Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Ladslaus,

Pamoja na kwamba sikubaliani na mengi uliyosema hilo hitimisho maana yake ni kwamba tutakuwa tunacheza pata potea kwa kubadilisha uongozi. Sasa swali kwako ni hili, tubaki na huu uongozi ambao kwa hali zote umeoza ama tujaribishe bahati yetu kwa uongozi mpya. Tukiweza kujenga tabia ya kubadilisha uongozi kila ukiboronga, hao watakaokuja wapya watajitahidi wakijua wazi kabisa hatma yao wasipotimiza wajibu. Hii ni kawaida duniani kote kwa nchi makini na ndio njia pekee ya kupata utawala bora.

Kuna wanaCCM wanaoona huu ubovu na wangependa uongozi ndani ya chama ndio ubadilike kama navyosema FMES. Sawa lakini wanasahau kuwa wamekuwa wakibadilisha uongozi ndani ya chama kila baada ya miaka mitano, lakini kila mara uongozi unaofuatia umekuwa mbovu zaidi. Hii maana yake nini - ni kuwa the party is rotten to the core. Tumesema mara nyingi humu kuwa huwezi kuogelea kwenye tope ukatoka msafi, na mimi naongezea kuwa huwezi kuishi kwenye uvundo usinuke.

UFISADI kwenye CCM imekuwa way of life ikilindwa na dola. Hii ndiyo maana kuna sauti za wanaCCM wanaomtetea JK na kusema kwamba kazungukwa na viongozi wanaompotosha. Jambo hili haliingii akilini na ukweli ulio sahihi ni kuwa CCM haisafishiki tena - kansa yake imeenea mwili mzima. Ambao hawajaathirika hawawezi kuendelea kubaki humo kama alivyoonyesha mfano Kijana Waitara. Ladslaus, muunge mkono Waitara kwa kuipa mgongo CCM na kupaaza sauti ya bye, bye na tufungue ukurasa mpya.

Mkuu Mag3;
Nimefuatilia maelezo yako kwa umakini mkubwa, lakini sikubaliani nawe kwenye mambo mengi.
Ufisadi ndani ya CCM sio 'way of life' kama ulivyosema bali ni wa baadhi ya 'wanachama' wachache kama walivyo mafisadi kwenye vyama vingine vya siasa hapa Tanzania (kwa sasa wakiongozwa na Mchungaji mwenzangu Mtikila).
Ni kweli kuwa Rais wetu (ambaye ni mwenyekiti wa CCM) ni MSAFI isipokuwa amezungukwa na baadhi ya washauri wanaompotosha.
Ufisadi ndani ya CCM sio sawa na kansa ambayo imeenea mwili mzima, bali inaweza kusafishika kwa kuwafurusha mafisadi wote.
Mie kuihama CCM kama Kijana Waitara haitawezekana maana hata Waitara tunamsubiri atarudi CCM muda mfupi ujao.

Napenda pia kukukumbusha suala la Zambia, ambapo Chiluba alikuwa fisadi lakini alipoingia Levy Mwanawasa (RIP) madarakani, ambaye alikuwa mtu wa karibu sana na Chiluba, alibadili chama na kuwashughulikia mafisadi wote akiwemo Chiluba.

Mwisho napenda ufahamu kuwa CCM bado ni Chama makini kuliko vyote hapa Tanzania; Karibu sana CCM uwe mmoja wa wanachama wake.
 
QUOTE=Field Marshall ES;302601]Kwa wakuu wote JF, kwanza heshima mbele sana, na pia kama mwanachama hai na mkereketwa wa CCM, nitoe heshima zangu nzito kwa kuutambua ushindi wa chama chetu cha taifa cha wananchi yaani Chadema, kwa ushindi mkubwa sana huko jimbo la ubunge la Tarime, infact jana nilikuwa sehemu ambapo pia alikuwepo Mama Migiro, ambaye at one point aliniuliza "...vipi huko JF, Tarime tupo wapi?..." nikamjibu kuwa hatujawahi kuwa popote huko zaidi ya chini, I mean:-

1. CCM tumeshindwa Tarime, vibaya sana tena sana na ni aibu tena kubwa sana, ukijumlisha maovu yote yaliyofanywa huko na baadhi ya viongozi wa CCM ambao nusu yao nimeongea nao leo, kwa kweli ni aibu kubwa sana, and I hope kwamba huu uchaguzi sio min-refferendum ya 2010, maana nina wasi wasi sana kwamba it is a refferendum tena kwa 100% ya uchaguzi wa 2010.

