Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu Waandishi hatujatimiza wajibu ipasavyo

Uchaguzi 2020 Uchaguzi huu Waandishi hatujatimiza wajibu ipasavyo

Kwenye hili nawatetea waandishi wa habari.. niambieni nchi hii kwa sasa nani anainua mdomo wake au kalamu yake kuandika tofauti na watawala wanataka? si maprof wala wanaojiita wananzuoni sijui... amebaki mtu mmoja tu antipas basi. wengine wote ...kimyaa
Ndio inatakiwa watu wawe kama Lisu sio Unafiki
 
Mihimili 3 ya dola hua ina "checks and balances" ila kwa awamu hii yote iko chini ya mtu mmoja wote wanaimba mapambio kulikua na sababu gani kuwanyima wananchi fursa ya kuona binge live kwa madai linapoteza muda watu hawafanyi kazi je kuna kitu kilichokua kinapoteza muda kama mwenge! Na mbona mwaka huu haujakimbizwa na hakuna tofauti so ni matumizi mabovu ya pesa tu na muda ilhali watu wamezibwa midomo wasihoji chochote sababu funguo za nyumba 3 anazo Mtu mmoja
 
Kuna tofauti kubwa sana iliyojitokeza jinsi tulivyo ripoti taarifa za uchaguzi za 2015 na hali ya sasa tunavyo endelea kuripoti.

Kwanza tumetawaliwa na woga usiokuwa na sababu, na woga huu ukiangalia ni kutokana na vyombo vyetu vya usimamizi kama MCT, TAMWA, JUKWAA LA WAHARIRI hata ile taasisi ya mtu binafsi ijiitayo UTPC kama mwamvuli wa vilabu vya upigaji hela za SIDA vijiitavyo Press Clubs kutojitoa na kuweka miongozo ya waandishi wako salama kiasi gani kutokana na wao kutumika.

Tunahitaji Uhuru zaidi wa habari siku za usoni, lakini ni muhimu hivi vyama kuundwa upya kukidhi mahitaji ya Uhuru huo wa habari na heshima ya taaluma nzima.

Kwanza karibu vyote viko hapa Dar vikiwa vimejikita kabisa kasoro kile kilichoko Mwanza kama mwamvuli wa Clubs ambacho kiuhalisia kinamilikiwa na mtu binafsi mjanja mjanja mmoja aliyetengeneza network ya ulaji na anaweka viongozi YES BWANA huko mikoani.
(Anyway hilo tutalijadili baadae ni hoja ndefu hasa kuelekea uchaguzi wa UTPC).

Je, wana habari hali hii ya kushindwa kutoa huduma yetu wakati muhimu kama huu wa uchaguzi twaionaje?
Nawewe pia ni Mwandishi wa habari?
 
Back
Top Bottom