Uchaguzi 2020 Uchaguzi Huru na wa Haki, ni haki ya Wananchi wala siyo hisani ya Watawala ama Viongozi walio madarakani

Uchaguzi 2020 Uchaguzi Huru na wa Haki, ni haki ya Wananchi wala siyo hisani ya Watawala ama Viongozi walio madarakani

RockCarnegie

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
963
Reaction score
1,927
"Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa"

Tunapoelekea Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani ni vyema tukawakumbusha waliopewa dhamana ya kusimamia zoezi upigaji na uhesabuji kura kuwa, ni haki ya wananchi kutangaziwa matokeo sahihi kulingana na jinsi walivyochagua viongozi wao.

Siyo hisani ya rais ama kiongozi yoyote kuwapatia wananchi maamuzi yao kupitia sanduku la kura!

Kutangaza matokeo 'fake' siyo kuwakomoa au kuwakomesha wapinzani! Ni kuwadharau wananchi, kuwaona wajinga, wanyonge, 'primitive' , wasiofaa na kuweza lolote!

Ni aibu na fedheha kwa viongozi, uchaguzi unakaribia taifa linahowafia kuwa mtaiba kura zao! Shame on you!

Mwananchi acha woga, piga kura na linda kura yako!
 
Back
Top Bottom