Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Hili la Diwani wa CCM kununua shahada ni vema kama Makamba akalitolea tamko. Zile tuhuma kuwa CCM inahadaa watu na kuiba kura wamekuwa wakizikanusha mara kwa mara lakini Kule Tarime alikamatwa kiongozi wa CCM akinunua shahada na sasa hili la Busanda.
Hivi kweli bado ujanja huo wa kijinga bado wanautumia? Hata viongozi wao wa juu kusimama na kusema "tuko madarakani kwa ridhaa ya wananchi" huku wakinunua shahada kwa wapiga kura ambao wanaziuza kutokana na umasikini wao na ujinga uliopandikizwa kwa miaka yote hii, hawaoni aibu? Sasa naanza kuamini kuwa CCM ule mshipa wa aibu ulikatwa siku nyingi zilizopita.
 
Hii kali huyu mwalimu mkuu wa hiyo secondary inabidi afuatiliwe kwa makini lasivyo jamaa akipita inabidi tumfanyie uchunguzi kama hajafuja fedha za shule ikibainika ataozea jela hivi hivi si angeecha tu kwani wewe ukiwa shabiki wa Simba kwa hiyo wanafunzi wasishangilie Yanga hii hapata.
Alafu huyo diwani amedhihilisha kuwa CCM maji ya shingo na ndo mchezo wao siku zote watakiona cha moto huko Busanda.
 
mimi huwa nahisi waandishi wa habari ndio wengi wachangiaji humu. Wanaona uvivu kuanza upya kuframe habari bora waitumie kama walivyoituma gazetini.
 
Kwani toka lini wanafunzi hawaruhusiwi kushabikia vyama vya siasa? au ndio yale ya kunya anye kuku akinya bata kaharisha? mbona chipukizi wa CCMhh ni wanafunzi?
 
Kitendo alichofanya Zitto cha kuchoma jeneza na kitambaa cha kijani, sio cha kistaarabu, hata kama jeneza halina mwili, linahitaji heshima yake kwa vile hutumika kusafirisha watu kwenye ile safari ya mwisho. Na kitambaa cha kijani, japo sio bendera halisi ya chama bali inafaahamika by implication.Uchaguzi huu wa Busanda, unanisikitisha sana jinsi wapinzani wanavyoukosa ushindi wa mteremko kwa kukubali kugawana kura kati ya CUF na Chadema hali ambayo itaipa ushindi CCM. Chadema na CUF wangeunganisha nguvu, for sure, Busanda ni yao.Najipanga kuelekea Busanda, kushuhudia hali halisi nisingoje kuhadithiwa.
 
The sideshows are going to distract the much eeded dialogue, and if CHADEMA is not focused, it runs the risk of confusing voters.


Yes kama ni kweli, basi hizi side show zinaharibu mambo; itsad that a highly regarded person like Zitto anafanya mambo kama yale. Kuna kitu kimejificha chadema--- it seems everytime they are on top of things, then suddenly they mess up and especially from their leaders

Tumeona Mbeya, Dowans, Coalition ya wapinzani, Busanda etc... what is going on???
 
safi sana Zutto. I also could burn it!! Lazima tuwakatae MAFISADI na mambo yao yote.
 

Mimi ningependa nijaribu kuweka baadhi ya mambo sawa hapa (walau kidogo).

Malecela ni mmoja wa viongozi wa juu wa CCM hadi leo. Ni Mjumbe wa CC, na ni Mjumbe wa NEC. Yeye na wengine (ndani ya CC na NEC) ndio wenye mamlaka ya juu kabisa ya utungaji, utekelezaji na usimamizi wa sera za CCM.

Nikumbushe tu pia kwamba, kila mwanachama wa chama chochote cha siasa (sio CCM pekee), anao wajibu wa kuhakikisha anakitetea chama chake na kusimamia sera zake kadiri anavyoweza. Mwananchama pia anaowajibu wa kimsingi kabisa kuhakikisha kuwa chama chake kinashinda uchaguzi na kushika hatamu za uongozi. Malecela ni mwanancha wa CCM na anachofanya Busanda ni wajibu wake wa kimsingi kabisa, kulingana na ahadi yake ya uanachama wa CCM. Sioni mantiki ya hofu inayosababishwa na uwepo wake kwenye kampeni hizo za Busanda (hasa kutoka upinzani). Kimsingi hayupo kule kusaidia upinzani kwa namna yoyote.
 
ndiyo demokrasia kazini.. tunapotaka demokrasia tuwe tayari kulipia gharama yake..
 
