Elections 2010 Uchaguzi 2010: ITV sasa imekuwa chombo cha CCM?

Elections 2010 Uchaguzi 2010: ITV sasa imekuwa chombo cha CCM?

kweli kuna chembe ya ujuha katika fani yetu ya uandishi wa habari as uzinduzi wa kampen wasnt new maana iliisha tangazwa mapema kuwa itafanyika

But kitendo cha kuanguka mgombea pale that serious news

Tena ilibidi iwe breaking news na sio biashara ya kukatisha matangazo na kuficha


Thats really nonsense and it shows how so many people in occupying senior posts in our nation

are still living in the 19th century.

This is the information age somebody ought to teach them!!
 
Bora watangaze watu wajue. Wanapodanganya au kukaa kimya kuhusu afya ya rais ndio watu wanapata maswali zaidi na njia za panya za habari -mitandao- inapata nguvu ya kuwa chanzo mahiri cha habari. Hongera sana kwa kampuni zilizopunguza bei za internet, huu ndio ukombozi wa Mtanzania na si magazeti na TV chovu
 
Mkuu...
msomaji wa ITV anapokuwa studio hayuko huru.... macho yake huwa anapepesapepesa kwa woga kuona kama Mengi yupo karibu...

Humu ndani hawamo watu wa IPP Media, watuthibitishie haya! Aibu! Mengi ni tajiri zaidi ya kutafuta kujipitisha kwa wanasiasa! Na atapata nini zaidi ya kutusababishia hasira na chuki dhidi ya vyombo vyake, ama kweli, minds zingine ni kama zege tu, kama alivyoanza anadhani ndivyo atakavyomalizia, kama aliwatumia CCM akafika hapa, anapaswa kutazama mbele zaidi, maana atatoswa hata kama atajipendekeza namna gani, CCM hii si ya zamani
 
Labda walijaribu kutangaza, lakini wakapigwa STOP na mkono (soma amri) from the TOP...lol... Hiding stupid things...These people think we are so stupid..nway :confused2:...life goes on...:smile-big:
 
ITV na redio one zinasikika nchi nzima, je unadhani ccm wataviachia vitangaze habari ya kuanguka kwa rais...
 
KAMA HABARI UMESHAIPATA......unataka irudiwe ili iweje? ......habari za kurudiwa zipo nyingi tu.....CHADEMA YAMUUA CHACHA WANGWE.......MBOWE KAFELI MASOMO.......CHADEMA CHAMA CHA WACHAGA.......!?
 
Hivi vyombo vya habari vimenunuliwa na CCM na ndio maana wanakuwa na ubaguzi katika kutoa habari!

...Mkuu, unadhani wakati mwingine hata vimenunuliwa na sisi M?? Walaa, wakati mwingine ni kujigonga gonga tu kwa wanaovimiliki!

 
Nimeamini nchi hii imejaa MOSTERS MAMFIA hata kwenye vyombo vya habari
leo asubuhi katika taarifa zao za habari hakuna aliyetangaza afya ya Rais wetu
wanatangaza juu bila kutoa maelezo ya uhakika kama uandishi wao ndo huu wa kuganga NJAA KWELI TANZANIA HAKUNA WAANDISHI WA HABARI.

wakati wa kusoma magazeti TBC1 walikuwa na magazeti yote likiwemo TANZANIA DAIMA ambalo limeandika ukweli kuhusu afya ya JK alivyozilai JANGWANI, lakini cha kushangaza hili gazeti alikusomwa kokote

JE MAFIA WA HABARI NDO WAKO ITV NA TBC1?

Si hivyo tu: ITV leo katika udondozi wa Magazeti, walisoma Mzalendo; Nipashe; Guardian ambayo yote hayaktilia mkazo juu ya kuanguka kwa JK bali tu uzinduzi uliofana na umati wa watu. magazeti yote yaliyokuwa na kichwa kikuu juu ya kuanguka jukwaani kama Mwananchi; Mtanzania; Tanzania Daima na Majira hayakusomwa kama ilivyo kawaida.

Nimjuavyo Joyce Mhaville alivyo na weledi wa hali ya juu asingeweza kuwatoa directives yasisomwe, labda tu kama aliagizwa na Mmiliki wa vyombo hivyo. Na mmiliki naye huenda kapewa maagizo kwamba hiyo ya kuanguka isisomwe wala kutangazwa.

Mtakumbuka jana mara baada ya JK kudondoka, camera ya ITV ilihamishwa toka kwa JK podium kwenda kwenye umati ili watu wasione.

Hii imeniduaza kutaka kujua maana yake ni nini. Haiingii akilini kuwa na wasiwasi kuwa Watanzania wakijua hili litaleta mushkeli . . . .
 
Siwaelewi hawa. Wanafanya biashara ya habari/wanapata story ya kujiuza halafu hawaitumii!!! pole zenu
 
Watu ni watumwa ndani ya nchi yao,

Ni wendawazimu kwa kuogopa watawala. Nasubiri raia mwema, mwanahalisi na Tanzania daima ilinipate ukweli.
 
Mhh,

Hii nchi kweli ina uhuru wa habari. Chan 10 jana walisema kuwa wataleta taarifa (baadaye) ya tukio la kuanguka kwa Rais Kikwete Jangwani. Ila kufikia asubuhi, ni vyombe 2 tumesema Kikwete alianguka (Mwananchi na Tanzania Daima) vingine vyote nilivyosoma au kusikiliza/kuona vimesema kuwa Rais aliishiwa nguvu na kwenda kupumzika. Nadhani hapa neno lilipigwa ban (marufuku) ni kusema kuwa JK alianguka!
 
Hiyo ndiyo kitu utaita upapa wa ufisadi!!!

wewe unadhani leo Mengi akianza kuponda CCM nini kitamtokea????

au Tido Mhando aanze kumponda JK ambaye ndiye aliyemteuwa nini Kitatokea???

lakini pamoja ya yote hayo mabadiliko lazima Tanzania,,, Miaka 49 wameshindwa leo wataweza?????
 
Mengi ni mnafiki tu, anayejikomba kwa serikali. Sijui halipi kodi? Mie nimeacha kutumia muda wangu kwenye media zake long time. Sana sana naangalia mizengwe siku ya jumapili.
 
Jana vyombo karibia vyote viliandikiwa barua ya kuwaambia wasionyeshe tukio la mkubwa kudondoka kwenye taarifa zao za habari,"Kitendo cha kurusha tokio ili hewani itakuwa ni kumzalilisha kongozi wetu kwauma" hiyo ni sehemu ya barua hiliyo tumwa kwa vyombo vyote vya habari jana
 
Eti Rais alijisikia vibaya! Wapi! mbwembwe za kujionyesha laivu zilituonyesha akianguka chini, tiii. Wakahangaika walivyoweza na aliporudi na panic yao wakasahau kwamba hata kichwani alikuwa na vumbi.

Hawa tunaowaita wanahabari nadiriki kusema ni WAPUUZI (ashakumu ..). Ndo hawa ambao hutumia kamera kutuonyesha maiti za watanzania wanaopata ajali. Tangu MV Bukoba walionyesha, ajari za barabarani ndo kabisa watakuonyesha hata miguu iliyonyofoka utadhani ni bidhaa ya kukuza uchumi. Lakini eti mwanasiasa anayeanguka hadhalani, haonyeshwi. Ili iweje? Tuendelee na Rais mugonjwa! Kwani mpaka afie Ikulu. Hopeless media house
 
Back
Top Bottom