Elections 2010 Uchaguzi 2010: Kibonde usijifanye kujua kila kitu, tafuta wataalamu wakusaidie

Elections 2010 Uchaguzi 2010: Kibonde usijifanye kujua kila kitu, tafuta wataalamu wakusaidie

Thanks for bringing back mjadala, tuna wanasheria watatuhabarisha... tukishindwa tutamuandikia mshauri wa rais atufundishe,
.....mwaveja sana DOCEBIT VOS OMNIA (D.V.O)......!

hivi na katiba inasemaje kuhusu mipaka ya rais na ya mgombea urais endapo anakua huyohuyo?
....D.V.O hili ni swali la msingi sana sana.....linahitaji sredi yake mkuu! binafsi naona kabisa kama hakuna provisions kny katiba on this, mgombea urais aliye rais anakuwa na added advantage kubwa sana.....kuna kuwa hakuna same playing field....na to me kwa hilo tu linatosha kuufanya uchaguzi mzima kutokuwa HURU na HAKI!

...
 
MR-II-PICS-742425.png
 
Katika kipindi cha Jahazi cha tar 31/8/2010 mtangazaji Kibonde amejifanya kuwa mtetezi wa JK na CCM kwa kuliponda pingamizi ya Dr Slaa na CHADEMA kuhusu JK kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Kwa bahati mbaya sana katika kutekeleza jukumu hilo Kibonde alizidi kudhihirisha umbumbumbu wake hadharani pale alipodai kuwa "Rais anayo mamlaka ya kuagiza matumizi ya fedha za Serikali atakavyo"

Kwa maoni yangu Kibonde ana ufahamu mdogo sana wa kitu kinachoitwa Separation of Powers between the State (Serikali), Legislature (Bunge) and Judiciary (Mahakama). Hajo ya CHADEMA katika sakata hili ni mgombea wa CCM Jakaya Kikwete na Serikali yake ni kufanya matumizi ya fedha za umma kwa kukiuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Kwa mujibu wa Katiba Bunge ndio lenye jukumu la kuidhinisha makusanyo na matumizi ya fedha za Serikali.

Kutokea mawaka 2006 TUCTA iliwasilisha madai ya nyongeza za mishahara kwa watumishi wa Serikali kufikia kima cha chini cha Shs 315,000/=.

Kutokea mwaka 2006 JK na Serikali yake hawakuchukua hatua zozote kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa maana ya kupeleka ombi kwa bunge la kufanya matumizi ya ya ziada katika kulipa mishahara ya watumishi. Hivyo Bunge la 2006, 2007, 2008, 2009 na hata la 2010 Kikwete na Serikali yake walishindwa kuwasilisha ombi hilo.

Wakati Serikali ya JK ilishindwa kuwasilisha ombi la kuongeza mishahara ya watumishi wake wanyoinge. Inadaiwa katika kipindi hicho iliwaongezea mishahara na marupurupu za viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Majaji n.k na pia kulipa malimbikizo ya nyongeza hiyo. Kama tutakumbuka vizuri wabunge wenye jukumu la kupitisha matumizi ya Serikali walipoona vigogo wenzao Serikalini wamejiongezea mishahara na marupurupu; wabunge nao wakawasilisha mapendekezo ya kuongezewa mishahara na marpurupu na wakapata.

Ni kwanini CCM , Kikwete na Serikali yake waliamua kuwadharau wafanyakazi kwa miaka minnne kutoka mwaka 2006, na kuendelea kuwadharau hata pale walipotishia kugoma mwi 2010? Jibu walifanya hivyo kwa kuwa walijua TUCTA inaongea peke yake, haina asasi ingine ya kuisaidia hivyo Serikali itaweze kutumia vitisho kuzima jeuri ya TUCTA na Mgaya.

Kuteuliwa kwa Dr Slaa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA kulikuja kama mshituko kwa CCM JK na watanzania walio wengi. Na hoja yake ya kwanza wakati anafanya mikutano ya kutafuta wadhamini katika mikoa mbali mbali ilikuwa kutamka wazi wazi kuwa anazihitaji kura za wafanyakazi zilizokataliwa na mgombea wa CCM Jakaya Kikwete katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salam Mei 2010, na akachapisha fulana zenye ujumbe huo.