2. Huu ushindi ni ujumbe tosha kwetu CCM, kwamba get rid of rogue leaders kama Makamba, na Msekwa get them out tena now, maana hawa ni kundi la mafisadi, I mean wachawi wako within us kwa sababu hawana uwezo wa kuongoza taifa kwenye level ya chama kinachotawala, sasa nashangaa Rais Kikwete akiwachekea hawa fukuza now!

3. Mwenyekiti Rais Kikwete, sasa baada ya huu ujumbe kusiwe na kuchekeana tena, otherwise tunakwenda down tena kwa kasi kali sana kwa sababu this is a true picture ya what to come mbele ya safari, Republicans waliposhindwa viti vichache tu ndani ya Congress pamoja na kwamba walikua bado ni majority, walimtoa mbio Spika Gingrich, sasa CCM tuache kuechekeana kwa sababu hakuna excuse hapo, CCM nzima ilikuwepo huko Tarime, sasa iliyoshindwa hapa ni CCM sio anybody else!

4. CCM tunapaswa kuwaomba radhi wananchi wa Tarime, kwa sababu nina uhakika kwa 100% kwamba niliyoyasikia kutoka huko yaani maovu yetu ni kweli yamefanyika, lakini simply politics ni kwamba wananchi wamekataa ujinga na uongo period!

5. CCM this time tuna viongozi wabovu sana, tena sana wakumbatiaji wa rushwa na mafisadi, wasiokuwa na uwezo wa kuongoza, wasiokuwa na uwezo wa kuona mbali, I mean Mheshimiwa rais wakati mwingine sijui unapewa ushauri na nani kwamba Msekwa, aliyekuwa spika kwa karibu miaka 15 kiongozi wa chama na serikali kwa miaka karibu 40, halafu siku moja anapigwa chini kisiasa na kukosa kila kitu na kuwa jobless, leo unamuona huyu anafaa kua makamu wako wa kuongoza chama tawala taifa?

- Eti ni mwanasiasa gani wa kweli asiyeweza ku-navigate political fate yake mwenyewe? Sasaa leo unampaje ku-navigate CCM taifa kama sio kufilisika kwa hao washauri wako wa siasa?

- Waziri ameacha jiji halina umeme, anakimbilia kupiga kampeni za uchaguzi hivi hawa wananchi wa Tarime, wanatakiwa kuwa wajinga kiasi gani jamani?

- Tizama akili ya siasa ya Mkamba, hivi kweli unaweza kumtumia Mtikila kushinda uchaguzi wa jimbo la wananchi wenye akili timamu kama Tarime?

6. Hawa ni viongozi gani wa chama ambao hawana hata heshima ndani ya chama chao kutoka kwa viongozi wengine wenzao kwa sababu ninaambiwa kuwa ilifika mahali wakagundua kua hawana uwezo wa kuongoza CCM kushinda huko Tarime, wakaanza kujaribu kuwashawishi baadhi ya viongozi wengine kwenda huko Tarime, lakini hata kusaini hizo barua za kuwaomba wameshindwa badala yake wakajaribu kusingizia kuwa zimeandikwa na kikao cha sekretarieti chini ya mwenyekiti wa CCM, ambaye kila mwananchi anajua kuwa hakuwepo wakati zikiandikwa licha ya hao viongozi waliotumiwa, what kind of leadership is this kama sio a joke?

I mean CCM tumeshindwa this one na it hurts badly, kwa sababu hakuna reasonable excuse hapa, zaidi ya kukosa dira na muelekeo kisiasa na kiuongozi, sasa ni wakati wa viongozi wasiokuwa na uwezo kuwajibika au wawajibishwe, ninasema hivi kwa wanachama wote wa CCM, tusijidanganye hapa kua eti hili ni jimbo moja tu, hapana haba na haba hujaza kibaba period! Huu ni mwanzo tu kama CCM hatujiangalii kwenye kioo, hata 2010 itakuwa aibu kubwa zaidi ya hii,

Na tusidanganyane hapa hii aibu inakwenda straight kwako mwenyekiti, rais wa jamhuri kabla ya mtu yoyote mwingine, ni kwamba tuna viongozi wabovu wasiokuwa na uwezo kabisaa, sasa waondolewe kabla ya aibu zaidi,

Halafu as a nation imefika wakati wa kuliangalia tena suala la ruzuku in general, mimi ninafikiri umefika wakati wa ku- do away na ruzuku kwa sababu zinasaidia one thing only, nacho ni ku-off balance ushindani wa kweli wa kisiasa kwa taifa letu, na kudhoofisha kabisa upinzani wa kweli wa kisiasa nchini iondolewe au itafutwe njia nyingine ya kuleta balance haiwezekani chama kimoja kipate shillingi millioni 99, na vingine millioni 10, mpaka 30 halafu ukategemea kuwepo na ushindani ambao ni balanced na politically heathy kwa taifa.

