Mkuu Kuna kitu naomba nikuulize, Jana Kuna kitu nimeshangaa sana nahisi huyu kocha na wachezaji wake watakua wamelogwa sijui au ni ujinga kichwani.... Hata wa yanga sikuwaelewa
Hawa jamaa ni kama walikuja zuia wapate hata draw... Wakaana 1st half kwa kupaki basi... Baada ya kuruhusu goli la kwanza nadhani 2nd half wakaja na plan Hio Hio wapaki basi wacheze counter ndipo wakashangaa ndani ya dakika 5 washapigwa chuma mbili
Sasa matokeo ya 3-0 bado hayakua mabaya sana maana wangetegemea yanga afungwe ye ashinde.... Kwenye dakika za 75 naona kina diarra wakaanza kupoteza muda ikiwa bado 3-0 nikawa siwaelewi kabisa nao... Ilipofika dakika ya 80 kwa kua huwezi rudisha goli nilitegemea jamaa wajilinde zaidi ili wafungwe hata 3-0 ndo kwanza wakajazana mbele wakaruhusu goli la nne
Technical kocha alifeli sana kuhandle dakika za mwisho akaruhusu goli na 4