Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 478
- 1,025
Ukitazama hali halisi ilivyo sasa ni wazi kabisa matajiri, watu wenye uchumi mzuri, biashara kubwa, na watu wa serikali ndo wanaridhika na mwenendo wa serikali kwa sasa. Sasahivi wanasukuma magari ya mill 300 na 400 kama wanaigiza ila ndo kweli hivo.
Kula kwa urefu wa kamba ndo slogan ya Tanzania. Pesa zinazotoka na Kodi za wananchi imekuwa ni halali kuliwa na Wanasiasa bila aibu. Kila wizara, kila sekta, na kila eneo pesa zinaliwa, huduma ni hafifu, viongozi wamejaa kiburi kwa kuwa wanatumia pesa zetu na hakuna wa kukemea.
Sasahivi kupata haki mahakamani kwa maskini ni ndoto, nidhamu katika utumishi wa umma ni msamiati, kuzulimiwa kiwanja au nyumba na mtu mwenye pesa ni jambo la kawaida.
Sasa ule wakati wa kuanza kuona viongozi wakija kwenye vijiwe vya kahawa ndo huu, tutawaona sana wakati huu huku vijijini, kujifanya kutembelea wananchi huku wakipiga mapicha ya show off, ila wakati huu ndo wakati wa kutambuana vizuri.
Nyakati za unafiki zimeisha, ni wakati wa kila mbunge sasa kuja kutuambia umefanya nini toka tumekuchagua. Wengi baada ya kuchaguliwa wamesahau majimbo yao, wanaishi dar es salaam wanaona majimboni ni mahali pa kuja kuchukua tu kura na kuondoka kwakua wananchi ni kama mbuzi au ng'ombe au wapuuzi wasojua Wala kustahili chochote. Maji, umeme, barabara na shule kwa baadhi ya maeneo ni kama hadithi ya kufikirika na kote Kuna wabunge na madiwani.
Uchaguzi huu unapaswa kutoa majibu sasahihi kwa wananchi. Wabunge ambao hawakufanya vizuri kwenye majimbo yao, kwasasa no chance.
Ni wakati wa wananchi sasa kufanya yetu. Mbunge ukija tutakusimamisha ujieleze, ukizingua tunaenda na Chadema wakati huu, CCM tumekuwa nanyi miaka 60 tangu uhuru sasa inatosha.
Uchaguzi huu ikawe kipimo cha nguvu ya umma na nguvu ya matajiri wa CCM.
Uchaguzi huu ukaje na majibu juu ya shida na mahitaji halisi ya watanzania
Uchaguzi huu ukawe nyenzo ya kurudisha uwajibikaji katika utumishi wa umma.
Uchaguzi huu ukawe suluhusho na mwisho wa ulaji kwa urefu wa kamba.
Uchaguzi huu ukarudishe nguvu ya umma kwa wananchi iliyopokwa na CCM na matajiri wote wanaoingia mkono kwakua CCM inalinda na kuheshimu maslahi ya matajiri.