Uchache wa idadi ya raia nimSababu kuu za nchi za uarabuni zenye maisha mazuri kwa raia wengi bila utawala bora

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Watu wengi wasiopenda demokrasia kila mara hupenda kutolea mifano ya nchi za uarabuni zenye raia wenye maisha bora sana kiuchumi pasipo kuwepo na utawala bora kwenye nchi zao. Watu wa haina hii hawazingatii mambo mawili kuhusu hizi nchi ambayo ni Utajiri mkubwa wa mafuta na gesi na idadi ndogo ya raia.

Kuhusu utajiri gesi na mafuta hili kila mtu analifahmu ila wengi hawajui kuwa hizi nchi zina idadi ndogo sana ya raia wake, chukulia mfano wa hizi nchi
Qatar-Laki 4
UAE- Milioni 1.3
Kuwait-Milioni 1.5
Oman-Milioni 3
Saudi Arabia-Milioni 19( Saudi Arabia ina ukubwa mara mbili na nusu ya Nigeria yenye raia milioni 230)
 
Shida sio uchache wa watu.

Kuna mataifa yana idadi ndogo hapa Africa ila wamezidiwa maendeleo na hao waarabu.
 
Tatizo sio uchache wa watu, changamoto kubwa ni matumizi sahihi ya rasilimali za taifa kumfaidisha raia mmoja mmoja zikiwemo huduma za lazima kama elimu bora, matibabu mazuri, mishahara inayo kidhi pamoja na kujali utu wa mtu
 
Sidhani kama suala ni uchache wa watu kwani hukohuko uarabuni kuna nchi kama Lebanon na yenyewe pia ina idadi ndogo ya watu kama chini ya milioni mbili hivi lakini wako choka mbaya kama sisi tu vile.

Tatizo la nchi za kiafrika kuwa na umaskini mkubwa kwa raia pamoja na bara kuwa na rasilmali kibao ni uongozi mbovu, hakuna kisingizio kingine.

Eti kodi zinakusanywa kutoka kwa watu katika wilaya na mikoa mbalimbali kisha zinapelekwa Dodoma halafu mtu mmoja ndiye anayeamua kwa raha zake zitumikeje na ikimpendezea anaweza akayanyima yale maeneo ambayo anaona hayakumpigia kura sasa kwa hali hiyo hayo maendeleo yatatoka wapi..!!!
 
Rwanda population ni 13 millions.
Egypt population 118 millions.
Algeria population ni 44 millions.

Kuna nchi nyingi Africa mathalan Rwanda,CAR zina idadi ndogo ya watu ila hazina maendeleo,pia Kuna nchi kama Misri Ina watu wengi sana ila Ina maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Maelezo uliyotoa ni nje na fikra za kisomi na mawazo huru.
Utanisamehe ila umeropoka sana.
Nenda kazifuatilie hizo nchi mathalan Qatar,Nigeria imeanza kuchimba mafuta kabla hata ya Qatar ila Qatar imekuja kuendelea kabla hata ya Nigeria.
Nchi za kiarabu zinajijali na zina mfumo Bora ya uongozi ya kujali raia wake,hilo mnatakiwa mkubali, wenzetu Wana hadi baytul maal sehemu zinapowekwa Mali kwaajili ya kusaidia wasiojiweza.Nchi kama hiyo mnashindwaje kuendelea?
Pia wenzetu wanajua nini wanataka na wanajua namna ya ku allocate resources sehemu sahihi.
Hizo nchi mathalan Dubai zinaalikwa wabobezi wa uchumi na sayansi nchini mwao kutoka China na Ulaya ili kutoa mawazo na inawalipa vizuri.
Ninyi kaeni mezeni matango pori sijui ya demokrasia sijui ya ujinga gani.
 
Lebanon haina mafuta wala gesi au rasilimali zozote za maana, pia kabla ya vita Lebanon ilikuwa nchi nzuri tu.
 
Lebanon haina mafuta wala gesi au rasilimali zozote za maana, pia kabla ya vita Lebanon ilikuwa nchi nzuri tu.
Ulifuatilia mipaka ya bahari walivyokua wanagombania Lebanon na Israel Ina nini chini yake?
Lebanon ina gesi na mafuta mengi sanaa ambayo hayakuanza kuchimbwa tangu 1999 Palipokuwa annexed na Israel na kuleta mvutano na Hizbollah,mwaka 2022 ndio walikubaliana kugawana pasu kwa pasu mipaka hiyo ya maji na Israel.
 