Kwa kumaliza ninapenda kutoa heshima zangu kwa Chadema, kwa huu ushindi mzito sana, kutoka jimbo la mkoa aliozaliwa Baba wa Taifa letu, mhasisi wa CCM, hiyo ni aibu kubwa sana kwa viongozi wetu wote wa CCM, mlioshirki huko Tarime, shame on you, yaani kwa mara ya kwanza kuona uchaguzi mdogo ambao mmeshindwa hata kumshawishi mwenyekiti wa CCM kushirki, sasa kama mwenyekiti mwenyewe amewashitukia itakuwaje wananchi wa huko? Kwa nini mwenyekiti hakuenda huko? Maana yake ni moja tu kua hawaamini hawa wasaidizi wake, sasa mheshimiwa rais unangoja nini kuwaondoa mara moja?

Again heshima kwa Chadema kwa ushindi wenu mzito, ambao kwa jinsi nilivyoambiwa na waliokuwepo kwa maneno ya kizungu, ilikuwa ni no contest na mimi ninaamini kwa 100% kuwa ni kweli!

Mungu Aibariki Tanzania.
[/QUOTE]

Mzee FMES,

Nimefurahishwa sana na uwazi wako, wa kukubali kushindwa; maneno yako ni mazito sana hasa kama kweli wewe ni mwana CCM damu. Kama wanasiasa wetu wote hasa walioko CCM ambao ndio wana madaraka wangekuwa na ubongo wa aina yako, nchi hii ingekuwa njiani kuelekea maendeleo ya uhakika.

Ingawa sikupata rekodi zote za uchaguzi wa Tarime, nilikatishwa tamaa kabisa pale Msekwa alipoamua kumwambia Rais aidhinishe matumizi ya nguvu za dola kwa ajili ya kuifaidisha CCM katika uchaguzi ule, na nadhani mojawapo ya post zangu za mwisho mwisho mwisho hapa ilikuwa ni katika kulaani matumizi hayo mabaya ya nguvu za dola. Baadaye kumbe rais akaingia mkenge kwa kuamua matumizi nguvu za dola kuwadhibiti wapinzani na wanachi wa Tarime kwa jumla; kajiwekea Mbeya nyingine tena kwenye utwala wake.


Sikutegemea kuwa chama kongwe kama CCM wangeshindwa kujenga nguvu za hoja kuwashawishi wananchi wawape kura zao, badala yakle wakaamua kutumia nguvu za mabavu bila hoja wakidhani zitawatikisa wananchi ili wawape kura bila kufikiri maana ya kura hizo.

Angalia, mimi nimekaa Tarime pale kwa mwaka mmja nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya Sabasaba; ninawajua sana watu wa Tarime, ukiwaletea ujinga wanakujibu ujinga papo kwa papo wakisema "ARIA". Kama walivyo watu wa wengi wa mkoa wa mara, jamaa hawa ni liberal kweli jkweli. Laiti kama watanzania wote tungekuwa kama watarime tungekuwa tumeshakomboka kutoka kwenye makucha ya wanasiasa uchwala wanautumia ruzuku tunazowapa kutunyanyasa wanachi hawa hawa tuliowapa dhamana hiyo.
[
 
Vuguvugu kama hili lililoonyeshwa Tarime lilikuwepo pia mwaka 1995 wakati huo likiongozwa na Mrema na NCCR aliyokuwa ameipa UHAI mpya baada ya kujiunga nayo akitokea CCM.
Hili la sasa litadumu? Kuna sababu yoyote kuamini kwamba sasa kuliko ilivyokuwa 1995 vuguvugu hili ni la WANANCHI na sio la VIONGOZI?
CCM ya sasa imemalizika kiasi hiki kwa sababu gani?
 
