Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi


- Ninasema hivi acha vitisho kama una hoja weka hapa, Zitto aka Dowans hana jipya ni CCM-Mtandao.

FMES!

Mbona mie sioni hizo unazoziita hoja kutoka upande wako?
FMES, unakimbia kivuli? labda uende busanda ukatupe karata yako huenda ukapunguza shari japo kuwa nusu shari.
 
Mbona mie sioni hizo unazoziita hoja kutoka upande wako?
FMES, unakimbia kivuli? labda uende busanda ukatupe karata yako huenda ukapunguza shari japo kuwa nusu shari.
i dont get the guy!!
 
Mbona mie sioni hizo unazoziita hoja kutoka upande wako?
FMES, unakimbia kivuli? labda uende busanda ukatupe karata yako huenda ukapunguza shari japo kuwa nusu shari.

Hakuna tusi wakuu, msitake kututoa kwenye hoja kwamba sasa mkonga wa tembo CCM umengatwa na sisimizi! Atajigonga kwenye miti weeee hadi ukatike ama aanguke pwaaaaa!

tangu lini CCM wakawalalamikia wapinzani? Tulizoea siku zote wapinzani wakilalamika, lakini taratiiiiiiibu kibao kina badilika, CCM ndo kwanza wanaanza kuwa walalamishi., mara hoo, hatuja zomewa, mara hoo mmeleta mamluki, waaaapi? yaani huwezi amini but ndo ukweli wakuu
 
..huu mjadala ni fruitless wakubwa, haujengi ila utaonyesha tu ushabiki zaidi...nilisikia serikali leo itatoa tamko kuhusu suala la Mengi na Rostam kuna mtu amepata habari yoyote?? na pia nimesikia subash patel nae amejibu mapigo lakini hataki kesi...
 
CCM ni Chama kikubwa sana na miaka mingi madarakani , kama kweli wanakubalika na kama kweli wana deliver kwa nini sasa tunaona mizengwe mingi hivi muda wote ? Tarime na sasa Busanda je mwaka 2010 itakuwaje ?Si lilikuwa jambo la kuonyesha mafanikio tu na wao wanachaguliwa tena ?
 
- Irrelevant na haina faida yoyote kwa masilahi ya taifa, Nchimbi sio Chadema!

Respect.

FMES!

Ukweli Unauma! naona umeamua kunipeleka kwa nchimbi ila kujikosha. Sasa nakwambia nchimbi ni mwanachama mwenzio kwenye chama chenu na wote nyie yes including you ndiyo mnaoua mama zetu waja wazito na watoto kabla hawajafika miaka mitano kwa policy zenu mbovu. Halafu unakuja hapa unajidai unalinda taifa kumbe ni soar looser ya mgomea wako 2005! and Yes RA aliwaliza kwani nyie wote ni majambazi na majambazi huzidiana kwa ujambazi. Utasikia sasa hivi oooh nilikuwa na waziri mmoja kaniambia kuwa bla bla bla! hayo ndiyo maslahi ya taifa!
 
Last edited:

Hizi ndo zile salamu kwa Mjomba za Mpoto, Wanatuahidi kutununulia viatu, lakini baada ya miaka mitano wanarudi na kutuuliza mnavaa viatu namba ngapi. Mbunge aliyekufa alikuwa wa CCM na sasa huo umeme, maeneo ya wachimbaji wadogo au mikopo kwa nini havikuja kwa miaka mitatu iliyopita (achilia mbali miaka mingine ya nyuma ambayo jimbo hili pia lilikuwa chini ya CCeM). Lakini si ni serikali ya CCeM hiihii ambayo iliwafukia wachimbaji wadogo kwenye migodi ya Bulyankulu wakati wakiwafukuza!!!! na pia nani asiyejuwa kuwa kule Mara wachimbaji wadogo walifukuzwa ili migodi hiyo wapewe hao waporaji ambao hawalipi kodi.

Ee Mungu waite kwako jamii ya kina JSM wasiotosheka na madaraka kutoka kwenye Uwaziri Mkuu hadi Ubunge. Mimi nadhani walitakiwa kuwa kama Warioba
 
“Nataka kuwaeleza iwapo mtamchagua mgombea huyu, basi serikali italeta umeme eneo hili….
Hizo ndio sera za tinga tinga.....akapumzike miaka 19 mjengoni hakuna alichofanya......hivi hawa wazee ni mpaka wafie mjengoni?
 
Waziri Ngeleja awekwa 'kiti moto' Busanda

Na Frederick Katulanda, Busanda

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja jana alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuzongwa na kundi la wananchi waliomuhoji juu ya ahadi zake za umeme alipowasili katika mji wa Katoro wilayani Geita.

Tukio hilo mithili ya mdahalo lilitokea kati ya majira ya ya saa 9:30 hadi saa 10:15 muda mfupi tu baada ya Ngeleja kuwasili Busanda akitokea Mwanza.

Maswali yalianza baada ya Waziri Ngeleja kusalimiana na wananchi hao na akajibiwa kwa kuonyeshwa alama za vidole viwili.

