Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji maarufu kama Babu Duni amewataka wananchi wa Mtaa wa mtaa wa Tupendane, kata ya Manzese katika jimbo la Ubungo kuondokana na uoga ambao unakwamisha jitihada za kuleta maendeleo katika mtaa wao.
Babu Duni ametoa wito huo Novemba 20, 2024 wakati akizindua rasmi kampeni za chama hicho kwa mtaa huo ambapo amewataka kujadili changamoto mbalimbali zinazowahusu na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika hivi karibuni
Aidha amesema kwamba ACT imekuja na Ilani ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao imeangazia masilahi yao ikiwamo masuala ya ajira, uchumi wa mtaa na kuwa na uongozi ambao unakubalika na wananchi wa mtaa.
============================================================
Ujumbe huu Muruwa umetolewa na Mzee Juma Duni Haji kwenye uzinduzi wa kampeni za Serikali za mitaa.
Mzee huyu anatusanua kwamba kumbe hizi Simba na Yanga zimekuwa zinatumika kupumbaza Wananchi na kuwasahaulisha dhiki ya Nchi ili CCM Iendelee kutapanya na kuuza Mali za Nchi na kuwarithisha madaraka watoto wa Viongozi
Zaidi Mzee Duni huyu hapa