Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi


Inategemea pia uraia wa wazazi wake.

"5. (2) A person shall not be deemed to be or to have become a citizen of the United Republic by virtue of this section if tit the time of his birth-
(a) neither of his parents is or was a citizen of the United Republic and his father possesses the immunity from suit and legal process which is accorded to an envoy of a foreign sovereign power accredited to the United Republic; or
​
(b) any of his parents is an enemy and the birth occurs in a place then under occupation by the enemy."
Source: The Tanzania Citizenship Act. 1995


​
 
Natumaini watu wakiwa na sheria yenyewe ya Uraia itasaidia katika mjadala. Ila nadhani ni muhimu kuangalia vipengele hivi, kwani vinajibu maswali mengi ya hapo juu.
"6. Every person born outside the United Republic on or after Union Day shall, with effect from the date of his birth, be deemed to have become and to have continued to be, and with affect from the commencement of this Act shall become and continue to be, a citizen of the United Republic if at the date of his birth his father or mother is or was a citizen of the United Republic otherwise than by descent, subject to the provisions of section 30.
​
7. (4) A citizen of the United Republic shall cease to be a citizen it
​
(a) having attained the age of eighteen years, he acquired the citizenship of some country other than the United Republic by a voluntary act other than marriage;
​
(b) having attained that age of eighteen years, he otherwise acquired the citizenship of some country other than the United Republic, or while a citizen of the former Republic of Tanganyika or the former People's Republic of Zanzibar; and has not, by the specified date renounced his citizenship of that other country, taken the oath of allegiance and made and registered a declaration prescribed by Parliament regarding his intention as to residence." Source: The Tanzania Citizenship Act 1995.
​
Fungua Ambatanisho kwa Sheria Ya Uraia 1995
 
Simba wa nyika amekwisha kufika huko mtasikia habari zake lazima waTanganyika watajua kama embe ntunda. 😀

Hivi kumbe Pemba kuna nyika zenye simba!!!!!

Kazi kwelikweli

omarilyas
 
Hivi kumbe Pemba kuna nyika zenye simba!!!!!

Kazi kwelikweli

Naona unashangaa majani kuota chini tena ndani ya bahari kama haitoshi unazidi kushangaa kuona mengine yanaota juu ya maji.
 

Du jamaa alimaliza la saba akiwa na miaka 20! Labda ndio maana alishindwa kumaliza sekondari.....
 
Nimesikia chadema wamemwekea pingamizi mgombea wa ccm kwa kuwa picha yake haikidhi matakwa yaani haionyeshi masikio yote. Walio huko jikoni embu tupeni update.

Pingamizi kama hili limeshawai kutumika na wagombea wakaenguliwa. Lakini inategemea uko chama gani. Sheria za uchaguzi zinahitaji kutafsiriwa kila wakati na wakitafsiri unajua tena wanaegemea upande ule ule...
 

Nimekaa kimya nafuatilia majadala mpya wa Uraia na wala sio wa Busanda tena manake huo ulioanzisha haupo.
Kuhusu kujichanganya ulikokusema; Nadhani Utakuwa unajichanganya wewe, awali nimekukubalia kuwa wagombe wa CCM na CUF waliwekewa pingamizi na msimamizi amekiri, lakini baada ya kupitia wameyatupilia mbali hivyo kampeni zinaendelea. So, mgombea hakuanza kampeni kwa sababu zake binafsi kwani pingamizi likitupa nje haliitwi pingamizi tena. Ingawa siyo msemaji wa CUF wala Mgombea nadhani hajaanza kampeni kwa sababu ya kumgojea Simba wa nyika ambaye nimekueleza kuwa tayari yuko Busanda. Unalingine manake nataka kwenda Kamanga Ferry kuangalia Polisi wanavusha siraha gani Kuelekea Busanda.
 


Hee? siraha? kwani kuna vuta huko? na hapo ndo kiini cha tatizo letu watanzania, doa inapogeuka kuwa mabavu ya kuhakikisha mafisadi yanaendelea kutawala!

Ninacho sikitika zaidi ni hali zao hao polisi wanao waumiza walala hoi wenzao!
 
1. Jamani hizi pesa za uchaguzi zinatoka wapi wakati wanasema tunafunga mkanda?

2. Kuna haja kuwa na mfumo mwingine: akifa mbunge basi aliyefuatia kwa kura awe mbunge au kama ni CCM au CUF yule no 2 ktk kura za maoni anakuwa mbunge!
Naona tunapoteza pesa nyingi unecessarily!
 
Ni kweli kuwa mgombea wa CUF aliwekewa pingamizi na mgombea wa CCM juu ya uraia wake , ila sijapata majibu ya pingamizi lake mpaka sasa kwani tume ilipaswa kutoa jioni hii ninaendelea kufuatilia huko.

Ni kweli kuwa mgombea wa CHADEMA alimwekea pingamizi mgombea wa CCM kwa yeye kupeleka picha ambayo haikidhi matakwa ya kisheria na haswa kutokuonyesha masikio yote mawili kama sheria na kanuni zinavyotaka , na pia haikuwa saizi ya post card kama sheria zinavyotaka , na wapo wagombea wengi waliwahi kuenguliwa huko nyuma kutokana na suala hili sasa sijui tume wataamua kufanya nini juu ya hili.