Msekwa ahoji matumizi ya helkopta Tarime

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Bw. Pius Msekwa, saa chache baada ya chama chake kushindwa kwenye uchaguzi wa ubunge na udiwani Tarime amekiri kushindwa na katika kutafakari, anahoji masuala kadhaa kama gharama kubwa za uendeshaji wa kampeni yakiwamo matumizi ya helikopta.

Bw. Msekwa alitoa maoni yake hayo katika makala yake ya kisomi aliyoiita "Reflections on the Tarime by-election," (Tafakuri juu ya uchaguzi mdogo wa Tarime) iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari jana.

"Vita ya uchaguzi wa Tarime CCM imeshaipoteza na CHADEMA ndio wameshinda. Wapiga kura wa Tarime wamenena. CCM inakubali matokeo hayo na kukubali kushindwa," alisema Bw. Msekwa akinukuu matukio mbalimbali kutoka vitabu vya mwanafasihi, William Shakespear katika sehemu kubwa ya makala yake hayo.

Katika makala hayo, zaidi Bw. Msekwa anasisitiza umuhimu wa kukitumia kipindi hiki cha baada ya uchaguzi kutafakari masuala na mafunzo muhimu kutokana na kampeni hizo.

Moja ya masuala yanayoonesha kumkera mwanasiasa huyo mkongwe aliyepata pia kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Spika wa Bunge, ni suala la gharama kubwa zinazotumika kwenye uchaguzi mdogo kama wa Tarime.

"Hata kama tutaliangalia suala hili kwa kutazama yale matumizi yanayoonekana kwa nje pekee, kama vile idadi kubwa ya wapambe wa kampeni, hivyo kuhitaji matumizi ya magari mengi zikiwamo helikopta za kukodi, inaweza kuthibitika kuwa gharama za uchaguzi kwa vyama, iwe CCM au CHADEMA ni kubwa," anaandika.

Anahoji pia vurugu zilizojitokeza kwenye kampeni hizo na kusema tangu katika kipindi chake alichofanya kazi chini ya Mwalimu Nyerere, hakuwahi kuona kampeni za vitisho kama za Tarime.

"Kwa nini basi kiti hiki kimoja tu kipiganiwe kiasi hiki, ikawa ni suala la kufa au kupona-wakati kwa hakika kiti hicho hakiathiri sana uwiano wa wingi wa wabunge bungeni?," anahoji.

Pamoja na kupendekeza masuala kadhaa, ikiwamo haja ya kutumia zaidi nafasi kwa kuangalia pia uwiano wa jinsia bungeni, Bw. Msekwa anashauri wanachama wenzake wa CCM kukubali matokeo.

"Kwa upande wetu, tusahau yaliyopita, tugange yajayo. Tukiwa wanasiasa, viongozi wa CCM na wanachama wake, tunapaswa sasa kuanza kufikiria uchaguzi ujao.

"Tunapenda kusisitiza kutambua uamuzi wa wapiga kura wa Tarime na tunatumaini kuwa watarejesha imani zao na kutuunga mkono katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na wa baada ya hapo," anasema katika makala hayo ya kurasa saba yaliyoandikwa katika lugha ya Kiingereza.
 
Na bado walimu jana walisema 2010,kura ni kwa CHADEMA.Walinyoosha vidole viwili juu,na kuwaambia CCM na Serikali isubiri kipigo kikali 2010

Gazeti la Majira
 
Safi..
Ingawa huyo aliyeandika na kuitafsiri amechagua yale tu aliyoyapenda, nina hakika taarifa ya kurasa saba itakuwa imebeba mambo mengi ya msingi katika suala zima la chaguzi za sasa hapa Tz
 
.Msekwa ameona hayo baada ya CCM kushindwa? Sitaki kuamini kuwa suala la CCM nao kuamua kukodi helikopta lilikuwa siri kwamba hakujua huo mkakati nadhani kama alijua kuwa ni gharama angeweza kuwashauri wenzake waache kukodi helikopta kwani hiyo si pesa ya CCM ni pesa za watanzania walipa kodi ambazo zingeweza kutumika katika kutoa huduma muhimu za jamii vijijini ambako mpaka leo kuna baadhi ya wilaya kuna shule za msingi wanafunzi wake wanakaa sakafuni na zahanati hazina dawa. Lakini alinyamaza kimya na pia alikuwa anapanda hizo helikopta hakujua hilo?