Hali hiyo ilimfanya waziri huyo kuwauliza wananchi hao sababu za kuichukia CCM wakati imekuwa ikijitahidi kuwaletea maendeleo na ndipo walipoanza kumuuliza maswali huku akiyajibu wakati fulani kugeuka mabishano.

"Hatuwezi kuwashangilia nyinyi... mmetuahidi umeme siku nyingi na hatuuoni, leo mnakuja kutuambia nini. Alikuja hapa sijui (Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam) Malima akasema umeme utakuja, lakini wapi hatujaona lolote mpaka leo," alisema mwananchi mmoja.

Ngeleja alipotaka kujibu, mwananchi mwingine alidakia kusema: "Hata kwenye machimbo mmekuwa mkitunyang'anya maeneo yetu na kuwapa wawekezaji. Sisi mnatuona hatufai kama vile ni wakimbizi ndani ya nchi yetu."

Ngeleja alilazimika kuwatuliza na kuwaomba wapunguze maswali ili ajibu swali moja baada ya jingine, lakini kila mtu akataka kumuuliza swali na kukawa na msuguano kati yake na wananchi.

Alianza kujibu kwa kusema kuwa serikali ipo mbioni na kwamba kinachofanyika sasa ni kufuata taratibu kwa sababu mchakato wa suala hilo hauwezi kumalizika siku moja, hivyo akawaomba wawe watulivu wakati mchakato ukiendelea.

Ngeleja alidai kuwa suala lao kuhusu umeme liko katika hatua ya kuridhisha na kwamba wanapaswa kutambua utaratibu wa kushughulikia miradi ya serikali umekuwa ukifanyika kwa hatua.

Majibu hayo yalipingwa na wananchi ambao walimwambia wamekuwa wakidanganywa kama watoto kwa sababu ya kutaka kura na wakishapata, hutoweka.

"Sikiliza basi nikujibu, wewe naona umetanguliza ushabiki tuu. Naomba unisikilize. Ni kweli tulipowaahidi umeme tulidhani mchakato ungekamilika mapema, lakini kuna mambo yametukwamisha, tunaomba mtuvumulie," alisema huku wananchi hao wakiendeleza maswali.

Wakati wakiendelea na mjadala huo, lilipita gari la mgombea CCM wa kiti cha ubunge cha Busanda, Lolensia Bukwimba na mara moja wananchi hao wakageuka na kuanza kuzomea msafara.

Wakati wakiendelea kuzomea ndipo Ngeleja alipopata mwanya na dereva wake akawasha gari na kuondoka.

Waziri Ngeleja alitaja mlolongo wa maeneo ambayo alisema mengi yatapata umeme kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, lakini mkakati wao wa umeme ulitibuliwa baada ya Bunge kukataa kuinunua mitambo ya umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited. CCM imekuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa kampeni za ubunge wa jimbo hilo lililoachwa wazi na Faustin Kabuzi Rwilomba ambaye alifariki akiwa nchini India alikoenda kutibiwa.
 
Last edited by a moderator:
Saaaaaaaaaaaaaaafi sana mtakiona cha moto mwakani sio mbali tunahesabu siku tu.
 
Duh!!! Dowans amewapa nini viongozi wetu jamani??????

Dowans! Dowans mpaka Busanda!
 
Waziri Ngeleja alitaja mlolongo wa maeneo ambayo alisema mengi yatapata umeme kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, lakini mkakati wao wa umeme ulitibuliwa baada ya Bunge kukataa kuinunua mitambo ya umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited.

Kumbe Ngeleja alikuwa na mipango ya muda mrefu na Dowans, mbona hakuliambia bunge?

Makubwa haya kumbe jenereta uamuzi ulishapita kuzinunua.
 
A very good move! hii inaonyesha watu wamechoka. Nilidhani hiyo sehemu wangekuwa hawjui kinchoendelea kwa kuwa hawana umeme lakini kumbe sasa kila mtu kokote anajua kinachoendelea...mbichi, mbivu kama kazi. Safi sana.
 
Picha sijaziona kwani nina usongo wa kulinganisha na malalamiko ya CCM jana!Tuwekee basi tuone.au nawewe ulipewa bahasha jana?
 
Picha sijaziona kwani nina usongo wa kulinganisha na malalamiko ya CCM jana!Tuwekee basi tuone.au nawewe ulipewa bahasha jana?

Jana kulikuwa na bahasha? zipi mkuu na zili husu nini? mwaga mkuu hapa ndo mahali pake
 
Jamani hamzioni kweli ama mnatania? Jamaa na vidole juu wakionyesha alama ya CHADEMA!
 
sasa watakuwa na tofauti gani na wale ambao wameshapewa nchi.. tumeshazoea si ndiyo?

Kutakuwa na tofauti kubwa sana. Kwamba watatuongopea in a different way sio kwa ile ambayo tumekua tumeizoea. Kwahiyo bora tu tu-experience the difference.

...mimi hata sijui kama nimeziona.
 
Re: CHADEMA Busanda katika picha.

Mmh! jamani mmeziona picha kweli, mbona nasubiri sioni nzito wala nyepesi... alihutubia hewa au ...wameshaingiza mkono kwenye mtandao tusione?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…