Leo Dr.Slaa ameenda kuzindua kamapeni za CHADEMA rasmi na nitawajulisha kitakachojiri huko kwani kwa sasa hawawezi kupokea simu kwani wapo jukwaaani , na pia timu ya Sangara iliyokuwa Kagera leo ilitokea CHATO na kuingia Busanda tayari kwa mapambano ya kuelekea ushindi.

Polisi wameongezwa sana huko na wameweka kambi nne tofauti jimboni humo wakisema ni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama huko.
 
...nataka kwenda Kamanga Ferry kuangalia Polisi wanavusha siraha gani Kuelekea Busanda.
Kinatokea nini huko! Mwanzoni tulisikia kuna makambi ya vijana wa CCM yanalalamikiwa kuwa wanaandaa mbinu za kuiba kura... sasa wanapeleka na silaha kabisa!
 
Kinatokea nini huko! Mwanzoni tulisikia kuna makambi ya vijana wa CCM yanalalamikiwa kuwa wanaandaa mbinu za kuiba kura... sasa wanapeleka na silaha kabisa!

CCM ni waoga sana na haswa kushindwa kwenye uchaguzi huu na wanajua kabisa ya kuwa watumishi wa serikali ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi hawapo upande wao ndio maana waliitisha semina ya waalimu wote na kuwatisha sana ,lakini baada ya kikao waalimu hao walitoa taarifa kwa viongozi wa CHADEMA juu ya mbinu ambazo zimeandaliwa na tayari kila kitu kipo hadharani.

CCM wanataka kupeleka mbolea ambayo wataiuza kwa bei poa jimboni Busanda kwa ajili ya kuwarubuni wapiga kura ya kuwa wao wanawajali ila baada ya taarifa hizo kuwekwa hadharani wananchi huko tayari wameshaambiwa na hivyo wanajua kuwa watapelekewa rushwa.

FFU wameongezwa sana kukabiliana na vyama na haswa CHADEMA baada ya wao kufanya mkutano na hata polisi walipotaka kuzuia wakashindwa kutokana na wingi wa watu,

Ifahamike kuwa Busanda ni jimbo lenye wachimbaji wengi wadogo wa madini kuanzia kule Katoro,Rwamgasa na hata huko walikofia maji majuma machache yaliyopita ni Jimboni humo hivyo vijana wengi na haswa wachimbaji wana hasira sana kutokana na kunyanyaswa kwao mara kwa mara na haswa na wazungu ambao wanapewa maeneo makubwa huku wazawa wakiwa wananyimwa kumilikishwa maeneo hayo.

Wananchi hawa pa wameadhiriwa sana kutokana na pamba yao kutokuuzika mwaka huu kutokana na global financial crisis na hivyo wana hasira sana .

Kamati Kuu ya CCM iliamua kuwa Makamba asiende huko ila ilitumwa timu iliyokwenda Mbeya ya akina Malecela na Makamba kabakishwa ofisini .
 
Mkuu wazo lako Zuri..tunapoteza pesa HOVYO. ila ktk hili kuna uwezekano wengine wakataka kuwaua wabunge waliopo ili tu watangazwe wao ndio wabunge....

Ushauri wangu akifa MB hakuna uchaguzi hadi next term. nafasi inaweza kukaimiwa na kiongozi yoyote ndani ya Jimbo au Mkoa kutegemea na fikra zingine. au hakuna kabisa. Mbunge wa Jirani na hapo anaweza kukaimu. kama kutakua issues serious wananchi watapeleka thru Mbunge wa Jirani.

Tutasave a lot of money. the same Akifa RAIS... makamu anakuwa rais hadi next term hii itapunguza gharama zisizo na msingi na kuwekeza pesa hizo ktk KILIMO au AFYA au ELIMU.
 

Dikteta, hebu rudia kusoma tena halafu utueleze taratibu kama unamaanisha hivyo.
 
Kuna mpya yeyote kutoka Busanda ?
 
Kuna mpya yeyote kutoka Busanda ?

Hakuna mpya. Lakini kama
CUF wanashindwa- kushinda Buguruni-. au pale Mikunguni (Zanzibar) watashindaje Busanda? Bao jengine hilo !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hakuna mpya. Lakini kama
CUF wanashindwa- kushinda Buguruni-. au pale Mikunguni (Zanzibar) watashindaje Busanda? Bao jengine hilo !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hata hiyo ni mpya maana sioni sababu ya Sultani CCM kushindwa kuleta maendeleo katika wilaya hata moja itawezaje kuleta maendeleo kwa Tanzania nzima.
 
Nimepata habari sasa ivi katibu wa chadema wilaya ya geita amekamatwa na polisi baada ya kuzuka vurugu kati yake na muuza magazeti.

Muuzaji alikua ananyofoa karatasi za ndani kwenye magazeti yote ya tanzania daima ili wananchi wasisome wasifu wa mgombea wa chadema.
 
Mambo gani tena hayo? Huo wasifu utolewe na kusambazwa kwa wingi hapo jimboni ili wananchi wausome, gazeti peke yake halitoshi, nashauri watengeneze vipeperushi vingi vya kutosha! Na pia gazeti la Tanzania daima liwachukulie hatua za kisheria hao wote vibaraka wa ufisadi wanaonyofoa kurasa hizo muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…