Suala la vitisho na vurugu Tarime wao CCM walichangia kwa kiasi kikubwa kutokana kwanza na tabia yao ya kucheza michezo michafu kuanzia kwenye kampeni , upigaji kura hadi kwenye matokeo. So watu walikuwa wanajihami kabisa na hiyo michezo yao. Lakini akumbuke pia kuwa uwamuzi wa kumwaga polisi wengi Tarime kulichangia pia kuvuruga utulivu.Watu walitishwa bila sababu ya msingi na lazima mtu atajiuliza kwa nini polisi wengi kiasi kile na yeye Msekwa aliwahi kutamka kuwa atamwambia Mwenyekiti wake Kikwete amuru polisi zaidi wapelekwe Tarime. Ina maana alishindwa kutumia akili ya kawaida tu kuwa suala halikuwa kujaza polisi bali CCM kujipambanua kwa wanatarime na kujisafisha na michezo yao michafu angalau jamii ione kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki?

Tarime yaweza kuwa ni mwanzo tu, lakini huko tuendako hali yaweza kuwa ngumu zaidi kwa CCM na viongozi wao endapo kale katabia ka usanii kwenye chaguzi hawataacha. Tunashuhudia hali zanzibar ilivyo kuhusu muafaka. Nina imani hali isingekuwa kama ilivyo sasa kama CCM wangekuwa fair katika chaguzi zinazofanyika huko. Msekwa akumbuke watanzania wa leo si wale wa miaka ya "Zidumu fikra za Mwenyekiti" hata kama anatoa fikra mbovu!!!

Wameshatandikwa ngumi za macho warudi wakajiulize na wajipange kwa 2010 wakiwa wasafi kwanza hapo wanaweza kuepukana na aibu kama iliyowakumba Tarime. Nina imani kama CCM wangeshinda uchaguzi wa Tarime Msekwa asingekumbuka suala la gharama za kukodi helikopta na vitisho na vurugu zilizotokea hadi watu kutiana vilema sana sana wangekuwa Serengeti au Nguldoto kujipongeza na mafisadi wao...
 
Pius Msekwa namuuliza swali hilo nani wakati jibu analo? Ndo hayo ya kutufanya sisi WaTz mazumbukuku na viongozi wetu.

Anataka kutuambia haujui yale mashangingi yaliyosaidia kampeni za CCM ni mali ya nani? Ina maana hajui zile helkopta 2 za CCM zimelipiwa na nani?
Anataka haju Malzi ya Polisi aliomwomba JK awapeleke huko TArime walilipiwa na nani?
Amuulize Makamba!
 
mbona anaonge kama vilie ahusiki.... jeshi lote lile la polisi lilikuwa kwa garama ya nani? hela zetu walipa kodi zinatumiwa vibaya na serikali ya CCM
 
Polisi wafurahia Chadema kushinda

Na Mussa Juma, Tarime

POLISI ambao walionekana kuwa maadui wakubwa wa vijana waliokuwa wakiishabikia Chadema wakati wote wa kampeni za uchaguzi wa mbunge na diwani wa Tarime, jana walikuwa wenye furaha baada ya purukushani za uchaguzi kutulia.

Mji wa Tarime jana ulirejea katika hali yake ya kawaida baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi yaliyompa Charles Mwera ubunge wa jimbo la Tarime kwa tiketi ya Chadema, na John Heche udiwani wa kata ya Tarime Mjini kwa tiketi ya chama hicho.

Na matokeo hayo yalikuwa ahueni kwa askari polisi hao ambao walifanya kazi kubwa ya kudhibiti vijana wa Chadema waliokuwa kwenye harakati nyingi wakati wa kampeni kiasi cha wakati fulani kutulizwa kwa mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na hata risasi kufyatuliwa hewani.

"Sisi tumefurahi sana Chadema kushinda kwani kama wangeshindwa

ingebidi tukae hapa kwa zaidi ya wiki mbili tena ili kulinda amani na

lolote lingetokea kutokana na hali ya hapa Tarime," alisema askari mmoja toka mkoani Mwanza.

Askari mwingine kutoka mkoa wa Arusha alisema wamefurahia ushindi wa Chadema kwa kuwa utawafanya waondoke Tarime ambako usalama wao ulikuwa mdogo na hali yao ya maisha kuwa mbaya kutokana na kupewa posho ya Sh1,000 tu kwa siku.