TUCTA ilipoona imepata msemaji wa kusaidiana naye katika kudai haki za wafanyakazi zilizokuwa zikipigwa danadana kutokea 2006, haikubweteka ikatoa tamko kwa wanachama wake kuwa wampatie kura mgombea anayeonyesha kuhitaji kura za wafanyakazi, kwa kuwa haiwezekani "ukampatia pilau mtu asiyeihitaji".

Ni kutokana na pressure hizi za kuanza kwa Kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2010 CCM, Kikwete na Serikali yake wakasalimu amri na kutoa nyongeza ya mishahara kutoka Shs 135,000/= kufika Shs 235,000/= kimya kimya. TUCTA, CHADEMA na wadau wengine wakataka kufahamishwa ni nini kinaendelea ndipo Rais akajitokeza katika mikutano ya Kampeni za CCM mkoani Mwanza kudai kuwa Serikali yake inawajali sana wafanyakazi na tayari imewaongezea mishahara.

Sasa Kibonde atuambie katika mtirirko huu wa matukio, ni kweli CCM ya leo na JK wanawajali wafanyakazi? Walikuwa wapi kwa miaka minne kuwapatia wafanyakazi nyongeza hiyo?

Hoja kubwa ya Dr Slaa na CHADEMA sio wafanyakazi kuongezewa mishahara, bali wafanyakzi kutumika kama busati la kusafisha miguu na kukumbukwa baada ua upepo wa kisiasa kuwa mbaya kwa CCM na mgombea wake Jakaya Kikwete. Tujiulize kwa mtirirko uliotajwa hapo juu, iwapo vyama vya siasa vingesimamisha watu wasio makini kama Dr Slaa katika nafasi ya Urais, nyongeza ya mishahara iliyokuwa ikipigwa danadana kwa miaka minne kutoka 2006 na iliyotolewa wakati wa kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu ingepatikana?

Sambamba na hilo Dr Slaa na CHADEMA wanahaji kitendo cha Rais na Serikali yake kukikuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Ni ukiukwaji huu uliosababisha kuwepo kwa Kashafa ya EPA, Meremeta, Tangold, n.k.

Naomba wana JF wanaofahamu mipaka ya Rais kuagiza matumizi ya fedha za umma wakati usiokuwa wa dharura (emergency) bila ya kupata idhini ya bunge watusaidie kumhabarisha Kibonde kupitia hapa

HAYA ANYOSEMA KIKWETE NI SAWA...NI SERA ZA CHAMA.CHAKE NA AHADI AMBAZO UTEKELEZAJI WAKE SIO LEO, BUNGE SI LITAKAA OCTOBER KUNA TABU GANI KUOMBA FEDHA ZA DHARURA....HIZI NI SERA ZA MAENDELEO NA MATUMIZI YA KAWAIDA YA SERIKALI ....KAMA HAPO MWANZO SERIKALI ILIKUA HAINA UWEZO ....SASA UMEPATIKANA NDIO MAANA ANAJUA WATAWEZA...
SASA UNAPOSEMA UTASHUSHA VAT !!! UTAONDOA USHURU WA VIFAA VYA UJENZI WAKATI HAIWEZEKANI..SHERIA HIZI ZINATAWALIWA NA SHERIA ZA KODI ZA JUMUIA YA AFRICA MASHARIKI...HUWEZI KUSHUSHA TU KODI KIHOLELA....NA KUFUTA KODI HAKUMFANYI MTU KEJENGA....WATU WANAHITAJI KUWEZESHWA...NTAKUPA MFANO LEO...VIFAA VYA SOLAR NI DUTY FREE ..WANGAPI WAMEWEZA KUWEKA SOLAR? COMPUTER PIA NI DUTY FREE ..WANGAPI WANA UWEZO WA KUNUNU ACOMPUTER ? SO HATA AKIPUNGUZA KODI IWE ZERO..KAMA WANANCHI HAWANA uwezo wataendelea kujenga kwa kutumia dongo...saruji itakuawa ndoto..
JEE UNAPOSEMA ELEIMU BURE MPAKA FORM 6 ....WHAT IS THIS????? ......KUWENI WAKWELI MAMBO NI MAZITO....WACHENI KULALAMIKA TWAMBIENI MUTATUFANYIA NINI ILI TUWAPE KURA ZETU MAMBO YA MIHEMKO HAYASAIDII KITU...
 
Bunge lipi litakaa October na hali limeshavunjwa? Kweli nyinyi CCM hamna hoja kabisa ndiyo maana hata mgombea wenu kaukimbia mdahalo kwa kuogopa hoja!!! Mnatia aibu kwelikweli!!!!
 
