Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 1,012
- 2,317
Katika uhalisia ndani ya uchaguzi kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi ikiwemo kuwaandikisha watoto chini ya miaka 18 kinyume cha sheria ikiwemo wananfunzi, ikiwemo wasimamizi wa uchaguzi kutofuata sheria za uchaguzi
Kwenye baadhi ya vituo mfano tukio la kukaa na karatasi za majina mkononi badala ya kubandika sehemu husika wakati wa zoezi la uchaguzi kinyume cha sheria huko Sinza, ikiwemo kuuawa kwa baadhi ya wagombea wa nafasi mbali mbali na wengine kupokea vitisho nafasi wanazo gombea.
Katika mazingira kama haya ni wazi uchaguzi haukuwa wa haki na wazi, hii ni mara ya kwanza nchi yetu kufanya uchaguzi mbaya zaidi tumeshuhudia hata wimbi la watanzania waliokuwa wakigombea nafasi mbali mbali wakifa kama nzige kwenye uchaguzi nchi nzima, pamoja na ukiukwaji wa wazi washeria za uchaguzi kwa wasimamizi walio simamia uchaguzi huo.
Licha ya matukio haya kufanyika hadharani huku vyombo mbali mbali vya habari vya ndani ya nchi vikiripoti, lakini hatuwaoni viongozi wa serikali wakikemea vitendo hivyo vibaya kwenye jamii ya watanzania akiwemo Rais, waziri mkuu, Waziri wa ulinzi na viongozi wengine wa kiserikali tulio wapa zamana kuisimamia nchi yetu na kituhakikishia usalama, maendeleo na demokrasia.
Kwahiyo huu unaweza kuwa uchaguzi mbaya zaidi kuwai kushuhudiwa nchini Tanzania tangu uhuru na hii inaonesha kuzorota kwa kiwango kikubwa cha demokrasia nchini.