"Bwana sisi kesho tunaondoka tutakutana Arusha... maisha ya Sh1,000 kwa siku yametushosha na kwa kuwa Chadema wameshinda hakuna kazi tena hapa," alisema askari huyo.

Karibu polisi 400 walipelekwa Tarime kusimamia usalama kwenye eneo hilo, ambalo kulipuka kwa vurugu wakati wowote ule ni kitu cha kawaida.

Baadhi ya askari walijeruhiwa kwa mawe wakati wakipambana na vijana waliokuwa wakiandamana mitaani wakati wa kutoka kwenye mikutano ya kampeni na wakati wa kushangilia matokeo.

Askari hao walipelekwa wilayani humo kutokana na kutegemewa kulipuka kwa vurugu


source: mwananchi
 
Kwanza naomba kukiri mimi sio mwanachama wa chama chochote ila ni mshabiki wa demokrasia ya kweli hivyo nimefurahishwa na walichofanya wanatarime kwamba wananchi wakiamua inawezekana.

Positionn ya Mhe. Makamba kama KM-CCM ni strategic hakuna asiejua elimu, uwezo na busara za Mzee Makamba. Niliamini amewekwa hapo ili awe ni zuga tuu huku masterling wakiendesha chama. Kumbe zuga kaachiwa kuendesha kiukweli kweli!. Hayo ndiyo matokeo yake.

Kinachohitajika 2010 ni awareness campaign kubwa nchi nzima kuhamasisha spirit ya kuwachagua viongozi bora bila kujali vyama wala pesa.

Watanzania wote wa maeneo yote wawe na msimamo wa
Nini wanachotaka.
Tatizo maeneo mengi haswa yale yenye umasikini uliokithiri hayana msimamo. Nilishuhudia mgombea mmoja wa upinzani ameleta maendeleo makubwa jimboni kwake na kujihakikishia ushindi. Siku ya mwisho ya kampeni lilimwaga pilau la bure la kufa mtu na kila mtu alipewa 1000 ya soda na nauli. Kesho yake ni kupiga kura. Matokeo alishinda aliyetoa shibe ya siku moja.

Hivyo 2010 kazi ipo ila Tarime ni ishara njema. Wapenda demokrasia wangependa kuona mabadiliko tatizo wanajikuta there is no serious oposition hivyo kuliko kupoteza kura za urais, unaona bora umpe mgombea wa CCM anayeonyesha seriousness. Wapinzani wakiungana wakasimamisha mgombea mmoja mmoja tangu urais mpaka udiwani watanzania watawaamini na 2010 CCM itang'oka!.
 
Polisi wafurahia Chadema kushinda

Na Mussa Juma, Tarime

POLISI ambao walionekana kuwa maadui wakubwa wa vijana waliokuwa wakiishabikia Chadema wakati wote wa kampeni za uchaguzi wa mbunge na diwani wa Tarime, jana walikuwa wenye furaha baada ya purukushani za uchaguzi kutulia.

Mji wa Tarime jana ulirejea katika hali yake ya kawaida baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi yaliyompa Charles Mwera ubunge wa jimbo la Tarime kwa tiketi ya Chadema, na John Heche udiwani wa kata ya Tarime Mjini kwa tiketi ya chama hicho.

Na matokeo hayo yalikuwa ahueni kwa askari polisi hao ambao walifanya kazi kubwa ya kudhibiti vijana wa Chadema waliokuwa kwenye harakati nyingi wakati wa kampeni kiasi cha wakati fulani kutulizwa kwa mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na hata risasi kufyatuliwa hewani.

"Sisi tumefurahi sana Chadema kushinda kwani kama wangeshindwa

ingebidi tukae hapa kwa zaidi ya wiki mbili tena ili kulinda amani na

lolote lingetokea kutokana na hali ya hapa Tarime," alisema askari mmoja toka mkoani Mwanza.

Askari mwingine kutoka mkoa wa Arusha alisema wamefurahia ushindi wa Chadema kwa kuwa utawafanya waondoke Tarime ambako usalama wao ulikuwa mdogo na hali yao ya maisha kuwa mbaya kutokana na kupewa posho ya Sh1,000 tu kwa siku.

"Bwana sisi kesho tunaondoka tutakutana Arusha... maisha ya Sh1,000 kwa siku yametushosha na kwa kuwa Chadema wameshinda hakuna kazi tena hapa," alisema askari huyo.

Karibu polisi 400 walipelekwa Tarime kusimamia usalama kwenye eneo hilo, ambalo kulipuka kwa vurugu wakati wowote ule ni kitu cha kawaida
.

