Uchaguzi DARUSO: Ni CHADEMA vs CCM?

Uchaguzi DARUSO: Ni CHADEMA vs CCM?

Han'some

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
283
Reaction score
76
Kampeni za Uchaguzi wa Rais, na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, zimeanza.

*Wagombea Urais ni watatu katika kinyang'anyiro hiki. Bw Egidy Mkolwe ambaye ni mmoja wa wagombea, anatarajiwa kuzindua kampeni zake katika ukumbi wa Yombo 4, hapa UDSM asubuhi hii;

*Kuna tetesi kwamba C.C.M. Wana mgombea wao, na wanafanya juu chini ili apite, kama walivyofanya kule SAUT-Mwanza na kuambulia patupu;

*Mwenye taarifa za ki-inteligensia kuhusu hili la C.C.M. kujipenyeza katika Uchaguzi wa DARUSO, atujuze zaidi na atuambie ni wagombea/mgombea yupi ni pandikizi la C.C.M. na ni yupi wa CHADEMA.

#Nawasilisha #
 
Mi nawatakia uchaguzi mwema usije ukaingiliwa na mabomu
 
we umetoa mada bila kuwa na datta kamili,kajipange upya
 
Kampeni za Uchaguzi wa Rais, na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, zimeanza.

*Wagombea Urais ni watatu katika kinyang'anyiro hiki. Bw Egidy Mkolwe ambaye ni mmoja wa wagombea, anatarajiwa kuzindua kampeni zake katika ukumbi wa Yombo 4, hapa UDSM asubuhi hii;

*Kuna tetesi kwamba C.C.M. Wana mgombea wao, na wanafanya juu chini ili apite, kama walivyofanya kule SAUT-Mwanza na kuambulia patupu;

*Mwenye taarifa za ki-inteligensia kuhusu hili la C.C.M. kujipenyeza katika Uchaguzi wa DARUSO, atujuze zaidi na atuambie ni wagombea/mgombea yupi ni pandikizi la C.C.M. na ni yupi wa CHADEMA.

#Nawasilisha #

Kweli umbeya nao kazi. Habari uilete wewe, utafiti tufanye sisi?
 
kama ccm imekataliwa vijijini ambako hamna tv ni kwa hao wasomi ndio wataichagua??
ccm this is time for you to go !!
 
Matokeo yake tutachagua na Vijana wanachagua watu wa hovyo tu eti kisa wako nao chama kimoja...
 
Kwa ninavyoijua UDSM chama tawala kina mkono mrefu tangu awali, tofauti na SAUT ambapo uhuru wa wanafunzi kwenye siasa za chuo na nje ni mkubwa.Let us wait and see!
 
Fanyeni utafitti mjue yupi ni pandikizi la ccm pigeni chini mapema tu, atawasumbua, wana tabia za kujipendekeza sana ili baadae waambulie ukuu wa wilaya
 
mkuu mambo ya uchaguzi vyuoni ya nini tena sisi hayatuhusu acha vijana wasome.
 
Npo yombo 4 ndan kampeni zimeanza viongoz wananadi sera zao.....
Uchama bado haujaanza kuonekana kwangu mm labda ck zijazo.......
 
Wakuu kijana anaetajwa kuwa ccm amepanda jukwaani wanafunz wakaanza kuimba.....,....
hatutak ccm x 5.....
Bado anatoa hotuba lakini kelele za buuuuuh n nyingi mno......
Kwa kwel kelele zimesabiba nsisikie jina lake akijitambulisha......
Anaonesha vyeti vyake vya ngaz za uongoz alizowah kushika bt haelewek......
 
inanifanya nikumbuke kipindi cha mwita na magesa enzi zetu watu walichangamka kweli
 
Back
Top Bottom