Deus J. Kahangwa
Senior Member
- Jan 7, 2013
- 189
- 122
DEUSDEDIT JOVIN KAHANGWA ni majina yangu matatu. Kupitia ukurasa huu, napenda kutangaza rasmi kwamba, ifikapo Oktoba 2015, nitagombea tena ubunge wa Karagwe, kupitia CHADEMA. Dhamira yangu inatokana na sababu sita zinazohusiana na: Kanuni za Kikatiba, Wasifu wa Mgombea, Ajenda ya Uchaguzi, Timu ya Kampeni, Uwezo wa Kifedha, na Akiba ya Kura. Sababu hizi tunaweza kuzikumbuka kwa kutumia kifupi "KWATUA."
1. KANUNI ZA KIKATIBA
Sifa za kikatiba kama zinavyotajwa katika ibara ya 67 ya Katiba ya Tanzania (1977) ninazo.
Mimi ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa; ninao umri zaidi ya miaka ishirini na moja; najua kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza; ni mwanachama wa chama cha siasa kiitwacho CHADEMA; na katika kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe ya uchaguzi kurudi nyuma nitakuwa sijawahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
Pia, mimi ninayo akili timamu; katika kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi nitakuwa sijapata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu; sikusudii kugombea kiti cha ubunge na Rais kwa mpigo; na kuna yamkini kubwa kwamba nitapendekezwa na CHADEMA kupeperusha bendera ya ubunge.
2. WASIFU WA MGOMBEA
Kifamilia, nilizaliwa Aprili 16, 1972. Baba ni Jovin Kahangwa na mama Matilda Zimbeiya. Makazi ya familia yetu ni Kitongoji Katamobwa, Kijiji Kibona, Kata Kanoni, Wilayani Karagwe. Wazazi wangu ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
Katika familia hii, kuna watoto 11, wote tuko hai, na kila mmoja ameanzisha familia yake, isipokuwa watoto watatu wa mwisho.
Kielimu, nimesomea taasisi zifuatazo: Shule ya Msingi Kibona, Karagwe (1981-87); Seminari ya Katoke, Biharamulo (1988-91); Sekondari ya Tambaza, Dar es Salaam (1992-94); na Chuo Kikuu Dar es Salaam (1995-98). Tambaza nilisomea Fizikia, Kemia na Hisabati (PCM). Na Chuo Kikuu nilisomea shahada ya Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Kiajira, nimefanya kazi zifuatazo: Ualimu katika Shule ya Mtakatifu Anthony, Dar es Salaam (1999); Usanifu wa Programu za Kompyuta katika kampuni ya CATS (T) Ltd, Dar es Salaam (2000); Ualimu katika Shule ya Shaaban Robert (2001); Uhadhiri katika Chuo cha LearnIT, Dar es Salaam (2002-03); Usanifu wa Programu za Kompyuta katika kampuni ya Simu (TTCL), Dar es Salaam (2003-2008); Uhadhiri katika Chuo cha IIT, Dar es Salaam (2009-10); Ualimu katika Shule ya Karaseco, Karagwe (2013-14); na kwa sasa ni mwajiriwa wa gazeti la MAWIO.
Kiuongozi, tangu 2007 nimekuwa Mkurugenzi wa Hexadecalogue Ltd ya Dar es Salaam. Kampuni hii inajishughulisha na ushauri, utafiti, upangaji, uendeshaji, na usimamizi wa miradi ya TEHAMA.
Pia, kwa miaka 10 iliyopita nimekuwa mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania (UNA Tanzania) yenye ofisi zake Dar es Salaam.
Kadhalika, kwa miaka mitano nilipokuwa mwajiriwa wa TTCL nilikuwa katibu wa Tawi la TEWUTA (Chama cha Wafanyakazi wa TTCL). Tawi hili liko Makao Makuu ya TTCL, katika jengo la Extelecoms, Mtaa wa Samora, Jijini Dar es Salaam.
Kidini, mimi ni Mkristo wa Madhehebu Katoliki. Nilibatizwa, kupata kumunio, kipaimara na kurudia maagano ndani ya Parokia ya Rwambaizi, Jimbo la Kayanga, Karagwe.
