MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,185
Jana vyombo karibia vyote viliandikiwa barua ya kuwaambia wasionyeshe tukio la mkubwa kudondoka kwenye taarifa zao za habari,"Kitendo cha kurusha tokio ili hewani itakuwa ni kumzalilisha kongozi wetu kwauma" hiyo ni sehemu ya barua hiliyo tumwa kwa vyombo vyote vya habari jana
Nashukuru kwa maelezo hayo lakini hawa akina Mengi na Ryoba (Lyoba?), akina Shivji, na wote ambao nimekuwa nikiwaona mbele kabisa kutetea uhuru wa habari na mengineyo yanayoongeza uhabarishaji wananchi, wako wapi? Habari kama hiyo inapopotoshwa kiasi hicho wanasema nini? Au busara zao huishia kwenye mahojiano ya TV. Kuuza sura.
Katika nchi hii ni nani anastahili kudhalilishwa? Mbona akina mama wajawazito wanaonyeshwa wakiwa wamelala chini na matumbo yao bila heshima kwao. Tena si kwa kosa lao!
Ina maana sasa hivi tunafichwa habari kwa msaada wa vyombo vya habari, vinavyolalamika kila siku kwamba serikali inaficha habari.