KERO Uchafuzi wa kelele Ilemela Nyagunguro: Ni lini mamlaka za Mwanza zitazinduka?

KERO Uchafuzi wa kelele Ilemela Nyagunguro: Ni lini mamlaka za Mwanza zitazinduka?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tumechoka, tumenyanyasika, na tunapuuzwa kabisa!

Kwa miezi kadhaa sasa, wakazi wa Ilemela Nyagunguro tumekuwa tukiteseka kwa kukosa usingizi usiku kucha kutokana na uchafuzi uliokithiri wa kelele. Muziki unaopigwa kwa sauti ya juu ya juu sana kutoka Kwa Tunza na Mamboleo umekuwa kero isiyovumilika—unafurushwa kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 11:00 alfajiri ya asubuhi iliyofuata.

Hebu vuta picha ya adha unayopata unapomwamsha mtoto wako asubuhi ya Jumatatu ili ajiandae kwenda shule, huku nyumba bado inatetemeka kwa muziki ule ule ulioanza usiku wa kuamkia leo. Watoto wetu wanaenda shule wakiwa wamechoka kwa kukosa usingizi, na sisi wenyewe tunaenda kazini tukiwa hoi. Hii si kero tu; ni hatari kwa afya zetu na ni ukiukwaji wa haki yetu ya msingi ya kuwa na amani kwenye nyumba zetu.

Kinachosikitisha na kukatisha tamaa zaidi ni ugonjwa wa kukwepa majukumu unaoonyeshwa na mamlaka husika. Tumetuma malalamiko yasiyohesabika. Tumetuma ushahidi wa video na sauti. Lakini kila mara tunapowasiliana nao, tunapewa visingizio visivyo na kichwa wala miguu:

"Sisi hatufanyi kazi usiku." (Kama ninyi hamfanyi kazi usiku, ni nani anayepaswa kusimamia sheria pale inapovunjwa usiku?)

"Nendeni mkalalamike BASATA ili waache kuwapa leseni."

"Nenda kwa Serikali ya Mtaa wako wakamalize hilo tatizo."

Kwanini wananchi tulazimike kuzungushwa kutoka ofisi moja ya serikali hadi nyingine ili tu kupata haki ya kusimamiwa kwa sheria ya udhibiti wa kelele? Kwa nini mzigo wa kuwazuia wafanyabiashara wasivunje sheria za mazingira uwekwe juu ya mabega yetu?

Hongera sana kwa Dar es Salaam kwa kuchukua hatua madhubuti, kupiga marufuku uchafuzi wa kelele, na kulinda wakazi wake. Kwa masikitiko makubwa, kwa upande wa Mwanza, inaonekana bado tuko nyuma kwa muongo mmoja (miaka 10).

Je, viongozi wetu wa hapa na maafisa wa mazingira hawaoni au hawajali kabisa ustawi wa wakazi wa Mwanza?

Tunatoa wito kwa Manispaa ya Ilemela, NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira), BASATA, na uongozi wa mkoa kwa ujumla: acheni kusukuma lawama na timizeni wajibu wenu. Tunahitaji utulivu, watoto wetu wanahitaji usingizi, na hawa wafanyabiashara wanapaswa kuheshimu jamii inayowazunguka.
 
Poleni sana ila kwa tunza ipo miaka nenda miaka rudi, sijui kama watawazingatieni ukiangalia ni sehemu inayomilikiwa na watu wenye pesa zao!
 
Back
Top Bottom