Baadhi ya askari walijeruhiwa kwa mawe wakati wakipambana na vijana waliokuwa wakiandamana mitaani wakati wa kutoka kwenye mikutano ya kampeni na wakati wa kushangilia matokeo.

Askari hao walipelekwa wilayani humo kutokana na kutegemewa kulipuka kwa vurugu


source: mwananchi


Serikali isiwaondoe Polisi hao Tarime itakuwa ni kutowatendea haki wanaTArime na WaTz kwa ujumla. Serikali ikumbuke kuwa iliwaambia WaTz kuwa Askari wale wamepelekwa kutuliza mapigano ya Kikoo huko Tarime na si kwa ajili ya Uchaguzi.
 
Msekwa unahoji baada ya kushindwa?
Mbona huku hoji wakati zinakuja?
Mbona huku hoji kule Kiteto mliko peleka 2 nako?
Kweli mfa maji haishi kutapa tapa.
 
Hata kama tutaliangalia suala hili kwa kutazama yale matumizi yanayoonekana kwa nje pekee, kama vile idadi kubwa ya wapambe wa kampeni, hivyo kuhitaji matumizi ya magari mengi zikiwamo helikopta za kukodi, inaweza kuthibitika kuwa gharama za uchaguzi kwa vyama, iwe CCM au CHADEMA ni kubwa," anaandika.

Anahoji pia vurugu zilizojitokeza kwenye kampeni hizo na kusema tangu katika kipindi chake alichofanya kazi chini ya Mwalimu Nyerere, hakuwahi kuona kampeni za vitisho kama za Tarime.

"Kwa nini basi kiti hiki kimoja tu kipiganiwe kiasi hiki, ikawa ni suala la kufa au kupona-wakati kwa hakika kiti hicho hakiathiri sana uwiano wa wingi wa wabunge bungeni?," anahoji.

Huyu naye anyamaze tu, haya si maswali ya kuulizwa na kiongozi wa CCM aliyeshiriki kuwaita polisi wakati wa uchaguzi kuthibiti wananchi wasiounga mkono chama chake, Haya si maneno ya kusemwa na kiongozi wa chama cha CCM kilichotumia shillingi billioni moja kwa uchaguzi mdogo kama huu,

Exactly anataka kusema nini kwamba yeye hakuhusika na maamuzi ya matumizi ya dola na mapesa yote hayo ndani ya chama chake? In the absence ya mwenyekiti wake huko Tarime nani aliyekuwa bosi wa kampeni za CCM kama sio yeye?

Mimi nilifikiri atazungumzia nani aliyempeleka Mtikila huko, na kwamba wananchi wamekataa siasa za ubabaishaji na ufisadi ambao yeye ni mmoja wa viongozi wakumbatiaji wake ndani ya CCM, huyu akubali ukweli kwamba wananchi huko wamekataa ujinga period!
 
Askari hao wameonyesha ni wavivu kiasi gani, mtu unaposhangilia kupungua kwa majukumu yako ya kawaida ni dalili tosha ya uvivu.
 
Whatever people say this oldman is held in high esteem by many of us and he is talking as an outsider because he is,CCM has been hijacked by people of Makamba's type who talk and think later.This defeat may be good for CCM because it may mean people like Msekwa having a say in how to run the party.
 
Mkuu Mwikimbi, heshma kwako.
kama inawezekana tuambatishie hiyo makala ya Mh. Pius Msekwa 'in .pdf' format.
Stay blessed.
 
Whatever people say this oldman is held in high esteem by many of us and he is talking as an outsider because he is,CCM has been hijacked by people of Makamba's type who talk and think later.This defeat may be good for CCM because it may mean people like Msekwa having a say in how to run the party.

Nadhani sasa wataanza kumkumbuka Phillip Mangula....na jinsi alivyokuwa anapinga timu ya wanamtandao ku-take over chama.....
 
Baada ya kushindwa sasa anafutwa mchawi nani ,wakati alikuwa mmojawapo wa waliokuwa wanawanga kuua haki ya kikatiba ya watu kuchagua wanayemtaka.Nadhani Tinga tinga anawacheka sana,Nguvu nyingi akili sifuri.Bado sasa kule Jimbo la Biharamulo Magharibi,maana Phares KABUYE naye anawasubiri kwa hamu sana.Tangazeni uchaguzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom