Elections 2010 Uchaguzi 2010: ITV sasa imekuwa chombo cha CCM?

Elections 2010 Uchaguzi 2010: ITV sasa imekuwa chombo cha CCM?

Mengi ni mnafiki sana, jana gazeti lake la Nipashe limekuwa kama yale ya Mzalendo na Uhuru - kurasa za mbele ni kijani tupu na picha za kampeni za CCM.
 
Tunashukuru kuna mdau alituletea kwenye 'youtube' at least tukaona kilichotokea. Ni kweli ukombozi wetu kwa sasa ni iternet na wala si Vyombo vya habari uchwara kama vya IPP. Watajua tu kuwa nguvu ya umma ni kubwa. TBC1 na yenyewe kama ya CCM vile, yaani wanasahau kuwa yenyewe ni chombo huru cha umma ambacho hakitakikani kufungamana na upande wowote! Shame on them all. Tutakuwa tunategemea internet ama vyombo vya habari vya nje! Wadau, mkihudhuria rekodini hayo matukio mkayapeperushe kule kwenye "youtube' ama mtuletee hapa. Mimi nikipata fursa hiyo sitasita kuzirusha! Tumechoka na uozo huu!
 
ITV bado wanendelea kujizilisha kuwa wabaguzi

LEO saa 12.45 katika kipindi cha magazeti, wamesoma Uhuru, mtanzania, NIpashe(haya ni ya CCM), TAnzania Daima lenye mlengo wa kushoto na lenyewe limesomwa

Mwanachi yenye kichwa mlengo amabayo siku hiz imebadilika sijui RA kaifanya nini haikusomwa
 
Kama unavyosema Mrema na Mengi wapumbavu ndiyo unataka ku generalize wachaga wote wapumbavu,Next time jaribu kutumia akili kabla ya kupost upupu.

MIMI SIONI ALIPO GENERALIZE maana 1 & 2 tayari ni wingi....and the list seems to go on....Next time jaribu kusoma kwa makini kabla ya kupost upupu
 
sometimes tunawalaumu bure....

hizo ni directives wamepewa na wakaidi waone


saa mbaya hizi
Kama ulikuwepo vile
Inaonesha kuna vitisho nyuma ya any release. Je nani yupo behind all this within CCM? je ni dola ama chama chenyewe?
 
MAMA MPENDWA MARIA NYERERE MKE WA RAISI WA KWANZA NA KIPENZI CHA WATANZANIA..ASIYE NA PAPARA WALA KIMBELEMBELE ALIKUWEPO ...!.....NILIMUONA AKISALI SANA MAMA HUYU MCHA MUNGU...!

Lakini anasali dhidi ya hao mafisadi, sio kuwashabikia kama wewe.:eyeroll2::eyeroll2:
 
Ukimzungumzia bwana huyu anasifika sana kwa kupambana na ufisadi kwa nguvu zake zote kila anapopita na kutoa kauli. Ilifikia kipindi alijiunga na wapambanaji kama Kina Ole Sendeka na wenzake akizunguka majimboni kwao na kumwaga pesa za Vikoba. Nakumbuka kipindi fulani akijibizana na Rostam Azizi kuwa ni Fisadi Papa.

Leo hii vyombo vyake vya habari vimebadili mwelekeo na kukipamba chama tawala CCM mpaka kufikia kuuficha ukweli wa mambo mpaka hata pale vilipodiriki kutotangaza JK alivyoanguka Jangwani lakini hata Kesho yake ITV haikusoma magazeti yaliyoandika hiyo habari badala yake yalisomwa ya kwake ambayo hayakuipa uzito habari nzito kama ile na kuificha kurasa za ndani. Lakini nilisituswa walivyoamua kusoma magazeti waliyoyaacha muda mrefu ya habari corporation ya yule aliyeitwa fisadi Papa yaani Rostam Azizi na huo Ukawa mwanzo wa IPP media kumpigia debe JK kuwa Rais 2010.

Wanafiki wakubwa hawa watu na magazeti yao hatuyapendi tena na wasitudanganye hatudanganyiki na wanafiki. Wanatuonesha hawaelewani kumbe wakikutana wanakula na kunywa kwa kutufanya sie mazezeta. Tena vyombo vya IPP kama NIPASHE waongo sana mpaka wanajifagilia eti Gazeti hilo ndo linasomwa Zaidi Tanzania Wakati wanazidiwa na Magazeti ya Udaku ya Bwana Shigongo.

Kwani hata Tambwe Hiza aliwahi Kusema kuwa CCM ni bora akazini na Mama yake mzazi lakini sasa hivi ndo anakula na kulala huko mpaka tunasubiri kusikia alimlalaje na lini mama yake na je alipata ujauzito?

Wana JF mimi Tanzania nafahamu Magazeti Manne tu la Kwanza Mwanahalisi, la Pili Raia Mwema, la Tatu Tanzania Daima na la Nne Mwananchi Mengine yote ni Vijarida vya Hovyo
 

Alipewa karipio kali na serikali, aachane na tabia yake ya kupinga mafisadi na kujipendekeza kwa kina mama na miradi yao ya vibindo, serikali ilienda mbali zaidi kwa kuzuia ujenzi wa hospitali ya magonjwa ya moyo aliyoanza kujenga mkoani Kilimanjaro, kwa kisingizio kuwa serikali ilikuwa na mipango kama hiyo ya kujenga hospitali ya magonjwa ya moyo ndani ya hospitali ya taifa ya Muhimbili.
 
Moto aliodai kuuwasha Mengi sasa utamchoma yeye, hilo akae akijua.
 
Kwani hamjui Mengi ni mnafiki mkubwa. Leo atajidai kula na walemavu na masikini kesho anakula na mafisadi wanaosababisa huo umasikini.

Wakati wa uchaguzi wa 1995 alikuwa anaongoza kuwatisha wananchi hasa wanawake kuwa wakichagua wapinzani itatokea vita kama Rwanda na akawa anarusha picha za vita na mauaji ya Rwanda.

Huyu jamaa ni hatari sana hat serikali lazima imwangalie kw karibu, ukimwona usoni anajifanya mpole kutoa michango makanisani kumbe roho yake ni tofauti kabisa. Ni mtu wa kuogopwa sana anaweza kutumia vyombo vyake hata kusababisha mapigano kwa faida ya bishara zake.
 
Hakuna tajiri hata mmoja nchi hii atathubutu kupambana na ufisadi. Ni juu ya Watanzania masikini kutambua kuwa nchi yetu imejaa viongozi wala rushwa. Wanafaidi raslimali za nchi hii wao na familia zao. Siku zote huwa ninasononeka ninapoona Mtanzania masikini anashabikia CCM. Kibaya zaidi hata siku ya uchaguzi anakwenda kukichagua chama hiki (kwa ujira wa 10000 au tisheti na kofia) kilichojaa watawala wenye dhambi tele.Chama Cha Matajiri.
 
Si yule nyangumi wa rostamu.fisadi wa mafisadi
 
Mnanishangaza kila mnayemsapoti kwa asilimia kubwa baada ya miezi michache mnamgeuzia kibao. Mimi ningewashauri mtizame tena upya uwezo wenu wa kupambanua mambo.
 
bado natafakari kama mengi ni mpinga ufisadi au anawaonea wivu mafisadi wasije wakampiga gap
 
Niliposoma madai kuwa mengi siyo mwema kama anavyoonekana,kupitia maandiko ya mwl.mkuu wa watu,sikuelewa.sasa nimekubali kuwa mzee huyu ni mnafiki mkubwa.magazeti na tv zake ni wapenzi wa kampeni za mafisadi.kumbe kweli mbwa mwitu huvaa ngozi ya kondoo
 
Si alisema ni mwana chama wa CCM na akataja namba ya kadi yake
 
Mnanishangaza kila mnayemsapoti kwa asilimia kubwa baada ya miezi michache mnamgeuzia kibao. Mimi ningewashauri mtizame tena upya uwezo wenu wa kupambanua mambo.

Ina maana mpaka leo hii hujauijua JF?
 
Kwani ukiwa mwanachama wa CCM na vyombo vyako vya habari vinakuwa wananchama wa CCM vile vile? Havitakiwi kuwa OBJECTIVE?

Kama kuna EVIDENCE kwamba viongozi fulani wameiba mali ya umma, au wamekutwa na nyara za seriakli, na wewe ukaamuru magazeti yako au TV yako iwapigie kampeni, basi wewe ni FISADI.

Kama Mengi angeipenda Tanzania kweli basi angeagiza vyombo vyake vya habari viwe OBJECTIVE.

It's time to boycott Mengi's papers, radio and TV. Ni vyombo vya mafisadi.
 
Back
Top Bottom