Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Elections 2010 Uchaguzi Igunga 2011: Uchukuaji fomu na kampeni kuelekea uchaguzi mdogo

Status
Not open for further replies.
Hata mimi najua ni wengi hawaiungi mkono CCM, lakini uhalali wa CDM unatakiwa uwe wa kimantiki na wala si wa kimazingira. Ukiwa na watu wawili wabaya watu watamchagua aliye nafuu zaidi kwa mwenzie, CDM kwa sasa inakubaliwa kwa sababu ya Mning'ino (hang over) ya CCM kutawala kama chama dola kwa muda mrefu.

Ninachotaka ni CDM kujijenga kwa falsafa yake na si kwa kutegemea udhaifu wa CCM. Leo CCM wakiwashitaki wale mafisadi na kubadili mifumo yake ya undeshaji mambo 'COme 2015" kazi itakuwa kubwa kwelikweli kwa CDM. Soma bandiko la mwanakijiji "CHADEMA 2010" utaelewa nini ninamaanisha. Vitani si mitulinga pekee inayotawala bali inahitajika mikakati (Strategies) iliyoegemea kwenye uhalisia na Lojistiki za kiukweli.
mkuu heshima, logistiki za kiukweli hapo sasa unalenga matumizi ya fedha. ccm imeporomka uungwaji mkono kwa kuwekeza heavily kwenye logistics. hawatekelezi ilani yao, wanawaza kuwanunua wapiga kura finished, cdm isipite njia hiyo
 
RA na BWM ni marafiki kutoka EPA. RA kasema anaachana na siasa uchwara, sasa anatafuta nini? Huo ndio unafiki wa viongozi wa CCM.
 
hapa gharama zinazozungumziwa ni za serikali au chama??
 
kama hujaelewa uliza uelezwa sio kuropoka non sense

hivi ni nchi zote duniani zina chaguzi ndogo?
nchi zingine wanafanyaje???????

unafikiri demokrasia imeanzia kwetu sio?
.....I now understand that words can reveal the self of a person!
 
Chama cha wanainchi CUF kimewashauri wanainchi wa jimbo la Igunga kutokichagua CHADEMA kikidai wagombea wake mara nyingi huhongwa fedha na kuwatelekeza wanainchi.

Hayo yalisemwa juzi na mgombea kupitia chama cha wanainchi CUF Leopold Mahona alipohutubia mamia ya wanainchi wa kata ya Simbo wilayani Igunga mkoani Tabora.

Uchaguzi wa mwaka jana tulikuwa wagombea 13 tuliochukua fomu. Katika mazingira ya njaa na kutowaonea huruma kati ya wagombea hao akiwamo wa CHADEMA waliwasaliti wanainchi kwa vipande vya fedha.

Mfano wa uaminifu wangu katika kuwatumikia tayari mmeuona mwaka 2010 nilibaki peke yangu kupambana na nguvu ya serikali na nguvu ya Rostam Azizi. Nilionyesha uaminifu wangu kwenu mkanipa kura zaidi ya 11,000. Sasa hata huyo mgombea waliyemleta huenda atawakimbia siku moja kama mwenzake, alisema Mahona huku akishangiliwa.

Akizungumzia azma yake ya kuleta maendeleo wanainchi wa jimbo la igunga, mahona alisema endapo akichaguliwa atahakikisha kila tarafa ya wilaya hiyo inakuwa na sekondari za kidato cha tano na sita, mbali na ujenzi wa secondari mgombea huyo wa CUF alisema atahakikisha anawahimiza marafiki zake wa ndani na nje ya nchi kusaidia ujenzi wa chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne wilayani humo.

Naye Meneja kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha CUF, Anthony Mayange aliwataka wanainchi wa igunga kuachana na ndoto za mchana za kuwachagua wagombea wa CHADEMA na CCM kwa vile hawana nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa watu wa Igunga.

Akianza kwa mgombea wa CHADEMA joseph kashindye , alisema mtu huyo aliingia Igunga kama mtumishi wa serikali ya Mafisadi unadhani ana jambo jipya juu yenu? alihoji Mayange na kuongeza; "Huyu ndiye chanzo cha wilaya ya Igunga kushindwa kufikia malengo ya kufanya vizuri kwenye elimu, na yeye ndiye mkaguzi wa elimu. "sasa kama ameshindwa elimu ataweza kuwaongoza?" alihoji.

Akimchambua mgombea wa CCM, Dk Peter Kafumu, Mayange alisema mtu huyo hafai kuwa kiongozi wa wanainchi wa wilaya ya Igunga kwani hana rekodi yoyote ya kuwatumikia wanainchi wa kundi la chini. Kwanza Kafumu anaishi Dar es salaam kwa hiyo mtakuwa mmerudi kule kule mlikotoka kwa Rostam. Huyu ana watu wake wa kuwatumikia siyo ninyi walalahoi.

Ninawaomba mumchague Mahona kijana wenu anayekula, kuzungumza na kushirikiana na nyinyi hapa Igunga" alisema Mayange.

Soma MTANZANIA.
 
Mkuu ni kweri kuamini ccm haiungwi mkono ni ujinga, lakini kuuiunga mkono ccm pia ni ujinga. Our part should remain to educate people that they may not support ccm period.

Na wajinga ni wengi. Wataunga kwa misingi ya ushabiki hata kwa ubwabwa. Watanzania hawana elimu ya kupima mambo kwa mantiki za kisayansi hasa huko vijijini ambako ndiko kuna watu wengi. Nimeshuhudia watu wanasema hawawezi kukiacha chama chao kwani kimewatoa mbali. Mtu mwenye imani hiyo ni vigumu kumbadilsha maana hata shida alizonazo kwake siyo tatizo. Once a slave always a slave.

More work has to be done to change the mindset of our people.
 
Asante Kigarama kwa kuwakumbusha wapenzi wenzako wa CHADEMA kwani ukisoma post za wengine humu ndani unahisi kuwa wanaishi katika ulimwengu wa kufikirika.

Ni kweli kuwa CHADEMA inaungwa mkono na vijana wengi lakini ni ukweli pia kuwa CCM bado inaungwa mkono na watu wengi wengine wakiwa ni vijana kama hawa wa CHADEMA. Unaweza ukajenga hoja kwa kuainisha sababu hasa zinazowavutia watu kuunga mkono chama kimoja na kuacha kingine.

Bahati nzuri nayaongea haya nikiwa sio mwanachama wa chama chochote cha siasa Tanzania ila ni mpiga kura na hivyo navifuatilia vyama vyote kujua vinachosimamia.

Tata acha kuwadanganya wenzio!mimi nina ushaidi kwamba wewe ni ccm tena damu ila tu huwa unaona aibu tu kusema.by the way "msomi anatakiwa kuwa objective na sio neutral".dr.M.KITILA. However, babu yangu alishaniambia kuwa ukiona mtu anasema hana upande,ujue huyo yuko upande wa waovu.
 
Ukiangalia hata idadi ya watu kwenye mikutano ya ccm ni maajabu ya kihistoria na wadau wa historia wanatakiwa kuweka rekodi hizi katika makabrasha yao,nahisi hata wale wanaochukuliwa kutoka majimbo na mikoa ya karibu ama hawatoshi ama nao wameanza kula pilau na kuingia mitini

tena navyoona mie kuwepo kwa Mkapa Igunga ni pigo jingine la KO kwa magamba maana imedhihirika wazi jinsi siasa zake zisivyoweza kushawishi hata kuwafanya wadau kula kona katika makundi makubwa wakati TANBEN akiendelea kuropoka...

Ni bora Mkapa asirudi Igunga vinginevyo aliyekataa kuongea na waandishi wa habari sasa anajivua nguo live tena mchana kweupe,ni fedhea kubwa!

