Uchaguzi huu ni vita kati ya matajiri, CCM na nguvu ya UMMA, CHADEMA vs CCM, Wananchi watakubali CCM irudi?

Unamwangusha sana 'hero' wako kwa mawazo ya aina hii.
 
Unamwangusha sana 'hero' wako kwa mawazo ya aina hii.
Kalamu ni ukweli. Fikiria hebu mtumbue mla rushwa uone pole zitakavyotolewa na ndugu jamaa na marafiki. Kwa ufupi Tanzania ni kizazi cha wala rushwa ndiyo maana mi nampenda sana Dkt Samia, yaani yeye anawaangalia tu na mifumo yenu ya kiwizi mfanye mtakalo maana governance yetu juu ya uwajibikaji ni broken, labda wakitofautiana migao ujue hapo utasikia mtu kakamatwa na DPP atafanya kazi yake etc
 
Mungu Mwenye Enzi Yuko upande wa umma.
 
Niseme tu kuwa ninakuelewa unacholenga hapa.; lakini kusema "unampenda sana" kiongozi asiyeona uchungu juu ya mambo mabaya inayofanyiwa nchi hii, sielewi kabisa kiongozi huyo unampendea kitu gani hasa!
Niliposema unamwangusha 'hero', maana yangu ilikuwa kwamba kundi lote kubwa lilolokuwa likipenda aliyokuwa akifanya kiongozi huyo; wakati huu, kundi hilo ndilo lingekuwa mstari wa mbele kabisa kuhakikisha kuwa hali hii mbovu ni lazima tuiondoe kwa njia zote.
Hivi wale" wanyonge" wote waliishia wapi, mbona wakati huu hawasikiki?

Kila mara ninapo andika juu ya maswala haya ya siasa za Tanzania, inanikumbusha watu wa aina ya akina Kalamaganda Kibudu; akina Kitila Mkumbo na wengineo wa aina hiyo; na sasa kuna wapya akina Kafulila!

Hapana. Sikubaliani na wewe juu ya dhana ya kuwahukumu waTanzania wa kizazi chochote. WaTanzania wapo tayari kabisa kuleta mabadiliko; kinacho kosekana tu ni uongozi wa kuwaelekeza njia hawa wananchi.
 
No reform, NO election". Ni kauli mbiu nzuri yenye maslahi mapana ya taifa letu. Changamoto ni kwamba inamlenga mtawala mkuu moja kwa moja.
Kama akikubali reform basi amekubali kuachia nchi.
Sasa wananchi kama ndiyo walikuweka madarakani na sasa wameamua kumuweka mwingine,shida iko wapi si awashukuru kwa kukuamini?
 
Sasa wananchi kama ndiyo walikuweka madarakani na sasa wameamua kumuweka mwingine,shida iko wapi si awashukuru kwa kukuamini?
Hapo hapo ndio shida ilipo kukubali kuachia madaraka kwa viongozi wetu wa africa bado ni tabu sana, kuangusha chama cha ccm na dola kwenda upinzani ni kitu asichotaka kuona. Ila vyote vinawezekana na nguvu ya wananchi tukiamua kwa dhati kabsa bila unafki.
 
Hapo dawa ni ugaidi tu wananchi Hawa wa tanzania wasio na silaha hawezi kuitoa ccm dawa yake kitokee kikundi chenye itikadi Kali kiwe kinaua viongozi uone kama hawatoachia nchi yaani ifike mda mtu anakataa uongozi lakini useme raia hapana hawawezi Kwa nchi zetu za kiafrica serikali ukipimbana nayo bila silaha unaumia sababu Kuna mazombi yanayotumwa kuua raia bila huruma
 
..HATA UNGEKUWA WEWE UNGEKUBALI KIRAHISI HIVYO?
 
Ila kumbuka hawa watanzania wa sasa ni vegeu geu, hawajui wanachosimamia. Can you imagine Dkt Salim Ahmed Salim alipokuwa anasemwa ni mhizbu? Unakumbuka Lowasa alisemwa fisadi ila mwisho wa siku watanzania walimpa kura za ushindi?
 
Mikiendelea ongea sana katiba inatenguliwa Mama anapewa kumi... Uchaguzi unawekwa kwapani. Africa hakuna lisilowezekana
Mmeanza kuingiza baridi...🫣🫣 Eti kwapani😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…