Elections 2010 Uchaguzi 2010: ITV sasa imekuwa chombo cha CCM?

Elections 2010 Uchaguzi 2010: ITV sasa imekuwa chombo cha CCM?

Ndugu zangu,

Kulalamika tu humu kwenye jamii forums haitoshi, inabidi tuwaandikie barua NYINGI za kuwaonya uongozi wa ITV KUACHA mara moja kuwachagulia watanzanzania habari wanazozitaka wao na kuacha unafki wa kujipendekeza kwa JK kwani huo ni ufisadi wa hhabari, Tuandikene barua pepe na barua za kawaida kwenda kwa ITV sasa hivi kwenye email zifuatazo info@itv.co.tz , admin@itv.co.tz , ITV@ipp.co.tz or call them out right now on +255 (0)22 277 5914 / 5916 or send them a letter on Mikocheni Light Industrial Area, Plot 82 A
P.O. Box 4374
City Dar Es Salaam
Country Tanzania

Ni kweli ni kutuma ujumbe huko huko kuwauliza kwanini wanafanya hivyo na kuwaeleza kuwa hiyo siyo fair kwani hicho chombo japo ni cha binafsi ni kama cha umma kwani kama siyo huo umma then kisingekuwepo. Tutume kwa wingi tueleze tunavyokerwa. Mimi nimeshatuma.
 
Mengi inaonyesha ni bingwa wa kuigiza, kwani ana uwezo wa kujifanya kuwa anaumia na kusikitishwa na umasikini wa watanzania kumbe na yeye ni miongoni mwa watu walioharakisha ufukara wa raia. Mwone jinsi anavyojitahidi kuwafunga speed governor wapambanaji wa kweli wenye nia ya kuleta mapinduzi ya maendeleo ya taifa kwa walio wengi. Kwa kutumia vyombo vyake vya habari sasa amejiunga rasmi na mafisadi kuhakikisha anawawashikilia katika madaraka yao. Kwanza hawampendi ila yeye ameamua kujipendekeza kwao kwa sababu anazozifahamu. Ngoja Masha arudi madarakani aje kukamilisha kazi ya kumtengua Mengi. Na safari hii tutakaa upande wa Masha maana tushajiridhia kuwa Mengi ni miongoni mwa mafisadi, tena Mengi anachukua nafasi ya juu zaidi katika ufisadi kwani kazi ya kudhulumu haki ya kujitambua ya masikini wa Tz anayoifanya kupitia vyombo vyake ni mbaya kuliko ufisadi uwao wote. Niliwahi siku za nyuma kuandika hapa Jf kuwa vyombo vya habari vya Mengi ni fimbo yake ya kuwachapa watanzania. Na sasa ndio kazi vinafanya, vishatumwa rasmi na boss wao kuhakikisha watanzania hawapati habari huru za campaign.
 
Leo hata mimi nimeshuhudia. Vichwa vinavyosomwa ni vile vinavyokuwa na habari njema kwa CCM tu.

Hata hivyo hiyo inaweza kuwageuka wenyewe, watanzania tuko macho zaidi.
 
sio kwenye tv tu,leo hata kipindi cha magazetini cha radio one wameruka habari ya dr slaa kumlipua kikwete jangwani,ila wajue kuwa revolutionary ideas will never die in that way they are thinking:mad2::mad2:
 
malalamiko yenu yote yanatokana na kutokuwa tayari kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko hapa nchini na badala yeke mnataka mabadiliko yaje kama Tanganyika ilivyopatiwa uhuru wa mezani. Tukiacha hivyo vyombo vya habari, mnaolalamika mmechukua hatua gani za kuelimisha wananchi wanaowazunguka yale ambayo mnayaleta humu.

Kama tutategemea TBC na ITV ni bora tukaacha hata kulalamika. ASK YOURSELVES WHAT TANGIBLE ACTIONS HAVE YOU TAKEN TO BRING CHANGE?
 
Tusitegemee TV zetu hata kidogo; tubuni njia mbadala; ile ya Multi SMS (bulk) inaweza kusaidia; kumbukeni wamiliki wa mitandao pia mawakala wa CCM; lakini sms zitapenya let us be aggressive lakini sio vyombo vyetu; ngoja nifunge kingamuzi cha internet nielekee morogoro road kuangalia namna mambo yatakavyoanza kuweza kuweka support
 
ccm iko kila mahali, wewe unadhani ITV kutakuwa hamna watu wa kuwasimamia
ccm wako tiyari kutumia mbinu yeyote ile na ukikataa utakiona cha mtema kuni
 
ITV imekuwa na msimamo huo wa kisera, wa kuyatangaza tu magazeti yaliyo upande wa Chama Tawala. Ndio maana asubuhi huwa sitazami taarifa ya habari ya ITV. TBC1 na Channel Ten wana afadhali kubwa kuliko ITV.

ITV inajishushia hadhi yake. Wananchi wataligundua hili, wataacha kuiangalia, itapoteza fedha nyingi za watangazaji wa kibiashara.

--> ONYO: Kamwe usiwadharau wananchi, wao ndio wenye nguvu ya hoja.
 
Andikeni barua za wazi, mzipeleke kwenye magazeti, kwani mkiwaandikia wao, wanazichana na kuzitupa kapuni, na email wana-DELETE!

Pia, tumeni nakala kwa TCRA-CCC, huko wana wajibu wa kushughulikia malalamiko yao.

TBC1 ina afadhali ya kuwa na msimamo neutral kuliko ITV. ITV haiko huru hata kidogo. Ni pro-CCM left, right and centre!
 
Ni kweli ITV ni chombo huru, ila tatizo liko kwa Mmiliki wake maana siku zote anataka kutuaminisha kuwa ni mtetezi wa wanyonge,mpiga vita rushwa na ufisadi hasa ufisadi papa, na muumini mzuri wa haki za binadamu pia mcha Mungu. Sasa iweje aviamrishe (kama ni hivyo) vyombo vyake vya habari viwatete na kuwanadi kwa nguvu zote wale waendao kinyume na hayo anayotuaminisha kuwa ndiyo anayofuata? Na wale waletao njia mbadala za kumkomboa Mtanzania kama asemavyo yeye hawapi nafasi ya kutosha? Imani yangu kwake inaanza kutoweka. Na ninadhani siko peke yangu.

Hapana yeye wala si mchukia ufisadi, na hata kuwataja wale mafisadi mapapa ilikuwa kwa ajili ya ubinafsi wake tu na si kwa mapenzi ya nchi. Sasa ndipo sura yake halisi inaonekana, yeye ni Nyangumi kweki kweli na ajue tu kuwa siku inakuja na haiko mbali mapapa watakaposhughulikiwa na nyangumi hataachwa.
 
Mkuu naungana na wewe kabisaaaaaa, lazima tuchukue hatua na si kunungunika tu. Jiulize umechukua hatua gani kwanza, ni vizuri kusema hapa JF lakini chukua hatua ya ziada. Kila mtu anao wajibu wa kuleta mabadiliko, Mtikila huwa nampenda sababu huwa anachukua hatua, katika midani ya sheria ni mtu aliyeweka historia.
Mtaalam mmoja akasema kuna Manunguniko na Malalamiko, Malalamiko yanakwenda kwa ushahidi na sehemu husika, Manunguniko yanaishia yalikoanzia na hayana positive impact.
Ndugu zangu,

Kulalamika tu humu kwenye jamii forums haitoshi, inabidi tuwaandikie barua NYINGI za kuwaonya uongozi wa ITV KUACHA mara moja kuwachagulia watanzanzania habari wanazozitaka wao na kuacha unafki wa kujipendekeza kwa JK kwani huo ni ufisadi wa hhabari, Tuandikene barua pepe na barua za kawaida kwenda kwa ITV sasa hivi kwenye email zifuatazo info@itv.co.tz , admin@itv.co.tz , ITV@ipp.co.tz or call them out right now on +255 (0)22 277 5914 / 5916 or send them a letter on Mikocheni Light Industrial Area, Plot 82 A
P.O. Box 4374
City Dar Es Salaam
Country Tanzania

Hali kadhalika TBC tuwaandikie maoni yetu sasa hivi Kijitonyama, Off Bagamoyo Road
P.O. Box 31519
City Dar Es Salaam
Country Tanzania
Telephone +255 (0)22 2700 011 / 062
Telefax +255 (0)22 2700 468
Email tvt-dg@africaonline.co.tz
 
ITV na Nipashe nilikuwa nawaamini sana na kupoteza muda wangu nikiwanao lakini hivi sasa nawaona kama ukoma, na kumbe Mzee Mengi siku zote anajifanya yupo na wapiganaji wakati ni wazi sasa kajionyesha kuwa ni Papa Nyangumi lililojificha wakati nundu ipo nje, bora angekuwa kama Mzee Sobodo
 
Ni kweli ITV ni chombo huru, ila tatizo liko kwa Mmiliki wake maana siku zote anataka kutuaminisha kuwa ni mtetezi wa wanyonge,mpiga vita rushwa na ufisadi hasa ufisadi papa, na muumini mzuri wa haki za binadamu pia mcha Mungu. Sasa iweje aviamrishe (kama ni hivyo) vyombo vyake vya habari viwatete na kuwanadi kwa nguvu zote wale waendao kinyume na hayo anayotuaminisha kuwa ndiyo anayofuata? Na wale waletao njia mbadala za kumkomboa Mtanzania kama asemavyo yeye hawapi nafasi ya kutosha? Imani yangu kwake inaanza kutoweka. Na ninadhani siko peke yangu.

Tupo wengi mkuu, ukweli ametukwaza sana, ametusonenesha sana, na anatia kinyaa harakati zote alizoonyesha hapo siku za nyuma
 
Ipp kageuka mpiga debe wa ccm. Kibaya zaidi hawampende ila anajipendekeza kwa sababu anazozifahamu yeye mwenyewe. Nimekosa imani na vyombo vya mengi kama ilivyokuwa kwa gazeti la uhuru. Toka 1995 skuwahi kulisoma.
MOD ONDOA NA HII P/SE!!
 
Wajameni, habarizi za asubuhi. Ni imani yangu kuwa nyote hamjambo.

Nimesikitika sana wakati wa kuangalia kipindi cha magazeti ITV leo saa moja kasoro robo. Isac Gamba aalikuwa na magazeti mengi lakini alisoma vichwa vya habari vinavyozungumzia CCM tuu! Sasa nashindwa kuelewa kama ni kwa mataka yake binafsi kama mpiga kampeni wa CCM, au ni kwa mamlaka ya ITV?

It is so sad!

Kwani magazeti msimu huu yana habari gani zaidi ya hizo? na je kama kuna habari za CCM pekee angefanyaje? kwani yeye ndie mmiliki au mhariri wa hayo magazeti? loo mwacheni kaka wa watu. mmekosa lakumsema
 
Si tummulize dada Joyce Mhavile usanii huu wameanza lini. inakuwaje siku hizi hata habalr zinakuwa laini laini tu? Mbona naona kama wanataka upinzani usisikike? Mimi natoa ushauri kwa wanamtandao: tutafute namna ya kushinikiza sheria ya habari ibadilike ili iwe rahisi kuanzisha TV ya CHADEMA, kama ilivyo kenya, nasikia kuna chama chenye TV yake.
 
Kwani magazeti msimu huu yana habari gani zaidi ya hizo? na je kama kuna habari za CCM pekee angefanyaje? kwani yeye ndie mmiliki au mhariri wa hayo magazeti? loo mwacheni kaka wa watu. mmekosa lakumsema

...Changanya na za kwako...
 
Back
Top Bottom