Mkapa wewe nawe ni mchafu tena mno,tunataka kujua rada ilikwendaje,tunataka utwambie kuhusu kiwira kisha utupe na maelezo ya ndege ya rais iliyotufanya walala njaa tule nyasi,mtwambie na EPA ni mdudu gani,kisha utaje ka-goda ndo kirusi gani...ujibu haya kwanza,umechafuka mno mR clean!
 
haya sasa CUF wameanza kujibu mapigo ni zamu ya cdm kumeza chungu ya siasa slaa aache kulalamika.
 
haya sasa CUF wameanza kujibu mapigo ni zamu ya cdm kumeza chungu ya siasa slaa aache kulalamika.

CDM haina sera ya mipasho kama CUF na mumewe CCM, CDM iko Igunga kuwaeleza wananchi jinsi itakavyoshirikiana nao kuondokana na umasikini ulioletwa na CCMK chini ya siasa zake za kifisadi.Dr. Slaa halalamiki bali anawafundisha wana Igunga jinsi ya kujikomboa toka minyororo ya wakoloni weusi CCM.
 
SIKU moja baada ya uzinduzi wa kampeni za CCM, juzi kutikisa mjini hapa, baadhi ya makada wa vyama vya upinzani wamekiri kwamba ni vigumu upinzani kushinda kiti hicho cha ubunge. Kampeni hizo zilizozinduliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi, zimeibua hisia za wananchi, kutokana na mambo mbalimbali yaliyowagusa. Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa makada wa CHADEMA alisema kuwa walidhani uzinduzi wa CCM ungedoda, lakini imekuwa kinyume cha matarajio yao. Alisema idadi ya watu waliohudhuria katika mkutano huo, uliwavunja nguvu za kuendelea kufanya kampeni, kwani imeonyesha dhahiri jimbo hilo bado ni mali ya CCM. “Sikufichi, pamoja na kwamba mimi naichukia CCM, lakini kwenye hili la uzinduzi halina ubishi, jamaa bado wanakubalika na kweli hapa upinzani tunasindikiza tu, kwani wale watu sio mchezo,” alieleza.

Alieleza kwamba pamoja na kwamba uzinduzi uliofanywa na CHADEMA Septemba 8, ulikuwa na watu, lakini ule wa CCM ulifunika mara tatu zaidi, jambo linaloonekana dhahiri kwamba upinzani una kazi ngumu. “Tutajitahidi kuendelea kufanya kampeni, lakini mpaka sasa kama hatutumii hisia za uchama, lazima ukiri kwamba jimbo hili ni la CCM, na ni ndoto kwenda upinzani,” alisisitiza. Akijibu swali juu ya kwa nini, hawakuiunga mkono CUF kutokana na mgombea wake kuwa na mtaji mkubwa kisiasa, alisema hakuna msimamo wa pamoja juu ya vyama vya upinzani, ndiyo maana kila chama kimeamua kusimamisha mgombea wake. “Kweli mgombea wa CUF ana mtaji mkubwa kuliko wa kwetu (CHADEMA), na kama tungeungana ni wazi tungewaangusha CCM, lakini bado vyama vya upinzani hatujawa na sauti moja,” alikiri.

Source: Gazeti la Uhuru, Jumatatu, Septemba 12, 2011

Katika hali ambayo inadhihirisha kukata tamaa kwa upinzani, juzi akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, alikiri kwamba sio rahisi kuiondoa CCM madarakani, kupitia siasa za mapambio zinazofanywa na baadhi ya vyama vya upinzani.

Mtatiro alikiri kwamba CCM bado ni chama imara, kina nguvu na miundombinu mingi ya ushindi, hivyo bila kutafuta mwafaka wa pamoja wa upinzani haitakuwa na maana.

“Wenzetu CHADEMA mwaka jana hawakusimamisha mgombea na sisi mgombea wetu alipata kura 11,000 tulidhani wangetuunga mkono, badala yake wamekuja kugawa kura Igunga,
”
alieleza.

Baadhi ya wananchi walisema kwamba uzinduzi uliofanywa na CCM na kueleza sera zake, kumewafanya wananchi kuendelea kuwa na matumaini na chama hicho.

