Uchaguzi 2020 Ubunge wa CCM wageuka kituko, Komandoo Mashimo naye atangaza nia Jimbo la Kibamba

Uchaguzi 2020 Ubunge wa CCM wageuka kituko, Komandoo Mashimo naye atangaza nia Jimbo la Kibamba

Dhihaka hizi ni matokeo ya jinsi Bunge la 11 lilivyoendeshwa chini ya kiwango kiasi kutoa picha kuwa haihitaji weledi tena kuwa Mbunge wa CCM. Tulishudia Bunge muhimu la bajeti likigeuzwa uwanja wa mipasho,wenye hoja za msingi wakizomewa na hadi kutolewa nje ya Bunge bali wenye mipasho,matusi na kejeli kwa wapinzani wakipewa airtime ya kutosha huku wakishangiliwa. Picha iliyochorwa ni kuwa kuwa Mbunge wa CCM ni kazi nyepesi sana ujue kutukana wapinzani, kusifia watawala, kugonga meza, kuzomea na mwisho kusema ndiyooooooo,nani atashindwa?
 
Bado nabii Tito wakamilishe usajiri..
.
1592413160144.jpg
 
Kama moja sifa ya kuwa Mbunge ni kujua kusoma na kuandika, sioni tatizo kwa huyo jamaa kutia nia.

Ila pia bunge hili lililoisha limevutia aina aina hii ya watu. Bunge la Samwel Sitta, na Makinda lisingevutia huu ujinga.
 
Watu wengi wameshtuka na kutambua kuwa Gwajima ni tapeli anayetumia neno la Mungu kutimiza uovu wake. Sasa ameamua kutafuta chanzo mbadala cha mapato.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama wanasema kuna manabii wa uongo Gwajima sidhani kama atakosa, waumini wake msinishambulie jmn
 
Back
Top Bottom