HAYA ANYOSEMA KIKWETE NI SAWA...NI SERA ZA CHAMA.CHAKE NA AHADI AMBAZO UTEKELEZAJI WAKE SIO LEO, BUNGE SI LITAKAA OCTOBER KUNA TABU GANI KUOMBA FEDHA ZA DHARURA....HIZI NI SERA ZA MAENDELEO NA MATUMIZI YA KAWAIDA YA SERIKALI ....KAMA HAPO MWANZO SERIKALI ILIKUA HAINA UWEZO ....SASA UMEPATIKANA NDIO MAANA ANAJUA WATAWEZA...
SASA UNAPOSEMA UTASHUSHA VAT !!! UTAONDOA USHURU WA VIFAA VYA UJENZI WAKATI HAIWEZEKANI..SHERIA HIZI ZINATAWALIWA NA SHERIA ZA KODI ZA JUMUIA YA AFRICA MASHARIKI...HUWEZI KUSHUSHA TU KODI KIHOLELA....NA KUFUTA KODI HAKUMFANYI MTU KEJENGA....WATU WANAHITAJI KUWEZESHWA...NTAKUPA MFANO LEO...VIFAA VYA SOLAR NI DUTY FREE ..WANGAPI WAMEWEZA KUWEKA SOLAR? COMPUTER PIA NI DUTY FREE ..WANGAPI WANA UWEZO WA KUNUNU ACOMPUTER ? SO HATA AKIPUNGUZA KODI IWE ZERO..KAMA WANANCHI HAWANA uwezo wataendelea kujenga kwa kutumia dongo...saruji itakuawa ndoto..
JEE UNAPOSEMA ELEIMU BURE MPAKA FORM 6 ....WHAT IS THIS????? ......KUWENI WAKWELI MAMBO NI MAZITO....WACHENI KULALAMIKA TWAMBIENI MUTATUFANYIA NINI ILI TUWAPE KURA ZETU MAMBO YA MIHEMKO HAYASAIDII KITU...

kwani hata Obama alipoahidi kurejesha majeshi ya USA nyumbani hakujua kuwa Senate iliidhinisha ? CHADEMA inaomba Ridhaa ya kuiongoza kwa namna wanayoona bora, na sikwakufuata yale ya CCM, wanataka kurejesha nidhamu na adabu katika matumizi ya Raslimali za umma.tunavyo vipaumbele vyetu, KWANZA KUBADILI KATIBA, kisha kukamata wezi woote wa pesa za umma, kuikisha wale woote walioiba fedha za kupitia EPA, deepgreen Meremeta , kisha kuwapeleka mahakamani waliohusika na ununuzi wa Rada, kuuza mashangingi, kupunguza mishahara ya Wabunge na mawaziri, kuongeza mishahara, kufuta Kodi kwenye mikataba ya madini, na kuongeza ukusanyaji kodi kupitia Loyarities katika export.toka ndani ya Box fikiri kwa makini.
 
bunge lipi litakaa october na hali limeshavunjwa? Kweli nyinyi ccm hamna hoja kabisa ndiyo maana hata mgombea wenu kaukimbia mdahalo kwa kuogopa hoja!!! Mnatia aibu kwelikweli!!!!

baada ya uchaguzi november..kama mkono umeteleza ...lakini hoja ya msingi umeipta..
Mdahalo unafanya na watu walo tulia na wanaoheshimu rules za midahalo....mihemko ubishani , haikubaliki....haina faida ...afadhali kufanya mdahalo na lipumba unajua kutakua na ustarabu....
 
Au Bunge likivunjwa, waziri anaendelea na uwaziri wake? Manake katiba inasema Waziri ni lazima awe mbunge!!!

Kama hiyo haitoshi na wale mawaziri waliopigwa chini hatakwenye kura za maoni bado wanaendelea kuhodhi nyadhifa za uwaziri.... imekaaje hii?

Lemme check with Teamo, sore, Kibonde....Hii mada itanisaidia sana kukabiliana na adha ya foleni ya leo jioni wakati wa JAHAZI na Efremu Kibondee!!:welcome::welcome:

Yeah nadhani there are more questions than answers, but that haimfanyi kibonde kuwa sahihi kukejeli wasio wanaCCM
 
Name calling aside.

TEAMO=KIBONDE=TEAMO.

AKIBISHA NA OPEN ZE FILE YAKE HAPA.

Namjua sana huyu XXXXX.
 
Back
Top Bottom