Nilipokuwa kidato cha tano Tambaza, nilikuwa Katibu wa TYCS katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Nilipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilikuwa Katibu wa IMCS Kanda ya Tanzania. Na tangu wakati huo nimekuwa natekeleza utume wangu kama mlei kupiti chama cha kitume cha CPT.
Kiuandishi, tangu 2003 nimekuwa mwandishi wa magazeti ya Tumaini Letu, Rai, Mtanzania, Tanzania Daima, na sasa Mawio. Pia nimeandika vitabu viwili, "Ilani ya Uchaguzi inayojali(2005)" na "An Empowerment Election Manifesto (2005)" kupita kampuni ya uchapaji ya Ruvu Publishers, Dar es Salaam.
3. AJENDA YA UCHAGUZI
Wilaya ya Karagwe inao wakazi wapata laki nne. Kuna wakulima, wafugaji na wavuvi. Kuna ardhi ya kutosha. Pia, kutokana na ukweli kwamba iko katika ukanda wa maziwa makuu, yaani Magharibu mwa Ziwa Viktoria, mvua zinanyesha mara mbili kwa mwaka. Kwa hiyo, ilitarajiwa kwamba iwe miongoni mwa wilaya zenye maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru iliyopita. Hata hivyo, hali ni tofauti.
Kuhusu Afya, zahanati, vituo vya afya na mahospitali mengi wilayani Karagwe vinayo matatizo mengi. Hakuna madawa mahospitalini, wahudumu hawatoshi, wagonjwa wanalala sakafuni, vituo vya afya viko umbali mrefu kuliko kawaida. Pia katika miaka 50 uhuru bado hakuna hospitali ya wilaya. Hivyo, nitapigania upatikanaji wa madawa mahospitalini, wahudumu wa kutosha, vitanda vya wagonjwa, ujenzi wa vituo vya afya vilivyo katika umbali mfupi. Pia nitahakikisha kwamba mchakato wa kujenga hospitali ya wilaya ya Karagwe inayomilikiwa na serikali unaanza mapema iwezekanavyo.
Kuhusu Elimu, Mashule mengi wilayani Karagwe hayana vitabu, walimu, maabara, madawati, nyumba za walimu, mabweni na hata madarasa. Kadhalika, katika miaka 50 ya uhuru iliyopita, bado Karagwe haina sekondari ya kidato cha tano na sita.
Hivyo, nitapigania huduma bora za elimu katika shule za awali, msingi, na sekondari kwa kusimamia upatikanaji wa vitendea kazi kama vile madarasa, madawati, walimu, maabara, vitabu, chaki na walimu wa kutosha. Nitasimamia ongezeko la nyumba za walimu na mabweni ya wanafunzi pia. Pia nitapigania kuanzishwa kwa shule ya A-level ya serikali Wilayani Karagwe.
Kadhalika, nitashirikiana na wadau wa maendeleo wilayani kuhakikisha kuwa Ndoto yao ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Karagwe inatimia haraka iwezekanavyo. Vile vile kwa ajili ya kufanikisha elimu kwa wote bila ubaguzi kwa misingi ya kipato, nitapigania mfumo wa elimu unaohakikisha kwamba, karo ya elimu inalipwa na serikali kutokana na kodi.
Kuhusu Itikadi ya uongozi, wananchi wa Karagwe wanayo haki ya kuwa na vyombo vya dola vinavyolinda na kukuza haki zao kwa usawa. Vyombo hivyo ni pamoja na jeshi la polisi, mahakamani, kwenye Mabaraza ya Kata, Baraza la Madiwani, na katika maofisi ya Halmashauri ya Wilaya. Katika vyombo hivi, nakusudia kupigania utendaji kazi unaozingatia utawala bora kwa kuzingatia misingi ya utu na haki za binadamu.
