Ubunifu: vyakula vya kibongo.. Bara na Pwani .... Makabila yote, mapishi yote

Ubunifu: vyakula vya kibongo.. Bara na Pwani .... Makabila yote, mapishi yote

Hatari kabisa mpwa.
Sijui kuna siri gani kwenye huyu samaki pweza.
Halafu pilipili zao sijui mtengenezaji ni mmoja.
Ukila pweza wa Kimara na wa Mbagala au Kinondoni wote pilipili yao ina ladha moja....utamu sasa😋

Ila mie napenda pweza jamani.
Huku Dodoma hawana mwamko wa ulaji wa pweza.
Au kwa kuwa hakuna bahari🤔🤔
Wagogo na pweza ni sawa na msukuma na mtory😀🏃🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿
 
Arikaa Mbwanyeni! Shighirija. Uyoga unalimwa sana huko mijini ila unauziwa watu wanaomilki maSupermarkets au Hoteli kubwa-kubwa. Sisi huku vijijini tunajiokotea huko maporini msimu ukifika ila Tahadhari; watoto au wasioujua hawaruhusiwi kuokota/kuchuma uyoga wa porini. Kosa kidogo tu; mwifwa.
Uyoga.. Maini pori akupikie mvimba macho bwana😋😋😋
 
Back
Top Bottom