Uchaguzi 2020 Uchaguzi huo unakaribia, ambae hajasema aseme asikike

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kila anaeiita Tanzania kwetu kuna vile anapenda iwe na atendendewe. Muda wako ni huu wa kusema kupendekeza, kushauri, kushawishi, kuonya, kutahadharisha, kulaani, na kulaumu na kuunga mkono yale unayoyapenda/usiyoyapenda, maana hakuna mwenye haki miliki ya Tanzania ni dhamana tu tunawapa wafanye kwa niaba yetu. Hakuna mtu anayeifahamu, kuipenda na kutuonea huruma Tanzania kwa niaba yetu.

Sisi sote tuunganishe nguvu zetu kusema juu ya Tanzania tunayoitaka, na huu ndio wakati wa kufanya hivyo, baada ya uchaguzi itakuwa too late na majungu kumuongelea yule aliyeshinda.

Usikubali mtu akutishe, usiseme unavyopenda na kuunga mkono upande unaouamini katika kuijenga Tanzania unayoitamani. Kama itakupasa upate adhabu kwaajili hiyo basi jihesabu kuwa huo ndio mchango wako na wewe kwenye kuifanya Tanzania unayoitaka wewe na kizazi chako kijacho.
 
MAGUFULI AMEKATALIWA MBINGU NA ANGA HAZIMTAKI.

Hata akipiga magoti.

2020 ni Yeye
 
Sababu 27 za kumkataa Magufuri.


1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8 .Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22.Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu,ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
25. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya approval ya bunge wala cabinet
26. Alisema tutaishi kama MASHETANI.. kwa madai kuwa tulikuwa tunaishi kama Malaika. Hakika amelitimiza hilo.🤔
27. Kuwa na kundi la watu wasiojulikana awamu hii ya tano na polisi hawajawai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…