Kuhusu ongezeko la Kaya bora, naamini kuwa familia ni taasisi ya kijamii ambayo ni kikonyo cha jumuiya nyingine zote katika taifa. Ni taasisi yenye haki kadhaa zinazopaswa kukuzwa na kulindwa na dola kwa njia mbalimbali. Haki hizo ni pamoja na kupatiwa hati ya kumiliki ardhi na mashamba kisheria; haki ya kuwa na nyumba ya kudumu; haki ya kuwa na watoto wenye vyeti vya kuzaliwa; haki ya kuwa na cheti cha ndoa kilichosajiliwa serikalini; na haki ya kupatiwa hifadhi ya jamii, endapo familia inawatunza walemavu, wazee au yatima. Kwa sasa haki hizi zimetelekezwa na serikali ya sasa. Hivyo, nitapigania mfumo utakaotuwezesha kukuza na kulinda haki hizi. Kati ya mambo mengine, nitapigania kushushwa kwa bei za vifaa vya ujenzi ili familia ziweze kujenga nyumba za kudumu kirahisi.
Kuhusu Uchumi, wananchi wa Karagwe wanazo haki kadhaa zinazopaswa kulindwa na kukuzwa na serikali. Kuna haki ya kufaidika na hazina ya taifa, haki ya kupata vitendea kazi kwa ajili ya uzalishaji, haki ya kupata masoko ya mazao yao, na miundombinu imara. Haki hizi zinatekelezwa kwa kusuasua wilayani Karagwe.
Kwa hiyo, nitapigania ongezeko la kipato cha vijana, wanawake, wazee, wakulima, na wafanyakazi kwa kuboresha tekinolojia, na kupigania masoko kwa ajili ya mazao yao. Nitaimarisha Chama cha Ushirika cha Kahawa Karagwe (KDCU) ili kuwapatia bei bora wakulima. Nitapigania program maalum kwa ajili ya kuwainua wakulima waliathiriwa na mnyauko wa migomba. Nitapigania kuanzishwa kwa benki ya maendeleo ya wilaya ya Karagwe (Karagwe Development Bank). Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo utaelekezwa katika kufanikisha uanzishwaji wa benki hiyo. Pia, miundombinu ya maji, umeme, barabara na biashara itaimarishwa.
Nitapigania barabara zinazopitika katika kipindi chote cha mwaka; nitahakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika kwa ajili ya matumizi ya nyumbani; nitahakikisha kwamaba vyanzo asilia vya maji vinatafutwa na kuendelezwa ili maji yanawafuata wananchi majumbani badala ya wao kuyafuata maji yaliko. Pia nitatoa mafunzo ya uvunaji wa maji ya mvua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Kadhalika, nitapigania ujenzi wa soko la kisasa mjini Kayanga pamoja na soko kubwa la kimataifa litakalovuta washiriki kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.
Kwa ujumla, ajenda yangu kuhusu Karagwe Mpya inavyo vipaumbele vitano muhimu. Napigania afya bora, elimu bora, itikadi ya utawala bora, ongezeko la familia bora (oikonomia bora), na uchumi bora. Hii ni ajenda inayoongelea "Afya, Elimu, Itikadi, Oikonomia, na Uchumi." Vokali tano za "a-e-i-o-u" ni njia rahisi ya kuvikumbuka vipaumbele hivi.
4. TIMU YA KAMPENI
Ninakusudia kuunda timu ya kampeni ya ushindi. Timu hii itajumuisha waratibu 5 wa kampeni tarafani, waratibu wa kampeni 22 katani, waratibu wa kampeni 77 vijijini, waratibu wa kampeni 630 vitongojini, wanahabari 2, mlinzi 1, watunza spika 2, fundi makanika 1, afisa mikakati 1, afisa habari 1, afisa tehama 1, meneja wa kampeni 1, mhazini wa kampeni 1, afisa usalama mkuu 1, kampena mwanamume 1, kampena mwanamke 1, kampena msichana 1, afisa kura 1, na afisa maakuli 1, dereva 1, na mshereheshaji 1, na mwanasheria 1.
Mbali na timu hii, Chadema ya Karagwe tayari imeenea kama taasisi kuanzia wilayani, katani, vijijini mpaka vitongojini. Kuna vijana, wanawake, na wazee walio tayari kukifia chama kila kona.
