Nimekuwa nikienda kwenye Soko Kuu la Tandika kwa muda sasa, hivi karibuni hali ya mazingira ya soko hilo imekuwa ikizidi kuwa tata na inayotia ukakasi kiafya.
Sehemu ya kupikia ambayo inatumiwa na Wanawake wengi kupika chakula cha biashara kuna jalala lililopo pembeni, kwa ujumla hali ya uchafu ni ya kutisha.
Eneo la jalala lenye mfereji unaotuamisha maji machafu.
Jalala hilo liko karibu kabisa na choo na mtaro wa maji machafu, maji ambayo naweza kusema ni ya kuoza, huku nzi wakiwa wametawala kwa wingi eneo hilo.
Nilipoulizia baadhi ya mama lishe kuhusu wanavyoweza kuuza chakula katika mazingira hayo, walinieleza kuwa wameruhusiwa na Halmashauri kuendelea na biashara zao.
Wanasema walipata ahadi ya ukarabati wa eneo hilo miezi kadhaa iliyopita, lakini mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Wao wanaamini kuwa ushuru wanaolipa kila siku Tsh. 500 kwa kila banda, ungetumika kuboresha mazingira ya soko hilo lakini hali haijabadilika.
Baadhi ya maeneo ya kupikia chakula, Soko la Tandika.
Nilipochunguza nimebaini kuna mabanda takribani 200, na ushuru unaokusanywa kila siku unapelekwa moja kwa moja Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Licha ya malipo haya ya ushuru ambayo ni zaidi Tsh. Laki Moja kwa siku, mazingira ya soko yameendelea kuwa duni, jambo ambalo limeathiri biashara za akina mama lishe kwa kiasi kikubwa, kwani wateja wengi wanapokutana na hali hii ya uchafu wanakosa ujasiri wa kununua chakula.
Mfereji uliopo pembezoni mwa soko.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wapo wa soko hilo ni kuwa suala la ukarabati limekuwa likizungumzwa lakini hakuna kinachofanyika.
Anasema hela zinazokufanya zinaishia kwenye uongozi wa Manispaa ya Temeke kwa kuwa Wafanyabiashara wao hawana mamlaka ya kutumia fedha hizo. Halmashauri ndiyo yenye uamuzi wa namna ya kutumia ushuru huo.
Katika uchunguzi wangu, niliona kuwa hata eneo la jalala linaendelea kutumika kwa shughuli za kibiashara, ambapo nazi zinaanikwa na kuuzwa palepale sokoni.
Nazi ambazo zimekatwakatwa na kuanikwa kwaajili ya biashara.
Hata hivyo, tatizo kubwa la mtaro wa maji machafu halikushughulikiwa. Nilipomwambia kiongozi mmoja wa hapo kuhusu afya za Wananchi kuwa hatarini, alikiri kuwa soko linahitaji ukarabati wa hali ya juu, lakini hakutoa muda maalum wa lini hatua hiyo itachukuliwa.
Upande wa akina mama lishe, wanasema hali ya uchafu imewahi kuwazuia kufanya biashara kwa siku tatu, lakini waliporejea baada ya kuzuiwa, mazingira yalikuwa hayajabadilika – walikuwa wamezoa tu takataka na kuacha tatizo kuu likiendelea.
Suala la uchafu limekuwa sugu, pamoja na kuwepo kwa biashara za vyakula ndani ya soko hilo, mazingira ya usafi hayazingatiwi. Biashara zinaendelea kama kawaida katika eneo hilo, lakini afya za Wananchi zinahatarishwa kila siku.
Sehemu ambapo mama lishe wanauzia chakula.
Uuzaji wa vyakula katika mazingira haya yasiyozingatia usafi ni tishio kubwa kwa afya ya jamii, hasa kwa watu wenye kipato cha chini ambao mara nyingi hutegemea vyakula vya bei nafuu sokoni.
Nikiwa mwananchi na mteja wa soko hili, napata wasiwasi mkubwa. Je, tutasubiri mpaka mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu au homa ya matumbo utokee ndipo hatua zichukuliwe?
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inapaswa kuchukua hatua haraka kuhakikisha soko hili linakarabatiwa na kuwa salama kwa biashara za vyakula. Ushuru unaokusanywa sokoni unapaswa kutumika kuweka mazingira safi na salama kwa wajasiriamali na wateja.