Tunaomba na za hao mfisadi wa CCM ili tuweze kulinganisha mhudhurio ya wanachama.Kwaniwao wanadai wanatisha huko
 

Ama kweli ukistaajabu ya Firauni, utaona ya Musa!
 



Philemon Michael!

Nakushukuru kwa kutoa mawazo ambayo yanafanana na ya kwangu! Kama unatoa taarifa ambayo chanzo chake kipo ni vizuri kuweka maoni yako na kutaja chanzo cha habari ili mwenye kuwa na muda ajisomee!

Watu waache uvivu wasome ndipo wachangie! Hakuna sababu ya kuweka habari yote humu! Do you know why nilishasema watu wengi hapa Jamiiforums wanatumia mitandao ya umma yaani ya ofisi na huu ni ufisadi ndiyo maana mtu anakopi na kupaste page nzima! Kama wangekuwa wanatumia pesa zao wangeona kwa kulipia hizo Megabites wangetia akili!

Pia moderator tumchangie pesa in the form of member fees ili awajibike watu wasichangamkie kumwaga hapa threads za kitoto kama mpira wa Arsenal vs Manchester United!

You can't buy airtime from your service provider kuleta utoto na utani!! Tujenge hoja za msingi na zilizotafitiwa ili kuokoa muda na pesa. Baada ya thread kuwa exhausted then moderator aombe majumuisho na kuiweka kwenye archive !

This forum should also be used for education kwani wengi hawapendi kusoma wangojea spoon feeding from some of us this is very unhealthy.

Let us add some colour where we could have live chats na majibu ya papo kwa hapo ukitoa hoja na ukashindwa kuitetea then tuweke fines kama kufungiwa etc!! au kuzomewa !!!!

Naomba kuwasilisha jamii leteni facts but with figures!!!!
 
Tunaomba na za hao mfisadi wa CCM ili tuweze kulinganisha mhudhurio ya wanachama.Kwaniwao wanadai wanatisha huko
 
Wanafanya makosa makubwa sana. Hawa watu katika maisha yao yote hawataweza kusahau kuwa walichapwa kwa kuizomea CCM na hawatakuwa na mapenzi na chama hiki zaidi ya kuangalia kama kuna opportunity ya kutunisha matumbo yao mbeleni.

Hizi zilikuwa ni zama za chama kimoja nakumbuka tulikuwa tunafanyishwa maandamano, tunachezeshwa halaiki na gwaride la chipukizi wa ccm hasa wakati wa kuazimisha kuzaliwa kwa chama. Nakumbuka mimi nilikuwa platoon kamanda mguu mpaka kichwani.

Ila kwa chama sasa kushikwa na wasanii na mafisadi mapenzi yale yalitoka siku nyingi. Chama kimekuwa mradi wa watu kujitajirisha na wengine kujipendekeza wasipoteze nafasi zao?, LOL!!
 
Wnafunzi ni wapiga kura hivyo wana haki ya kushabikia chama wanachokitaka. Sasa hili swala la ku-intimidate wapiga kura mimi silielewi. Naona mwisho wa SISIEM unakaribia. Pamoja na kwamba tunamlaumu JK kuwa ni mchovu, mimi sasa naanza kuamini kuwa huyu jamaa atatusaidia sana katika kuwatoa SISIEM madarakani.
 
Ndugu watz, kama mnakumbuka baadaya uchaguzi mwaka 2005, Kikwete alisema CCM ilipata ushindi wa kishindo kwa kuwa walitumia mbinu za kisayansi! Hizo ni mojawapo ya hizo! Ujanja wao watu wameanza kuujulia. Na niwafahamishe kwamba hiyo si mara ya kwanza, mbinu hii ndiyo iliyotumika kumg'o Wilfred Lwakatare aliyekuwa mbunge wa Bukoba mjini kupitia CUF.Shahada zilinunuliwa na baadaya uchaguzi zikakutwa zimetupwa njia panda!Janja yao tushaijua, mwaka 2010 ya EPA haitakuwepo, na hii janja ya kununua shahada inabidi tukomae nayo.Heko chadema, hawa wajumbe wa nyumba kumi ndo vyombo vikuu vinavyotumika kurudisha demokrasia nyuma, hawa ndo hutumika kwenda nyumba kwa nyumba kugawa kanga, kofia, sukari na pombe.Lakini mbinu zingine inabidi tuzione mapema, nimekuta mbunge wa Bukoba mjini akigawa takrima mapema akijiandaa na 2010. Je ni kazi ya mbunge kugawa sukari wakati wa krismas na mwaka mpya? Je ni kazi ya mbunge kuwa father Christmas? Je hii si rushwa ya mapema?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…