Uchafuzi wa Sensa 2022

Bado tu unategema CCM ibadilike? Ohooo dear! Yaani mpaka leo hujashtuka tu? Bado umekaa chini ya mchongoma ukisubiri embe dodo idondoke? Eti unaamini mama Samia hajawatuma? Ni kweli hajawatuma lakini pia hana habari wala muda wa kusikiliza matatizo ya wananchi. Aaache kutumbua keki zabure aje ajishughulishe na shida zako? Kama una akili basi dai mpya mfumo mzuri wa kuongoza nchi yetu haraka sana.
 
Umesema kweli ndugu, nchi haina uwajibikaji hii. Rushwa imetembea Sana kupata nafasi ya sensa
 
Rushwa iliyopo Tanzania inaurudisha uchumi nyuma vibaya mno. Wengi wa watumishi wa uma ni wala rushwa. Hufanyiwi chochotw kwenye ofisi ya uma bila kutoa kidogo. Hali hii hurudisha maendeleo nyuma maana huduma hazitolewi kwa wakati stahiki. Nakadiria asilimia tano ya pato la taifa linaishia kwenye rushwa. Hapa sizungumzii Ufisadi wa watu kuiba hela za serikali nazungumzia rushwa za kipolisi, mahakamani, ofisi za kata, ofisi za vijiji na kwenye halmashauri. Kwa ilivyokita mizizi kwenye system sijui kama itawezekana kuiondoa.
 
Ni bora hiyo kazi wangepewa walimu wa shule za msingi angalau wana uzoefu na weledi wa kuifanya hiyo kazi kuliko kuokoteza watu wasio na sifa kwa tamaa ya kupata fedha kwa njia ya rushwa.
 
Asingetoa mfano wa mhusika bado ungesema ni umbea tu.
Kila sehemu mambo ni hayohayo tu, kufanya alichokifanya ni uchawi na roho mbaya tu Kwa huyo mtoto wa Diwani........wangapi wanabebwa nchi hii tena Kwa nafasi sensitive kabisa sembuse Diwani
 
"Ukiona kwako kunaungua ujue kwa mwenzio kunateketea " Huku kwetu Wamechukuliwa hata ambao hawakuwemo kwenye orodha ya watu waliotakiwa kufanya interview , Pili form Four losers ( Wahuni wa mtaani ) wamechomekwa . Ukijumlisha Rushwa halafu na UCCM basi mambo yamekuwa hivyo .
 
Ni vigumu sana haki kutendeka baada ya wahitimu kutoajiriwa kwa zaidi ya miaka mitano kutoajiriwa.Huko Busokelo mjukuu wangu kaitwa kwenye usaili kambiwa lete Kwanza kitambulisho cha nida ambacho hakuwa nacho lakini akawapa namba za nida ambazo walizikataa na mchezo ukaishia hapo.
 
Ni nani miongoni mwetu mwanae akiomba mkate atampa jiwe..??
 
Huu mchakato umeingiliwa sana, lakini pia fikria kama ni wewe una mtoto,umuache tu umuweke mtu baki?
 
Siku Moja tuchague Kiongozi mwenye Sera ya Wasionacho First na wenye nacho kaa Pembeni. Haiwezekani Watumishi wa Umma wenye Vipato Ndio wanapewa Ajira za Muda, Vijana Wasomi Jobless wasio na kipato wakiachwa.
 
Pole sana kwa kuwaamini CCM .

Yaani unaamini watu wanaokuwa na kura hata kabla hazijapigwa siku ya uchaguzi ?
 
Mkiambiwa andamana kushikiza katiba mpya mnaanza kusema atangulie Mbowe na familia yake wenye mabilion ndani!!. Haya pambaneni wenyewe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…