Pre GE2025 Uchaguzi CHADEMA: Aliye kipenzi cha upande unaotia shaka

Pre GE2025 Uchaguzi CHADEMA: Aliye kipenzi cha upande unaotia shaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mbenge

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
4,864
Reaction score
10,483
Mshikemshike nguo kuchanika unazidi kushika kasi, pale nafasi ya M/Taifa wa CDM inapokwenda kushikwa tena katika kipindi kijacho cha miaka mingine mitano. Miamba wakubwa wawili wamejotokeza kugombea natasi hii nyeti sana ndani ya chama kikuu cha upinzani.

Hizi kambi kubwa mbili zinatofautiana kimtizamo na hata kimkakati katika kubaliana na mazingira ya kisasa ambayo chasma kiliiyokwisha kuyapitia na hata pia yajao ambayo kinategemea kuyapitia.

Yes! History is the path set by the past, and paints the forthcoming way about the future.

Watesi wa kihistoria wangali bado wapo madarakani, kumbukumbu za za udhalimu wao zingali bado zipo akilini mwa wana CDM. Mateso, ufedhuli, na vifo vya makada vingali bado katika vichwa vya wanachama wengi.

Lakini jamb la ajabu upande mmoja wa kambi za wagombea ukiungwa mkono kwa hali na mali na waliokuwa watesi wao kwa hoja dhaifu sana. Wakati kila mtu alitarajia ni firsa nzuri ya kuunganisha nguvu ili harakari mpya zizaliwe na chama kifuate mkondo mpya, lakini tunashuhudia mambo kuanza kwenda kombo.

Wakati matarajio ya wengi yalikuwa mtu sahihi apatikane ndani ya CDM, katika wakati sahihi, ili kuendana na matakwa ya wakati ili kuleta mageuzi ya kweli. Tunacho kishuhudia ni ukinzani wa ndani wenye kufifisha kwa makusudi matamanio hayo ya wengi

Wajumbe wa Mkutano Mkuu mna wajibu mkubwa sana wa kusahihisha makosa kupitia funzo la kihistoria linavyotuashiria. Aliye kipenzi na kushabikiwa mno na mfumo, serikali, na chama tawala, pamoja na machawa wake hafai hata kidogo. Kupanga ni kuchagua.

Nawatakia kila la heri
 
Mimi nikiwa mmojawapi wa watu wenye kujali hatma ya CDM na upinzani kwa ujumla, namsihi sana Mh. Mboye anpishe kada mwingine, aliyoyafanya kwa muda wa miaka 20 yanatosha.
 
Back
Top Bottom