Uchaguzi Afrika Kusini 2021

Uchaguzi Afrika Kusini 2021

las Casas

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2015
Posts
575
Reaction score
720
Kesho Afrika kusini itafanya uchaguzi wa serikali za mitaa(LGE). Ushindani mkubwa ni kati ya ANC, DA na EFF .
Licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali Kama madini nchi hii ya bondeni mwa Afrika imekumbwa na wimbi kubwa la.
*Ukosefu wa ajira
*Umaskini
* Ukosefu wa usawa
*Uhalifu
*Rushwa

Uchaguzi huu ni kipimo kwa chama tawala ANC ambacho wachambuzi wa kisiasa wanakiona ni chama kinachopoteza ushawishi licha ya kuwa chama tawala toka 1994 baada ya serikali ya makaburu kukoma baada ya uchaguzi.

Katika uchaguzi Afrika kusini Kuna haki ya kupiga kura maalumu (special vote). Kura hizi hupigwa na watu wote waliojiandikisha kupiga kura lakini wao wanapiga kura kabla ya siku ya uchaguzi. Watu hawa ni wagonjwa , wajawazito , walemavu nk. Kwa mfano mwaka huu katika uchaguzi wa serikali za mitaa upigaji wa kura maalumu ambazo zitaonganishwa na kura nyingine ni siku mbili tarehe 30 na 31 oktoba. Uchaguzi ni kesho tarehe 1 Novemba.

Natamani NEC yetu ifanye Kama ilivyo South Afrika katika suala la special vote ili watanzania ambao wataona siku za uchaguzi hawawezi kushiriki kikamilifu kutokana na magonjwa au ujauzito kwa kuhofia kupanga mistari kwa muda mrefu wawe wanapiga kura maalumu kabla ya siku ya uchaguzi

ANC ni mojawapo ya vyama vikongwe Afrika ambavyo vinajivunia kupambania uhuru lakini vimeshindwa kuboresha Maisha ya raia.
 
Hii spesho vote ndo ilitumika kuibia Kura Zanzibar
 
Back
Top Bottom