Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe kwenu !
Natumai wote mu wazima na mnaendelea vizuri na majukumu yangu.
Kama kawaida yangu kazi yangu ni kuangalia na kuonya ivyo Leo napenda niseme kwa macho yangu naona CCM anapambana na nani hasa kwenye uchaguzi wa mwaka huu??
Kwa maoni yangu katika mwaka huu CCM anapambana na watu wafuatao!
1. Wapinzani
Hawa kila mtu anawajua. Ni vyama pinzani ambavyo nao majukumu yao ni kushika dola. Wao ni maadui wanaoonekana na wanajulikana hasa kwa CCM
2. Watu wa System wasioridhishwa na mwenendo wa JPM
Hawa ni watu hatari zaidi. Hili ndo kundi linaloongozwa na kina Kigogo. Kuna watu wanadhani kigogo wa Twitter ni mtu mmoja ila la hasha. Kwa mtazamo wangu hawa ni mjumuiko wa watu very smart within the system ambao hawarudhishwi na jinsi nchi inavyoenda.
Hawa ni watu wenye akili sana na wanajua kila move wanayoifanya na wanajua wanafanya nini ili wapate nini.
CCM kuweni makini sana na hawa watu
3. Western World.(Mabeberu kwa lugha ya vijana wa Lumumba)
Hawa ingawa Ccm wanawajua ila hawajui wamepanga nini. Hawa ni watu smart zaidi kuliko kundi la pili tajwa hapo juu. Hawa wanajua kupanga. Wanajua kila kitu kinachoendelea nchini na serikalini na hata pia ikulu. Siku zote Ccm walikuwa wanajua kuishi kinafiki na kundi hili ila bahati mbaya sasa wameshindwa kuishi nao kinafiki ivyo kupelekea hili kundi kuamua kuanza kupiga simu maaana kwa awamu hii wameshabipiwa saana na serikali ya awamu ya tano.
4. CCM Asili
Hili ni kundi pia linalojulikana ila limebanwa sana. Hawajui watoke vipi ila wakipata nafasi tu wametoka. Hawa hawapatani kabisa na mzee Magu na wanaona ilikuwa bahati mbaya sana mzee Magu kuchukua usukani. Hawa wanasubiri tu support kutoka kwa kundi namba 2 na 3 na wakipata nafasi wamemaliza
5. Watumishi wa Umma
Hawa ni watu waliojeruhiwa sana na awamu hii. Ni miaka 4 sasa hawajaona nyongeza ya mishahara na kwa sasa wako tayari kufanya kazi na yeyote atakaeonesha anaweza kuwasikiliza mahitaji yao.
Wito
CCM kati ya Mwaka mnaotakiwa kuwa makini na kujiandaa kwa lolote ni mwaka huu!
Kwa Mzee wangu Magu!
You need smart people wanaoweza kucheza huu mchezo. Achana na hao wanaokupaka mafuta kwa Mgongo wa Chupa. Nafasi bado unayo jipange vizuri.