Ubunifu: vyakula vya kibongo.. Bara na Pwani .... Makabila yote, mapishi yote

Ooh ni vile viteketeke
Ndiyo. Huwezi kuvichoma hivyo. Unavichemsha na maji kidooogo sana kwani na vyenyewe hutoa maji(Mchuzi). Ukianza kuvila hivyo unatakiwa uchukue tahadhari kwani kwa utamu wake unaweza kujikuta umemaliza (umevuna) shamba.
 
Attachments

  • DSC02944.JPG
    1,009.5 KB · Views: 3
Sijawahi kula pweza. Ladha yake ni kama samaki wengine?
 
Yaani ana ladha ya kipekee sana.
Yaani sijui utamu wake niuelezeeje.
Yaani ni mtamu haswaaaa.
Ukichanganya na ile pilipili yake....basi raha sana
Na wewe unasimama kwenye meza na ''kutungua'' vipande kwa kijiti au unabeba na kwenda kula nyumbani? Hivi unaweza kula kwa ugali au ananoga unaposimama kwenye meza na kula vipande huku unachvya kwenye pilipili?
 
Mie kwa kweli nikibeba nyumbani nashindwa kula sijuivkwa nini.
Napenda kula palepale mezani.
Wapo wanaodonoa mezani na wapo wanataka kuwekewa kwenye bakuli, inategemea na uhitaji wako.

Wapo wanaonunua na kwenda kurumangia na ugali au kachori nyumbani.
Ila palepale mezani ndo ananoga
 
Nmekumbuka vi-mishikaki jamaa mmoja kama mwarabu alikuwa anauza. Anakata vidogo vidogo halafu vikiiva anachovya kwenye pilipili. Unaweza kula vingi kweli bila kukinai. Nadhani pweza inatakuwa inanoga kama hivyo. Ntakuja kujaribu siku moja.
 
Yeah, vitamu sana.
Ukijaribu uje kunipa mrejesho.
Watu wanamaliza mpaka 50 elfu kwenye meza za pweza.
Sijui kuna ushirikina au vp🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…