Zanzibar pia kuna Watu 1.5M ni maskini wa kutupwa. Rwanda je?
 
Rwanda ni ndogo kuliko hata mkoa wa Tanga lakini inazidwa kwa rasilimali na mkoa wa Tanga, fikiria eneo la namna hiyo wanaishi watu milioni 14. Sijui kwa nini umezitaja Egpty na Algeria.
Qatar mafuta yameanza kuchimbwa 1940, Nigeria mafuta yameanza kuchimbwa 1958
 
Rwanda ni ndogo kuliko hata mkoa wa Tanga lakini inazidwa kwa rasilimali na mkoa wa Tanga, fikiria eneo la namna hiyo wanaishi watu milioni 14. Sijui kwa nini umezitaja Egpty na Algeria.
Egypt ni nchi za kiarabu zenye population kubwa na zenye maendeleo ya mid income nations.
Kwahiyo Qatar nayo ni kubwa kieneo au siyo!?.
 
Waafrika tuko na tatizo kwenye DNA. Matajiri wengi wa kiafrika wakifa ,mali zao zinafilisika. Waarabu na wazungu mali zao zinaendelezwa kizazi hadi kizazi.

Waafrika tuko na mentality za ajabu ajabu sana linapokuja suala la utafutaji. Kwanza wengi wetu tunaaminishwa kwamba kuwa masikini ni uzalendo.

Wasomi wengi wa Afrika uwezo wao umejikita kwenye kuiba, ufisadi na uvivu uliotopea
 
Waafrika tuko na tatizo kwenye DNA. Matajiri wengi wa kiafrika wakifa ,mali zao zinafilisika. Waarabu na wazungu mali zao zinaendelezwa kizazi hadi kizazi
Hii Tanzania tu Pesa zote ziko kwa Waarabu na wahindi.

Nitakupa mifano

1. Mo
2. Manji
3.Bakhresa
4. Rostam
5.Abood
6. Shabiby

Vituo vya mafuta, Makampuni ya usafirishaji Mizigo na Abiria- 90% ni wao.

Anayepinga aje kwa hoja.
 
Hii Tanzania tu Pesa zote ziko kwa Waarabu na wahindi.

Nitakupa mifano

1. Mo
2. Manji
3.Bakhresa
4. Rostam
5.Abood
6. Shabiby

Vituo vya mafuta, Makampuni ya usafirishaji Mizigo na Abiria- 90% ni wao.

Anayepinga aje kwa hoja.
Exactly!

Mali za Reginald Mengi zinayumba vibaya tangu alipofariki
 
Egypt ni nchi za kiarabu zenye population kubwa na zenye maendeleo ya mid income nations.
Kwahiyo Qatar nayo ni kubwa kieneo au siyo!?.
GDP per capita ya $3500 ni ya kawaida sana. Qatar ni kama mkoa wa Kilimanjaro ila raia wake ni laki nne tu na ni nchi namba 3 kwa akiba ya wingi wa gesi duniani, iko top 20 kwa wingi wa mafuta duniani.
 
GDP per capita ya $3500 ni ya kawaida sana. Qatar ni kama mkoa wa Kilimanjaro ila raia wake ni laki nne tu na ni nchi namba 3 kwa akiba ya wingi wa gesi duniani, iko top 20 kwa wingi wa mafuta duniani.
Usizungumzie tu per Capita ambayo inakua judged due to population when divided by GDP.
Itizame GDP yake ni ngapi.
Pia tuje kwa ground social and economic development ikoje.
Tuzungumzie maendeleo kiujumla.
 
Usizungumzie tu per Capita ambayo inakua judged due to population when divided by GDP.
Itizame GDP yake ni ngapi.
Pia tuje kwa ground social and economic development ikoje.
Tuzungumzie maendeleo kiujumla.
GDP per capita ni kiashiria kikuu cha maendeleo, Misri bado ni nchi yenye masikini wengi sana.
 
GDP per capita ni kiashiria kikuu cha maendeleo, Misri bado ni nchi yenye masikini wengi sana.
GDP per Capita inapatikana kwa kugawanya annual GDP na idadi ya watu.
Idadi ya watu ndio inahukumu GDP kuwa ndogo ama kubwa kwa asilimia kubwa.
Pia hata wanauchumi haya masuala ya per Capita wanayachukulia ni fictious sana,maana hiyo per Capita hawapewi raia na wakatumia.
Kipimo sahihi ni maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…