Kwa wakuu wote JF, kwanza heshima mbele sana, na pia kama mwanachama hai na mkereketwa wa CCM, nitoe heshima zangu nzito kwa kuutambua ushindi wa chama chetu cha taifa cha wananchi yaani Chadema, kwa ushindi mkubwa sana huko jimbo la ubunge la Tarime, infact jana nilikuwa sehemu ambapo pia alikuwepo Mama Migiro, ambaye at one point aliniuliza "...vipi huko JF, Tarime tupo wapi?..." nikamjibu kuwa hatujawahi kuwa popote huko zaidi ya chini, I mean:-
1. CCM tumeshindwa Tarime, vibaya sana tena sana na ni aibu tena kubwa sana, ukijumlisha maovu yote yaliyofanywa huko na baadhi ya viongozi wa CCM ambao nusu yao nimeongea nao leo, kwa kweli ni aibu kubwa sana, and I hope kwamba huu uchaguzi sio min-refferendum ya 2010, maana nina wasi wasi sana kwamba it is a refferendum tena kwa 100% ya uchaguzi wa 2010.
2. Huu ushindi ni ujumbe tosha kwetu CCM, kwamba get rid of rogue leaders kama Makamba, na Msekwa get them out tena now, maana hawa ni kundi la mafisadi, I mean wachawi wako within us kwa sababu hawana uwezo wa kuongoza taifa kwenye level ya chama kinachotawala, sasa nashangaa Rais Kikwete akiwachekea hawa fukuza now!
3. Mwenyekiti Rais Kikwete, sasa baada ya huu ujumbe kusiwe na kuchekeana tena, otherwise tunakwenda down tena kwa kasi kali sana kwa sababu this is a true picture ya what to come mbele ya safari, Republicans waliposhindwa viti vichache tu ndani ya Congress pamoja na kwamba walikua bado ni majority, walimtoa mbio Spika Gingrich, sasa CCM tuache kuechekeana kwa sababu hakuna excuse hapo, CCM nzima ilikuwepo huko Tarime, sasa iliyoshindwa hapa ni CCM sio anybody else!
4. CCM tunapaswa kuwaomba radhi wananchi wa Tarime, kwa sababu nina uhakika kwa 100% kwamba niliyoyasikia kutoka huko yaani maovu yetu ni kweli yamefanyika, lakini simply politics ni kwamba wananchi wamekataa ujinga na uongo period!
5. CCM this time tuna viongozi wabovu sana, tena sana wakumbatiaji wa rushwa na mafisadi, wasiokuwa na uwezo wa kuongoza, wasiokuwa na uwezo wa kuona mbali, I mean Mheshimiwa rais wakati mwingine sijui unapewa ushauri na nani kwamba Msekwa, aliyekuwa spika kwa karibu miaka 15 kiongozi wa chama na serikali kwa miaka karibu 40, halafu siku moja anapigwa chini kisiasa na kukosa kila kitu na kuwa jobless, leo unamuona huyu anafaa kua makamu wako wa kuongoza chama tawala taifa?
- Eti ni mwanasiasa gani wa kweli asiyeweza ku-navigate political fate yake mwenyewe? Sasaa leo unampaje ku-navigate CCM taifa kama sio kufilisika kwa hao washauri wako wa siasa?
- Waziri ameacha jiji halina umeme, anakimbilia kupiga kampeni za uchaguzi hivi hawa wananchi wa Tarime, wanatakiwa kuwa wajinga kiasi gani jamani?
- Tizama akili ya siasa ya Mkamba, hivi kweli unaweza kumtumia Mtikila kushinda uchaguzi wa jimbo la wananchi wenye akili timamu kama Tarime?
6. Hawa ni viongozi gani wa chama ambao hawana hata heshima ndani ya chama chao kutoka kwa viongozi wengine wenzao kwa sababu ninaambiwa kuwa ilifika mahali wakagundua kua hawana uwezo wa kuongoza CCM kushinda huko Tarime, wakaanza kujaribu kuwashawishi baadhi ya viongozi wengine kwenda huko Tarime, lakini hata kusaini hizo barua za kuwaomba wameshindwa badala yake wakajaribu kusingizia kuwa zimeandikwa na kikao cha sekretarieti chini ya mwenyekiti wa CCM, ambaye kila mwananchi anajua kuwa hakuwepo wakati zikiandikwa licha ya hao viongozi waliotumiwa, what kind of leadership is this kama sio a joke?
I mean CCM tumeshindwa this one na it hurts badly, kwa sababu hakuna reasonable excuse hapa, zaidi ya kukosa dira na muelekeo kisiasa na kiuongozi, sasa ni wakati wa viongozi wasiokuwa na uwezo kuwajibika au wawajibishwe, ninasema hivi kwa wanachama wote wa CCM, tusijidanganye hapa kua eti hili ni jimbo moja tu, hapana haba na haba hujaza kibaba period! Huu ni mwanzo tu kama CCM hatujiangalii kwenye kioo, hata 2010 itakuwa aibu kubwa zaidi ya hii,
Na tusidanganyane hapa hii aibu inakwenda straight kwako mwenyekiti, rais wa jamhuri kabla ya mtu yoyote mwingine, ni kwamba tuna viongozi wabovu wasiokuwa na uwezo kabisaa, sasa waondolewe kabla ya aibu zaidi,
Halafu as a nation imefika wakati wa kuliangalia tena suala la ruzuku in general, mimi ninafikiri umefika wakati wa ku- do away na ruzuku kwa sababu zinasaidia one thing only, nacho ni ku-off balance ushindani wa kweli wa kisiasa kwa taifa letu, na kudhoofisha kabisa upinzani wa kweli wa kisiasa nchini iondolewe au itafutwe njia nyingine ya kuleta balance haiwezekani chama kimoja kipate shillingi millioni 99, na vingine millioni 10, mpaka 30 halafu ukategemea kuwepo na ushindani ambao ni balanced na politically heathy kwa taifa.
Kwa kumaliza ninapenda kutoa heshima zangu kwa Chadema, kwa huu ushindi mzito sana, kutoka jimbo la mkoa aliozaliwa Baba wa Taifa letu, mhasisi wa CCM, hiyo ni aibu kubwa sana kwa viongozi wetu wote wa CCM, mlioshirki huko Tarime, shame on you, yaani kwa mara ya kwanza kuona uchaguzi mdogo ambao mmeshindwa hata kumshawishi mwenyekiti wa CCM kushirki, sasa kama mwenyekiti mwenyewe amewashitukia itakuwaje wananchi wa huko? Kwa nini mwenyekiti hakuenda huko? Maana yake ni moja tu kua hawaamini hawa wasaidizi wake, sasa mheshimiwa rais unangoja nini kuwaondoa mara moja?
Again heshima kwa Chadema kwa ushindi wenu mzito, ambao kwa jinsi nilivyoambiwa na waliokuwepo kwa maneno ya kizungu, ilikuwa ni no contest na mimi ninaamini kwa 100% kuwa ni kweli!
Mungu Aibariki Tanzania.