Kwa sehemu kubwa, Kamati za Utendaji za Chadema wilayani na katani, haziyumbishwi na upepo wa siasa za tumboni. Red Brigedi nayo sasa ni imara. Karagwe hatusemani kwa mafumbo, hatupakani matope wala kupikiana majungu. Tunao "umoja wa roho" ambayo ni silaha ya ushindi.
5. UWEZO WA KIFEDHA
Uendeshaji wa kampeni unahitaji fedha na rasilimali nyingine. Kwa mfano, mahesabu yangu ya awali yanaonyesha kwamba bajeti ifuatayo inahitajika:
Kwanza kuna kukodi gari moja la Land Cruiser kwa siku 70 kwa gharama ya 50,000/= kila siku, sawa na 3,500,000/=. Pili, kuna kukodi gari moja la Pickup Double Cabin kwa siku 70 kwa gharama ya 50,000/= kila siku, sawa na 3,500,000/=. Tatu, kuna kukodi seti moja ya vipaza sauti kwa siku 70 kwa gharama ya 50,000/= kwa siku, sawa na 3,500,000/=. Nne, kuna kukodi jenereta moja kwa ajili ya vipaza sauti kwa siku 70 kwa gharama ya 20,000/= kila siku, sawa na 700,000/=. Tano, kuna mafuta ya magari mawili ambayo ni lita 30 kwa siku kwa kila gari kwa siku 70 kwa gharama ya 2,000/= kwa lita, sawa na 8,400,000/=.
Sita, kuna mafuta ya jenereta moja ambayo ni lita 15 kila siku kwa siku 70 kwa gharama ya 2,000/= kila lita, sawa na 2,100,000/=. Saba, kuna vipeperushi vya mgombea ambavyo ni 50 kwa kila moja ya vitongoji 630, kwa gharama ya 500/= kila kipeperushi, sawa na 15,750,000/=. Nane, kuna kampeni za ufunguzi makao makuu ya wilaya sawa na 500,000/=. Tisa, kuna kampeni za kufunga makao makuu ya upinzani sawa na 500,000/=.
Kumi, kuna kulipa mafuta ya pikipiki kwa waratibu wa kampeni 734 (tarafani 5, kata 22, vijini 77, vitongojini 630) kwa siku 70 kwa gharama ya 1,500/= kila siku, sawa na 77,070,00/=. Kumi na moja, kuna kulipa lunch kwa makampena wakuu wilayani wapatao 20 katika siku 70 kwa gharama ya 5,000/= kwa siku, sawa na 7,000,000/=. Kumi na mbili, kuna kulipa dinner kwa makampena wakuu wilayani wapatao 20 katika siku 70 kwa gharama ya 5,000/= kwa siku, sawa na 7,000,000/=. Kumi na tatu, kuna malazi ya makampena 20 kwa siku 70 kwa gharama ya 5,000/=, sawa na 7,000,000/=.
Kumi na nne, kuna nauli kwa ajili ya semina kwa mawakala 300 ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=. Kumi na tano, kuna chakula kwa ajili ya semina kwa mawakala 300 ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=. Kumi na sita, kuna nauli kwa ajili ya mawakala 300 siku ya kupiga kura ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=. Kumi na saba, kuna chakula kwa ajili ya mawakala 300 ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=.
Kumi na nane, kuna nauli kwa ajili ya semina kwa walinzi 300 ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=. Kumi na tisa, kuna chakula kwa ajili ya semina kwa walinzi 300 ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=. Ishirini, kuna nauli kwa ajili ya walinzi 300 siku ya kupiga kura ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=. Ishirini na moja, kuna chakula kwa ajili ya walinzi 300 siku ya kupiga kura ambayo ni 10,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=.
Ishirini na mbili, kuna kukodi pikipiki 100 siku ya kupiga kura kwa ajili ya kusafirisha mawakala hadi vituoni, kwa gharama ya 30,000/= kwa siku, sawa na 3,000,000/=. Ishirini na tatu, kuna kukodi magari 22 siku ya kupiga kura kwa ajili ya kuratibu ukusanyaji wa fomu za matokeo katika kila kata, kwa gharama ya 100,000/= kwa siku, sawa na 2,200,000/=. Ishirini na nne, kuna gharama za mkutano wa kushukuru baada ya uchaguzi, sawa na 1,000,000/=. Ishirini na tano, kuna gharama za masafa ya redio kwa saa moja katika siku 70 kwa gharama ya 100,000/= kwa siku, sawa na 7,000,000/=. Na ishirini na sita kuna gharama za bendi ya kutumbuiza mikutano kadhaa kwa gharama ya 26,000,000/=. Gharama zote hizi ni sawa na Milioni Mia Moja tisini na tisa na Laki saba na ishirini elfu za Kitanzania (TZS 199,720,000/=).
