Heshima kwenu wana JF .
Uzi huu tachukiza wengi, ambao hawajawahi naleta thread za namna hii.
Jumapili iliyopita kabla ya Jumapili ya jana, ulifanyika uchaguzi wa CHADEMA kanda bya Kusini mjini Masasi.
Ni uchaguzi ambao buligubikwa na rushwa kutoka nje ya CHADEMA.
wapiga kura waliuuza kura zao kwa bei ya shilingi 150,000/ zilizotolewa na mbunge wa CCM wa kike mtalamu wa kutoa taarifa bungeni na anayevuma kwa style
ya kugagaa mavumbini anaposhukuru kwa miradi iliyotekelezwa jimboni mwake ,amabaye yupo katika Jimbo ambalo Lina Taasisi kubwa ya watawa wa kanisa Katoliki mkoani Ruvuma na anayehusika na wizara bya SIHA za watu.
Mbunge huyo amefadhili na kufanya malipo ya pesa kwenye mnada huo uliotwa UCHAGUZI wa Kanda ya kusini.
Mbunge huyo alifanya hivyo kwa lengo la kuhakikisha CHADEMA haipati Viongozi bwa kusimamia vision yake, kufanya mobilization ya shughuli za chama kusini ya Tanzania Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Kitu kilichokiwa kinaangaliwa ni kuhakikisha Viongozi wasio na vision mamluki wanapita,na Viongozi wenye vision na wenye influence na mtaji mkononi wanashindwa.
Kwahiyo baada ya matokeo hayo walioshinda wote wanatoka Songea, ambako harakati na movement za CHADEMA haziko hai kama ilivyo Lindi , Mtwara hasa NACHINGWEA,MTAMA,Tandahimba, na Masasi mjini ambalo chama kina nguvu ila kimekosa Viongozi wa kanda wenye vision.
Katika uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Benson Sigo Kigaila ambaye ni mwenza wa Mbunge mmoja wa Covid 19.
Jitu lenye ushawishi na vision Daktari mahadhi Mmoto Daktari bwa binadamu alianguka kwa kupata kura 19, kutoka kwa wajumbe wanaojielewa ambao hawakutaka kuuza utu wao kwa shilingi 150,000/.
Daktari Mahadhi Mmoto ni mbunge bwa mioyo bya watu ambaye aliporwa ushindi 2020 Jimbo la Nachingwea na kubambikiwa kesi magumashi na utawala wa Kambale.
Mahadhi Mmoto bwas real a right person kwa nafasi ya UENYEKITI WA kanda.
Katika uchaguzi huo Walioibuka wenyeviti yaan Chairperson na Makamu wake, Mmoja ni Mganga bwa kienyeji mpiga Ramlib na mmoja Herbalist ndo taaluma zao au shughuli zao.
Hao wote wawili ni kutoka Songea Ruvuma Lindi Mtwara hamna top leader zaidi ya mweka hazina wa Kanda.
Kitendo cha Viongozi wote wa juu kutoka Ruvuma kwa MBELEKO ya rushwa za mbunge wa ccm, ni dalili tosha kuwa CHADEMA ni CCM in character katika kanda bya Kusini.
Hawana muda hawatakiwa na muda wa kufanya chochote Cha maana kwa vile wako pale kutimiza matakwa ya kuhujumu CHADEMA.
Kichekesho , nafasi ya Mwenyekiti walifungana kwa kura sawa, ikaridiwa kura iliyobadiri matokeo ilinunuliwa kwa shilingi 550,000/ ililipiwa na mbunge huyohuyo wa CCM.
CHADEMA MAKAO MAKUU, imekuwa na tabia ya kuachia chaguzi za Kanda zijieendee tu, hakuna focus au msistitizo wa CHADEMA kuwatamani kuwa na mtu flani mwenye potentialities awe kiongozi hasa kanda ya Kusini, badala yake yeyote atakayeshinda hakuna tatizo Kwao.
Kwa matokeo ya uchaguzi wa 2020, CHADEMA Ina mtaji mkubwa wa kura na uungwaji mkono hasa majimbo manne, likiwemo Jimbo mama kwa uungwaji mkono Nachingwea na Mtama.
Uchaguzi wa Kanda uliopita ni KABURI rasmi la CHADEMA kanda ya kusini ikiwa makao makuu ya CHADEMA hayataingilia uchaguzi huo.
Kwa kuonesha bkuwa Kuna kitu sio Cha kawaida kati ya CCM Ruvuma na CHADEMA kanda, hakuna mbunge yoyote wa CCM Toka NDANDA Mwambe C, na Mwambe G wa Masasi, aliyeonesha interest ya kusaidia kuhujumu Uchaguzi huo, ila mbunge wa ccm kutoka kilometa zaidi bya mia 450 ndo kaingia Infront na kusimika Viongozi mamluki kutoka nyumbani kwake Ruvuma.
Mheshimiwa Mwenyekiti Mbowe na Kamati kuu, na Viongozi headquarters, ni wakati sasa wa kusafisha nyumba.
Tengua msisibitishe huo uchaguzi, urudiwe tena.
Katibu wa Kada Kaduma ni kirusi kikubwa kwa afya ya CHADEMA kanda bya kusini, ondoa badili aje katibu mwingine tena.
MKAKATI WA KUUZA MAJIMBO YA KUSINI.
Kuna baadhi ya wanachama watakaopitishwa kwa baadhi
ya majimbo hasa ya mkoa wa Ruvuma,na mengineyo
pia, wamejipanga kuuza majimbo kwa kati ya milioni 300 to mia 500 kutegemea ugumu wa jimbo,ili wasirudishe fomu, au wajipoteze bkwa kutopatikana kwa cm siku chache kabla vya kurudisha fomu ili CCM ishinde kwa urahisi this time.
Singo KIGAILA BENSON aangaliwe kwa jicho pekenyevu.
Kwa uchaguzi wa Kanda ya Kusini uliofanyika Masasi hajaonesha qualities zozote za uongozi na kusimamia vema uchaguzi ule, alikuwa yupo yupo tu, bila shaka hata yeye labda alikuwa na HESABU YAKE kutoka kwenye huo mnada uliofadhiliwa na huyo mbunge wa CCM.
Nilipaswa niandike Uzi huu mapema sana soon after election, nilikosa nafasi kutonanna shughuli za kilimo Korosho zimeanza kudondoka.
Nimewiwa kuandika kama mtanzania hasa mpenda mageuzi.
Nipende kuwatakia siku njema.
Karibuni sana Kijijini Chinongwe Ruangwa.