LGE2024 Ubungo: Kiongozi wa ACT Wazalendo aonya wananchi kupumbazwa na mambo ya Simba na Yanga

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji maarufu kama Babu Duni amewataka wananchi wa Mtaa wa mtaa wa Tupendane, kata ya Manzese katika jimbo la Ubungo kuondokana na uoga ambao unakwamisha jitihada za kuleta maendeleo katika mtaa wao.

Babu Duni ametoa wito huo Novemba 20, 2024 wakati akizindua rasmi kampeni za chama hicho kwa mtaa huo ambapo amewataka kujadili changamoto mbalimbali zinazowahusu na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika hivi karibuni

Aidha amesema kwamba ACT imekuja na Ilani ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao imeangazia masilahi yao ikiwamo masuala ya ajira, uchumi wa mtaa na kuwa na uongozi ambao unakubalika na wananchi wa mtaa.

============================================================

Ujumbe huu Muruwa umetolewa na Mzee Juma Duni Haji kwenye uzinduzi wa kampeni za Serikali za mitaa.

Mzee huyu anatusanua kwamba kumbe hizi Simba na Yanga zimekuwa zinatumika kupumbaza Wananchi na kuwasahaulisha dhiki ya Nchi ili CCM Iendelee kutapanya na kuuza Mali za Nchi na kuwarithisha madaraka watoto wa Viongozi

Zaidi Mzee Duni huyu hapa

View attachment 3157796
Mjinga huyo mzee, Simba na Yanga ni walipa kodi wakubwa kuliko hao ACT hivyo awaongelee kwa adabu.

Mpira huwapunguzia watu machungu yanayosababishwa na wao wanasiasa na ulafi unaowasumbua.

Anapiga makelele akiwa upinzani, leo hii apewe ikulu na hazina ya nchi, ataongea hayo masuala ya Simba na Yanga?.
 
Kati ya wewe na huyo mzee nani mjinga?Kama hata yaliyomo kwenye muhtasari wa Katiba yako ya nchi hujui pumbavu.
 
Muda si mrefu simba na yanga zinaenda kudumaaa....zinapigwa vita sana siku hizi
Wanaozipiga vita ni wajinga wachache humu majukwaani, lakini huko mitaani hakuna wa kupunguza umaarufu wa hivi vilabu.

Vinaendeshwa kisasa na vinapambana vikichukua nafasi zao barani Afrika.

Mtanzania wa kawaida anadhani kila kitu kilichopo mbele yake kina haki ya kunyooshewa vidole, matatizo yake ya kimaisha anataka kuyahamishia kwa watu wengine!.
 
Kati ya wewe na huyo mzee nani mjinga?Kama hata yaliyomo kwenye muhtasari wa Katiba yako ya nchi hujui pumbavu.
Pumbavu ni wewe na huyo mzee mnaodhani ni haki kwa kila mtu kuipenda siasa ya nchi iliyojaa ulaghai wa kila aina.

Dunia nzima mpira unapendwa sana tu, kudhani kuwa mchezo huu ndio sababu ya umaskini wetu ni kukosa akili za ziada za kutatua matatizo yanayotukabili.
 
Amesema yeye ni mchezaji kwa asili na kusisitiza kuwa pamoja na mapenzi ya Simba na Yanga tuangalie zaidi yale yanayogusa maisha yetu ya kila siku,kwa hiyo yeye kakosea wapi?Mapenzi ya mpira yapo lakini hayaongezi wala kupunguza chochote katika maisha ya mwanadamu.Ambapo kuna watu hawapendi mpira lakini hawawazidi maisha wale wanaopenda mpira.Mpira huu wa Tanzania upo kisiasa zaidi kwa ajili ya kuimarisha chama cha mapinduzi na kudhoofisha mfumo wa vyama vingi nchini.
 
Wadau wa mpira nchi nzima hawazidi milioni 25 kati ya watanzania milioni 63 tuliopo hivi sasa. Hao milioni 38 wanaobakia hawatoshi kujihusisha na siasa za kimaendeleo?.

Kama yeye haupendi mpira na aufunge mdomo wake awaachie watu waufurahie. Hawanunulii tiketi za kwenda viwanjani, hawanunulii ving'amuzi vya kila mwezi, hawanunulii magazeti ya michezo na bando za kufuatilia habari za dunia.

Wanasiasa wapuuzi sana wa aina hiyo, kibaya unapozeeka unapoteza hata akili ya kawaida tu.
 
Mawazo yake yaheshimiwe hata kama yanaudhi lakini yaheshimiwe.
 
Wanaozipiga vita ni wajinga wachache humu majukwaani, lakini huko mitaani hakuna wa kupunguza umaarufu wa hivi vilabu.

Vinaendeshwa kisasa na vinapambana vikichukua nafasi zao barani Afrika.

Mtanzania wa kawaida anadhani kila kitu kilichopo mbele yake kina haki ya kunyooshewa vidole, matatizo yake ya kimaisha anataka kuyahamishia kwa watu wengine!.
Endelea kushabikia mipira.....wafrika ndio.kazi yenu, na pombe
 
Ili kuwa mgombea mwenza wa Lowassa, nasikia alivuta billions kadhaa
 
Huko ccm ndio wamejaa....ila mpirani ni janga zaidi
Wote tu kwa ujumla,. Hata hao wanaokimbilia kuutupia mpira lawama ni wapuuzi wakubwa.

Mpira unatoa ajira nyingi sana. Fikiria leo Mbwana Samatta kajenga majumba mengi huko mbagala, ni mafundi wangapi ameweza kuwaajiri?.

Obi Mikel ana malori yanayozunguka Nigeria nzima, ni madereva, mafundi wangapi ameweza kuwapa ajira kupitia hayo malori yake?.

Ronaldo wa Ureno kajenga hospitali kwao Ureno inayotibu masuala ya moyo kwa watoto. Ni watoto wangapi ameweza kuyaokoa maisha yao kupitia operesheni zinazofanyika hospitalini hapo?.

Huyo Mzee anapiga makelele hajui anaongea kitu gani kuhusu mpira wa miguu, kwa bahati mbaya akili za aina hiyo zipo sana Tanzania. Tunakuwa mbali na dunia halisi inayokuwepo.
 
Back
Top Bottom