Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,550
Heshima kwenu wakuu!
Kama wengi tunavyojua watanzania tunatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Kwa kujifunza kutokana na uchaguzi mkuu uliomalizika nchini Kenya hivi karibuni ni wakati sasa kwa Tanzania kuendesha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa pamoja, yaani tuchague. Rais, mbunge, diwani, mwenyekiti wa mtaa/Kijiji na mwenyekiti wa kitongoji.
Ikiwezekana pia wabunge wa viti maalumu tuwachague sisi WANANCHI badala ya kuteuliwa na vyama.Kama Kenya wameweza kupiga kura 6 kumchagua Rais, Gavana, Seneta, mbunge na mwakilishi wa wanawake kwa nini sisi tushindwe?
Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza gharama za uchaguzi kwa kiasi kikubwa na pia uchaguzi Tanzania utakuwa unasimamiwa na chombo kimoja ambayo ni tume ya Taifa ya uchaguzi badala ya uchaguzi wa serikali za mitaa kusimamiwa na serikali kupitia TAMISEMI.