Kuhusu gharama hizi, tayari wapiga kura wangu 30,000 walionikubali mwaka 2010 wameahidi kunichangia "buku buku" kila mmoja. Wasomaji wa makala zangu magazetini wameahidi kunichangia.
Watu niliosoma nao Kibona, Katoke, Tambaza, na Chuo Kikuu wako nami bega kwa bega. Wana TYCS wote hawawezi kunitelekeza. Hata wafanyakazi wenzangu katika Kampuni ya Simu (TTCL) wamekwisha anza kukusanya michango. Familia yangu nayo iko tayari kunichangia. Hivyo, endapo nitateuliwa na chama changu kugombea ubunge, uwezo wa kuchangia gharama za kuendesha kampeni kwa wastani wa 33% ninao. Sehemu inayobaki chama kitamalizia.
6. AKIBA YA KURA
Mbali na sababu zilizotangulia, kuna ukweli kwamba mwaka 2010 nilipata zaidi ya 30,000 ya kura zote. Hii ni sababu muhimu katika uamuzi wangu kwani kura hizi badi ziko hai. Kura zote zilihesabiwa kwa zaidi ya siku tatu. Mabomu na risasi za moto vikapigwa. Hatimaye zikatangazwa 36% kama kura zangu. Mimi na wapiga kura wangu hatukuridhishwa na tangazo hili. Ni wazi tuliibiwa.
Kwa sababu ya uchungu wa kuibiwa ushindi, watoto wengi waliozaliwa siku hiyo waliitwa "Kahangwa." Leo kuna "Kahangwa Watoto" wengi Karagwe. Hivyo, jina "Kahangwa" tayari limejisimika mioyoni mwa wapiga kura wengi wa Karagwe.
7. HITIMISHO
Kutokana na yaliyosemwa hapo juu ni wazi kwamba, kama kazi ya kumtafuta mbunge ni kazi ya kujenga nyumba, basi Chadema Karagwe tumekwisha fika kwenye linta wakati watani zetu ndio wanachimba msingi. Kama kazi hii ni riadha, basi Chadema Karagwe tumekwisha fika kati kati ya uwanja wakati watani zetu ndio wanaanza mbio golini.
Hivyo, katika ngazi ya ubunge, mapambano yaliyopo leo kati ya Chadema Karagwe na vyama vingine vya siasa ni sawa na mapambano kati ya sungura na tembo, kama sio mapambano kati ya kichuguu na mlima! Kwa maneno mengine, Chadema Karagwe tumebakiza kazi moja tu. Kazi hiyo ni kutafuta wagombea wazuri katika ngazi ya udiwani kwa ajili ya kukamata kata zote 22 zilizopo.
Hivyo, nawasahauri rafiki zangu kama vile Prince Rwazo, Victor Runyoro, Elias Muganyizi, na watia nia wengine kujielekeza katani ili tuweze kuing'oa CCM kuanzia kona zote. Kiti cha ubunge ni kimoja lakini tuna viti 22 vya udiwani vinatusubiri. Napendekeza kwamba, kipaumbele chetu kiwe kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, na sio kushinda ubunge tu! Nawaomba viongozi wetu wa Wilaya, Mkoa na Taifa wasaidie katika kulisisitiza jambo hili muhimu.
Baada ya kusema hayo, niseme tena kwamba, kuhusu Ubunge wa Karagwe, alama za nyakati zinaonyesha kwamba, Mwaka 2015 ni Zamu yangu Kahangwa. Naomba uniunge mkono kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo, na kwa rasilimali kupitia barua pepe deus.jovin@gmail.com na simu namba 0758-341-483.