“Unajua wapinzani ni watu wa ajabu sana, kila kitu kwao tatizo, hawajui hata historia ya jimbo hili, lilikuwa mwisho kwa maendeleo mkoani Tabora, lakini leo ni wa kwanza, lakini wanasema hakuna kitu kilichofanyika,” alieleza Juma Herman.

Herman alisema kwamba wananchi wamekuwa wakitaka kusikia sera za vyama, lakini wanachukizwa na sera za kutukana viongozi wa kitaifa na kupakana tope, kitu ambacho hakiwasaidii wananchi.

“Hivi mtu akisema huyu mbaya, mwananchi anajua ubaya wake nini... ni bora wakaeleza sera na namna ya kuwasaidia wananchi, lakini wao matusi na maandamano, ambayo hayana faida kwetu,” alieleza.

Alisema CCM itaendelea kuongoza jimbo hilo na kushika dola kutokana na mikakati yake imara ya kuwaondolea wananchi umasikini na kuwahimiza katika kufanya kazi kuliko kuandamana.

Katika uzinduzi wa kampeni hizo, Mkapa aliwataka wananchi kuwapuuza CHADEMA kutokana na kukosa sera nzuri za kuendeleza nchi zaidi ya kuandamana bila kutoa sera mbadala.

Katika hatua nyingine, baadhi ya vijana wamelaani kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CHADEMA cha kummwagia tindikali kijana mwenzao.

Jacob Maduhu (25) alisema kwamba kitendo hicho kimewasikitisha vijana na imekuwa matusi kwao kutokana na chama hicho kujitangaza kwamba ni mkombozi wa vijana.

“Hivi mkombozi wa vijana anaweza kuwaua vijana, hapana hiki ni chama cha mauaji, huwezi kumuharibia maisha kijana unayetaka kumkomboa kwa kumwagia tindikali,” alisema Mahudu.

Naye Salma Hamisi alisema kwamba amekuwa haelewi maana ya nguvu ya umma inayohubiriwa na chama hicho, kumbe maana yake ni kuangamiza umma kwa tindikali.

“Kila siku utasikia nguvu ya umma, hawaelezi sera zao, wao ni fujo na maandamano na kuwapiga wanaopingana nao, hizi ni siasa za wapi, maana waasisi wa taifa walitujengea siasa nzuri, sasa hizi za kumwagiana tindikali si zitatumaliza?” aliuliza.
 
Hoja ni kwamba wamchague na sio kama magwanda mnavyo potosha! Shame on you magwanda na magwanda yenu kama mgambo!
vipi mtaalam mbona unakurupuka?umekunywa chai?
ccm mmezoea kutumia majina ya watu angalia hilo jina siku unakutana na akina rev masanilo watakulisha kiti moto wakidhani ni mshirika,
tumia jina lako wewe ni mtu mzima bwana.
au ni gia ya kuoa mlokole kwa sababu nyie watoto wa uswahilini hamtabiriki.
 
"MNAMUONA HUYU? HUYU NDIE MKE WANGU, MAMA KAFUMU, ALINICHAGUA MIMI NIWE MUME WAKE, KWA HIYO NA NYINYI NYOOTE FANYENI HIVYOHIVYO!"
Naomba hio picha yake jamani
 
Labda ungesema kwa kitendo chao cha kumpa madaraka makubwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya taifa kumtaja mtu kuwa Rais na maamuzi yake kuwa ni ya mwisho na hakuna uwezo wa ku question na ku challenge maamuzi yake si kwenye chombo chochote nchini ikiwemo hata mahakama yeyote ile. hii inamaanisha kwamba hata kama mgombea A atapata kura 10 na mgombea B akapata kura 5 basi anao uwezo wa
kumtangaza mgombea B kuwa mshindi na hakuna mahakama inaweza kuskiliza malalamiko ya Mgombea A kwa maana uamuzi wa tume ni wa mwisho na hakuna mtu anaweza kuhuoji.
 
Jamani tunaomba mtuwekee magazeti angalau yanayojaribu kuwa fair angalau kidogo usitulete hapa gazeti liloandikwa na nape na mhariri akiwa kikwete mwenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom