Elections 2015 Ubunge wa Karagwe 2015 ni zamu ya Kahangwa

Elections 2015 Ubunge wa Karagwe 2015 ni zamu ya Kahangwa

kahangwa nimekutafuta nimekupata video zako za kwenye youtube nimeziona nimesoma azania miaka hiyo hiyo na bila shaka tunafahamiana so please tuwasiliane nijue namna tunaweza kusaidia juhudi zako kupitia jf email contact please
 
You have my support, kutoka jimbo jirani la Kyerwa. Bila shaka unaujua mziki wa chadema kutokea huko...
 
Bwana Kahangwa

Wewe ni Jembe, kwa hiyo songa mbele uwakomboe wana-Karagwe.

Ila maelezo yako kidogo yanajikanganya. Mfano, utawezaje kujenga hospitali ya Wilaya ya Kyerwa, wakati wilaya yako ni Karagwe? Pia, unasema utaondoa vizuizi barabarani ili Kahawa iuzwe nchi za nje, kwa maana ya Uganda/Rwanda/Burundi. Kweli wewe ni Mzalendo? Ukiruhusu Kahawa kwenda nje kwa njia za magendo, Halmashauri na Serikali kwa vyovyote watakosa mapato. Utawezaje kutekeleza yote hayo unayoyahaidi bila fedha kutoka Halmashauri na Serikali? Mshahara na stahiki zako wewe kama Mbunge zitatoka wapi? Au unasema tu kwa sababu unataka watu wakuchague?

Naomba unisaidie kujua: Utawezaje kuondoa tatizo la wahamiaji haramu hususani wale wanaoifanya Karagwe kuwa sehemu ya malisho ya mifugo yao?

Maoni: 1. Jitahidi kutokuhaidi vitu visivyotekelezeka, maana ikitokea ukachaguliwa...miaka 5 siyo mingi.

Ninakuombea kwa Mungu Baba ili ndoto yako iwe kweli!

Mkuu,amesema atahakikisha Wilaya ya Karagwe inapata Hospital na sio Kyerwa,soma vizuri
 
Hebu weka na ajenda ya kujenga soko kubwa LA kibiashara hapo jimboni mwako kwa ajiri ya kuteka soko LA ukanda huo na nchi jrani,baada ya hapo usiache kuchochea ujenzi uliokwisha anza wa ujenzi wa chuo kikuu karagwe na vyuo vingine kama vya afya ili kuiback up elimu ya ndugu zetu ...kila LA kheri kaka!
 
Ile lami ambayo inawekwa na wachina kutoka Kyaka mpaka Bugene kupitia Kiyanga (Makao makuu ya Karagwe) mpaka sasa kifusi kimefika Omurushaka nadhani itakuwa gear ya magamba kuomba nafasi kumalizia hiyo sehemu. Ujipange. Btw nakuombea sana
 
Mkuu unapaswa ujipange kwasababu miaka mitano kuna mambo yamefanyika na yanaonekana mf.kuna umeme umepelekwa vijijjini kama Nyabwegira, Kakiro,Nyainsozi,Iembe n.k pili kuna barabara za mjini Kayanga katikati zimewekewa rami na nyingine ni barabara kutoka Kyaka to Bugene kujengwa kwa rami.
Kwa mifano kama hyo CCM wanaweza kuongea mbele ya wananchi wakasikiwa nakupewa ridhaa ya kuongoza jimbo la karagwe tena.
Mh.Kahangwa jaribu kutafta mbinu mathubuti ili kuwatoa CCM jimboni karagwe.
 
Kazi bado unayo chama kukuamini. Unajua RB uliyonayo polisi watu wanasubiri uchukue fomu? Umeomba radhi matusi uliyomtukana M/kiti -wako wa mkoa? Umeondoa wasi wasi wa watu kuhusu uhusiano wako na Kitila? Safari ni ndefu ili uaminike!

Noted. Ila naingatia yafuatayo: (1) Kwa sasa sina RB iliyo hai katika kituo chochote cha polisi. Kama unaifahamu nitajie namba yake, mpelelezi, aina ya shitaka, na nani ananishitaki. (2) Kwa kuzingatia viwango vya siasa mamboleo, kauli za ukosoaji wa wazi kwa kuzingatia kanuni ya ukweli sio matusi kamwe. Fikra kongwe za kuzuia ukosoaji kwa madai eti 'wewe nakuzidi umri' zimepitwa na wakati. (3) Hakuna mtumwenye wasi wasi nami kwa sababu yoyote ile.
 
Mkuu unapaswa ujipange kwasababu miaka mitano kuna mambo yamefanyika na yanaonekana mf.kuna umeme umepelekwa vijijjini kama Nyabwegira, Kakiro,Nyainsozi,Iembe n.k pili kuna barabara za mjini Kayanga katikati zimewekewa rami na nyingine ni barabara kutoka Kyaka to Bugene kujengwa kwa rami. Kwa mifano kama hyo CCM wanaweza kuongea mbele ya wananchi wakasikiwa nakupewa ridhaa ya kuongoza jimbo la karagwe tena. Mh.Kahangwa jaribu kutafta mbinu mathubuti ili kuwatoa CCM jimboni karagwe.

Nimekupata Sodium. Lakini nazingatia haya. Kuhusu umeme unaopelekwa vijijjini kama Nyabwegira, Kakiro,Nyainsozi, na Ihembe huo ni mradi wa REA ambao unatekelezwa na fedha ya mkopo itakayolipwa na wananchi upitia kodi. Huo ni umeme wa wananchi. Haujaletwa na CCM. Lakini pia, umeme wa LUKU utadumu kwa muda gani? Kuhusu barabara za mjini Kayanga katikati zilizowekewa lami hiyo ni kodi ya wananchi. Sio pesa kutoka CCM. Kuhusu barabara kutoka Kyaka to Bugene hiyo ni barabara ya TANROADS.Hivyo, Halmashauri ya Wilaya Karagwe haiwezi kuitumia kama sehemu ya mafanikio yake. Lakini pia pesa ya kujenga barabara ni kodi ya wananchi. Haikutoka CCM. Kuna matatizo makubwa katika kutekeleza kalenda ya maendeleo ya Karagwe. Najipanga kulifafanua hilo mkuu. Karibu.
 
You have my support, kutoka jimbo jirani la Kyerwa. Bila shaka unaujua mziki wa chadema kutokea huko...

Kamanda, naijua sana Kyerwa. Kyerwa ikipiga chafya Karagwe inaugua mafua and vice versa. Tufuteni Kamanda mzuri tuje tufanye alliance ya ku-delete CCM accross Karagwe-Kyerwa corridor.
 
Ile lami ambayo inawekwa na wachina kutoka Kyaka mpaka Bugene kupitia Kiyanga (Makao makuu ya Karagwe) mpaka sasa kifusi kimefika Omurushaka nadhani itakuwa gear ya magamba kuomba nafasi kumalizia hiyo sehemu. Ujipange. Btw nakuombea sana

Noted sir. Ila kuna angalizo: Bara hiyo ni kwa faida ya nani kama migomba na Kahawa vinateketea kwa sababu ya mnyauko na hakuna bail-out plan kama tulivyowafanyika wale business people? Naongelea tatizo la vipaumbele.
 
Hebu weka na ajenda ya kujenga soko kubwa LA kibiashara hapo jimboni mwako kwa ajiri ya kuteka soko LA ukanda huo na nchi jrani,baada ya hapo usiache kuchochea ujenzi uliokwisha anza wa ujenzi wa chuo kikuu karagwe na vyuo vingine kama vya afya ili kuiback up elimu ya ndugu zetu ...kila LA kheri kaka!

Yamezingatiwa mkuu.
 
Nimekupata Sodium. Lakini nazingatia haya. Kuhusu umeme unaopelekwa vijijjini kama Nyabwegira, Kakiro,Nyainsozi, na Ihembe huo ni mradi wa REA ambao unatekelezwa na fedha ya mkopo itakayolipwa na wananchi upitia kodi. Huo ni umeme wa wananchi. Haujaletwa na CCM. Lakini pia, umeme wa LUKU utadumu kwa muda gani? Kuhusu barabara za mjini Kayanga katikati zilizowekewa lami hiyo ni kodi ya wananchi. Sio pesa kutoka CCM. Kuhusu barabara kutoka Kyaka to Bugene hiyo ni barabara ya TANROADS.Hivyo, Halmashauri ya Wilaya Karagwe haiwezi kuitumia kama sehemu ya mafanikio yake. Lakini pia pesa ya kujenga barabara ni kodi ya wananchi. Haikutoka CCM. Kuna matatizo makubwa katika kutekeleza kalenda ya maendeleo ya Karagwe. Najipanga kulifafanua hilo mkuu. Karibu.

Nimekuelewa ila point yangu ilikuwa kukuweka antetion kuwa sehemu kubwa ya karagwe ni vijijini amboko watu awana uelewa na maswala kama TANROADS ,REA so CCM unaweza kusema ndyo ili propose miradi kama hyo na kuisimia na wanainchi wakakubari kwa sababu ya ukosefu wa elimu.
 
Mkuu vipi hukutia nia?
 
Kwa Bajeti hii maskini asiye na mtandao atafanikiwa kweli kuwa mbunge,ni rahisi kwa mtu mwenye bajeti kama hii kutoa ka rushwa kiaiana aiseee.
 
Back
Top Bottom