwa na silaha wakienda kuwavamia wale wanao pelekeka matokeo Jimboni kwenyewe na sasa wako ndani .


Asanteni sana na tungoje maamuzi ya mwisho lolote laweza kuwa ndilo jibu .

Viongozi wote wa CCM wamekimbilia Musoma Mjini na wachache wako Tarime .Shangwe zimeanza na askari wameshikwa na butwaa hapa mjini .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom