"Rais anayo mamlaka ya kuagiza matumizi ya fedha za Serikali atakavyo"[/COLOR][/FONT][/I]
Kwa maoni yangu Kibonde ana ufahamu mdogo sana wa kitu kinachoitwa Separation of Powers between the State (Serikali), Legislature (Bunge) and Judiciary (Mahakama).
Kuteuliwa kwa Dr Slaa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA kulikuja kama mshituko kwa CCM JK na watanzania walio wengi. Na hoja yake ya kwanza wakati anafanya mikutano ya kutafuta wadhamini katika mikoa mbali mbali ilikuwa kutamka wazi wazi kuwa anazihitaji kura za wafanyakazi zilizokataliwa na mgombea wa CCM Jakaya Kikwete katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salam Mei 2010, na akachapisha fulana zenye ujumbe huo.
Ni kutokana na pressure hizi za kuanza kwa Kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2010 CCM, Kikwete na Serikali yake wakasalimu amri na kutoa nyongeza ya mishahara kutoka Shs 135,000/= kufika Shs 235,000/= kimya kimya. TUCTA, CHADEMA na wadau wengine wakataka kufahamishwa ni nini kinaendelea ndipo Rais akajitokeza katika mikutano ya Kampeni za CCM mkoani Mwanza kudai kuwa Serikali yake inawajali sana wafanyakazi na tayari imewaongezea mishahara.
Hoja kubwa ya Dr Slaa na CHADEMA sio wafanyakazi kuongezewa mishahara, bali wafanyakzi kutumika kama busati la kusafisha miguu na kukumbukwa baada ua upepo wa kisiasa kuwa mbaya kwa CCM na mgombea wake Jakaya Kikwete. Tujiulize kwa mtirirko uliotajwa hapo juu, iwapo vyama vya siasa vingesimamisha watu wasio makini kama Dr Slaa katika nafasi ya Urais, nyongeza ya mishahara iliyokuwa ikipigwa danadana kwa miaka minne kutoka 2006 na iliyotolewa wakati wa kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu ingepatikana?
Sambamba na hilo Dr Slaa na CHADEMA wanahaji kitendo cha Rais na Serikali yake kukikuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Ni Naomba wana JF wanaofahamu mipaka ya Rais kuagiza matumizi ya fedha za umma wakati usiokuwa wa dharura (emergency) bila ya kupata idhini ya bunge watusaidie kumhabarisha Kibonde kupitia hapa
Sijui kwa undani lakini asichojua Kibonde ni mgawanyo wa madaraka kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa uchache sana, matumizi ya serikali yanaidhinishwa na bunge, ndio maana bungeni waliidhinisha matumizi ya ikulu na hata vyombo vya usalama. Kama rais angekuwa na uwezo wa kutumia pesa atakavyo, ni kwanini serikali iliomba pesa za ukarabati wa ikulu na matumizi mengine?
Hata hivyo Rais ana nguvu za kisheria kuidhinisha matumizi ya pesa katika dharura kwa kitu kinaitwa [Executive power]. Dharura [emergency] inaelezwa kuwa ni
pamoja na mambo ya usalama wa taifa na majanga yasiyotarajiwa ambayo udharura wake huotoi nafasi kwa taratibu za kawaida kufuatwa, kwa uchache tu. Kuongeza mishahara halikuwa jambo la dhahrura,lakini pia linaweza kuhojiwa, ni kutoka fungu gani lililoidhinishwa na bunge nyongeza hiyo imepatikana!!!!
Wanacholalamika Chadema si ongezeko la mishahara kama inavyobadilishwa. Wana hoja ya kuwa taratibu za kuidhinisha nyongeza hazikufuata taratibu na kibaya zaidi suala hili limefanywa katika mikutano ya kisiasa hasa baada ya chadema kuichukua kama hoja. Hapa kuna ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi ambao CCM wenyewe wameridhia. Ukiukwaji huu ndio umesababisha kukiukwa kwa taratibu kwa sababu Wafanyakazi walionekana kuwaelewa chadema zaidi, na hakukuwa na njia ya kujibu mapigo[counter attack] isipokuwa kuongeza mishahara bila utaratibu na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.
Tatizo la vyombo vyetu vya habari ni kukosa wataalam katika fani ya uandishi wa habari. Hata kama kibonde angekuwa na utaalam bado aliwajibika kuwasiliana au kuwakaribisha wataalam wa mambo ya sheria ili kufafanua na sio kuwafanya wasikilizaji waamini maoni yake. Pamoja na hayo Kibonde hakutumia kanuni za asili '' natural justice'' kwa kuwasikiliza Chadema nao. Kwa wale wanaoangalia TV au kusikiliza radio zilizokwenda school, pande husika hupewa nafasi ya kusikilizwa.
Na mwisho kama CCM walifuata taratibu, basi watueleze kwa kutumia kumbukumbu gani za bunge ''Hansard'' wapi jambo hili lilikubaliwa na bunge.
Endapo 'rais anaweza tumia pesa atakavyo, kama kibonde anavyoamini, ni kwanini tuwalipe watu 320 kwa siku 60 pale Dodoma kupitia makadirio ya fedha '' Budget'' ? Kibonde jiulize na utafakari kama una uwezo huo.