Pre GE2025 Uchaguzi Chadema waanza, hivi ndivyo uhakiki wapiga kura unavyofanyika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
IMG_2649.jpeg
Ni rasmi; agenda ya uchaguzi utakaoamua nani atakayeiongoza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa miaka mitano ijayo imeanza, na uhakiki wa wajumbe watakaofanya uamuzi umeanza.

Uhakiki wa wajumbe hao unafanyika kwa kuita majina ya wajumbe wa kanda mojamoja ili kupata uhalali wa wapigakura wanaotambulika ndani ya katiba ya chama hicho, ambao wataamua kati ya Freeman Mbowe, Tundu Lissu, na Charles Odero nani apewe kijiti kuiongoza Chadema.

Mbowe anatetea nafasi hiyo aliyoiongoza kwa miaka 21, anachuana vikali na Makamu wake bara, Tundu Lissu. Uchaguzi huu unafanyika leo, Jumanne, Januari 21, 2025, katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Agenda hiyo imetangazwa na Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika. Uchaguzi huu unasimamiwa na wazee wanane wastaafu wa Chadema, ambao ni Profesa Raymond Mushi (Mwenyekiti), na Katibu akiwa Dk Azaveli Lwaitama. Wengine ni Ruth Mollel, Ahmed Rashid, Alfred Kinyondo, na Azumuli Kasupa.
 
View attachment 3209136

Kila la Kheri....leo hapalaliki mpaka tumjue Tundu Lissu Rais ajaye
 
Twende kazi wajumbe, kura yako mjumbe itaandikwa kwa wino wa dhahabu endapo utaipiga kwa kuangalia watz, wanachama wanataka nini, leo sio siku ya kuangalia sura ya mtu , leo ni siku ya kuangalia kesho ya taifa hili chini ya chadema, Mungu awatangulie.
Ameen
 
Wajumbe wanaitwa ili kuhakikiwa
 
Watanzania wote wapenda haki na mabadiliko wanategemea wajumbe hawatawaangusha. Kura zao zimebeba jasho, machozi, damu na mateso ya maelfu ya wahanga wa kuipigania Chadema ambao wamekufa, wamefungwa, wamepotezwa, wamepata ulemavu wa kudumu, wamefilisiwa, wamebakwa, wamepoteza kazi nk.

Ole wenu wajumbe mtakaopiga kura.
Laana na baraka zipo mikononi mwenu.
 
Kila la kheri wajumbe, watanzania wanataka mabadiliko
 
Watanzania wote wapenda haki na mabadiliko wanategemea wajumbe hawatawaangusha. Kura zao zimebeba jasho, machozi, damu na mateso ya maelfu ya wahanga wa kuipigania Chadema ambao wamekufa, wamefungwa, wamepotezwa, wamepata ulemavu wa kudumu, wamefilisiwa, wamebakwa, wamepoteza kazi nk.

Ole wenu wajumbe mtakaopiga kura.
Laana na baraka zipo mikononi mwenu.
Ndio, mkuu ujumbe Murua kabisa
 
Wazungu wamechoka kukaa wanafanya kusimama na kukaa tena
 
Mnyika amezeeka siku mbili tu 😂

Ndio ajue ugumu alipopata Waziri Mchengerwa Kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Mchengerwa kapata ugum gani? Acha fananisha vitu vya msingi na ujinga ,

Hivi unaweza sema kwamba tulikua na uchaguzi wa serikali za mtaa kweli? Acheni utani
 
Back
Top Bottom